Jumapili, 11 Desemba 2022

MAISHA YA USHINDI DHIDI YA ADUI

 MWL: REV. AMOS

CONTACT: 0625313609

WHATSAPP: 0759199463

E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com


SOMO: *MAISHA YA USHINDI DHIDI YA MAADUI*

Maisha ya Ushindi yanahitaji kanuni za kiroho.

Zituatazo ni hatua kadhaa za kutufanya tuishi maisha ya Ushindi.

1. Usikubali kutenganishwa na MUNGU kwa namna yoyote

πŸ‘‰πŸ½Mawakala wa Giza wanafanya kazi ya kututenganisha na MUNGU

*Ayubu 19:25* 

[25]Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, 

Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.


2. Usitoe Siri zako kwa kila mtu

πŸ‘‰πŸ½Kitendo cha Samson kutoa Siri kwa Delila kilisababisha Samson atobolewe macho, aondolewe nguvu zake, awatumikie MAADUI zake wafilisti.

πŸ‘‰πŸ½ Jifunze kutotoa Siri zako usije ukawatumikia MAADUI zako


*WAAMUZI 16:16-18* 

[16]Ikawa, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa. 

[17]Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu. 

[18]Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao.


3. Usiruhusu Uoga na hofu vikaingia ndani yako

πŸ‘‰πŸ½ Hofu ni moja ya SILAHA ya Shetani kukushinda wewe kirahisi.


*ZABURI 56:4* 

[4]Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. 

Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; 

Mwenye mwili atanitenda nini?


4. Mtumaini MUNGU siku zote

πŸ‘‰πŸ½Ukitaka Ushinde Vita ya KIROHO hakikisha unamtumaini MUNGU siku zote


*Mithali 3:5-6* 

[5]Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, 

Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; 

[6]Katika njia zako zote mkiri yeye, 

Naye atayanyosha mapito yako.


5. Tumia mamlaka kumkabili Adui

a) Mamlaka ya jina la Yesu

*YOHANA 14:14* 

[14]Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.


b) Mamlaka ya DAMU ya YESU

*UFUNUO wa Yohana 12:11* 

[11]Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.


c) Mamlaka ya NENO LA MUNGU

*ZABURI 107:20* 

[20]Hulituma neno lake, huwaponya, 

Huwatoa katika maangamizo yao.


 *HITIMISHO* .

KILA SILAHA ITAKAYOINUKA HAITAFANIKIWA JUU YAKO

*ISAYA 54:17* 

[17]Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.


.............. Mwisho...........

Rev. Amos

0625313609

0759199463

Jumatano, 30 Novemba 2022

POKEA JAMBO JIPYA

 *MUNGU AKUTENDEE JAMBO JIPYA MWEZI DECEMBER* 

ISAYA 43:18-19

[18]Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. 


[19]Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.

Jumatatu, 28 Novemba 2022

NAFASI YA MWANAMKE KWA MWANAUME KIUCHUMI

 MWL. REV. AMOS FROM TABORA.

MAWASILIANO: +255759199463

+255625313609

E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com


SOMO:

 *NAFASI YA MWANAMKE KIUCHUMI KWA MMEWE*

➡️Mwanamke ana nafasi kubwa na ya muhimu kwa mmewe kiuchumi kama ifuatavyo:-


1. Kumwinua Mme anapoanguka kiuchumi

 *πŸ‘‰πŸ½MHUBIRI 4:9-10* 

[9]Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; 

Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. 


[10]Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!


2. KUMSHAURI Mme kuhusu mambo ya uchumi

 *πŸ‘‰πŸ½*MITHALI 31:26-28** 

[26]Hufumbua kinywa chake kwa hekima, 

Na sheria ya wema i katika ulimi wake. 


[27]Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; 

Wala hali chakula cha uvivu. 


[28]Wanawe huondoka na kumwita heri; 

Mumewe naye humsifu, na kusema,


3. Kumsaidia Mme mambo ya kiuchumi

πŸ‘‰πŸ½*MWANZO 2:18* 

[18]BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.


4. Mlinzi wa mapato ya Mme

πŸ‘‰πŸ½*YEREMIA 31:22* 

[22]Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana BWANA ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.


5. Mjenzi wa kipato cha Mme

 *πŸ‘‰πŸ½*MITHALI 14:1** 

[1]Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; 

Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.


6.. Kumtia moyo Mme katika mambo ya kiuchumi


*MITHALI 15:4* 

[4]Ulimi safi ni mti wa uzima; 

Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo.


*HITIMISHO* .

➡️Mwanamke wewe ni wa muhimu sana katika ujenzi wa uchumi wa mmeo na FAMILIA.


➡️Mwanaume usimdharau mkeo katika mambo ya kiuchumi.


_______Mwisho_____


Rev. Amos

Tabora

pasteronesmo@gmail.com

+255759199463

+255625313609

Jumatatu, 14 Novemba 2022

UMEFUNGWA NA MACHOZI YAKE

 ~~*MACHOZI YAO/YAKE YAMEKUFUNGA WEWE MWANAUME..!!!*~~ 

πŸ“Œ Kumbuka binti yule uliyemdanganya kwamba akilala na wewe utamuoa kisha akamwacha.

πŸ“Œ Kumbuka binti uliyemchumbia naye akajimimina kwako lakini ukamsaliti.

πŸ“Œ Kumbuka binti wa kazi uliyembaka.

πŸ“Œ Kumbuka binti yatima uliyemfanyia ukatili ukamwongezea machungu.

πŸ“Œ Kumbuka alivyokuamini akakutambulisha kwa marafiki zake, ndugu zake na wazazi wake ila ukamtenda.

πŸ“Œ Kumbuka binti yule aliyekupa vitu na zawadi nyingi akijua utamuoa ila baadaye ukamuoa rafiki yake

πŸ“Œ Kumbuka miaka aliyokaa akikusubiri umalize masomo ila baadaye ukamsaliti.

πŸ“Œ Aliwakataa wengi kwa ajili yako ila baadaye ukajifanya haumjui

πŸ“Œ Alivumilia mangapi kwa ajili yako?

πŸ“Œ Kumbuka uliyempa mimba baadaye ukamkataa. Analea mtoto peke yake. Ana maumivu kiasi gani?

Huyu binti akimlilia Mungu akasema usizae, *utazaa* ??


✳️Unadhani binti huyu anapomlilia MUNGU MACHOZI yake yanapita *BURE* ?

✳️ Machozi ya binti huyu, yamekufunga usifanikiwe.

✳️ Binti alilia Machozi mengi.

✳️ Binti huyu wakati analia kuna maneno alitamka ambayo ndiyo yamekukamata.


➡️ACHA MAHUSIANO YA UONGO UONGO IPO SIKU UTAJUTA.

➡️ Tengeneza na MUNGU


*Ufunuo wa Yohana 2:5* 

[5]Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; *ukatubu* , ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.


.......... Barikiwa.........

Rev. Amos

+255759199463

+255625313609

E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com

Jumamosi, 5 Novemba 2022

KIFUNGO KITOKANACHO NA NADHIRI

 MWL. REV. AMOS

MAWASILIANO: +255759199463

+255625313609

E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com


SOMO: *KIFUNGO KITOKANACHO NA NADHIRI* 


UTANGULIZI

Nadhiri ni ahadi inayotolewa kwa MUNGU.

*MHUBIRI 5:4-5* 

[4]Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri. 


[5]Ni afadhali usiweke nadhiri, 

Kuliko kuiweka usiiondoe.


Nadhiri ya mtu inaweza kuwa.

πŸ“Œ Nadhiri mbaya

πŸ“Œ Nadhiri nzuri


Nadhiri hufanyika kwa

πŸ“Œ Maneno

πŸ“Œ Mawazo


Kuna Nadhiri zimefanywa na watu ambazo zimegeuka mtego kwao.

Nadhiri hizo zimewafunga wasifanikiwe.

✳️ *Matendo ya Mitume 21:23* 

[23]Basi fanya neno hili tunalokuambia. Wako kwetu watu wanne waliofungwa na *nadhiri* .


✳️ *MITHALI 6:2* 

[2]Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, 

Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,


MIFANO YA NADHIRI

➡️ Nadhiri ya Yakobo

*MWANZO 28:18-21* 

[18]Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. 


[19]Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu. 


[20]Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; 


[21]nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu.


πŸ‘‰πŸ½Mungu aliitazama Nadhiri ya Yakobo

*MWANZO 31:13* 

[13]Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.


➡️ Nadhiri ya Hana

*1 Samweli 1:11,27-28* 

[11]Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe. 


[27]Naliomba nipewe mtoto huyu; BWANA akanipa dua yangu niliyomwomba; 


[28]kwa sababu hiyo mimi nami nimempa BWANA mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa BWANA. Naye akamwabudu BWANA huko.


NADHIRI INAMFUNGA MTU ASIPOITIMIZA.

*HESABU 30:1-2* 

[1]Kisha Musa akanena na wale vichwa vya kabila za wana wa Israeli, na kuwaambia, Neno hili ndilo aliloliagiza BWANA. 


[2]Mtu atakapomwekea BWANA nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa kifungo, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.



✳️ Ukiweka Nadhiri usiiondoe ni dhambi na inakufunga. Nadhiri haisamehewi.


*Kumbukumbu la Torati 23:21* 

[21]Utakapoweka nadhiri kwa BWANA, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako.


✳️ Nadhiri inaweza kuwa ni ya

πŸ“Œ Muda

πŸ“Œ Daima (Milele)


HITIMISHO.

Ondoa Nadhiri yako ili ufunguke 

πŸ“ŒKIMAISHA

πŸ“ŒKIUCHUMI

πŸ“ŒKIROHO



...............END............

Jumapili, 23 Oktoba 2022

MTUKUZE MUNGU KATIKATI YA TAABU ZAKO ATAONEKANA

MWL. REV. AMOS E. ONESMO
MAWASILIANO: +255759199463
+255625313609

SOMO: *MTUKUZE MUNGU KATIKATI YA TAABU ZAKO ATAONEKANA* .

➡️ Usitikisike, usijikatie tamaa wakati wa Taabu yako msaada wa MUNGU utatokea.

ZABURI 125:1
[1]Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, 
Ambao hautatikisika, wakaa milele.

➡️ Paul na Sila walimwona MUNGU Gerezani

MATENDO ya Mitume 16:25-26
[25]Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. 

[26]Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa. 

➡️ Katikati ya Moto Shadrack, Abdnego, Meshack walimwona MUNGU.

Danieli 3:15-25
[15]Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi na mikono yangu? 

[16]Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. 

[17]Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. 

[18]Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha. 

[19]Ndipo Nebukadreza akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuru mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto. 

[20]Kisha akawaamuru baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, na Meshaki, na Abednego, na kuwatupa katika ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto. 

[21]Basi watu hao wakafungwa, hali wamevaa suruali zao, na kanzu zao, na joho zao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto. 

[22]Basi kwa sababu amri ya mfalme ilikuwa ni kali, na ile tanuru ilikuwa ina moto sana, mwako wa ule moto ukawaua wale watu waliowashika Shadraka, na Meshaki, na Abednego. 

[23]Na watu hao watatu, Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakaanguka, hali wamefungwa, katikati ya ile tanuru iliyokuwa inawaka moto. 

[24]Ndipo Nebukadreza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme. 

[25]Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu.

➡️ Katikati ya Taabu Daniel alimwona MUNGU

Danieli 6:16
[16]Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.

✅ Endelea kumshukuru Mungu, usimwazie MUNGU kwa ujinga/Ubaya

*AYUBU 1:22* 
[22]Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu.

*****MWISHO****

MAELEZO ZAIDI
+255625313609
pasteronesmo@gmail.com

Ijumaa, 21 Oktoba 2022

KIFUNGO KITOKANACHO NA LAANA ZA WAZAZI

MWL. *REV. AMOS E. ONESMO* 

MAWASILIANO: +255759199463

+255625313609


E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com


SOMO: *KIFUNGO KITOKANACHO NA LAANA ZA WAZAZI*



πŸ‘‰πŸ½Laana ni uundaji wa maneno unaolenga kuleta MADHARA.


πŸ‘‰πŸ½ Biblia inaelekeza kuwatii WAZAZI.


*KUTOKA 20:12* 

[12]Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.


*WAEFESO 6:1* 

[1]Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.


πŸ‘‰πŸ½ *AINA ZA WAZAZI* 

a) Wazazi wa kiroho

b) Wazazi wa kimwili


πŸ‘‰πŸ½ Baraka ni nguvu hai ya kiungu iletayo mafanikio.


πŸ‘‰πŸ½ Kuna nguvu ya kukufanikisha (BARAKA) katika vinywa vya Wazazi wako.

πŸ‘‰πŸ½ Heshimu Wazazi upate BARAKA

πŸ‘‰πŸ½ Tengeneza mazingira Wazazi wakutamkie BARAKA na siyo LAANA kwani Laana itafunga mafanikio yako..

πŸ‘‰πŸ½ BARAKA za Wazazi zinatekwa


*MWANZO 27:1-4* 

[1]Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa. 


[2]Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu. 


[3]Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo; 


[4]ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa.


πŸ‘‰πŸ½ BARAKA za Isaka kwa Watoto wake


πŸ‘‰πŸ½ BARAKA za Labani kwa Watoto wake (Leah na Rahel)


*MWANZO 31:55* 

[55]Labani akaondoka asubuhi na mapema, akawabusu wanawe na binti zake, akawabariki; kisha Labani akaenda zake, akarudi kwao.


πŸ‘‰πŸ½Yusufu alimtunza Mzazi


*MWANZO 45:9-11* 

[9]Fanyeni haraka, mmwendee baba yangu, mkamwambie, Hivi ndivyo asemavyo mwanao Yusufu, Mungu ameniweka kuwa bwana katika Misri yote, basi unishukie, usikawie. 


[10]Nawe utakaa katika nchi ya Gosheni, utakuwa karibu nami, wewe, na wanao, na wana wa wanao, na wanyama wako, ng’ombe zako, na yote uliyo nayo. Nami nitakulisha huko; 


[11]maana bado imesalia miaka mitano ya njaa; usije ukaingia katika uhitaji, wewe, na nyumba yako, na yote uliyo nayo.


*MWANZO 47:11-12* 

[11]Yusufu akawakalisha babaye na nduguze, na kuwapa milki katika nchi ya Misri, katika mahali pazuri pa nchi, katika nchi ya Ramesesi, kama Farao alivyoamuru. 


[12]Naye Yusufu akawalisha babaye na nduguze na nyumba yote ya babaye, kwa kadiri ya hesabu ya watoto wao.


➡️ Mafanikio ya mtu yanaweza kufungwa na Laana za Wazazi wake wa kiroho au kimwili.

➡️ Fungua kifungo kinachokufanya uwasahau Wazazi.


### *BARIKIWA* ###


MAELEZO ZAIDI

+255759199463


E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com

Jumatano, 19 Oktoba 2022

KITI CHA ENZI CHA SHETANI

 MWL. REV. AMOS E. ONESMO

SIMU: +255759199463

+255625313609

E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com


SOMO: KITI CHA ENZI CHA SHETANI

Utangulizi

Kiti ni kifaa cha kukalia.

Kiroho kiti humaanisha utawala.

Ninapoongelea kiti cha enzi cha Shetani namaanisha utawala wa shetani.


UFUNUO WA YOHANA 2:13

[13]"Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani"


Kiti cha enzi cha Shetani kinaweza kujengwa:-

πŸ“Œ Nyumbani

πŸ“Œ Eneo la biashara

πŸ“Œ Shuleni na maeneo mengine


Pia, kiti cha enzi cha Shetani kinaweza kuwa ndani ya mtu kwa kuwa mtu ni NYUMBA/JENGO.


2WAKORINTHO 5:1-4

[1]"Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni. 


[2]Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni; 


[3]ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi. 


[4]Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima"


2 WAKORINTHO 6:16

[16]"Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu"


Mtu ni NYUMBA

MATHAYO 12:43-45

[43]"Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. 


[44]Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. 


[45]Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya"


Mwili ni NYUMBA

Mtu mwenye kiti cha Shetani ndani yake anaweza kutembea nacho ofisini, sokoni, Shuleni na kinaweza kuleta madhara makubwa Sana.


UFUNUO WA YOHANA 13:2

[2]"Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi"


Shetani anaweza kuweka kiti chake ndani ya mtu na akawa tegemeo la watu wengi.


MATENDO 16:16-19

[16]"Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. 


[17]Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu. 


[18]Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile. 


[19]Basi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji;"


πŸ‘‰πŸ½ Kama utagusa kiti cha enzi ambacho ni tegemeo la watu wengi jipange vizuri.

πŸ‘‰πŸ½ Kiti cha ENZI cha Shetani ndani ya mtu kinamtia nguvu mtu huyo kufanya mambo ya kipepo.


BOMOA KITI CHA ENZI CHA SHETANI KINACHOKUTESA. KILA KILIPOJENGWA KIANGUSHE KWANI NDIYO CHANZO CHA MATESO YAKO NA MATESO YA FAMILIA YAKO.


FUATANA NAMI KATIKA MAOMBI HAYA YA KUANGUSHA KITI CHA ENZI CHA SHETANI.


πŸ“Œ MaombiπŸ“Œ

Ewe Kiti cha ENZI cha Shetani nakukabiri na kuanzia sasa ninakukamata na kukuvunja kwa jina la Yesu. Ewe Kiti cha ENZI uliyewekwa ndani yangu, uliyewekwa katika eneo ninaloishi ninakubomoa kwa jina la Yesu.

#####AMEN#####


MAELEZO ZAIDI

+255625313609

Jumatatu, 17 Oktoba 2022

UMEAMBATANA NA NANI?

 MWL. REV. AMOS E. ONESMO

SIMU: +255759199463

+255625313609

E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com


SOMO: *UMEAMBATANA NA NANI?*

Utangulizi

AMBATANA ni neno linalomaanisha kushikamana, gandamana, fungamana.


Maendeleo ya mtu kiroho au kiuchumi hutegemea, ameambatana na nani?

Wanaotembea pamoja wamepatana.


Amosi 3:3

[3]Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?


Rafiki anaweza kukuvusha na anaweza kukupoteza.


MITHALI 27:17

[17]Chuma hunoa chuma; 

Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.


MITHALI 13:20

[ 20]Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; 

Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.


Ukitaka kufanikiwa na kuongezeka kiroho, ambatana na waliookoka.


2 Wakorintho 6:14-18

[14]Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 


[15]Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?

Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 


[16]Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 


[17]Kwa hiyo, 

Tokeni kati yao, 

Mkatengwe nao, asema Bwana, 

Msiguse kitu kilicho kichafu, 

Nami nitawakaribisha. 


[18]Nitakuwa Baba kwenu, 

Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, 

asema Bwana Mwenyezi.


Mpendwa katika mambo ya kiuchumi ambatana na mtu anayeona FURSA.

Mtu asiyeona FURSA hakufai


HESABU 13:27-33

[27]Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake. 


[28]Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni hodari, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko. 


[29]Amaleki anakaa katika nchi ya Negebu; na Mhiti, na Myebusi, na Mwamori wanakaa katika milima, na Mkanaani anakaa karibu na bahari; na kando ya ukingo wa Yordani. 


[30]Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka. 


[31]Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi. 


[32]Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno. 


[33]Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.



Marafiki wanaokuletea habari mbaya za kukukatisha tamaa hawatakufikisha katika mafanikio unayoyataka.

πŸ“Œ Ogopa kuambatana na Waoga.

πŸ“Œ Ogopa kuambatana na wasiothubutu.

πŸ“Œ Ogopa kuambatana na walalamikaji wa kila jambo.

πŸ“Œ Ogopa kuambatana na wanaojiona si kitu (Mapanzi).

πŸ“Œ Ogopa kuambatana na wasiojadili maendeleo.

πŸ“Œ Ogopa kuambatana na wanaoona mijitu badala ya Asali na maziwa.

πŸ“Œ Ogopa wanaoona matatizo tu


HITIMISHO.

Ambatana na watu wanaoyageuza matatizo kuwa FURSA


HESABU 14:6-9

[6]Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao; 


[7]wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu. 


[8]Ikiwa BWANA anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali. 


[9]Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye BWANA yu pamoja nasi; msiwaogope.


Kwa maelezo zaidi Tuwasiliane

+255759199463

+255625313609

Alhamisi, 13 Oktoba 2022

MAHUBIRI REDIONI

 Bwana YESU asifiwe.

Mimi Rev. Amos kutoka Tabora naomba ufadhili wa unachoguswa katika kuchangia vipindi vya MAHUBIRI REDIONI vinavyotaraji kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao (November).

Sadaka haina kiwango.

Naomba kila mwezi uwe unafanya jambo.

Ukiwa tayari nijuze nikuadd group maalumu ikiwezekana uweke Nadhiri.

Kwa mwezi malipo yatakuwa LAKI MOJA. Kila kipindi *nitahubiri dk15* 

Nikipata watu *20* wa kunishika mkono kwa kila mwezi nitaweza kulipia vipindi.

Kwa watu *20* kila mwezi kila mtu atanichangia *5,000* .


Kwa watu *10* kila mwezi kila mmoja atanichangia *10,000/=* 


Nitahubiri REDIO UHAI FM TABORA

NAOMBA UWE MMOJA WA WATAKAONIUNGA MKONO.


NAMBA YA HUDUMA

HALOPESA *0625313609* 

JINA: *AMOS ONESMO* 

Rev. Amos

TABORA

Jumatano, 12 Oktoba 2022

MTAZAMO

 MWL. REV. AMOS E. ONESMO

MAWASILIANO: +255759199462

+255625313609

E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com


SOMO: *MTAZAMO* 

Utangulizi

Mtazamo

1.Ni hali ya ndani ya mtu inayosema juu ya msimamo aliyonayo mtu juu ya jambo fulani au hali fulani.

2. Ni jinsi mtu anavyoyaona na kuyachukulia mambo

3. Ni Hali ya ndani ya mtu inayoamua msimamo wake.


*Mithali 23:7a* 

[7]Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.......


 *AINA ZA MITAZAMO* 

1. Mtazamo sahihi

2. Mtazamo usio sahihi


Mtazamo wa mtu juu ya MUNGU unatakiwa uwe sahihi.

Mtazamo humpelekea mtu:-

a) Kutenda jambo

b) Kuamua Jambo

c) Kushauri jambo kwa usahihi


Mtazamo usio sahihi huvuruga uhusiano wako na MUNGU.


*Ezekieli 38:10* 

[10]Bwana MUNGU asema hivi; Itakuwa katika siku hiyo, mawazo yataingia moyoni mwako, nawe utakusudia kusudi baya;


Shetani anatafuta njia ya kuvuruga mtazamo kati ya Mume na Mke na kusababisha Ndoa kuvurugika.


 *MTAZAMO USIO SAHIHI HUSABABISHA MADHARA YAFUATAYO* :-

1. Woga katika kumkabili Adui

2. Kupuuza vita kama vile haipo



Ulivyo katika mtazamo wako itaamua kiwango cha mamlaka na nguvu ambazo utakuwa unatembea nazo kukabiliana na nguvu za GIZA.


Badili mtazamo wako ili uzivunje kazi za Ibilisi.


*1 Yohana 3:8b* 

[8]...........Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.


*WAEBRANIA 2:14-15* 

[14]Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, 


[15]awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.


Mapepo hayana nguvu juu yetu


*WAKOLOSAI 2:15* 

[15]akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.


Uwe na mtazamo wa kushinda


 *Warumi 8:37* 

[37]Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.


*1 Yohana 4:4* 

[4]Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.


KUMBUKA:-

Mtazamo wako juu ya MUNGU utaamua kiwango cha MUNGU kuonekana kwako.



Maelezo zaidi

Rev. Amos

0625313609

Jumatatu, 10 Oktoba 2022

MAOMBI YA KUKOMBOA MALANGO YA TANZANIA

*MAOMBI MAALUMU* .
SIKU YA TAREHE *14/10/2022* TUTAKUWA NA MAOMBI MAALUMU YA KUKOMBOA MALANGO YA TANZANIA.

 *Itakuwa saa 12 Alfajiri hadi saa 12:30 Alfajiri* .
Kila mwanamaombi popote ulipo utaombwa kushiriki maombi hayo. Watakaoweza kusimama barabarani na mahali pengine hata kama ni chumbani kwako wewe shiriki maombi hayo na MUNGU atakubariki.

REV. AMOS
 *MKURUGENZI*

Jumamosi, 8 Oktoba 2022

MADHABAHU

 MWL: REV. AMOS E. ONESMO

+255759199463

+255625313609

SOMO: MADHABAHU

Ni eneo maalumu la kukutana na Mungu/mungu.

Kila madhabahu ina watu wanaoiabudu.


 *VINAVYOUNDA MADHABAHU* 

1. Mungu wa madhabahu.

Kila madhabahu ina Mungu wake

2. Kuhani wa madhabahu

Hawa ni wahudumu wa madhabahu. Waganga wa kienyeji na wachawi ni makuhani kwenye madhabahu za shetani. Ukiona kwenye ukoo wenu waganga wa kienyeji wanapishana pishana tambua katika ukoo wenu iko madhabahu ya shetani.

3. Nguvu ya madhabahu

Kila madhabahu ina nguvu yake ambayo ndiyo inayowashikilia watu wanaoiabudu madhabahu hiyo

4. Kafara ya madhabahu.

Sadaka ina imarisha madhabahu.

Kuna wengine katika familia zao walishatolewa kafara katika madhabahu za ukoo wao sawa sawa na andiko la 

Zaburi 106:35-37

[35]Bali walijichanganya na mataifa, 

Wakajifunza matendo yao. 


[36]Wakazitumikia sanamu zao, 

Nazo zikawa mtego kwao. 


[37]Naam, walitoa wana wao na binti zao 

Kuwa dhabihu kwa mashetani.


MADHABAHU ZINAZOTAWALA DUNIA.

1. Madhabahu ya Mungu

2. Madhabahu ya shetani


Gidioni alipewa jukumu la kuvunja madhabahu iliyojengwa na Baba yake.

WAAMUZI 6:23-31

[23]BWANA akamwambia Amani iwe pamoja nawe; usiogope; hutakufa. 


[24]Ndipo Gideoni akamjengea BWANA madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu

; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri. 


[25]Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Mtwae ng’ombe wa baba yako, yaani ng’ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe madhabahu ya Baali, aliyo nayo baba yako, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo; 


[26]ukamjengee BWANA, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng’ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata. 


[27]Ndipo Gideoni akatwaa watu kumi miongoni mwa watumishi wake, akafanya kama BWANA alivyomwambia; lakini ikawa kwa sababu aliwaogopa watu wa nyumba ya baba yake, na watu wa mji, hakuweza kuyatenda hayo wakati wa mchana, basi aliyatenda usiku. 

 

[28]Hata watu wa mji walipoondoka asubuhi na mapema, tazama, madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ng’ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu iliyojengwa. 


[29]Wakaambiana, Ni nani aliyetenda jambo hili? Hata walipotafuta habari na kuuliza, wakasema, Gideoni, mwana wa Yoashi, ndiye aliyetenda jambo hili. 


[30]Ndipo watu wa mji wakamwambia Yoashi Mlete mwanao, afe; kwa sababu ameibomoa madhabahu ya Baali na kwa sababu ameikata ile Ashera iliyokuwa karibu nayo. 


[31]Yoashi akawaambia watu wote waliokuwa wakishindana naye, Je! Mtamtetea Baali? Au mtamwokoa ninyi? Yeye atakayemtetea na auawe hivi asubuhi; kama yeye ni Mungu, na ajitetee nafsi yake, kwa sababu mtu mmoja ameibomoa madhabahu yake.


Tuna nafasi ya kujenga madhabahu inayohukumu kila aina ya wabaya kama madhabahu ya eliya iliyowahukumu kifo manabii 450 wa Baali.

IWAFALME 18:30-40

[30]Kisha Eliya akawaambia watu wote, Nikaribieni mimi. Watu wote wakamkaribia. Akaitengeneza madhabahu ya BWANA iliyovunjika. 


[31]Eliya akatwaa mawe kumi na mawili, kwa hesabu ya kabila za wana wa Yakobo, aliyejiliwa na neno la BWANA na kuambiwa, Jina lako litakuwa Israeli. 


[32]Naye akaijenga madhabahu kwa mawe hayo katika jina la BWANA; akafanya mfereji, kama wa vipimo viwili vya mbegu, ukiizunguka madhabahu. 


[33]Kisha akazipanga zile kuni, akamkata yule ng’ombe vipande vipande, akaviweka juu ya kuni. Akasema, Jazeni mapipa manne maji, mkayamwage juu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya kuni. 


[34]Akasema, Fanyeni mara ya pili. Wakafanya mara ya pili. Akasema, Fanyeni mara ya tatu. Wakafanya mara ya tatu. 


[35]Yale maji yakaizunguka madhabahu; akaujaza mfereji maji. 


[36]Ikawa, wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, Eliya nabii akakaribia, akasema, Ee BWANA, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimefanya mambo haya yote kwa neno lako. 


[37]Unisikie, Ee BWANA, unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, BWANA, ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza moyo wakurudie. 


[38]Ndipo moto wa BWANA ukashuka, ukaiteketeza sadaka ya kuteketezwa, na kuni, na mawe, na mavumbi, ukayaramba yale maji yaliyokuwamo katika mfereji. 


[39]Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, BWANA ndiye Mungu, BWANA ndiye Mungu. 


[40]Eliya akawaambia, Wakamateni hao manabii wa Baali, asiokoke hata mmoja. Wakawakamata; na Eliya akawachukua mpaka kijito cha Kishoni, akawaua huko.


KAZI YA MADHABAHU YA GIZA

1. Kupitisha vitu vya Giza kabla ya kudhihirika katika ulimwengu wa kawaida.

2. Kutengeneza vitu vya kishetani ili viwaletee madhara watu.

3. Mawakala wa shetani hujiimarisha, hupata nguvu za kipepo, kufanya vikao na kupanga mipango yao ya ki-pepo.

4. Ni makazi ya mawakala ya shetani (makuhani/Wahudumu)

5. Ni mahali ambapo shetani au ujumbe wa shetani hukutana na wanadamu wanaompenda ili lifanyike jambo la kishetani.

6. Ni mahali ambapo shetani huabudiwa.

7. Ni mahali pa kutolea kafara za kipepo au kufanyia kafara za ki-pepo


KIPI KIFANYIKE JUU YA MADHABAHU ZA GIZA 


Kumbukumbu la Torati 7:5

[5]Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga.


1. Vunja Madhabahu za Giza kwa MAOMBI ya vita kwa kutumia DAMU YA YESU.


Ufunuo wa Yohana 12:11

[11]Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.


2. Bomoa nguzo zilizobeba madhabahu za GIZA

3. Kata Maashera ya hiyo madhabahu

4. Teketeza kwa moto sanamu zote

Kumbukumbu la Torati 12:2-3

[2]Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi; 


[3]nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo.


5. Vunja na kupaharibu mahali walikoziweka madhabahu za kishetani

6. Futa jina lao mahali hapo au mawakala wa shetani wenye madhabahu hizo


KWA MSAADA ZAIDI TUWASILIANE

+255759199463

+255625313609


E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com

Ijumaa, 7 Oktoba 2022

ITAMBUE HUDUMA YA WANAMAOMBI TANZANIA

 *WANAMAOMBI TANZANIA* .

Ni huduma inayowaunganisha wanamaombi wenye mzigo wa kuliombea TAIFA letu la Tanzania.

Mimi Rev.  Amos E. Onesmo kutoka Tabora kwa neema ya Mungu Huduma hii niliianzisha  *11/08/2018* baada ya MUNGU kunipa maono ya kuanzisha chombo kitakachowaleta pamoja wanamaombi wenye mzigo wa kuliombea TAIFA letu Tanzania.


 *DIRA YA HUDUMA YA WANAMAOMBI TANZANIA* .

Ni Tanzania ipone kwa maombi sawa sawa na andiko la *2 MAMBO YA NYAKATI 7:14* .

Kupitia andiko hilo kauli mbiu (motto) ni _"Tanzania bila maombi inaangamia_ "



 *DHIMA YA HUDUMA YA WANAMAOMBI TANZANIA* 

Ni kuwaleta wanamaombi wote pamoja ili kuliombea TAIFA letu kwa pamoja.

Mifumo ya maombi ni:-


1. Maombi ya mnyororo

2. Maombi kwa njia ya makongamano


 *MIPANGO MIKAKATI YA HUDUMA YA WANAMAOMBI TANZANIA* 

1. Kutoa Elimu ihusuyo huduma hii mikoa yote Tanzania bara na visiwani

2. Kutangaza huduma hii kwa upana ili wanamaombi wengi wajitokeze kuliombea TAIFA

3. Kuhamasisha Amani na Upendo TANZANIA

4. Kuwaleta watanzania pamoja bila kubaguana kwa misingi ya Dini zao, ukabila, Siasa na tofauti zingine

5. Kuomba bila kuchoka kwa kuliombea TAIFA


*MAFANIKIO YA HUDUMA* 

Mungu ametufanikisha kama ifuatavyo:-

1. Tumefanikiwa kufanya makongamano matatu ya kitaifa ya kuliombea TAIFA letu Tanzania.

Kongamano la kwanza mkoani Tabora 2019

Kongamano la pili jijini dodoma 2020

Kongamano la tatu mkoani Singida 2021


2. Tumefanikiwa kufika mikoa zaidi ya 15 Tanzania bara na mikoa yote ya Tanzania visiwani (Zanzibar)


3. Tumefanikiwa kuwaleta wanamaombi Pamoja


4. Tumefanikiwa kuwa na maombi mara moja kwa mwezi kimkoa


5. Tumefanikiwa kwa sehemu kufanya ziara za kutoa Elimu kwa baadhi ya mikoa Tanzania


 *MATARAJIO YA HUDUMA YA WANAMAOMBI TANZANIA* 

Tunatarajia yafuatayo:-

1. Huduma kupanuka nchi nzima na kuwafikia wanamaombi wengi wenye mzigo wa kuliombea TAIFA.


2. Kuendelea kuiona Amani ya Tanzania kwa maombi yetu


3. Kuendelea kuungwa mkono na umoja wa makanisa Tanzania.


4. Kuona uchumi wa Taifa letu Tanzania ukiimarika.


5. Taifa limjue MUNGU


 *MAPENDEKEZO YA HUDUMA YA WANAMAOMBI TANZANIA* 

Yafuatayo ni mapendekezo:-

1. Kuunganisha nguvu ya maombi ya kuliombea TAIFA bila kubaguana kwa misingi ya Dini, kabila na hata siasa kwani Tanzania ni mali yetu sote.


2. Watanzania wote tuhubiri Amani nchini Tanzania, tukemee viashiria vyote vinavyohatarisha Amani ya Tanzania


3. Tufanye maombi ya Toba ya Taifa mara kwa Mara ili MUNGU alirehemu Taifa


4. Tuimarishe misingi ya Amani, Upendo na umoja kama tulivyofundishwa na waasisi wa TAIFA letu Tanzania


 *CHANGAMOTO ZA HUDUMA YA WANAMAOMBI* .

Huduma hii toka tumeanza ziko changamoto nyingi. Zifuatazo ni baadhi ya changamoto hizo:-

1. Gharama za kuendesha huduma hii ni changamoto kubwa kwani Tanzania ni kubwa Jambo linalopelekea ugumu kufanya ziara za kutoa Elimu. Pia, makongamano yana gharimu Sana.


2. Mitazamo tofauti ya baadhi ya watumishi wakidhani ni Dini mpya imeanza jambo linalopelekea kuwa na hofu ndani yao.


3. Kuungwa mkono na wanamaombi wachache ukilinganisha na idadi ya watanzania.

4.  Kukosa ofisi za huduma hii makao MAKUU ya nchi jijini dodoma.


5. Kukosa vyombo vya mziki vya kutumia katika makongamano yetu ya maombi


 *UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA HUDUMA YA WANAMAOMBI* TANZANIA

1. Kupata wadau wa kuchangia gharama za kuendesha huduma hii ya Wanamaombi Tanzania


2. Elimu ihusuyo huduma ya Wanamaombi Tanzania kuwafikia watu wengi kupitia Vyombo mbali mbali vya habari na taasisi mbali mbali za Ki-Dini


3. Kupata wadau wa kutusaidia kupata ofisi jijini dodoma


 *MAONI/WITO KWA JAMII/WADAU/UMMA* .

Mimi Rev. Amos E. Onesmo mkurugenzi na muasisi wa huduma hii ya Wanamaombi Tanzania natoa wito huu kwa jamii

1. Kuliombea TAIFA letu Tanzania ni muhimu sana kwani lolote linaloonekana kwa macho limeamliwa na ulimwengu wa roho. Maombi ni silaha ya kupigana na ADUI katika ulimwengu wa roho ili asiridhuru TAIFA letu la Tanzania. Hivyo, wanamaombi wote Tanzania, watanzania wote bila kujali tofauti zetu imetupasa kuliombea TAIFA kwa nguvu zetu.


2. Pia, jamii yote ya Tanzania ninawakaribisha kuungana nasi katika kubeba gharama za kuendesha huduma hii ya Wanamaombi Tanzania kwani Tanzania ni yetu sote.


 *TUMKUMBUKE MUASISI WA TAIFA LETU TANZANIA* .

Hayati Mwl. J.k Nyerere muasisi wa TAIFA letu la Tanzania naye alituasa kuwa wamoja bila kubaguana.

Mwl. J.k Nyerere Baba wa Taifa, alisimama kwa moyo wa uzalendo kulitetea TAIFA letu Tanzania. Alipigania Taifa lake ili kuhakikisha watanzania tunakuwa huru. Alifanikiwa kutuunganisha watanzania bila kujali tofauti zetu.

Mchango wa Mwl. J.k Nyerere kwa TAIFA la Tanzania hauwezi kusahaulika utatukuzwa. Watanzania tuna jambo la kujifunza kwa Baba wa TAIFA yaani moyo wa uzalendo kwa TAIFA letu. Tuoneshe moyo wa uzalendo kwa

1. Kuliombea TAIFA

2. Kudumisha Amani, Upendo na Umoja Tanzania

3. Kulinda na kutunza rasilimali za Taifa.


MUNGU ibariki Afrika, MUNGU ibariki Tanzania


Nawasilisha

Ni mimi

Rev. Amos E. Onesmo

Tabora

Mkurugenzi Taifa huduma ya Wanamaombi Tanzania

+255759199463

+255625313609

E-mail: pasteronesmo@gmail.com

KONGAMANO LA MAOMBI LA KITAIFA 2022

 Mkurugenzi Taifa wa huduma ya wanamaombi Tanzania anawakaribisha wanamaombi wote katika KONGAMANO la kitaifa la maombi mkoani SINGIDA. Ni kongamano la kuliombea Taifa la TANZANIA

Ni TAREHE 13-16 December 2022 SINGIDA mjini.

Kujisajili: Tuma jina na mkoa kwenda namba 0625313609


 *Hakuna Ada*

UKOMBOZI WA KIBALI CHAKO

 MWL: REV. AMOS E. ONESMO

MAWASILIANO:

 0759199463

 0625313609

SOMO *: UKOMBOZI WA KIBALI* 

Utangulizi

Kibali ni kukubaliwa katika jambo fulani.

Kibali kinampa mtu kutenda anavyotaka.


1 Samweli 2:26

"Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa BWANA, na kwa watu pia"


Shetani akikuibia kibali chako huwezi kukubalika kwa lolote unalolifanya.

Kibali ni ruhusa inayovisukuma nje vizuizi vyote katika maisha ya mtu.

Kibali kina nguvu Sana Sana katika maisha ya mtu.

Ukishindana na mwenye kibali unajisumbua.


KITABU CHA ESTA 2:17

"Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti"


Kilichompa kukubalika ESTA ni kibali na si kwa sababu alikuwa bikra kwani bikra walikuwa wengi na si kwa sababu alikuwa mzuri wa uso kwani wazuri walikuwepo. Kilichomstahilisha Esta ni KIBALI.


KAZI YA KIBALI

1. Kibali kinamfanya mtu, watu wamkubali

2. Kibali kinawafanya watu wakuheshimu

3. Kibali kinawafanya watu wakufuate katika unayoyasema na kuyafanya.

4. Kibali kinakutengeneza ufae hata kama ulikuwa haufai

5. Kibali kinawafanya watu wakupende


Omba MUNGU akupe kibali


Zaburi 106:4

"Ee BWANA, unikumbuke mimi, 

Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako. 

Unijilie kwa wokovu wako"


MITHALI 3:3-4

"[3]Rehema na kweli zisifarakane nawe; 

Zifunge shingoni mwako; 

Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. 


[4]Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, 

Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu"


ZABURI 19:14

"Maneno ya kinywa changu, 

Na mawazo ya moyo wangu, 

Yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, 

Mwamba wangu, na mwokozi wangu"


DALILI ZA MTU ALIYEIBIWA KIBALI


1. Hafanikiwi hata kama ana sifa zote za kufanikiwa

2. Kukataliwa bila sababu, kuonewa na kupuuzwa bila sababu.

3. Kutumia NGUVU sana hata pale ambapo asingetumia nguvu nyingi.



HITIMISHO.

Komboa kibali chako kwa maombi kama mawakala wa shetani wamekiharibu.


Mafanikio yako hutegemea kibali chako


KWA MSAADA ZAIDI TUWASILIANE

+255759199463

+255625313609


E-MAIL

pasteronesmo@gmail.com

Jumatatu, 30 Mei 2022

NGUVU YA DAMU YA YESU

SOMO.

IJUE NGUVU YA DAMU YA YESU

1.  Husafisha dhambi

IYOH 1:7, UFUN 1:5


2. Inatutakasa

WAEB 10:19


3. Inatupa uzima

YOHANA 6:53


4. Inatusogeza Karibu na MUNGU

WAEFESO 2:13


5. Inatupa uhakika wa kupaingia patakatifu

WAEBRANIA 10:19


6. Inanena mema

WAEBRANIA 12:24


7. Inatuongezea Neema ya Amani

IPETRO 1:2


8. Inatulinda na kutushindia Vita

UFUNUO 12:11