Jumatatu, 14 Novemba 2022

UMEFUNGWA NA MACHOZI YAKE

 ~~*MACHOZI YAO/YAKE YAMEKUFUNGA WEWE MWANAUME..!!!*~~ 

📌 Kumbuka binti yule uliyemdanganya kwamba akilala na wewe utamuoa kisha akamwacha.

📌 Kumbuka binti uliyemchumbia naye akajimimina kwako lakini ukamsaliti.

📌 Kumbuka binti wa kazi uliyembaka.

📌 Kumbuka binti yatima uliyemfanyia ukatili ukamwongezea machungu.

📌 Kumbuka alivyokuamini akakutambulisha kwa marafiki zake, ndugu zake na wazazi wake ila ukamtenda.

📌 Kumbuka binti yule aliyekupa vitu na zawadi nyingi akijua utamuoa ila baadaye ukamuoa rafiki yake

📌 Kumbuka miaka aliyokaa akikusubiri umalize masomo ila baadaye ukamsaliti.

📌 Aliwakataa wengi kwa ajili yako ila baadaye ukajifanya haumjui

📌 Alivumilia mangapi kwa ajili yako?

📌 Kumbuka uliyempa mimba baadaye ukamkataa. Analea mtoto peke yake. Ana maumivu kiasi gani?

Huyu binti akimlilia Mungu akasema usizae, *utazaa* ??


✳️Unadhani binti huyu anapomlilia MUNGU MACHOZI yake yanapita *BURE* ?

✳️ Machozi ya binti huyu, yamekufunga usifanikiwe.

✳️ Binti alilia Machozi mengi.

✳️ Binti huyu wakati analia kuna maneno alitamka ambayo ndiyo yamekukamata.


➡️ACHA MAHUSIANO YA UONGO UONGO IPO SIKU UTAJUTA.

➡️ Tengeneza na MUNGU


*Ufunuo wa Yohana 2:5* 

[5]Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; *ukatubu* , ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.


.......... Barikiwa.........

Rev. Amos

+255759199463

+255625313609

E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni