Alhamisi, 31 Machi 2016

SOMO LA UTOAJI



SOMO LA UTOAJI.
“Lakini kama vile mlivyo mbele sana katika yote: Katika imani, katika usemi, katika maarifa, katika uaminifu wote na katika upendo wenu kwetu sisi, vivyo hivyo tunataka pia mzidi katika neema hii ya kutoa.” (2 Wakor.8:7).
·         Utoaji haujaanza leo,ulifanywa hata enzi za mitume.
“Njaa hiyo ilitokea wakati wa utawala wa Klaudio. Mitume wakaamua kwamba kila mtu, kulingana na uwezo wake alio nao, atoe msaada kwa ajili ya ndugu wanaoishi Uyahudi..” (Matendo.11:29).
·        Utoaji ni pando lenye kuleta matokeo,pia tutoe kwa moyo wa kupenda.
“Ye yote apandaye kwa uchache pia atavuna kwa uchache, naye apandaye kwa ukarimu pia atavuna kwa ukarimu. Kila mtu ATOE KAMA ANAVYOKUSUDIA MOYONI MWAKE, si kwa UCHOYO au kwa KULAZIMISHWA, kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu.” (2 Wakor.9:6,7).
·        Tutoe kwa ajili ya kufanikiwa kwetu.
“Basi kuhusu changizo kwa ajili ya watakatifu. Kama nilivyoyaagiza makanisa ya Galatia, fanyeni vivyo hivyo. Siku ya kwanza ya kila juma, kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, KWA KADIRI YA KUFANIKIWA KWAKE…” (1 Wakor.16:1,2).
 ZINGATIO:
                    “Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu.”
·         Utoaji hauna mipaka.
“…wale waliokuwa na mashamba na nyumba waliviuza, wakaleta thamani ya vitu vilivyouzwa, wakaiweka miguuni kwa wale mitume, kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake.” (Matendo 4:34,35).
“ingawa walikuwa maskini kupindukia, kwa upande wao walifurika kwa wingi wa ukarimu. Kwa maana nashuhudia kwamba wao walitoa kwa kadiri wawezavyo, hata na zaidi ya uwezo wao, kwa HIARI yao wenyewe,” (2 Wakor.8:2,3) Luka 6:38.
Mistari inayohusu MAFUNDISHO juu ya utoaji katika Agano Jipya.
“Katika kila jambo nililofanya, nimewaonyesha kwamba kwa njia hii ya kufanya kazi kwa bidii imetupasa kuwasaidia WADHAIFU, mkikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe jinsi alivyosema, ‘NI BARAKA ZAIDI, KUTOA KULIKO KUPOKEA.’ ” (Matendo 20:35).
“Changieni katika mahitaji ya watakatifu…” (Warumi 12:13). Kutoa pesa kwa ajili ya ndugu maskini ilikuwa jambo la muhimu sana makanisani wakati wa mitume! Petro alipozungumza na Paulo juu ya Injili alimwambia, “Walichotuomba ni kwamba tuendelee KUWAKUMBUKA MASKINI, jambo ambalo ndilo nililokuwa na shauku ya kulifanya.” (Wagalatia 2:10).
“Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.” (1 Yoh.3:17,18).

 

KANUNI ZA KIROHO JUU YA UTOAJI.

 i) Mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake.
ii) Si kwa uchoyo.
iii) Usitoe kwa kulazimishwa.   1 Wakorintho 16:1-3

MAANDIKO KATIKA  YANASEMAJE KUHUSU UTOAJI AU MSAADA KWA WACHUNGAJI NA WATUMISHI WENGINEO?.

“Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi?” 1Wakor 9:7.
 13-14“Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu? Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.”

·         1 Timotheo 5:17-18

“Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.” (Kwa lugha ya Kigiriki neno ‘wazee’ ni sawa na ‘wachungaji’.)-Hapo hataji ‘fungu la kumi’
 “Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni; mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao.”
1 Wathesalonike 5:12-13
Ø  MFANO KANISA  LILIMTAMBUA PAULO.
Wafilipi 4:10-17
Kutokana na mistari hiyo hapo juu, tunaona Wafilipi walichagua kwa hiari yao kumsaidia Paulo kwa ajili ya kazi yake kwa ajili yao na kwa ajili ya Injili. Na utoaji huo ulitokana na upendo wa Mungu ndani ya mioyo yao – wala hamna aliyewalazimisha kufanya hivyo!
“Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi, tena nimejaa tele; nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.”
==============================UBARIKIWE!============================
Pastor.AMOS E.ONESMO-0756391498

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni