MWL. REV. AMOS E. ONESMO
SIMU: +255759199463
+255625313609
E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com
SOMO: KITI CHA ENZI CHA SHETANI
Utangulizi
Kiti ni kifaa cha kukalia.
Kiroho kiti humaanisha utawala.
Ninapoongelea kiti cha enzi cha Shetani namaanisha utawala wa shetani.
UFUNUO WA YOHANA 2:13
[13]"Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani"
Kiti cha enzi cha Shetani kinaweza kujengwa:-
📌 Nyumbani
📌 Eneo la biashara
📌 Shuleni na maeneo mengine
Pia, kiti cha enzi cha Shetani kinaweza kuwa ndani ya mtu kwa kuwa mtu ni NYUMBA/JENGO.
2WAKORINTHO 5:1-4
[1]"Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.
[2]Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni;
[3]ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi.
[4]Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima"
2 WAKORINTHO 6:16
[16]"Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu"
Mtu ni NYUMBA
MATHAYO 12:43-45
[43]"Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate.
[44]Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.
[45]Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya"
Mwili ni NYUMBA
Mtu mwenye kiti cha Shetani ndani yake anaweza kutembea nacho ofisini, sokoni, Shuleni na kinaweza kuleta madhara makubwa Sana.
UFUNUO WA YOHANA 13:2
[2]"Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi"
Shetani anaweza kuweka kiti chake ndani ya mtu na akawa tegemeo la watu wengi.
MATENDO 16:16-19
[16]"Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua.
[17]Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu.
[18]Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.
[19]Basi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji;"
👉🏽 Kama utagusa kiti cha enzi ambacho ni tegemeo la watu wengi jipange vizuri.
👉🏽 Kiti cha ENZI cha Shetani ndani ya mtu kinamtia nguvu mtu huyo kufanya mambo ya kipepo.
BOMOA KITI CHA ENZI CHA SHETANI KINACHOKUTESA. KILA KILIPOJENGWA KIANGUSHE KWANI NDIYO CHANZO CHA MATESO YAKO NA MATESO YA FAMILIA YAKO.
FUATANA NAMI KATIKA MAOMBI HAYA YA KUANGUSHA KITI CHA ENZI CHA SHETANI.
📌 Maombi📌
Ewe Kiti cha ENZI cha Shetani nakukabiri na kuanzia sasa ninakukamata na kukuvunja kwa jina la Yesu. Ewe Kiti cha ENZI uliyewekwa ndani yangu, uliyewekwa katika eneo ninaloishi ninakubomoa kwa jina la Yesu.
#####AMEN#####
MAELEZO ZAIDI
+255625313609
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni