Jumapili, 20 Machi 2016

YATAKAYOTOKEA BAADA YA UNYAKUO



UFUNUO 6:1
Kunyakuliwa kwa kanisa siyo kuja kwa Yesu mara ya pili,mitajo yote inayotajwa au kumuonyesha Bwana Yesu akionekana Duniani inataja juu ya kuja mara pili kwa YESU.Watu wengi wamekuwa wakihubiri kuwa kunyakuliwa kwa kanisa kuwa ndo mwisho wa dunia tunaposema hivyo ni makosa lakini tujuavyo kanisa litanyakuliwa kwanza baada ya miaka 7,ndipo Yesu atakapokuja hapo ndipo ule mwisho utafika .
v  YOWELI 2:2 AMOS 5:18-20
Kunyakuliwa kwa kanisa kutafuatana na mambo makuu mawili.
i)Hukumu ya watakatifu,watadhihirisha kazi yao.
v  1WAKORITHO 3:12-15    IIWAKORINTHO 5:10
ii)Hukumu ya Mungu kwa watakaobaki Duniani,kama alivyoona katika maono YOHANA.
01.Kisha Yohana akamuona Yesu akichukua kile kitabu mkononi mwa Mungu naye akaanza kuzifungua kurasa zake.
02.Hukumu za Mungu zimegawanyika katika sehemu kuu tatu:-
            i)Muhuri.
          ii)Baragumu.
         iii)Vitasa.
03.Hivyo Yesu akaonekana akafungua hicho kitabu na muhuri zake ambazo ni zile SIRI
MUHURI YA KWANZA
01.Ilipofunguliwa hii muhuri kulitokea fahari mweupe naye aliyempenda alikuwa na UTA.
-Pia alipewa taji tena alitoka akishinda tena apate kushinda  UFUNUO 6:1-2
02.Baada ya kanisa kuondolewa Mpinga Kristo ataruhusiwa kuanza kazi DANIELI 7;23
v  2THESALONIKE 1:2    UFUNUO 13:1.8
A)Farasi mweupe-Huyu jamaa alikuja akiwa na mavazi meupe ambayo ni ishara ya Amani;Kwa hiyo baada ya kanisa kupaa atakuja ili kuleta AMANI duniani DANIELI 9:27
-Lakini huyu jamaa ni MUONGO maana yeye siye mtu wa AMANI bali ni mtu wa VITA.
03.Kuwa na uta mkononi
B)Uta ni silaha ya vita,pia hutudhihirishia kuwa huyu ni MTU WA VITA.
C)Taji hii ni kumanisha kuwa ni MFALME.
-Huyu jamaa japokuwa anakuja katika alama ya WEUPE pamoja na kuwa amepanda FARASI MWEUPE kama Yule ambaye kristo atakuja amempanda.
v  UFUNUO 19:11-21
-Ila tofauti ni hii yesu atakuja bila uta bali atakuja kuvunja UTA huu.
v  YEREMIA 49:35 ZABURI 46:9
-Pia huyu jamaa atafuatwa na matukio ya kutisha lakini ni kristo atakuja kuyakomesha matukio hayo hivyo huyu jamaa atakapotokea atakuwa amevaa Uovu.
v  2 THESALONIKE 2:3-9
-Basi dunia itakuwa imeshakuwa juu ya mtu huyu wa dhambi ambaye atakuwa na ahadi nyingi za amani katika dunia hii ambayo itakuwa imejaa VURUGU nyingi na MACHAFUKO.
-Kipindi hicho matatizo ya kijamii,kiuchumi yataongezeka mashirika ya kimataifa yatajitahidi kuyaondoa lakini hayataweza.Hivyo huyu mtu wa dhambi akiwa na nguvu pamoja na ushawishi atakuwa na uwezo wa kuzivuta serikari na kuwa na usikivu wa kimataifa maana atakuwa amepitia njia yake ya kwenda kutimiza azima yake yakutisha sana huku akiwa mwenye kuigiza sana juu ya kristo yeye anaonekana kuwa juu ya farasi mweupe ambao ni mfano wa Amani lakini yeye hana mpango wowote wa kuleta Amani.Bali mpango wote wa kishetani ni kuiondoa Amani duniani hata ile kidogo ambayo itakuwepo.
-Hivyo ile kusema eti njoo ni kuruhusiwa kwa shetani kuanza kazi ndani ya huyu mtu hivyo ruhusa yake imo katika muhuri wa kwanza ambayo Yesu aliivunja.
MUHURI YA PILI (2)
VITA VYA KIMATAIFA.MATHAYO 24:7A
-Yohana aliona kulipovunjwa mhuri ya pili kulitokea farasi mwekundu aliyempanda akaambiwa kuiondoa AMANI Duniani kisha akapewa UPANGA mkubwa sana
v  UFUNUO 6:3-4
A.Farasi mwekundu ni ishara  ya Damu.
B.Kuiondoa Amani ni kuachia watu wauane .
C.Upanga mkubwa ishara ya kuchinjana .
-Hivyo muhuri hii inahusika na vita vya kimataifa na matetesi ya vita MATHAYO 24:6-7
-Hivyo hii vita siyo ya nchi kwa nchi bali ni mataifa ambayo yatakua yanajiunga kunyukana yenyewe kwa yenyewe ndiyo maana huyu jamaa alipoiondoa Amani duniani alipewa na upanga wa kuchinja.
-Hivyo Amani ikiondolewa chuki,ubaguzi wa kimakabila vitaongezeka tendo ambalo litafanya machinjano makali.
MUHURI YA TATU (3).
NJAA YA KIMATAIFA MATHAYO 24:7B
-Yohana aliona baada ya kuvunja muhuri ya tatu farasi mweusi naye aliyempanda ana mizani katika mkono wake akaambiwa kibaba cha ngano kwa nusu rupia na vibaba vitatu vya shayili nusu rupia lakini asiyadhuru mafuta wala divai. 
v  UFUNUO 6:5-6
A.Farasi mweusi ni kumanisha giza yaani hakuna kitu.
B.Mizani ni ishara ya kupimiwa chakula.
C.Kibaba cha ngano nusu rupia ni kuonesha ni chakula kidogo kitauzwa kwa fedha nyingi kazi ya ngano ni kutengeneza mkate au ugali.
D.Vibaba vitatu vya shayiri nusu rupia.shayiri ni zao ambalo hulimwa kama mbonga
E.Usiyadhuru mafuta wala divai ni kuonyesha kuwa katika muhuri hii hivi havitaharibika.
-Hivyo mahali popote ambapo maandiko huzungumza juu ya kupimwa kwa ngano au nafaka au shayiri basi hilo ni tendo la njaa kali.
v  2 WAFALME 7:1      EZEKIELI 4:10-17    MATHAYO 24:7B
-Hivyo,dunia itakuwa imeharibiwa na vita pamoja na njaa.
MHURI WA NNE (4).
MAUTI NA KUZIMU
-Baada ya kufunguliwa kwa muhuri hii ya nne kulitokea farasi wa KIJIVU naye aliyempanda aliitwa MAUTI na kuzimu itafuatana naye na wataua kwa upanga na kwa njaa na kwa Tauni na kwa hayawani wa nchi.
v  UFUNUO 6:7-8
A.Mauti kazi yake ni kuua.
B.Kuzimu kazi yake ni kupokea walio kufa.
C.Kupewa kuharibu robo ni kuonyesha kuwa mihuri hii minne itahusika na robo ya duniani tu.
D.Waue kwa njaa hii njaa ni tofauti na ile kwa muhuri ya tatu maana ile ilihusika na vibaba lakini hii hakuna mtu kununua wala kuuza mpaka awe na namba ya Yule jamaa.
v  UFUNUO 13:16-18
-Kwa hiyo hapo watakaofanikiwa ni matajiri ila maskini wengi watakufa.
E.TAUNI-Ni mojawapo ya magonjwa yasiyozuilika.
v  2 SAMWELI 24:13
F.HAYAWANI WA NCHI-Hawa ni wanyama wa kila aina pamoja na ndege wa kila aina ndiyo hayawani
-Kwa hiyo baada ya njaa hiyo wanyama watakosa chakula,ndege pia watakosa chakula hivyo ule utisho ambao Mungu aliuweka ndani ya mwanadamu hapo alipomuumba Adamu ili wanyama wamuogope utakwisha hivyo wanyama pamoja na ndege watakuwa wanamwinda mwanadamu ili wapate chakula pia hata wanyama wa kufugwa watamla mwanadamu.
MUHURI YA TANO (5).
ROHO ZAO WALIO CHINJWA CHINI YA MADHABAHU{UFUNUO 6:9-11}
-Baada ya kufungwa kipindi cha unyakuo neema ilikoma hivyo Yohana katika muhuri hii anaona watu wanaokatwa vichwa vyao kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu kristo.
-Muhuri hii ilipofunguliwa aliziona Roho chini ya madhabahu zikidai ni lini Mungu atazipatia haki juu ya damu zao nao wakawaambia kuwa wapumzike hata itakapotimia hesabu ya ndugu zao.
A.Madhabahu-hii iko mbele za Mungu nayo ni kwa ajili ya Yesu kufukiza uvumba ili azidi kutupatanisha na Mungu wetu.
v  UFUNUO 8:3-4
B.Roho zikidai haki-Ikiwa na maana hata lini Mungu atawaadhibu watu walio wakata vichwa.
C.Kungoja mpaka watakapotimiza hesabu ya ndugu zao ina maana kuwa hawa watu waliokatwa vichwa waliuawa katika dhiki ile ya kwanza ya mitatu(3 ½). na nusu miaka ya kwanza.Hivyo Mungu aliwaahidi kuwa kutakuwepo watu wengine watakaouawa katikati ya dhiki kuu yaani kati ya miaka ile ya mwisho mitatu na nusu(3 ½).
v  UFUNUO 7:9-17
-Hivyo hawa wakipatikana ndipo Mungu atakapo wapatia wale wa kwanza haki zao.
MUHURI YA SITA (6).
HASIRA ZA MWANA KONDOO.{UFUNUO 6:12-17,MATHAYO 24:25}.
-Katika muhuri hii ya sita Yohana anaona mambo ya ajabu yaliyotokea.
A.Tetemeko kuu la nchi.
B.Jua kuwa jeusi kama gunia la singa.
v  MATHAYO 24:29-30
C.Mwezi kuwa damu.
D.Nyota kuanguka kama mapooza ya miti.
E.Mbingu kuondolewa kama ukurasa uliokunjwa.
F.Milima na visima kuhamishwa.
G.Watu wa kila aina watajificha katika mapango ya mawe.
H.Watu kuiambia milima iwasitili na uso wa Yesu au Mwana kondoo.
J.Siku kuu ya hasira na hakuna mtu awezaye kusimama.
-Hivyo baada ya kufunguliwa muhuri hii Yesu kristo akaruhusiwa kuja duniani kutawala ndiyo maana majemedali watalia maana atakuwa amekuja na utisho ambao haujawahi kuonekana duniani .
v  UFUNUO 1:7
-Jambo la ajabu wanadamu wanashindwa kumlilia Mungu wanaililia milima eti tusitili na hasira ya Mwana kondoo .
-Jambo la kuzingatia ni kwamba muhuri hii itafunguliwa baada ya kumalizika vitasa,baragumu na mihuri mingine hapo ndipo huu nao utafunguliwa .
MUHURI YA SABA (7).
UKIMYA MBINGUNI KAMA MUDA WA NUSU SAA{UFUNUO 8:1}
-Muhuri hii inapigwa katika sura ya nane maana sura ya saba inatoa mlolongo wa mambo yatakayo tokea baada ya kupigwa baragumu.Maana malaika wanne tayari kuidhuru nchi lakini wanaambiwa bado mpaka watakapotia muhuri wateule wa Mungu.
-Tukumbuke kuwa mataifa tutalithi neema kutoka kwa waisraeli. Baada ya Mungu kufanya mizito mioyo yao ili wasiamini .
v  WARUMI 11:15, 11:25-26
-Kwa hiyo kanisa likiondoka hii neema kwa mataifa itakoma na kurudi Israeli ndiyo maana huyu malaika aliwazuia hawa malaika katika sura ya nne wasidhuru nchi hadi hao 144,000 ambao ni malimbuko ya Mungu watiwe muhuri ya Mungu,
-Basi tuangalie muhuri hii yohana anaona nini?.
A.Anaona ukimya mbinguni jambo hili nila kutisha sana maana vinanda vinakoma kuimba nusu saa.(30dk).
B.Pia kwa mahesabu ya mbinguni nusu saa ni kubwa mno,mfano tunasoma kuwa siku moja ni sawa na miaka elfu moja kwa Mungu hivyo hatujui huo ukimya ulikuwa siku ngapi?
C.Wazee ishirini na wanne walikaa kimya hakuna cha kuanguka wala kupiga kinubi.
D.Wenye uhai wanne walitulia hakuna chakusema eti mtakatifu ni Bwana.
Hapa inamaanisha Mungu alisimama ili aihukumu dunia sawasawa ndiyo maana vitu vyote vilikaa kimya maana mzee amesimama,pia ndiyo maana huyu malaika aliwahi kuwatia muhuri kabla Mungu hajainuka.
-Hicho kitendo cha Mungu kusimama kinatisha mno na mlololngo unaotokea hapo unafuatana na siku ya BWANA iliyoko ndani ya muhuri ya sita(6).
-Kutiwa muhuri kwa watu hawa ni ishara ya kulindwa na mapigo ya zile baragumu.
BARAGUMU YA KWANZA.
MVUA YA MAWE,MOTO NA DAMU{UFUNUO 8:7}.
-Yohana aliona mvua ya mawe,moto uliochanganywa na damu,miti na majani yakateketea.
v  KUTOKA 9:22-25
i)Mvua ya mawe siyo haya tuliyozoea kuyaona bali ni mawe yanayo haribu kabisa bila huruma
v  KUTOKA 9:22-25 YOSHUA 10:11
ii)Moto huu ni kumalizia visiki na vitu vingine ambavyo vimeachwa na ile mvua.
v  MALAKI 4:2
iii)Damu hii ni kuthibitisha kuwa kutakuwa ni uharibifu mkubwa mno usio wa kawaida.
v  KUTOKA 12:23,20 na 30
BARAGUMU YA PILI.
MLIMA UNAOWAKA MOTO{UFUNUO 8:8}.
-Yohana aliona kitu mfano wa mlima unaowaka moto kikitupwa ndani ya bahari.
-Kilisababisha theluthi ya bahari kuwa damu,theluthi ya viumbe vikafa na theluthi ya merikebu kuharibiwa.
-Baragumu hii inahusiana na ile muhuri ya tatu maana baada ya kupigwa ile ya kwanza na kuharibu mimea na miti watu wengine wataamua kuvua samaki na wengine kutuma misaada kupitia baharini wakibeba makontena na kuyapakia ndani ya merikebu.
-Hivyo,baragumu hii inapopigwa Mungu anaamua kuua theluthi ya samaki pamoja na kuangamiza theluthi ya zile Merikebu zinazobeba misaada.Hivyo njaa inazidi maana Mungu ameiharibu kila njia ya kupitia chakula.
BARAGUMU YA TATU.
NYOTA KUBWA INAYOITWA PAKANGA.{UFUNUO 8:10-11}
-Ilipopigwa Yohana aliona nyota kubwa ambayo ilikuwa inawaka nayo ilikuwa ikiitwa PAKANGA nayo ilianguka katikati ya theluthi ya mito na juu ya chemichemi za maji nayo maji yote yakawa PAKANGA.
a)PAKANGA-Maana yake ni Uchungu.
b)Chemichemi za maji-Ni mahali ambapo bahari na mito huanza.
-Hivyo,Baragumu hii inahusika na mapigo juu ya maji.Pamoja na kuwa Mpinga kristo ana nguvu bado anaendelea kuchanganyikiwa  na kutazama huku watu wakiendelea kufa baada ya kunywa maji yale.Na mpinga kristo anashindwa kutoa msaada wowote.
BARAGUMU YA NNE.
MWEZI,NYOTA KUWA GIZA.{UFUNUO 8:12}
-Baragumu hii inahusika na mapigo juu ya nyota,mwezi na jua.
-Vitatiwa giza,wataalamu wa nyota watahangaika ili wajue sababu lakini hawataweza maana Mungu atataka kuwaonesha kuwa anaweza.


BARAGUMU YA TANO.
KUACHIWA NZINGE NA MWANZO WA OLE{UFUNUO 9:10}.
-Yule malaika aliyekuwa analia akisema eti ole
v  UFUNUO 8:13
-Alikuwa anatoa tahadhari maana hizi baragumu tatu yaani zinahusika na mapigo juu mwanadamu mwenyewe
v  YOHANA 5:6-7.
-Baragumu hii ilipopigwa Yohana aliona nyota ikianguka juu ya nchi naye akapewa ufunguo na kulifungua shimo nalo ndani yake kukatoka mfano wa moshi ukifuatwa na nzige walio kuwa ni wa adhabu mno.
v  UFUNUO 9:1-10
A.Nyota yenye ufunguo =hii siyo nyota bali ni malaika.
B.Shimo=Ni mahali ambapo ni kifungo cha mapepo wachafu.
C.Moshi=Huu sio moshi wa kawaida bali ni kwa kuwa hawa nzinge walikuwa wengi walionekana mithili ya moshi.
D.Nao walikuwa wengi mno.
v  UFUNUO 9:I-3.
E.Kudhuru miezi mitano ni mipaka waliyo wekewa
F.Mfalme wa kwao naye ni malaika wa kuzimu huyu huitwa ABADONI KWA KIEBRANIA,KIYUNANI huitwa APOLIONI
                                 SERIKALI YA SHETANI IKO HIVI
                                                    Shetani(Isaya 14:13-14).


                                 
                                           Belzebuli(Luka 11:15)                    Apolioni(Ufunuo 9:11)
-Hivyo huyu Apolioni ni mkuu wa majeshi ya shetani ya huko kuzimu
-Belizebeli naye ni mkuu wa majeshi ya shetani duniani BELIZEBULI APOLIONI
v  UFUNUO 9:11
-Hivyo hawa siyo nzinge wa kawaida bali ni aina Fulani ya mapepo hivyo wanapo funguliwa ni manufaa ya shetani maana viumbe wake wameachiwa huru kwa wale malaika alioanguka nao wamo katika shimo hilo.
-Hivyo waamuliwa kutesa kila mtu asiye na muhuri ya Mungu kwenye paji la uso na watu wenye muhuri ni wale 144,000 tu nao ni wayahudi peke yao.
-Pia hawatadhuru binadamu wote bali ni theluthi tu na nguvu ya nzige hawa itakuwa katika mikia yao .
BARAGUMU YA SITA (6).
KUFUNGULIWA KWA MALAIKA WALIOFUNGIWA KWAENYE MTO FRATI.                  UFUNUO 9:13-19.
-Baada ya kupigwa kwa  baragumu ile ya sita Yohana alisikia sauti ikisema kuwa wafunguliwe malaika wanne waliofungiwa kwenye mto mkubwa ule  FRATI.Nao wamewekwa kwa ajili na tayari  ile saa na siku na mwezi na mwaka ili waue theluthi ya wanadamu.
-Malaika hawa walikuwa na jeshi wapanda farasi wapatao 200,000,000.Na farasi hao walikuwa wa ajabu.
-Hivyo baragumu hii ya sita inahusiana na muhuri ya nne ambayo ilitokea na mauti na kuzimu.
v  UFUNUO 6:7-8.
-Farasi hawa wana nguvu zaidi ya wale Nzinge maana wao wanatesa pia wanaua kwa kupiga mapigo:-
i)Moto
ii)Moshi
iii)Kiberiti
v  UFUNUO 9:18
-Farasi hawa wana vinywa kama simba kuonesha nguvu zao pia wana mikia kama nyoka kumaanisha ukali wao.
-Jambo la ajabu aliloliona Yohana,wanadamu waliosalia hawakuzitubia dhambi zao wala kuacha kuabudu sanamu zao za miti,mawe,dhahabu,Fedha na shaba.Pamoja na Mashetani
v  UFUNUO 9:20-21

BARAGUMU YA SABA.
SHETANI ANYANGANYWA UFALME.
UFUNUO 11:15-18
-Baragumu hii inaendana na muhuri ya sita.
-Muhuri hii na Baragumu hii vinatoa utawala wa Shetani na kuurudisha kwa Yesu kristo.
-Baragumu hii na Muhuri hii ndivyo vitakavyokuwa vya mwisho katika hukumu zote.

VITASA.
Kitasa Cha Kwanza{Ufunuo 16:1-2}.
-Pigo hili ni juu ya wale waliopokea chapa ya mnyama pamoja na kuisujudia.
-Jipu baya=maana yake ni kufuru au kujaza usaa mwingi.
-Bovu humaanisha kuwa yatakuwa yanajipasua yenyewe nayo yatashika kila sehemu bila kuchagua.
Kitasa Cha Pili{Ufunuo 16:3}.
-Hukumu hii inapiga juu ya bahari na kuigeuza kuwa damu.
-Theluthi ya maji inabadilika kuwa damu.Na hii ni tofauti na ile ya baragumu.
v  UFUNUO 8:9
-Kitasa kilipomiminwa bahari nzima iligeuka damu viumbe wote wa bahari wakafa.Bahari nzima ikawa na harufu ya mauti maana yatakuwa mekundu pia meusi.
Kitasa Cha Tatu{Ufunuo 16:4-6}.
Mito Kuwa Damu.
-Katika Baragumu ya tatu maji yaligeuka kuwa machungu,lakini katika hukumu hii ya kitasa maji yamekuwa damu kila mahali penye mto duniani utakuwa damu ndiyo maana imeandikwa kwa kila chemichemi ya maji iligeuka.
-Hivyo hata mtu akichimba kisima kitakuwa damu na watu watainywa maana hawana la kufanya.
-Kisha Yohana akasikia sauti ikisema,”Ni za haki hukumu zako maana waliimwaga damu ya watakatifu nawe umewapa wainywe”.
Kitasa Cha Nne{Ufunuo 16:8-9}.
Joto Kali
- Katika pigo hili jua litashushwa kidogo na kutoka lilipo sasa hivyo litakuwa linachoma na kuunguza hakutakuwa na kivuli chochote maana miti imeshakauka yote.
-Maana baragumu ya kwanza miti yote imeshateketezwa
v  UFUNUO 8:7
-Kutakuwa na joto mara mia(x 100).
Kitasa Cha Tano{Ufunuo 16:10-11}
Ajali Ya Mpinga Kristo.
-Mpinga kristo atakuwa amekwisha hama Yerusalemu na kusimamisha chukizo la UHARIBIFU.
-Lakini kwa kuwa alipewa kufanya kazi miezi 42 au miaka mitatu na nusu ya kwanza sasa imeshamalizika.
-Malaika huyu aliongoza moja kwa moja kwenye utawala na ufalme wa Mpinga kristo.Na alipomimina kitasa chake juu ya ufalme kulikuwa na:-
i)Giza zito-Huumaanisha kila taa ilizimika.
ii)Maumivu-Huumanisha kufuatana na yale majipu na madonda mengi tena na hapana mwanga watakuwa wanaumia sana na kupiga kelele.
v  EZEKIEL 14:12-13.
iii)Wakatafuna ndimi zao-Huumaanisha kutafuna ndimi zao hapa ni kutokana na maumivu mazito.
-Wala hapa Mpinga kristo hana msaada juu yao yeye mwenyewe yuko hoi,hivyo Mungu audhihirisha uwezo wake juu ya Mashetani.
Kitasa Cha Sita{Ufunuo 16:12-16}.
Frati Unakaushwa.
-Kitasa hiki ni cha kuruhusu vita ya HALMAGEDONI.
-Huu mto FRATI ulikauka mara moja ili kutengeneza njia ya kupitishia Majeshi ya nchi za mashariki na nchi za mawio ya jua.mfano:China watakuja kupigania PALESTINA lakini wataifikia ajali yao.
-Mto ulipokauka Yohana aliona Roho tatu mfano wa vyura zikitoka katika kinywa cha joka(shetani) pia ndani ya mnyama ,mpinga kristo pia ndani ya nabii wa uwongo.
-Hizi ndizo Roho za utatu mchafu wa shetani zilizokuwa zinafanya miujiza sasa zinakwenda kuwadanganya mataifa ili waje kupigana upande wa mpinga kristo ili uzuie Yesu kristo asije kutawala dunia.
-Nayo yanakusanyika yakiwa ni majeshi mengi sana mno kutoka mawio ya jua pia magharibi pia vikosi vya kasikazini pia mfalme wa kusini ambaye ni AFULIKA.Hivyo majeshi hayo yote yatakusanywa pamoja katika bonde la halmagedoni Maana yake bonde la kukata maneno au la Yoshafati.
v  YOELI 3:2
Kitasa Cha Saba
Babeli Kuhalibiwa.
 Ufunuo 16:17-21.
-Katika msitari huu wa kumi na saba tunaona kuwa kitasa kina mwanga juu ya anga kunakuwa na tetemeko kuu milima ina hama pia na Babeli unakumbukwa na kuhukumiwa.
-Maana ya hizi tetemeko na kuhama kwa milima na viziwa ni kurudi kwa Yesu kristo kutawala.Ebu linganisha na kufunguliwa kwa muhuri ya sita.
v  UFUNUO 6:12-17
-Yohana alimskia malaika akisema imekwisha kuwa,kudhibitisha kuwa ni mwisho wa jambo Fulani.Maana kipindi cha dhiki kuu kinaishia hapo,utawala wa mnyama unakoma ,kuteswa kwa watu kunakoma,pia shetani ananyanganywa ushawishi wake juu ya watu pamoja na nguvu zake
-Hivyo matokeo ya kumwagwa kwa kitasa cha 7 ni kuharibiwa kwa Babeli halisi ambayo tunaikuta sura ya 18.Pia miji mingine inaathiriwa na matetemeko makali sana pamoja na kuanguka kwa yale mawe makubwa ya barafu yenye uzito wa latili 114.
UBARIKIWE KWA SOMO HILI!.
NI MATUMAINI YANGU SOMO HILI LIMEKUONGEZEA KIWANGO CHA KUMJUA MUNGU.
Somo limeandaliwa na:-
                               Pastor.AMOS E.ONESMO-0756391498/0658727799

Maoni 1 :

  1. Mungu akubariki sana mtumishi wa kwa somo zuri sana

    JibuFuta