Jumamosi, 2 Aprili 2016

SOMO LA NYOTA YA MTU



SOMO: NYOTA YA MTU.
-Biblia imeeleza kuhusu nyota ya Yesu ilivyoonekana kutoka mashariki,
MATHAYO  2:1
-Hii inadhihirisha wazi kuwa kila mtu ana nyota yake.
-Nyota katika Biblia inawakilisha kipawa, hatima ya mtu, lengo lililomfanya Mungu akulete hapa duniani na kusudi lako la maisha.
-Hivyo tunaposema nyota yako ipo au imechukuliwa maana yake hayo mambo yamechukuliwa au yapo. Kimsingi hakuna mtu asiye na maana tangu kuzaliwa kwake, kwasababu kila mtu aliye duniani amekuja kwa kusudi lake. Kuna tofauti kati ya elimu na nyota; elimu sio nyota lakini elimu yaweza kunoa nyota. Na si kwamba kujifunza kunaleta nyota bali nyota ipo kwa wote lakini elimu inainoa nyota; na ndio maana ni rahisi kumwona mtu hana elimu lakini anamafanikio mahali fulani.
MHUBIRI 9:11
-Biblia inasema wakati na bahati huwapata wote na sio swala la elimu au ujuzi tu.
KAZI YA NYOTA.
-Nyota humfanya mtu kuwa mahiri katika utendaji kazi wake. (Effectiveness)
-Nyota huleta ubunifu katika maisha ya kila siku (Creativity)
-Nyota inamfanya mtu anatenda kwa ufanisi (Efficiency)
-Nyota huleta mvuto kwa watu kutoka mbali ili kuleta vitu kwa ajili yako(Attraction)
-Nyota humfanya mtu awe na maisha yenye mwelekeo na kibali mbele za watu. (Acceptance and Favor)
-Nyota humfanya mtu kusikilizwa katika jamii. Kuna vitu ambavyo mtu anaweza kuvipata kwasababu nyota yake imeonekana.
-Nyota yaweza kuvuta zawadi yaani vile vitu ambavyo hujavitaabikia, na ndio maana Yesu alipokuwa mdogo aliletewa zawadi na mamajusi wa mashariki.
MATHAYO 2:11
-Kwahiyo nyota ikichukuliwa maana sahihi ni kwamba hayo mambo hapo juu yote hayapo. MATHAYO 2:1-2
-Wakati Yesu anazaliwa kulikuwa na watu wanaitwa mamajusi, ambao walikuwa na uwezo wa kusoma nyota. Hivyo katika ulimwengu wa roho waweza kuona watawala wajao, maisha yajayo au yale yatarajiwayo. Na ndio maana Mamajusi wa mashariki ya mbali waliweza kuifuata nyota ya Yesu. Nyota inapoonekana inaweza kufuatwa, yaani watu wanaona zile kazi zake na kumfuata mtu. Kimsingi tunaposema mtu hana nyota maana yake umahiri, ufanisi na kibali vimechukuliwa. Lakini nyota ikionekana maana yake haya mambo yote yamerudishwa na hapo utamwona mtu anafanikiwa hata kama elimu yake siyo kubwa.

NYOTA ILIYOCHUKULIWA/ ILIYOFUNIKWA KICHAWI
Nyota ikifunikwa au kuchukuliwa kichawi maana yake mvuto, umahiri, ufanisi na uwezo unakuwa umechukuliwa au umefunikwa. Na ndio maana kuna watu wanahangaika kuanzisha kampuni, kujenga nyumba, kulima, au kufanya biashara kama nyota imefunikwa au kuchukuliwa kichawi huwezi kupokea mafanikio ya sahihi kwenye maisha. Watu wengi wanahangaika kuonekana au kukubalika lakini kumbe tatizo lipo kwenye nyota yaani imefunikwa au imechukuliwa kichawi. Wachawi wanaweza kuona nyota ya mtu na kuifunika ili isionekane.Hivyo ni muhimu kupambana Kwa Jina la Yesu ili nyota yako ionekane.

MADHARA YA KUISHI BILA NYOTA YAKO
-Kwa kuwa nyota ndiyo inamwezesha mtu kuwa na kila kitu, ndio kusudi la mtu, upendeleo wa mtu; hivyo madhara ya kutokuwa na nyota ni kutokuwa navyo vyote vile.
-Siku zote unakuwa unatenda chini ya kiwango (Under performance). Na kwa namna hiyo hakuna mtu anakubali kile unachotenda; yaani elimu na maarifa yote yakuwa chini ya kiwango.    -Utapata na kuibiwa;unapata kazi baadaye unaibiwa au unapata mchumba baadaye anaibiwa. Kimsingi huwezi kudumu na haya mambo. Unapata lakini anatumia mtu mwingine.
DALILI ZA NYOTA ILIYOFUNIKWA.
-Maisha kukosa mwelekeo; mtu akikosa nyota hata kama akiwa na elimu kama nyota haipo lazima mtu huyo atakosa mwelekeo.
-Kukwama kibiashara na kuishi maisha kwenye madeni.
-Unafanya kazi lakini hupati maendeleo. Yaani mtu anapata mshahara mzuri lakini anakosa mafanikio halisi.Wewe ni kiongozi lakini jamii haikutambui,Ukichangia hoja za mijadala mbalimbali hakuna anayekusikiliza. Umesoma lakini hupati kazi, na ukipata kazi haiendani na elimu yako Maisha ya upweke na hakuna anayekujali katika familia. Unatenda kazi kwa bidii lakini hupandi cheo. Kama ni binti sifa zote unazo lakini hakuna anayekuchumbia maana huonekani. Kuandamwa na mabalaa na mikosi. Kupotelewa na watu wa muhimu
UTAJUAJE NYOTA YAKO NI IPI?
-Usithubutu kwenda kwa mganga wa kienyeji au kusoma kwenye magazeti ili kujua nyota yako. -Ni muhimu kujua kilichoibiwa ni kipi katika maisha yako.
Isaya 47:13 “Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata.” FALAKI ni elimu juu ya mambo ya nyota.
-Lakini kuna mambo kadhaa yanayoweza kukuonyesha nyota yako ni ipi:
Moyo wako, akili zako na mawazo yako yanakuwa katika hilo jambo AMBALO NI NYOTA YAKO.
Mfano kama nyota yako ni biashara basi utakuta moyo wako upo kwenye biashara, Kama nyota ni kuimba au siasa lazima moyo utakupeleka kwenye kuimba na siasa.

NYOTA YAWEZA KURUDISHWA
-Kuokoka na kumpokea Yesu awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako ili upate uwezo wa kushindana.
-Ni kushindana kwa maombi.
KUMBUKA:
Hivyo tambua kuwa kwenye nyota yako ndipo kuna Baraka zako. Jambo ambalo ni nyota yako utalitenda bila kupambana; Yaani hutatumia nguvu kwenye kulitekeleza jambo hilo.
………………………………………………………………………………………………………
Pastor Amos E.Onesmo-0756391498

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni