Ndoto
ni njia mojawapo ambayo Mungu husema,na kuwaelekeza watoto wake waleo.
YOWELI
2:28-29
Shetani
pia huzungumza,hushambulia na kuwamiliki watu kupitia ndoto.Maombi yenye nguvu
yanaweza kukuwezesha kuyashinda mashsmbulizi kama hayo ya ndoto.Jifunze kushughulika
na ndoto ili kupambana na ndoto za vitisho na za uongo za shetani.
ZEKARIA
10:2
AINA
ZA NDOTO.
i)Ndoto
za ki-binadamu.
Hizi
hutokana na shughuli nyingi tunazoshinda nazo za kila siku.
MHUBIRI
5:3
ii)Ndoto
za ki-pepo(shetan).
Hizi
ni ndoto za vitisho ,uwongo na mashambulizi juu ya wanadamu zisababishwazo na
nguvu za giza ili kuwamiliki na kuwatawala wanadamu.
YUDA
1:8
iii)Ndoto
za Ki-Mungu.
Hizi
ni ndoto zitokanazo na Mungu ili kutupasha taarifa Fulani katika maisha
yetu.Mungu hutupa maelekezo mbalimbali kwa njia ya ndoto ili tuweze kumshinda
mwovu.
HESABU
12:6
YEREMIA
23:28
KITABU
CHA AYUBU 33:13-17
Ifuatayo
ni mifano ya watu waliopewa maelekezo na Mungu kwa njia ya ndoto kibiblia.
i)ABIMELEKI
Mungu
alimkemea Abimeleki mfalme wa Gerari kwa ajili ya Ibrahimu.
MWANZO
20:3-7
ii)YAKOBO
Mungu
alimfunulia Yakobo kuhusu mateso ya Israeli kwa Wamisri na mwisho wake.
MWANZO
46:2-4
iii)PAULO
Mungu
alimpa maelekezo Mtume Paulo kuhusu huduma yake kupitia ndoto.
MATENDO
YA MITUME 16:9
iv)YUSUFU
Mungu
aliyatunza na kuyalinda maisha ya motto YESU kupitia ufunuo wa ndoto kwa
Yusufu.
MATHAYO
2:12-13,19-20
BAADHI
YA NDOTO NA MAANA ZAKE.
01.WANYAMA:Kuota
unakimbizwa na wanyama wakali inaasshiria mashambulizi ya kipepo,yaaani nguvu
za giza zimejizatiti dhidi ya maish yako.
02.DAMU:Kuota/kuona
damu kunaonesha kuna hatari mbele.Inaashiria kifo na ajali.Kwa mama mjamzito
huashiria kuharibu mimba.
03.NYUKI:Kujiona
au kumuona mtu amezingirwa na nyuki ni ishara ya shambulizi la kiroho na
kutofanikiwa kimaisha.
04.KUOGA:Inaonesha/inaashiria
utakaso wa rohoni(utakatifu).
05.BIBLIA:Kuipoteza
biblia yako inaashiria kurudi nyuma kiroho na kukosa imani.
06.PAKA:Kuota
paka ndotoni huashiria kuwa wachawi wanafuatilia maisha yako.
07.KUIBIWA
TAJI:Inaonyesha kupoteza umaarufu na kurudi nyuma .pia inaweza kuashiria
kushushwa cheo au wadhifa ofisini au katika nafasi yako kiuchumi au kisiasa.
08.MLANGO
ULIOFUNGWA:Unapo ota mlango wa ofisini kwako umefungwa dhidi yako inaashiria
kupoteza kibali au kufukuzwa kazi.kama ni mlango wa biashara yako inamaanisha
kunahatari ambayo itaua biashara yako.
09.JENEZA:Inaonesha
kuwa roho ya mauti (kifo)inafuatiria maisha yako au umpendaye (rafiki wa
karibu)
10.AGANO:Kufanya
agano/kuingia kwanye agano na mtu yeyote ndotoni ni kifungo cha kiroho.
11.MSALABANI:Inaashilia
mzigo mkubwa na shida /taabu.
12.GIZA:Inaashiria
kuchanganyikiwa na kurudi nyuma.Iinaashiria kuzolota kiroho.
13.DENI:Kukupa
ndotoni au kudaiwa kuashiria kudorora kiuchumi kiasi cha kuonyesha dalili zote
za kufilisika.
14.MBWA:Kucheza
au kumbeba mbwa kunaashiria roho chafu (uovu) hasa wa usherati (uzinzi)
15.NDGU
ALIYEKUFA:Kuota cha ndugu inaashiria uwepo wa mzimu wa familia.Uwe mwangalifu
na ujumbe unaoweza kuonekana kama unapata taarifa muhimu lakini mungu hatumii
njia za kipepo kusema na watoto wake SOMA 2WAKORINTHO 11:14 NA
MHUBIRI 3:21.
16.KUNYWA
POMBE:Kuota unakunywa pombe inaashiria kupenda ya dunia
17.ALAMA
ZA KIPEPO:Unapoumizwa ndotoni au
unapoamka na kukutwa alama mwilini mwako inaashiria magereza ya kiroho na
kutumikishwa na mapepo.
18.PUNDA:Inaashiria
ugumu wa mateso au shida katika maisha.
19.MITIHANI:Unaashiria
majaribu na hali,kipindi kigumu.
20.KUPAA:Inaashiria
kutawaliwa na wachawi,shambulizi la kiroho yaani kwamba huenda
utachanganyikiwa.
21.KUVUA
SAMAKI:Kuvua samaki inaashiria kuhubiri injili ya wokovu(soul winning)kama
ilivyo katika biblia.
22.MOTO:Inaashiria
kupoteza na majanga.
23.MAUA:Kupokea
maua kutoka jinsi nyingine (kwa ambao hawajaoa au kuolewa)inaashiria kuwa
mwenzi wako huenda atakujakuwa huyo huyo kwa maisha yako.
24.KUPIGWA
RISASI(KUJERUHIWA):Inaonyesha udhaifu wa kiroho,shambulizina maadui wamejipanga
kuharibu maisha yako.
25.KUPIGWA
RISASI (ISIKUJERUHI):Inaonyesha ulinzi waakiungu na ushindi juu ya adui zako.
26.KUVUNA:Unapoota
unavuna viazi,mihogo n.k.inaashiria Baraka za Mungu.
27.ASALI:Inaashiria
Afya na mafanikio maishani mwako.
28.NYUMBA
TUPU:Inaashiria hili ngumu na umaskini.
29.KUJIFICHA:Inaashiria
maadui wanapigana/wanafuatilia maisha yako lakini uko chini ya ulinzi wa Mungu.
30.SAFARI:Unapoona
na kujiona /kuona upo kwenye safari isiyokuwa na mwisho(kikomo)ina maanisha
unachofanya au unachotaka kufanya itakuwa ni kupoteza-poteza muda na
nguvu.Hakutakuwa na matunda.
31.KUPOTEZA
FUNGUO:Unapopoteza ufunguo wako ndotoni,inaashiria mlango wa Baraka zako
utafungwa.Inaweza hali hiyo ikakuletea hitimisho la mipango chanya,matarijio na
matumaini yako kuhusu mafanikio.
32.
FUNGUONYINGI:Unapoota na kukuta au kugundua umeshika funguo nyingi,inaashiria
Baraka za fursa nyingi zinakusubiri maishani mwako.
34.KUPOTEZA
PESA AU MALI:Inaashiria mambo mabaya au wezi wanaweza kuiba pesa au vitu
vyako.Inaweza kumaanisha unataka kufanya biashara isiyo sahihi au kuangukia
kwenye mitego ya matapeli na makundi ya mafisadi.
35.MZIGO:Kubeba
mzigo inaashiria hili mbaya katika mateso na umasikini.
36.PESA:
Unapoota mtu anakupa msaada au akukupa pesa bure,inaashiria kibali au neema
maalumu na mpenyo wa kipesa mbele yako.
37.MOCHWARI:Inaonyesha/inaashiria
mauti inakufuatilia/imekuzunguka wewe au mtu uliye muona kwenye hiyo ndoto.
38.UKICHAA:Unapoota
umekuwa kichaa ndotoni,inamanisha shetani anataka kusababisha mvurugano katika
maisha yako.Inamaanisha shetani anataka/yuko tayari kukudhuru.unapoota unacheza
na vichaa au watu wenye ukichaa pia inaashiria shambulizi la kiroho ili
kukusambaratishia amani na utulivu.
39.WAHUNI:Unapoota
umekimbizwa/umefukuzwa na wahuni,inaashiria nguvu za giza na wachawi wanajaribu
kukuharibu(kukuua).
40.RUNGU:Niishara
ya nguvu,pia inaashiria ukakamaavu
kiroho na ulinzi wa kiungu.
41.
NDOA:Unapoona unafunga ndoa na mtu asiyemjua,inaweza kuashiria mume/mke wa
kipepo (kama ni mtu unayemjua lakini ameao/ameolewa,ni ishara ya kufanya kosa kubwa/hatari
katika ndoa.Kama ni mtu unayemjua vizuri na wote mko na vijana na kama huna
tama za mwili kwake (naye)hiyo inaweza kuwa ishara ya mwenzi wa maisha.
42.MIMBA
KUTOKA/KUHARIBIKA:Kama mwanake mjamzito ,umeota mimba
imetoka/imeharibika,usilichuklie kirahisi,pasipo kuangalia ni nani
aliyesababisha hilo,kwani linaweza kutokea kiuhalisia.
43.UCHI/KUVUA
NGUO:Inaashiria aibu au fedheha .
44.SIMBA:Kama
katika ndoto yako umeshambuliwa na simba na ukafanikiwa kumuua,inamaanisha
umemshinda na kumua mtu aliyekuwa anataka kuharibu maisha yako.
45.BUNDI:Kuona
bundi ndotoni inaashiria ubaya.ni taarifa kwamba kitu kibaya
kitatokea/kinakwenda kutokea.
46.MTU
ANAKUFUKUZA/ANAKUKIMBIZA:Kama katika ndoto yako umeota mtu unayemjua
amekukimbiza akitaka kukua, mtu huyo anaweza kuwa hana mawazo/makusudi mazuri
juu yako.Hata hivyo katika nyakati zingine wachawi hutumia sura ya mtu yeyote
kulaghai,ilimradi tu ayaweke maisha yako hatarini.
47.NGURUWE:Ukijiona
unacheza na nguruwe au hata kuwaona nguruwe ,huo ni uchafu kiroho,uzembe na
kutokuwa makini katika maisha ya kiroho.
48.SHIMO:Inaashiria
shetani ana mipango mibaya dhidi yako ili akuharibu.
49.KUCHEZWA
NANYOKA:Hiki ni kuashiria kwamba umefungwa/unatawaliwa na Yule nyoka shetani.
50.KONOKONO:Inaashiria
kudumaa na kuzuiliwa kwa (maendeleo)au kukua kwa mtu.
51.SHULE:Unapoota
mara kwa mara kurudi shule kusoma au kuwa shuleni,inamanisha unahitaji
(mafunzo)kupata/kupitia mafunzo ili kufanya vizuri katika taaluma yako au utumishi
wako katika maisha.kurudi shule za chuni au madarasa inaashiria kudumaa,yaani
badala au kupiga hutua mbele unaridi nyuma kimaendeleo.
52.NGONO.Kufanya
mapenzi na mtu ambaye siyo mwenzi wako wa maisha ni njia ya kwanza
inayothibisha kutawaliwa na tama ya mwili,pili inaweza kuwa msukumo wa pepo kama unaendelea kufanya
mapenzi na mtu usiyemjua.Roho ya uzinzi imeshakutawala.
53.MAJOKA:Inaashiria
imetawaliwa na roho za majini au umeigia/umeingizwa kwenye agano hilo la
mapepo/majini ya pwani baharini au mtoni.
54.NYOTA:Inaashiria
ukuu.
55.MOSHI:Inaashiria
shutuma na majaribu.
56.RADI:Kamakulikuwa
na mvua kubwa iliyoambatana na mawe ngurumo na radi,inaashiria matatizo na
kuchanganyikiwa siku za usoni.
57.KIJIJI:Unapoota
kijiji chako mara kwa mara wakati wewe unaishi mjini hali hiyo inaashiria kuwa
laana za mizimu zinajitokeza kukurudisha nyuma.
58.KUNGURU:Inaashiria
kifo au mauti mbele yako.
59.PETE
YA NDOA(1):Kama mwanandoa umeota unapoteza pete yako ya ndoa,inaweza
kuonyesha/kuashiria unahitaji kuwamwangalifu sana (ndoa)pia inaashiria matatizo
ya ndoa mbele yako.
60.PETE
YA NDOA(2)Kama umepewa pete ya harusi ukiwa kijana,inaashiria kuolewa hivi
karibuni,pia inaweza kumaanisha mtu (mhusika)ni mwenzi wako wamaisha
61.KUTEMBEA
BILA VIATU:Inaashiria shetani anataka kukuchanganya kukupa aibu na hali ngumu
(shida au taabu) .
……………………………….BARIKIWA………………………………………………………..
MAWASILIANO
0759199463
MAWASILIANO
0759199463
Asante kwa kazi nzuri ya kuijuza jamii, ila Nina swali kuhusu ndoto yangu hii, "nimeota ndoto ninechukua konokono nyumbani na kwenda kuyatupa jalalani" je,ndoto hii ina maana gani??
JibuFutaWASILIANA NAMI KWA NAMBA 0756391498.
JibuFutavp kwa mtu anayevamiwa na kushambuliwa na kunguru mara kwa mara na siyo ndotoni hii ni kweli kabisa?
JibuFutaAsante kwa tafsiri, ila mimi nina ndoto niliyoiota ambayo naomba tafsiri yake
JibuFutaNiliota hivi.Niliwaona dege aina ya Tai wengijuu angani wazuri wenye manyoa laini sana wanpendeza sana ila wanazunguka juu ya anga usawa wa kitanda nilipo lala nilikuwa nawaona kutokea kitandani nilipolala naomba kusaidiwa, waweza kunitumia kupitia email yangu, smwitap@gmail.com
Amina
JibuFutaEliza
JibuFutaAsante kwa tafsiri, naomba maana ya ndoto nilyoota. Nimeota navalishwa kiatu
KUFALISHWA VIATU DADA ANGU NI ULIKUWA NA KIATU MOJA KWANI AUNA NDOA SASA UMEFALISHWA VIATU VYAKO YOTE SASA UKO NA VIATU VYAKO YOTE DADA ANGU
FutaTumaini
FutaHapo Cha kwanza Cha kujua Nani anakuvalishwa kiatu? Na ni katika Mazingira Gani.
FutaIla ukiota unavalishwa kiatu..
1. Moja inahusu Mambo ya utayari
2. Lango la nafsi yako.
3. Kufungwa masikio ya Rohoni usisikie.
Kutoka 3:5
Nimeota Mvua inanyesha lakini sikuona mvua ila radi zikawa zinapiga mbali kama mita 200 kutoka Nyumba yetu. Nikawa nimewashika wadogo zangu wawili. Zile radi zilikuwa zikipiga zinawaka moto kama BOMU na zikawa zinapiga sana lakini pale kwetu palikuwa salama hakuna radi ila tulikuwa na hofu sana kwani moto ulikuwa unalipuka sana kule kulikokuwa zinapigwa radi.
JibuFutaEmail yangu ni "malimam2@live.com
HUA NAOTA NIKO KIJIJINI KWETU MARA KWA MARA MAANA YAKE NI NINI NA NIFANYEJE?
JibuFutaHII NDIO GIMEL YANGU olesongoyolendimi@gmail.com
FutaMUNGU AKUBARIKI SANA KAKA NA JE NAFUTA NJIA YA KUPITA NA SIPATI
JibuFutaJANA NIMEOTA NATAFUTA NJIA YA KUPITA NA SIKUPATA NA NILIPO ENDELEA MBELE NILIFIKA KWA KIWANJA MOJA KUNA NGOMBE WENGI NA NILIPO FIKA APO NILI WAKUTA NGOMBE WENGI NA KUNA NDAMA ALIKUWA ANATAKA KUNIPIGA NIKAWA NAKIMBIYA SASA IKAWA KUNA NGOMBE MWAINGINE KUBWA ALI JITOKESA IKAWA NIMEKIMBIYA
JibuFutaNgo'mbe kwa lugha ya kiunabii ni watu so ndoto yako inamanisha kuna mioyo ya watu inakuja kukujeruhi au kukuumiza kwa kitu au jambo fulani na kama ulifanikiwa kukimbia ina maana hao maadui hukuwaruhusu wafanye hivyo nikiwa namaanisha walishindwa kutimiza maudhui yao
FutaNA GIMEL YANGU NI olesongoyolendimi@gmail.com
JibuFutaAhsante kwa tafsiri ila Mimi nimeota watu wawili ninaowafahamu ni vichaa
JibuFutaKuvurugika kwa maisha ya watu hao.
FutaMaelezo zaidi nitafute 0756391498
Na ukiota upo darasani umevaa viatu siyo vyako nin maana yake
JibuFutaKurudi darasani ni kurudi nyuma kiroho, au Mungu anataka kukufundisha jambo jipya ambalo hulijui au kurudi nyuma kiuchumi.
FutaKuvaa viatu visivyo vyako maana yake ni kubeba kitu kisicho chako, kama vile LAANA au jambo lolote lisilo zuri.
Maelezo zaidi nitafute 0756391498
Napenda mafundisho yako ....barikiwa
JibuFutaBarikiwa sana
FutaCHANGIA SADAKA YA UNUNUZI WA CHOMBO CHA UINJILISTI VIJIJINI
JibuFutaMpendwa nakusalimu katika jina la Yesu! Mimi ni ndugu yako Mchungaji Amos E. Onesmo. Licha ya kuchunga Kanisa, nimekuwa nikifanya UINJILISTI vijijini Katika mikoa na maeneo mbali mbali. Nimekuwa nikimwona Mungu kwa viwango vya juu sana.
Kumekuwa na changamoto kubwa kwa wahubiri wengi kutofika vijijini kutokana na mazingira ya vijijini kuwa magumu sana. Usafiri ni mgumu, malazi, hata chakula wakati mwingine si bora sana. Kiukweli, watu wa vijijini wanamhitaji Mungu sana wapo katika vifungo vikubwa vya giza vinavyosababishwa na:-
• MIZIMU
• MAAGANO
• MAPEPO
• MAJINI n.k
Katika huduma hii ninayoifanya ninauhitaji mkubwa wa SPEAKER moja ambayo ikishachajiwa inaweza kutumika bila ya kuunganishwa moja kwa moja kwenye Umeme. Nina uhitaji wa SPEAKER hii kwa sababu vijijini kuna shida kubwa ya umeme.
Kwa heshima kubwa, naomba mchango wako ili kuniwezesha kupata SPEAKER hiyo yenye thamani ya LAKI 3 (Tsh300,000/=). Unaweza kunichangia FEDHA au Unaweza kuninunulia SPEAKER hiyo ukaniletea, Baraka za Mungu zitamiminika kwako maana utakuwa umehudumu pamoja nami.
Unaweza kuchangia kwa namba hii;
NAMBA JINA LA USAJILI
0658727799 AMOS ONESMO
Pia, unaweza kuchangia kwa account ya BENKI.
NAMBA YA ACCOUNT (NMB BANK) JINA LA ACCOUNT
51010032134 AMOS EZEKIA ONESMO
Ukichangia nitumie jina lako na mahitaji yako ili nikuombee kwa namba hizi za mawasiliano;
0756391498 / 0658727799
Whatsapp number:
0756391498
MPENDWA JISIKIE KUTUMIKA PAMOJA NAMI KWA NJIA YA SADAKA.
…………………………..…….BARIKIWA MNO!..................................................
By
Pastor Amos E. Onesmo
July 2018
Shaloom,Kuota nafanya mtihani halafu unakusanywa ghafla cjamaliza,nn maanayake paster
JibuFutaShaloom,Kuota nafanya mtihani halafu unakusanywa ghafla cjamaliza,nn maanayake paster
JibuFutaNdugu yangu Upo kwenye Mapito mazuri. Nakama Upo kwenye maombi ongeza maombi Mpaka uone upokwenye mtihani na ufanya vizuri
FutaShalom Mtumishi wa Mungu. Nimeota nimevaa viatu ila cha mguu mmoja sio changu na nikaenda kukitafuta nikakuta viatu vingi sana ila changu sikukiona.
JibuFutaNabarikiwa sana ila jana niliota mabomba mawili yanatoa maji lkn kidogo kidogo ila yote yangu
JibuFutaAmina mtumishi wa mungu ila katika fasri za ndoto ambatanisha na mistari ya Biblia ili kuwa na uhakika amen.
JibuFutaHabari mtumishi,
JibuFutanaitwa jenifer niliota nimeona nyoka weusi watatu kwenye nyumba yetu mama akafanikiwa kummua mmoja akamtupa karibu na kidimbwi cha maji ya mvua yule nyoka mweusi akafufuka na kutembea tena akamuua tena. tukatoka hapo nje tukaingia ndani mimi na mdogo wangu jikoni kuna jiwe mdogo wangu aliinua lile jiwe la kusagia vitu tukaona nyoka weusi wawili wafupi wanataka kutung'ata nikajaribu kumuua mmoja na mwiko lakini alinasa kwenye mwiko na kutaka kuning'ata nikatupa mwiko. nilishtuka bila kufanikiwa kumuua nyoka
Nimeota nakimbia bila ya viatu ikafika SEHEMU kunakikwazo Nikapita Muda wakurud kikashidwa kuvuka kikwazo nikajishikiza kwenye mti juu na chini kunashimo Lina Mavi na maji machafu Kuna watu2 nilipishana nao nikaita akaja kuniokoa nilimshukuru Sana akaomba namba ya simu nilimpa ya uongo
JibuFutaBarikiwa Mtumishi. Nimeota ninkwenda kijini kwetu. Mara simba wakwa shambani kwetu na mwanangu kawafungulia nguruwe ili wasinidhuru. Akaniambia mama endelea tu hawatakudhuru kwanu wanakula nguruwe. Nilipowapita tu kwa nyuma nikamwona simba ananifukuza na mwanangu akawa anamkimbiza ili asinidhuru. Mara akamshika mguu wa nyuma akamvuta, na hakuweza kunishambulia.
JibuFutaBarikiwa Mtumishi. Nimeota nimekwenda kijini kwetu. Mara simba wakawa shambani kwetu na mwanangu kawafungulia nguruwe ili wasinidhuru. Akaniambia mama endelea tu hawatakudhuru kwani wanakula nguruwe. Nilipowapita tu kwa nyuma nikamwona simba ananifukuza na mwanangu akawa anamkimbiza ili asinidhuru. Mara akamshika mguu wa nyuma akamvuta, na hakuweza kunishambulia.
JibuFutaSamahani ningependa kuuliza 'kama unaota unakojoa na inatokea umeanza kukojoa kweli kitandani' hii ndoto ina maana gani?
JibuFutaHyo si rahisi tu, Hapo unapewa taarifa kwamba amka ukakojoe kabla mambo hayajaharibika
FutaMi nimeota mguu wangu wa kushoto kwenye nyayo kuna kitundu kinatoa damu na maziwa baada ya hapo akatoka panya mkubwa.nini maana yake pastor
JibuFutaBarikiwa mtumishi
JibuFutaUjambo mtumishi wa mungu Nikita niko kwenye maji yamenifika shingoni na nimepepa mtoto na nilikuwa na hovi ya kusonga mwenyewe,yamaanisha Nini mtu wa mungu?
JibuFutaMungu akibariki. Elimu nzur itanisaidia Sana
JibuFutaMtumishi naomba ufafanuzi wa ndoto nimeota tunang'atwa n nyuki n ndugu zangu n mifugo yetu
JibuFutaAsante mtumishi ubarikiwe pia samahani nilipata ndoto napigana na mtu ety inaashiria nn??
FutaGeorgina
FutaShalom mtumishi kuota unatembelewa na siafu kitandani wengine wakakung'ata ila mtoto nilolala naye kitandan wanamtembelea ila hawamng'ati...maana yake ni nini tafadhal
JibuFutaNimeota naona Rais Watanzania Samia anapita katika nyumba moja nilikua na simama na wengine watu naye alikuwa napiga Guitar na mwengine mwanamke alikua anamshika kiunoni wana dancer rais alikua hana viatu.wimbo ni liwambia watu kwamba hiyo ni Lugha ya
JibuFutakiha siwezi kutafsiri yaani nilikua na wazulu.kisha watoka nje nilibaki na wakodolea macho dirishani.inamaana gani Mkuu.
Nliota nmefanya mtihani na nikapata Kila kitu mpaka nliokuwa nao wakanishangaa.....hiyo manake Ni Nini?
JibuFutambarukunyando@gmail.com
JibuFutaNimeota ndoto ninaokota pesa nyingi ya sarafu nini maana yake
JibuFutaBwana yesu asifiwe ukiota unakimbizwa na kund la ndege aina ya tai inamaanisha nn? Pia ukiota unaaga maiti iliyo kwenye jeneza na kwenda kuzika ina maana gan
JibuFutaShalom pastor!
JibuFutaLeo ndio nimeufahamu huu ukurasa wako.
Nimeufurahia sana, ubarikiwe!
Je, Kuna group la Whatsapp uniunge tafadhali?
Kama lipo, naomba uniunge.