MWL. REV. AMOS E. ONESMO
SIMU: +255759199463
+255625313609
E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com
SOMO: *UMEAMBATANA NA NANI?*
Utangulizi
AMBATANA ni neno linalomaanisha kushikamana, gandamana, fungamana.
Maendeleo ya mtu kiroho au kiuchumi hutegemea, ameambatana na nani?
Wanaotembea pamoja wamepatana.
Amosi 3:3
[3]Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?
Rafiki anaweza kukuvusha na anaweza kukupoteza.
MITHALI 27:17
[17]Chuma hunoa chuma;
Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.
MITHALI 13:20
[ 20]Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima;
Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.
Ukitaka kufanikiwa na kuongezeka kiroho, ambatana na waliookoka.
2 Wakorintho 6:14-18
[14]Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
[15]Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?
Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?
[16]Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
[17]Kwa hiyo,
Tokeni kati yao,
Mkatengwe nao, asema Bwana,
Msiguse kitu kilicho kichafu,
Nami nitawakaribisha.
[18]Nitakuwa Baba kwenu,
Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,
asema Bwana Mwenyezi.
Mpendwa katika mambo ya kiuchumi ambatana na mtu anayeona FURSA.
Mtu asiyeona FURSA hakufai
HESABU 13:27-33
[27]Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake.
[28]Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni hodari, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko.
[29]Amaleki anakaa katika nchi ya Negebu; na Mhiti, na Myebusi, na Mwamori wanakaa katika milima, na Mkanaani anakaa karibu na bahari; na kando ya ukingo wa Yordani.
[30]Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka.
[31]Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi.
[32]Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.
[33]Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.
Marafiki wanaokuletea habari mbaya za kukukatisha tamaa hawatakufikisha katika mafanikio unayoyataka.
📌 Ogopa kuambatana na Waoga.
📌 Ogopa kuambatana na wasiothubutu.
📌 Ogopa kuambatana na walalamikaji wa kila jambo.
📌 Ogopa kuambatana na wanaojiona si kitu (Mapanzi).
📌 Ogopa kuambatana na wasiojadili maendeleo.
📌 Ogopa kuambatana na wanaoona mijitu badala ya Asali na maziwa.
📌 Ogopa wanaoona matatizo tu
HITIMISHO.
Ambatana na watu wanaoyageuza matatizo kuwa FURSA
HESABU 14:6-9
[6]Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao;
[7]wakanena na mkutano wote wa wana wa Israeli wakasema, Nchi ile tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi njema mno ya ajabu.
[8]Ikiwa BWANA anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii atupe iwe yetu, nayo ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali.
[9]Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye BWANA yu pamoja nasi; msiwaogope.
Kwa maelezo zaidi Tuwasiliane
+255759199463
+255625313609
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni