Ndoto
ni njia mojawapo ambayo Mungu husema,na kuwaelekeza watoto wake waleo.
YOWELI
2:28-29
Shetani
pia huzungumza,hushambulia na kuwamiliki watu kupitia ndoto.Maombi yenye nguvu yanaweza
kukuwezesha kuyashinda mashsmbulizi kama hayo ya ndoto.Jifunze kushughulika na
ndoto ili kupambana na ndoto za vitisho na za uongo za shetani.
ZEKARIA
10:2
AINA
ZA NDOTO.
i)Ndoto
za ki-binadamu.
Hizi
hutokana na shughuli nyingi tunazoshinda nazo za kila siku.
·
MHUBIRI 5:3
ii)Ndoto
za ki-pepo(shetan).
Hizi
ni ndoto za vitisho ,uwongo na mashambulizi juu ya wanadamu zisababishwazo na
nguvu za giza ili kuwamiliki na kuwatawala wanadamu.
·
YUDA 1:8
iii)Ndoto
za Ki-Mungu.
Hizi
ni ndoto zitokanazo na Mungu ili kutupasha taarifa Fulani katika maisha
yetu.Mungu hutupa maelekezo mbalimbali kwa njia ya ndoto ili tuweze kumshinda
mwovu.
·
HESABU 12:6 YEREMIA 23:28 KITABU CHA AYUBU 33:13-17
Ifuatayo
ni mifano ya watu waliopewa maelekezo na Mungu kwa njia ya ndoto kibiblia.
i)ABIMELEKI
Mungu
alimkemea Abimeleki mfalme wa Gerari kwa ajili ya Ibrahimu.
·
MWANZO 20:3-7
ii)YAKOBO
Mungu
alimfunulia Yakobo kuhusu mateso ya Israeli kwa Wamisri na mwisho wake.
·
MWANZO 46:2-4
iii)PAULO
Mungu
alimpa maelekezo Mtume Paulo kuhusu huduma yake kupitia ndoto.
·
MATENDO YA
MITUME 16:9
iv)YUSUFU
Mungu
aliyatunza na kuyalinda maisha ya motto YESU kupitia ufunuo wa ndoto kwa
Yusufu.
·
MATHAYO 2:12-13,19-20
BAADHI
YA NDOTO NA MAANA ZAKE.
01.WANYAMA:Kuota
unakimbizwa na wanyama wakali inaasshiria mashambulizi ya kipepo,yaaani nguvu
za giza zimejizatiti dhidi ya maish yako.
02.DAMU:Kuota/kuona
damu kunaonesha kuna hatari mbele.Inaashiria kifo na ajali.Kwa mama mjamzito
huashiria kuharibu mimba.
03.NYUKI:Kujiona
au kumuona mtu amezingirwa na nyuki ni ishara ya shambulizi la kiroho na
kutofanikiwa kimaisha.
04.KUOGA:Inaonesha/inaashiria
utakaso wa rohoni(utakatifu).
05.BIBLIA:Kuipoteza
biblia yako inaashiria kurudi nyuma kiroho na kukosa imani.
06.PAKA:Kuota
paka ndotoni huashiria kuwa wachawi wanafuatilia maisha yako.
07.KUIBIWA
TAJI:Inaonyesha kupoteza umaarufu na kurudi nyuma .pia inaweza
kuashiria kushushwa cheo au wadhifa ofisini au katika nafasi yako kiuchumi au
kisiasa.
08.MLANGO
ULIOFUNGWA:Unapo ota mlango wa ofisini kwako umefungwa dhidi yako
inaashiria kupoteza kibali au kufukuzwa kazi.kama ni mlango wa biashara yako
inamaanisha kunahatari ambayo itaua biashara yako.
09.JENEZA:Inaonesha
kuwa roho ya mauti (kifo)inafuatiria maisha yako au umpendaye (rafiki wa
karibu)
10.AGANO:Kufanya
agano/kuingia kwanye agano na mtu yeyote ndotoni ni kifungo cha kiroho.
11.MSALABANI:Inaashilia
mzigo mkubwa na shida /taabu.
12.GIZA:Inaashiria
kuchanganyikiwa na kurudi nyuma.Iinaashiria kuzolota kiroho.
13.DENI:Kukupa
ndotoni au kudaiwa kuashiria kudorora kiuchumi kiasi cha kuonyesha dalili zote
za kufilisika.
14.MBWA:Kucheza
au kumbeba mbwa kunaashiria roho chafu (uovu) hasa wa usherati (uzinzi)
15.NDUGU
ALIYEKUFA:Kuota cha ndugu inaashiria uwepo wa mzimu wa familia.Uwe
mwangalifu na ujumbe unaoweza kuonekana kama unapata taarifa muhimu lakini
mungu hatumii njia za kipepo kusema na watoto wake SOMA 2WAKORINTHO 11:14,MHUBIRI
3:21.
16.KUNYWA
POMBE:Kuota unakunywa pombe inaashiria kupenda ya dunia
17.ALAMA
ZA KIPEPO:Unapoumizwa ndotoni
au unapoamka na kukutwa alama mwilini mwako inaashiria magereza ya kiroho na
kutumikishwa na mapepo.
18.PUNDA:Inaashiria
ugumu wa mateso au shida katika maisha.
19.MITIHANI:Unaashiria
majaribu na hali,kipindi kigumu.
20.KUPAA:Inaashiria
kutawaliwa na wachawi,shambulizi la kiroho yaani kwamba huenda
utachanganyikiwa.
21.KUVUA
SAMAKI:Kuvua samaki inaashiria kuhubiri injili ya wokovu(soul
winning)kama ilivyo katika biblia.
22.MOTO:Inaashiria
kupoteza na majanga.
23.MAUA:Kupokea
maua kutoka jinsi nyingine (kwa ambao hawajaoa au kuolewa)inaashiria kuwa
mwenzi wako huenda atakujakuwa huyo huyo kwa maisha yako.
24.KUPIGWA
RISASI(KUJERUHIWA):Inaonyesha udhaifu wa kiroho,shambulizina maadui
wamejipanga kuharibu maisha yako.
25.KUPIGWA
RISASI (ISIKUJERUHI):Inaonyesha ulinzi waakiungu na ushindi juu ya
adui zako.
26.KUVUNA:Unapoota
unavuna viazi,mihogo n.k.inaashiria Baraka za Mungu.
27.ASALI:Inaashiria
Afya na mafanikio maishani mwako.
28.NYUMBA
TUPU:Inaashiria hili ngumu na umaskini.
29.KUJIFICHA:Inaashiria
maadui wanapigana/wanafuatilia maisha yako lakini uko chini ya ulinzi wa Mungu.
30.SAFARI:Unapoona
na kujiona /kuona upo kwenye safari isiyokuwa na mwisho(kikomo)ina maanisha
unachofanya au unachotaka kufanya itakuwa ni kupoteza-poteza muda na
nguvu.Hakutakuwa na matunda.
31.KUPOTEZA
FUNGUO:Unapopoteza ufunguo wako ndotoni,inaashiria mlango wa Baraka
zako utafungwa.Inaweza hali hiyo ikakuletea hitimisho la mipango
chanya,matarijio na matumaini yako kuhusu mafanikio.
32.FUNGUONYINGI:Unapoota
na kukuta au kugundua umeshika funguo nyingi,inaashiria Baraka za fursa nyingi
zinakusubiri maishani mwako.
34.KUPOTEZA
PESA AU MALI:Inaashiria mambo mabaya au wezi wanaweza kuiba pesa au
vitu vyako.Inaweza kumaanisha unataka kufanya biashara isiyo sahihi au
kuangukia kwenye mitego ya matapeli na makundi ya mafisadi.
35.MZIGO:Kubeba
mzigo inaashiria hili mbaya katika mateso na umasikini.
36.PESA:Unapoota
mtu anakupa msaada au akukupa pesa bure,inaashiria kibali au neema maalumu na
mpenyo wa kipesa mbele yako.
37.MOCHWARI:Inaonyesha/inaashiria
mauti inakufuatilia/imekuzunguka wewe au mtu uliye muona kwenye hiyo ndoto.
38.UKICHAA:Unapoota
umekuwa kichaa ndotoni,inamanisha shetani anataka kusababisha mvurugano katika
maisha yako.Inamaanisha shetani anataka/yuko tayari kukudhuru.unapoota unacheza
na vichaa au watu wenye ukichaa pia inaashiria shambulizi la kiroho ili
kukusambaratishia amani na utulivu.
39.WAHUNI:Unapoota
umekimbizwa/umefukuzwa na wahuni,inaashiria nguvu za giza na wachawi wanajaribu
kukuharibu(kukuua).
40.RUNGU:Niishara
ya nguvu,pia inaashiria ukakamaavu
kiroho na ulinzi wa kiungu.
41.NDOA:Unapoona
unafunga ndoa na mtu asiyemjua,inaweza kuashiria mume/mke wa kipepo (kama ni
mtu unayemjua lakini ameao/ameolewa,ni ishara ya kufanya kosa kubwa/hatari katika
ndoa.Kama ni mtu unayemjua vizuri na wote mko na vijana na kama huna tama za
mwili kwake (naye)hiyo inaweza kuwa ishara ya mwenzi wa maisha.
42.MIMBA
KUTOKA/KUHARIBIKA:Kama mwanake mjamzito ,umeota mimba
imetoka/imeharibika,usilichuklie kirahisi,pasipo kuangalia ni nani
aliyesababisha hilo,kwani linaweza kutokea kiuhalisia.
43.UCHI/KUVUA
NGUO:Inaashiria aibu au fedheha .
44.SIMBA:Kama
katika ndoto yako umeshambuliwa na simba na ukafanikiwa kumuua,inamaanisha
umemshinda na kumua mtu aliyekuwa anataka kuharibu maisha yako.
45.BUNDI:Kuona
bundi ndotoni inaashiria ubaya.ni taarifa kwamba kitu kibaya
kitatokea/kinakwenda kutokea.
46.MTU
ANAKUFUKUZA/ANAKUKIMBIZA:Kama katika ndoto yako umeota mtu
unayemjua amekukimbiza akitaka kukua, mtu huyo anaweza kuwa hana
mawazo/makusudi mazuri juu yako.Hata hivyo katika nyakati zingine wachawi
hutumia sura ya mtu yeyote kulaghai,ilimradi tu ayaweke maisha yako hatarini.
47.NGURUWE:Ukijiona
unacheza na nguruwe au hata kuwaona nguruwe ,huo ni uchafu kiroho,uzembe na kutokuwa
makini katika maisha ya kiroho.
48.SHIMO:Inaashiria
shetani ana mipango mibaya dhidi yako ili akuharibu.
49.KUCHEZWA
NANYOKA:Hiki ni kuashiria kwamba umefungwa/unatawaliwa na Yule
nyoka shetani.
50.KONOKONO:Inaashiria
kudumaa na kuzuiliwa kwa (maendeleo)au kukua kwa mtu.
51.SHULE:Unapoota
mara kwa mara kurudi shule kusoma au kuwa shuleni,inamanisha unahitaji
(mafunzo)kupata/kupitia mafunzo ili kufanya vizuri katika taaluma yako au utumishi
wako katika maisha.kurudi shule za chuni au madarasa inaashiria kudumaa,yaani
badala au kupiga hutua mbele unaridi nyuma kimaendeleo.
52.NGONO:Kufanya
mapenzi na mtu ambaye siyo mwenzi wako wa maisha ni njia ya kwanza
inayothibisha kutawaliwa na tama ya mwili,pili inaweza kuwa msukumo wa pepo kama unaendelea kufanya
mapenzi na mtu usiyemjua.Roho ya uzinzi imeshakutawala.
53.MAJOKA:Inaashiria
imetawaliwa na roho za majini au umeigia/umeingizwa kwenye agano hilo la
mapepo/majini ya pwani baharini au mtoni.
54.NYOTA:Inaashiria
ukuu.
55.MOSHI:Inaashiria
shutuma na majaribu.
56.RADI:Kamakulikuwa
na mvua kubwa iliyoambatana na mawe ngurumo na radi,inaashiria matatizo na
kuchanganyikiwa siku za usoni.
57.KIJIJI:Unapoota
kijiji chako mara kwa mara wakati wewe unaishi mjini hali hiyo inaashiria kuwa
laana za mizimu zinajitokeza kukurudisha nyuma.
58.KUNGURU:Inaashiria
kifo au mauti mbele yako.
59.PETE
YA NDOA(1):Kama mwanandoa umeota unapoteza pete yako ya
ndoa,inaweza kuonyesha/kuashiria unahitaji kuwamwangalifu sana (ndoa)pia
inaashiria matatizo ya ndoa mbele yako.
60.PETE
YA NDOA(2):Kama umepewa pete ya harusi ukiwa kijana,inaashiria
kuolewa hivi karibuni,pia inaweza kumaanisha mtu (mhusika)ni mwenzi wako
wamaisha
61.KUTEMBEA
BILA VIATU:Inaashiria shetani anataka kukuchanganya kukupa aibu na
hali ngumu (shida au taabu)
62.KUVIKWA
TAJI:Inaonyesha utainuriwa katika kazi yeyote uliyoko au taaluma
utafanywa kuwa kiongozi katika muda muafaka.
63.MAHAKAMA:Inaashiria
kutoelewana baina yako na jirani zako,wadau wa biashara,ndungu au hata mkeo.
64.KUSHINDA
KWENYE USHINDANI:Inaashiria habari nzuri na mpenyo kwako siku za
usoni katika shughuli zako.
65.KUTOA/KUFUKUZA
MAPEPO KWA USHINDI:Unapoota
unakemea mapepo na yakatii na kukimbia kwa jina la YESU inaonyesha ushindi juu
ya adui yako,nguvu za mungu au upako na udhihirisho wakarama za Roho mtakatifu.
66.KUSHINDWA
KUTOA MAPEPO:Kama unatoa pepo kwa jina la Yesu na hakuna
kinachotokea unashiria udhaifu wa kiroho,uvivu wa kuomba na kukosekana kwa
upako (nguvu za Roho mtakatifu)
67.WATOTO(1):Unapokuwa
umeolewa au hujaolewa na unatafuta mtoto na kugundua kila ndoto zako una mtoto
au kuona motto,inaashiria wake/waume wa kipepo,watoto hao ni wakipepo.
68.WATOTO(2):Unapo
kuwa umeolewa na kujiona na mtoto mwingine,inaashiria kuwa utapata ujauzito
karibuni.
69.KUENDESHA
GARI LA GHARAMA:Inaashiria Baraka nzuri.
70.KUSHINDWA:Kama
unashindwa vita ndotoni inaonyesha udhaifu wa kiroho na tayari uko kwenye mtego
au wavu wa adui yako.
71.NYWELE
ZENYE MVI:Inaashiria uzee,inaashiria utaishi maisha marefu.
72.MAANDISHI
YA MKONO:Haijarishi kama yameandikwa kwenye ukuta au karatasi,kama
maandishi hayo yako kwa muajibu wa biblia (fahamu kwamba Mungu anakupa
maelekezo muhimu (taarifa muhimu).
73.UPONYAJI:Kupona
ndotoni anaashiria tatizo(ugonjwa)lako limekwisha katika ulimwengu wa
roho.uponyaji wa mwilini utathibitika kwa haraka.
74.BARUA/SIMU:Inaonyesha
hivi karibuni utapokea ujumbe utakaobadilisha maisha yako,kwa uzuri au ubaya.
75.SIMBA:Kama
katika ndoto anashambuliwa na samba na ukafanikiwa kumuua,inamaanisha
umemshinda na kumua mtu aliyekuwa anataka kuharibu maisha yako.
76.NZIGE:Hii
inaashiria/inaonyesha hasara na njaa.inaashiria mashambulizi ya aduii yako
kwenye uchumi (fedha)yako,yaani umelengwa uwe duni/lofa.
77.WOSIA/MIRATHI:Inaashiria
mauti/kifo,mazishi na shughuli za misiba kushamiri.
78.MAFUTA
MEKUNDU/NGUO NYEKUNDU:Inaashiri hatari kwa mwanamke mjamzito
inaashiria kuharibika kwa mimbi,kama umevaa mavazi mekundu
(ndotoni)inadhihirisha pia matambiko ya kipepo.
==============================UBARIKIWE!============================
Pastor.
AMOS E.ONESMO-0756391498
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni