Alhamisi, 31 Machi 2016




SADAKA YA FUNGU LA KUMI.

Ni sadaka yenye mkataba/agano na Mungu. Na mungu ametoa maelekezo kwamba endapo mtu hatatoa aina hii ya sadaka zipo adhabu zitakazofuatia baada ya yake. MWANZO 14:20…[Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.]…. Hapa aina hii ya sadaka inaitwa fungu la kumi. WALAWI 27:30…[ Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana.]… Hapa aina hii ya sadaka inaitwa ‘zaka’. Ni sadaka ambayo mbele za Bwana ni ‘takatifu’, kwa ajili ya matumizi ya kazi ya Bwana. MWANZO 28:22…[Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.]…. Ni sadaka ambayo pia hujulikana kama fungu la kumi. Kawaida, mtu akila vitakatifu vya Bwana hukumbana na adhabu.
-Vile uvifanyavyo vyaweza kufa, ikiwemo mifugo, kazi n.k.
TARATIBU ZA UTOAJI WA FUNGU LA KUMI
Ni mpango wa Mungu wa Kuwabariki watu waliookoka. MITHALI 15:8…[Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.]…Dhambi ni kikwazo cha kupata majibu kutoka kwa Bwana. Hata uzima wa milele tulio nao unatokana na utoaji wa Mungu kwa ajili yetu. Ibrahimu alitoa fungu la Kumi (MWANZO 14:17….[Abramu aliporudi kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme. 18 Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. 19 Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. 20 Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.]….
MATHAYO 23:23…[Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.]… Ni mpango wa Mungu kwa watu kutoa fungu la kumi.

KAZI YA FUNGU LA KUMI
i)Ni kuhakikisha kuwa nyumbani mwa Mungu pana chakula.
MALAKI 3:8-10…[Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. 9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. 10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.]… Kwa hiyo mojawapo ya kazi ya fungu la kumi ni kuona kuwa kipo chakula katika nyumba ya Bwana. Chakula kwenye nyumba ya Bwana kina maana gani? YOHANA 4:33-34…[Akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi. 33 Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula? 34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.]… Chakula katika nyumba ya Bwana ni kufanya kanisani pasiwe ukiwa, bali Injili ya Mungu iweze kusonga mbele.

ii) Mungu atakufungulia madirisha ya mbinguni.
MALAKI 3:10….[Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.]...

iii)Mungu atamkemea ibilisi alaye biashara zetu, afya zetu, ndoa yak n.k.
(MALAKI 3:11…[ Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.])….Ibilisi anakula. Kanuni inasema kuwa, Kama humtolei Bwana fungu la kumi, basi unamtolea Yule alaye. Ndiyo maana, unamkuta mtu Mataifa yatakuita heri. MALAKI 3:12…[Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.]… Siyo kwamba kwa kutoa fungu la kumi,Mungu atakupa fedha, bali atakupa vitu vya rohoni, mfano akili nzuri, karama, ujuzi n.k ambavyo vitawafanya watu/mataifa kukuita heri.
Swali: Nani Wa Kutoa Fungu La Kumi?
Kila mtu ana wajibu wa kutoa fungu la kumi. 1WAFALME 17:10-14…[Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa. 11 Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako. 12 Naye akasema, Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe. 13 Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao. 14 Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi.]…
ZINGATIO:
                Siri ya kutoa siyo kwa sababu vipo vingi, bali hata katika vidogo ni muhimu kutoa      fungu la kumi. Baraka zetu zimeambatanishwa na kutoa, tena hasa kwa watumishi wa Bwana.
MSINGI WA UTEKELEZAJI KATIKA KUTOA FUNGU LA KUMI
Kwa wale wafanyabiashara, endapo umechukua mkopo wako benki kwa ajili ya bishara, unapaswa kutoa sehemu ya kumi ya ule mkopo (mfano: mkopo wa sh.100,000 fungu lake la kumi ni shs. 10,000 na hivyo mtaji wako utakuwa shs. 90,000). Endapo biashara hii itaongezeka kwa kutoa faida. Mathalani mtaji na faida umefikia sh. 150,000, cha kufanya hapo ni kuondoa ule mtaji lakini kwenye faida (sh.60,000) unapaswa kutoa fungu la kumi ambalo ni sh. 6,000. Kawaida mtaji hautolewi fungu la kumi kama awali ulishatolea fungu la kumi. Mke asiye na kazi, hapaswi kuigusa pesa ya matumizi anayoachiwa na mumewe ili iwe fungu la kumi. Kama mumewe ameshalipa fungu la kumi yatosha. Hata hivyo, mume na mke wakiwa na kazi, kila mmoja anapaswa kutoa fungu la kumi. Mwanafunzi aweza kutoa fungu la kumi la ile pocket money apewayo na wazazi wake.
NB:
       Haipaswi kutoa fungu la kumi la fedha ya ADA upewayo ukiwa mwanafunzi kulipa shuleni.
MAMBO YA KUZINGATIA
Fungu la kumi hutolewa nyumbani mwa Bwana (Kanisani) mahali ambapo wewe ni mshirika, unapolelewa. Halitolewi tu kila mahali, bali pale ambapo Bwana ametuelekeza. Halitolewi kwenye mikutano ya Injili, wala kwa wajane wala kwa masikini na wagonjwa.
MADHARA YA KUTOTOA FUNGU LA KUMI
·         Laana kuitesa nyumba/Kazi za mikono yako.
ZEKARIA 5:1-4…[Basi, nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, gombo la chuo lirukalo. 2 Akaniuliza, Unaona nini? Nikajibu, Naona gombo la chuo lirukalo; na urefu wake ni dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa kumi. 3 Ndipo akaniambia, Hii ndiyo laana itokayo kwenda juu ya uso wa nchi yote; maana kwa hiyo kila aibaye atatolewa kama ilivyo upande mmoja, na kwa hiyo kila aapaye atatolewa kama ilivyo upande wa pili. 4 Nitaituma itokee, asema Bwana wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwivi, na katika nyumba yake yeye aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katikati ya nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.]…. Haijalishi wizi unaofanyika ni wa aina gani, lakini kutotoa fungu la kumi ni wizi kama wizi mwingine.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni