Jumatano, 12 Oktoba 2022

MTAZAMO

 MWL. REV. AMOS E. ONESMO

MAWASILIANO: +255759199462

+255625313609

E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com


SOMO: *MTAZAMO* 

Utangulizi

Mtazamo

1.Ni hali ya ndani ya mtu inayosema juu ya msimamo aliyonayo mtu juu ya jambo fulani au hali fulani.

2. Ni jinsi mtu anavyoyaona na kuyachukulia mambo

3. Ni Hali ya ndani ya mtu inayoamua msimamo wake.


*Mithali 23:7a* 

[7]Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.......


 *AINA ZA MITAZAMO* 

1. Mtazamo sahihi

2. Mtazamo usio sahihi


Mtazamo wa mtu juu ya MUNGU unatakiwa uwe sahihi.

Mtazamo humpelekea mtu:-

a) Kutenda jambo

b) Kuamua Jambo

c) Kushauri jambo kwa usahihi


Mtazamo usio sahihi huvuruga uhusiano wako na MUNGU.


*Ezekieli 38:10* 

[10]Bwana MUNGU asema hivi; Itakuwa katika siku hiyo, mawazo yataingia moyoni mwako, nawe utakusudia kusudi baya;


Shetani anatafuta njia ya kuvuruga mtazamo kati ya Mume na Mke na kusababisha Ndoa kuvurugika.


 *MTAZAMO USIO SAHIHI HUSABABISHA MADHARA YAFUATAYO* :-

1. Woga katika kumkabili Adui

2. Kupuuza vita kama vile haipo



Ulivyo katika mtazamo wako itaamua kiwango cha mamlaka na nguvu ambazo utakuwa unatembea nazo kukabiliana na nguvu za GIZA.


Badili mtazamo wako ili uzivunje kazi za Ibilisi.


*1 Yohana 3:8b* 

[8]...........Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.


*WAEBRANIA 2:14-15* 

[14]Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, 


[15]awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.


Mapepo hayana nguvu juu yetu


*WAKOLOSAI 2:15* 

[15]akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.


Uwe na mtazamo wa kushinda


 *Warumi 8:37* 

[37]Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.


*1 Yohana 4:4* 

[4]Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.


KUMBUKA:-

Mtazamo wako juu ya MUNGU utaamua kiwango cha MUNGU kuonekana kwako.



Maelezo zaidi

Rev. Amos

0625313609

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni