*WANAMAOMBI TANZANIA* .
Ni huduma inayowaunganisha wanamaombi wenye mzigo wa kuliombea TAIFA letu la Tanzania.
Mimi Rev. Amos E. Onesmo kutoka Tabora kwa neema ya Mungu Huduma hii niliianzisha *11/08/2018* baada ya MUNGU kunipa maono ya kuanzisha chombo kitakachowaleta pamoja wanamaombi wenye mzigo wa kuliombea TAIFA letu Tanzania.
*DIRA YA HUDUMA YA WANAMAOMBI TANZANIA* .
Ni Tanzania ipone kwa maombi sawa sawa na andiko la *2 MAMBO YA NYAKATI 7:14* .
Kupitia andiko hilo kauli mbiu (motto) ni _"Tanzania bila maombi inaangamia_ "
*DHIMA YA HUDUMA YA WANAMAOMBI TANZANIA*
Ni kuwaleta wanamaombi wote pamoja ili kuliombea TAIFA letu kwa pamoja.
Mifumo ya maombi ni:-
1. Maombi ya mnyororo
2. Maombi kwa njia ya makongamano
*MIPANGO MIKAKATI YA HUDUMA YA WANAMAOMBI TANZANIA*
1. Kutoa Elimu ihusuyo huduma hii mikoa yote Tanzania bara na visiwani
2. Kutangaza huduma hii kwa upana ili wanamaombi wengi wajitokeze kuliombea TAIFA
3. Kuhamasisha Amani na Upendo TANZANIA
4. Kuwaleta watanzania pamoja bila kubaguana kwa misingi ya Dini zao, ukabila, Siasa na tofauti zingine
5. Kuomba bila kuchoka kwa kuliombea TAIFA
*MAFANIKIO YA HUDUMA*
Mungu ametufanikisha kama ifuatavyo:-
1. Tumefanikiwa kufanya makongamano matatu ya kitaifa ya kuliombea TAIFA letu Tanzania.
Kongamano la kwanza mkoani Tabora 2019
Kongamano la pili jijini dodoma 2020
Kongamano la tatu mkoani Singida 2021
2. Tumefanikiwa kufika mikoa zaidi ya 15 Tanzania bara na mikoa yote ya Tanzania visiwani (Zanzibar)
3. Tumefanikiwa kuwaleta wanamaombi Pamoja
4. Tumefanikiwa kuwa na maombi mara moja kwa mwezi kimkoa
5. Tumefanikiwa kwa sehemu kufanya ziara za kutoa Elimu kwa baadhi ya mikoa Tanzania
*MATARAJIO YA HUDUMA YA WANAMAOMBI TANZANIA*
Tunatarajia yafuatayo:-
1. Huduma kupanuka nchi nzima na kuwafikia wanamaombi wengi wenye mzigo wa kuliombea TAIFA.
2. Kuendelea kuiona Amani ya Tanzania kwa maombi yetu
3. Kuendelea kuungwa mkono na umoja wa makanisa Tanzania.
4. Kuona uchumi wa Taifa letu Tanzania ukiimarika.
5. Taifa limjue MUNGU
*MAPENDEKEZO YA HUDUMA YA WANAMAOMBI TANZANIA*
Yafuatayo ni mapendekezo:-
1. Kuunganisha nguvu ya maombi ya kuliombea TAIFA bila kubaguana kwa misingi ya Dini, kabila na hata siasa kwani Tanzania ni mali yetu sote.
2. Watanzania wote tuhubiri Amani nchini Tanzania, tukemee viashiria vyote vinavyohatarisha Amani ya Tanzania
3. Tufanye maombi ya Toba ya Taifa mara kwa Mara ili MUNGU alirehemu Taifa
4. Tuimarishe misingi ya Amani, Upendo na umoja kama tulivyofundishwa na waasisi wa TAIFA letu Tanzania
*CHANGAMOTO ZA HUDUMA YA WANAMAOMBI* .
Huduma hii toka tumeanza ziko changamoto nyingi. Zifuatazo ni baadhi ya changamoto hizo:-
1. Gharama za kuendesha huduma hii ni changamoto kubwa kwani Tanzania ni kubwa Jambo linalopelekea ugumu kufanya ziara za kutoa Elimu. Pia, makongamano yana gharimu Sana.
2. Mitazamo tofauti ya baadhi ya watumishi wakidhani ni Dini mpya imeanza jambo linalopelekea kuwa na hofu ndani yao.
3. Kuungwa mkono na wanamaombi wachache ukilinganisha na idadi ya watanzania.
4. Kukosa ofisi za huduma hii makao MAKUU ya nchi jijini dodoma.
5. Kukosa vyombo vya mziki vya kutumia katika makongamano yetu ya maombi
*UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA HUDUMA YA WANAMAOMBI* TANZANIA
1. Kupata wadau wa kuchangia gharama za kuendesha huduma hii ya Wanamaombi Tanzania
2. Elimu ihusuyo huduma ya Wanamaombi Tanzania kuwafikia watu wengi kupitia Vyombo mbali mbali vya habari na taasisi mbali mbali za Ki-Dini
3. Kupata wadau wa kutusaidia kupata ofisi jijini dodoma
*MAONI/WITO KWA JAMII/WADAU/UMMA* .
Mimi Rev. Amos E. Onesmo mkurugenzi na muasisi wa huduma hii ya Wanamaombi Tanzania natoa wito huu kwa jamii
1. Kuliombea TAIFA letu Tanzania ni muhimu sana kwani lolote linaloonekana kwa macho limeamliwa na ulimwengu wa roho. Maombi ni silaha ya kupigana na ADUI katika ulimwengu wa roho ili asiridhuru TAIFA letu la Tanzania. Hivyo, wanamaombi wote Tanzania, watanzania wote bila kujali tofauti zetu imetupasa kuliombea TAIFA kwa nguvu zetu.
2. Pia, jamii yote ya Tanzania ninawakaribisha kuungana nasi katika kubeba gharama za kuendesha huduma hii ya Wanamaombi Tanzania kwani Tanzania ni yetu sote.
*TUMKUMBUKE MUASISI WA TAIFA LETU TANZANIA* .
Hayati Mwl. J.k Nyerere muasisi wa TAIFA letu la Tanzania naye alituasa kuwa wamoja bila kubaguana.
Mwl. J.k Nyerere Baba wa Taifa, alisimama kwa moyo wa uzalendo kulitetea TAIFA letu Tanzania. Alipigania Taifa lake ili kuhakikisha watanzania tunakuwa huru. Alifanikiwa kutuunganisha watanzania bila kujali tofauti zetu.
Mchango wa Mwl. J.k Nyerere kwa TAIFA la Tanzania hauwezi kusahaulika utatukuzwa. Watanzania tuna jambo la kujifunza kwa Baba wa TAIFA yaani moyo wa uzalendo kwa TAIFA letu. Tuoneshe moyo wa uzalendo kwa
1. Kuliombea TAIFA
2. Kudumisha Amani, Upendo na Umoja Tanzania
3. Kulinda na kutunza rasilimali za Taifa.
MUNGU ibariki Afrika, MUNGU ibariki Tanzania
Nawasilisha
Ni mimi
Rev. Amos E. Onesmo
Tabora
Mkurugenzi Taifa huduma ya Wanamaombi Tanzania
+255759199463
+255625313609
E-mail: pasteronesmo@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni