MWL: REV. AMOS E. ONESMO
MAWASILIANO:
0759199463
0625313609
SOMO *: UKOMBOZI WA KIBALI*
Utangulizi
Kibali ni kukubaliwa katika jambo fulani.
Kibali kinampa mtu kutenda anavyotaka.
1 Samweli 2:26
"Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa BWANA, na kwa watu pia"
Shetani akikuibia kibali chako huwezi kukubalika kwa lolote unalolifanya.
Kibali ni ruhusa inayovisukuma nje vizuizi vyote katika maisha ya mtu.
Kibali kina nguvu Sana Sana katika maisha ya mtu.
Ukishindana na mwenye kibali unajisumbua.
KITABU CHA ESTA 2:17
"Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti"
Kilichompa kukubalika ESTA ni kibali na si kwa sababu alikuwa bikra kwani bikra walikuwa wengi na si kwa sababu alikuwa mzuri wa uso kwani wazuri walikuwepo. Kilichomstahilisha Esta ni KIBALI.
KAZI YA KIBALI
1. Kibali kinamfanya mtu, watu wamkubali
2. Kibali kinawafanya watu wakuheshimu
3. Kibali kinawafanya watu wakufuate katika unayoyasema na kuyafanya.
4. Kibali kinakutengeneza ufae hata kama ulikuwa haufai
5. Kibali kinawafanya watu wakupende
Omba MUNGU akupe kibali
Zaburi 106:4
"Ee BWANA, unikumbuke mimi,
Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako.
Unijilie kwa wokovu wako"
MITHALI 3:3-4
"[3]Rehema na kweli zisifarakane nawe;
Zifunge shingoni mwako;
Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
[4]Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri,
Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu"
ZABURI 19:14
"Maneno ya kinywa changu,
Na mawazo ya moyo wangu,
Yapate kibali mbele zako, Ee BWANA,
Mwamba wangu, na mwokozi wangu"
DALILI ZA MTU ALIYEIBIWA KIBALI
1. Hafanikiwi hata kama ana sifa zote za kufanikiwa
2. Kukataliwa bila sababu, kuonewa na kupuuzwa bila sababu.
3. Kutumia NGUVU sana hata pale ambapo asingetumia nguvu nyingi.
HITIMISHO.
Komboa kibali chako kwa maombi kama mawakala wa shetani wamekiharibu.
Mafanikio yako hutegemea kibali chako
KWA MSAADA ZAIDI TUWASILIANE
+255759199463
+255625313609
pasteronesmo@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni