KUKOMBOLEWA KUTOKA KATIKA NGUVU ZA
GIZA.
Ni kusudi la Mungu mwanadamu aishi maisha mazuri na
yakumpendeza yeye,tena Mungu alimuweka mwanadamu kuwa mtawala katika
ulimwengu huu ambao Mungu aliuumba ila tu mwanadamu alipoteza nafasi hiyo
baada ya kufanya dhambi (Yer.5:25)lakini Mungu kwa neema yake na upendo wake
alimtuma Mwanawe wa pekee Yesu Kristo awakomboe wanadamu(Yoh.3:16)
nakuwapatanisha na Mungu na hivyo kuirudisha nafasi ile ambayo Mungu alimuwekea
mwanadamu ila shetani kwa ujanja wake aliichukua(Mwanz.3:13)
Fuatana nami katika mafundisho
haya,tafakari kwa kina kisha chukua hatua
Ukisoma katika Uf.12:17 utaona kuwa shetani amekasirika
dhidi ya mwanamke na amedhamiria kufanya vita juu ya uzao wa mwanamke lakini
hasira yake ni juu ya wale wazishikao sheria za Mungu na wenye ushuhuda wa
Yesu (Ebra.12:1); nia yake ni atawale kizazi cha mwanamke,wale wasiompinga
hana hasira nao maana wanakuwa chini yake (Ef.2:1-3).
Katika Mwanzo 3 tunaona kuwa Wazazi wetu wa kwanza,adamu
na hawa,walimkabidhi shetani dunia waliyopewa na Mungu (2Kor.4:3-4), hivyo
basi shetani akatumia hila na uongo (Yoh.8:44) ili awafunge waweke
patano/mkataba nao
Shetani ni mwerevu mwenye ngazi ya kimalaika,kumbuka hapo
mwanzo alikuwa malaika mwenye cheo kizuri huko
Mbinguni(Isa.14:9-17),anafahamu tabia za Mungu na mambo yote mazuri ambayo
Mungu ameyaweka kwaajili ya mwanadamu ndio maana alitaka kumpindua Mungu
akashindwa na badala yake amekusudia kumpotosha mwanadamu ili asipate yale ambayo
Mungu ameweka kwaajili ya wanadamu
Kumbuka mwanadamu nizaidi ya malaika ndio maana malaika
hakupewa kutawala na Mungu isipokuwa mwanadamu(Mwanz.1:26, 1Kor.6:3).
Shetani naye anatamani kuabudiwa na kuogopwa na mwanadamu
ndio maana anafanya yote haya(Isa.14:13); biblia inasema shetani alipambana
na malaika,hivyo mwanadamu peke yako huwezi kupambana naye isipokuwa ukiwa na
Nguvu za Mungu na kwa kumkubali Yesu katika maisha yako maana yeye ni
Jemedari wa vita(Rum.10:9-10).
Shetani anaelewa kwamba Mungu ni wa maagano,na agano
linadumu kizazi hata kizazi (Torati 8:18,Zab.102:12) Shetani anafanya mbinu
za kuwadanganya wanadamu wapuuze mkataba wao na Mungu halafu anawashawishi
kuanzisha mkataba mpya nao(2Tim.2:26)
Shetani baada ya kuiteka dunia kutoka kwa Adamu na Eva
aliweka mtandao wake kabambe wenye ‘programs’ ili ashinde,ana
‘administration’ yenye vyeo mbalimbali,mfano Ef.6:12,Ef.2:3
Falme na mamlaka,Wakuu wa giza hili,Jeshi la pepo wabaya
Shetani alipomjaribu Yesu alimuonyesha milki hizo na
alitaka Yesu amsujudie lakini Yesu alimshinda(Luka 4:5-13).
Mfano wa program za kishetani ni kutambika mizimu,ibada za
sanamu,uzinzi n.k.(1Kor.6:9-10)
Kizazi kinapoanza kumdharau Mungu na kuingia mikataba
mingine na shetani laana inaanza kutembea kwa kasi mfano;laana ya
magonjwa,umaskini na ‘abnormalities’ zisizotibika (Kut.20:5)
Laana inarithiwa kama vile ambavyo Baraka inavyoweza
kurithiwa,Kutoka 20:1-6, Mungu aliamua laana itembee,agano linapowekwa si
rahisi kulivunja, Gal.3:15,Yer.6:16-20
Nimuhimu pia kufahamu baadhi ya aina za laana kama
ifuatavyo;
Laana zitokazo kwa Mungu zisababishwazo na kwenda kinyume
na sheria za Mungu Tor.11:26-29
Zitokanazo na watumishi wa Mungu Mk.11:20-24,Mdo.13:8-12, 2Waf.5:20-27, 1Waf.16:34, Josh.6:26-27 Laana za mahusiano
i) Mtu kujilaani mwenyewe Mwn.27:24-25
ii) Kumtendea mtu mwingine uovu Mwn.4:9-11
iii)Mzazi kwa mototo Mwn.31:22-29 (kumbuka laana isiyo na
sababu haimpati mtu)
iv)Mtu kujiunganisha na nafsi nyingine,hapa kuna njia
nyingi kwa mfano;
Kuchanjiana damu,Kwa njia ya zinaa
Laana zenye mkono wa ibilisi au kupitia wajumbe wake
mfano;kwa njia za matambiko,kwenda kwa waganga n.k
Kumbuka milango ya madhabahu za shetani;
Kupewa majina ya waaguzi na wachawi,Kupewa majina mabaya,ibada
za ndoa za kienyeji
kuchanjwa na wajumbe wa shetani,kutoa vitu kwa mganga au kutumia vitu vilivyotolewa kwa mganga kuvaliana nguo,kutoa mimba
Matokeo ya laana ni;
v Magonjwa yasiyotibika
v Ndoa zinazovunjikavunjika,kutokuolewa au kuoa ktk koo
v Mimba kuharibikaharika
v Watu kujinyonga au vifo visivyoeleweka ktk ukoo
v Vifo vinavyofanana ktk ukoo
v Hali ya kichaa au mataahira ktk ukoo
v Ukoo kusambaratika na kuchukiana
v Roho za zinaa,ulevi n.k ktk ukoo
Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo yanaweza kukusaidia
umetoka wapi,uko wapi na unakwenda wapi au unatakiwa kufanya nini katika
maisha yako ya kimwili na kiroho pia,hivyo basi;
Nini chakufanya:
Kumbuka swala la kumpendeza Mungu
na kwenda Mbinguni ni lako binafsi (2Kor.13:5)
Mungu hakukuumba uishi maisha ya taabu bali ya raha na ya kiutawala (Mwanzo 1:26) Baadhi ya laana na mikataba ya giza unaweza kuivunja kwakusema kwa kinywa chako maneno yaliyo kinyume na mikataba hiyo na kuamua kuachana nayo kabisa (Rum.10:9-10, Mat.12:37, Mith.18:21). Kuzivunja laana na mikataba/maagano ya giza na kukubali kumpokea Yesu katika maisha yako,Damu yake iliyomwagika Msalabani inatakasa laana na maagano yote kwa agano jipya ktk damu yake takatifu,na jina la Yesu ndilo pekee linaloweza kuvunja laana na kukuweka huru (Mat.4:12,Fil.2:9-10,Mat.1:21)
By. Onesmo-0756391498
|
Jumatatu, 21 Machi 2016
KUKOMBOLEWA KATIKA NGUVU ZA GIZA
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni