Jumatatu, 25 Aprili 2016

USILIPIZE KISASI



USILIPIZE KISASI
 
 

"Wapenzi, msijilipizie kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, kisasi ni juu yangu Mimi, Mimi nitalipa, anena Bwana" (Warumi 12:19)
Kuna hasara zinazoweza kukupata ukiamua kulipa kisasi kwa mambo uliyofanyiwa ambayo hayakupendezi. Ikiwa ni masuala ya kikabila, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kidini, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kifamilia, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya kikazi, usilipe kisasi. Ikiwa ni masuala ya uhusiano wako na majirani zako, usilipe kisasi.Ndiyo! Usilipe kisasi! Kwa nini? Kwa sababu "imeandikwa kisasi ni juu yangu Mimi; Mimi nitalipa, anena Bwana".

                                              HASARA ZA KULIPA KISASI.
01.Utashindwa.
-Ukiamua kulipa kisasi utashindwa wewe kwa sababu vita hivyo si vya mwili na wala silaha ambazo Mungu amekupa si za mwili!
2 Wakorintho 10:3- 5 imeandikwa hivi:"Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi yamwili; maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome, tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo".

Waefeso 6:12
imeandikwa hivi: "Kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho".
02.Matatizo hayatakwisha.

-"Yeye arudishaye mabaya badala ya mema, mabaya hayataondoka nyumbani mwake"
(Mithali 17:13)
-Ukiamua kulipiza kisasi kwa kumfanyia ubaya yule wa nyumbani mwako - Biblia inasema "mabaya hayataondoka nyumbani mwako" Hii ndiyo maana matatizo mengi katika ndoa na katika jamii hayaishi - kwa sababu mtu akifanyiwa ubaya naye analipa kisasi.
-Ukiamua kulipa kisasi kwa kumfanyia ubaya yule wa nchini mwako ujue hakika mabaya hayataondoka nchini mwako.
-Warumi 12:21 inasema; "Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema".
03.Unamzuia Mungu kukupigania
-Mungu hawezi kukusaidia kwa sababu imeandikwa "msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana, imeandikwa, kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana".
04.Unajichumia dhambi!

Unapoamua kulipa kisasi, unajichumia dhambi! Hii ni kwa sababu kulipa kisasi huja kwa njia ya chuki iliyojengeka ndani yako kwa ajili ya mambo mabaya uliyofanyiwa.
"Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajuaya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake" (1 Yohana 3:15).
05.Kutosamehe
Biblia inatuambia kwamba Mungu huyu ambaye amesema anafuta na kuyasahau makosa yetu, kwa ajili yake mwenyewe, anakaa ndani ya watu wote waliompokea. Hebu soma na kutafakari maneno yafuatayo:
-Yesu Kristo anapoingia ndani ya moyo wako, baada ya wewe kumwamini na kumpokea, unapewa uzima wa milele ndani yako, na unaanza maisha mapya.Imeandikwa kwamba, " Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita; tazama! Yamekuwa mapya (2Wakorintho 5:17)
-Katika maisha mapya utatakiwa usamehe na kusahau kwa ajili yako mwenyewe, ili kuomba kwako kusizuiliwe na baraka zako zisizuiliwe.
Hatua tano zifuatazo zitakupa msingi imara wa kuishi siku zote katika upendo na amani na jirani zako na ndugu zako.
1. Fahamu kuwa si wewe bali Kristo.
"Nimesulibiwa pamoja na Kristo, lakini ni hai, wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu" (Wagalatia 2:20)
"Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu, yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu" (Wakolosai 3:1-3)
-Mtu akikufanyia ubaya, usione kuwa anakufanyia wewe, ona kama vile Mungu aonavyo kuwa, ubaya huo anafanyiwa Kristo aliye ndani yako.
 "Vita hivyo si vyako ni vya Bwana" (2 MAMBO YA NYAKATI 20:15).
2. Mpende adui yako Umuombee
"Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako na umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi ...." (Mathayo 5:43, 44)
-Msamaha wa kweli unadhihirisha upendo ulio ndani ya mtu. Pasipokuwa na upendo, kusameheana hakupo.
- Usiwachukie wanaokuudhi, wapende.
-Ni upendo unamuondolea mtu chuki, uchoyo na ubinafsi.
" Lakini nawaambia ninyi mnaosikia wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi" (Luka 6:27,28)
3. Samehe na Kusahau.
"Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? Yesu akamwambia, sikuambiii hata mara saba, bali hata saba mara sabini" (Mathayo 18:21, 22)
"Na kama akikukosea mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba , akisema, nimetubu msamehe. Mitume wakamwambia Bwana tuongezee imani" (Luka 17:4,5).
-Ukiishaamua kumsamehe mtu hakikisha kwamba hulisemi tena jambo hilo katika kinywa chako.Kumbuka kinywa kinanena yaujazayo moyo (Mathayo 12:34)
4. Hasira ipeleke kwenye maombi
"Mwe na hasira, ila msitende dhambi jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; wala msimpe Ibilisi nafasi" (Waefeso 4:26, 27)
"Uchungu wote na ghadhabu na HASIRA na kelele na matukano YAONDOKE KWENU" (Waefeso 4:31)
"..... HASIRA ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu" (Yakobo 1:20)
-Unapoona kuwa kuna jambo limekuudhi, usiwe mwepesi kujibu au kufanya kitu. Tulia kimya na tafuta nafasi uanze kuomba.
       i)Tubu kwa Baba juu ya kukasirika kwako.
      ii)Mwambie Baba jinsi unavyojisikia moyoni mwako, bila kumficha kitu.
     iii)Mwombe kitu ambacho unataka akufanyie katika jambo hilo.
5. Furahi siku zote.
Siri ya ushindi katika matatizo yoyote, inatokana na furaha ya Kristo iliyo ndani ya mtu.
(Wafilipi 4:4)
-" Heri ninyi watakpowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia;kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu" (Mathayo 4:11, 12)
-"Upole wako ujulikane na watu wote"
Usiwe mwepesi kumwambia mtu maudhi ya nyumbani mwako, au ofisini mwako. Utajikuta umeingia katika kusengenya na hutafaulu kamwe kujifunza kusamehe.

 
(Wafilipi 4:5)

==============================UBARIKIWE!============================

====================================================================
Pastor. AMOS E.ONESMO-0756391498
E-mail:pasteronesmo@gmail.com
www.amosonesmo.blogspot.com

Jumatatu, 18 Aprili 2016



·        Hapa nilikuwa nachoma uchawi wa mtu aliyesalimisha maisha kwa Yesu kwenye mkutano niliouhubiri eneo la KILOLENI TABORA MJINI APRIL 2015.

·        Tarehe 08-10/04/2016 nilikuwa na semina kubwa ya Injili ya Yesu aliye hai,mkoani KIGOMA eneo la Kazuramimba kijiji cha Nyanganga.Wengi walifunguka na kupona kabisa.Mama mmoja alipata tatizo la kuteswa na maumivu mazito ya mbavu akiwa bado binti na sasa ana nzao kumi(10) baada ya maombezi alifunguka na kupona kabisa.

MUNGU ANAWEZA

USHUHUDA



USHUHUDA.

·        Tarehe 08-10/04/2016 nilikuwa na semina kubwa ya Injili ya Yesu aliye hai,mkoani KIGOMA eneo la Kazuramimba kijiji cha Nyanganga.Wengi walifunguka na kupona kabisa.Mama mmoja alipata tatizo la kuteswa na maumivu mazito ya mbavu akiwa bado binti na sasa ana nzao kumi(10) baada ya maombezi alifunguka na kupona kabisa.

MUNGU ANAWEZA

Jumamosi, 16 Aprili 2016

NDOTO NA MAANA ZAKE




Ndoto ni njia mojawapo ambayo Mungu husema,na kuwaelekeza watoto wake waleo.
YOWELI 2:28-29
Shetani pia huzungumza,hushambulia na kuwamiliki watu kupitia ndoto.Maombi yenye nguvu yanaweza kukuwezesha kuyashinda mashsmbulizi kama hayo ya ndoto.Jifunze kushughulika na ndoto ili kupambana na ndoto za vitisho na za uongo za shetani.
ZEKARIA 10:2
AINA ZA NDOTO.
i)Ndoto za ki-binadamu.
Hizi hutokana na shughuli nyingi tunazoshinda nazo za kila siku.
·         MHUBIRI 5:3
ii)Ndoto za ki-pepo(shetan).
Hizi ni ndoto za vitisho ,uwongo na mashambulizi juu ya wanadamu zisababishwazo na nguvu za giza ili kuwamiliki na kuwatawala wanadamu.
·         YUDA 1:8
iii)Ndoto za Ki-Mungu.
Hizi ni ndoto zitokanazo na Mungu ili kutupasha taarifa Fulani katika maisha yetu.Mungu hutupa maelekezo mbalimbali kwa njia ya ndoto ili tuweze kumshinda mwovu.
·         HESABU 12:6       YEREMIA 23:28      KITABU CHA AYUBU 33:13-17
Ifuatayo ni mifano ya watu waliopewa maelekezo na Mungu kwa njia ya ndoto kibiblia.
i)ABIMELEKI
Mungu alimkemea Abimeleki mfalme wa Gerari kwa ajili ya Ibrahimu.
·         MWANZO 20:3-7
ii)YAKOBO
Mungu alimfunulia Yakobo kuhusu mateso ya Israeli kwa Wamisri na mwisho wake.
·         MWANZO 46:2-4
iii)PAULO
Mungu alimpa maelekezo Mtume Paulo kuhusu huduma yake kupitia ndoto.
·         MATENDO YA MITUME 16:9
iv)YUSUFU
Mungu aliyatunza na kuyalinda maisha ya motto YESU kupitia ufunuo wa ndoto kwa Yusufu.
·         MATHAYO 2:12-13,19-20
BAADHI YA NDOTO NA MAANA ZAKE.
01.WANYAMA:Kuota unakimbizwa na wanyama wakali inaasshiria mashambulizi ya kipepo,yaaani nguvu za giza zimejizatiti dhidi ya maish yako.
02.DAMU:Kuota/kuona damu kunaonesha kuna hatari mbele.Inaashiria kifo na ajali.Kwa mama mjamzito huashiria kuharibu mimba.
03.NYUKI:Kujiona au kumuona mtu amezingirwa na nyuki ni ishara ya shambulizi la kiroho na kutofanikiwa kimaisha.
04.KUOGA:Inaonesha/inaashiria utakaso wa rohoni(utakatifu).
05.BIBLIA:Kuipoteza biblia yako inaashiria kurudi nyuma kiroho na kukosa imani.
06.PAKA:Kuota paka ndotoni huashiria kuwa wachawi wanafuatilia maisha yako.
07.KUIBIWA TAJI:Inaonyesha kupoteza umaarufu na kurudi nyuma .pia inaweza kuashiria kushushwa cheo au wadhifa ofisini au katika nafasi yako kiuchumi au kisiasa.
08.MLANGO ULIOFUNGWA:Unapo ota mlango wa ofisini kwako umefungwa dhidi yako inaashiria kupoteza kibali au kufukuzwa kazi.kama ni mlango wa biashara yako inamaanisha kunahatari ambayo itaua biashara yako.
09.JENEZA:Inaonesha kuwa roho ya mauti (kifo)inafuatiria maisha yako au umpendaye (rafiki wa karibu)
10.AGANO:Kufanya agano/kuingia kwanye agano na mtu yeyote ndotoni ni kifungo cha kiroho.
11.MSALABANI:Inaashilia mzigo mkubwa na shida /taabu.
12.GIZA:Inaashiria kuchanganyikiwa na kurudi nyuma.Iinaashiria kuzolota kiroho.
13.DENI:Kukupa ndotoni au kudaiwa kuashiria kudorora kiuchumi kiasi cha kuonyesha dalili zote za kufilisika.
14.MBWA:Kucheza au kumbeba mbwa kunaashiria roho chafu (uovu) hasa wa usherati (uzinzi)
15.NDUGU ALIYEKUFA:Kuota cha ndugu inaashiria uwepo wa mzimu wa familia.Uwe mwangalifu na ujumbe unaoweza kuonekana kama unapata taarifa muhimu lakini mungu hatumii njia za kipepo kusema na watoto wake SOMA 2WAKORINTHO 11:14,MHUBIRI 3:21.
16.KUNYWA POMBE:Kuota unakunywa pombe inaashiria kupenda ya dunia
17.ALAMA ZA KIPEPO:Unapoumizwa  ndotoni au unapoamka na kukutwa alama mwilini mwako inaashiria magereza ya kiroho na kutumikishwa na mapepo.
18.PUNDA:Inaashiria ugumu wa mateso au shida katika maisha.
19.MITIHANI:Unaashiria majaribu na hali,kipindi kigumu.
20.KUPAA:Inaashiria kutawaliwa na wachawi,shambulizi la kiroho yaani kwamba huenda utachanganyikiwa.
21.KUVUA SAMAKI:Kuvua samaki inaashiria kuhubiri injili ya wokovu(soul winning)kama ilivyo katika biblia.
22.MOTO:Inaashiria kupoteza na majanga.
23.MAUA:Kupokea maua kutoka jinsi nyingine (kwa ambao hawajaoa au kuolewa)inaashiria kuwa mwenzi wako huenda atakujakuwa huyo huyo kwa maisha yako.
24.KUPIGWA RISASI(KUJERUHIWA):Inaonyesha udhaifu wa kiroho,shambulizina maadui wamejipanga kuharibu maisha yako.
25.KUPIGWA RISASI (ISIKUJERUHI):Inaonyesha ulinzi waakiungu na ushindi juu ya adui zako.
26.KUVUNA:Unapoota unavuna viazi,mihogo n.k.inaashiria Baraka za Mungu.
27.ASALI:Inaashiria Afya na mafanikio maishani mwako.
28.NYUMBA TUPU:Inaashiria hili ngumu na umaskini.
29.KUJIFICHA:Inaashiria maadui wanapigana/wanafuatilia maisha yako lakini uko chini ya ulinzi wa Mungu.
30.SAFARI:Unapoona na kujiona /kuona upo kwenye safari isiyokuwa na mwisho(kikomo)ina maanisha unachofanya au unachotaka kufanya itakuwa ni kupoteza-poteza muda na nguvu.Hakutakuwa na matunda.
31.KUPOTEZA FUNGUO:Unapopoteza ufunguo wako ndotoni,inaashiria mlango wa Baraka zako utafungwa.Inaweza hali hiyo ikakuletea hitimisho la mipango chanya,matarijio na matumaini yako kuhusu mafanikio.
32.FUNGUONYINGI:Unapoota na kukuta au kugundua umeshika funguo nyingi,inaashiria Baraka za fursa nyingi zinakusubiri maishani mwako.
34.KUPOTEZA PESA AU MALI:Inaashiria mambo mabaya au wezi wanaweza kuiba pesa au vitu vyako.Inaweza kumaanisha unataka kufanya biashara isiyo sahihi au kuangukia kwenye mitego ya matapeli na makundi ya mafisadi.
35.MZIGO:Kubeba mzigo inaashiria hili mbaya katika mateso na umasikini.
36.PESA:Unapoota mtu anakupa msaada au akukupa pesa bure,inaashiria kibali au neema maalumu na mpenyo wa kipesa mbele yako.
37.MOCHWARI:Inaonyesha/inaashiria mauti inakufuatilia/imekuzunguka wewe au mtu uliye muona kwenye hiyo ndoto.
38.UKICHAA:Unapoota umekuwa kichaa ndotoni,inamanisha shetani anataka kusababisha mvurugano katika maisha yako.Inamaanisha shetani anataka/yuko tayari kukudhuru.unapoota unacheza na vichaa au watu wenye ukichaa pia inaashiria shambulizi la kiroho ili kukusambaratishia amani na utulivu.
39.WAHUNI:Unapoota umekimbizwa/umefukuzwa na wahuni,inaashiria nguvu za giza na wachawi wanajaribu kukuharibu(kukuua).
40.RUNGU:Niishara ya nguvu,pia inaashiria ukakamaavu  kiroho na ulinzi wa kiungu.
41.NDOA:Unapoona unafunga ndoa na mtu asiyemjua,inaweza kuashiria mume/mke wa kipepo (kama ni mtu unayemjua lakini ameao/ameolewa,ni ishara ya kufanya kosa kubwa/hatari katika ndoa.Kama ni mtu unayemjua vizuri na wote mko na vijana na kama huna tama za mwili kwake (naye)hiyo inaweza kuwa ishara ya mwenzi wa maisha.
42.MIMBA KUTOKA/KUHARIBIKA:Kama mwanake mjamzito ,umeota mimba imetoka/imeharibika,usilichuklie kirahisi,pasipo kuangalia ni nani aliyesababisha hilo,kwani linaweza kutokea kiuhalisia.
43.UCHI/KUVUA NGUO:Inaashiria aibu au fedheha .
44.SIMBA:Kama katika ndoto yako umeshambuliwa na simba na ukafanikiwa kumuua,inamaanisha umemshinda na kumua mtu aliyekuwa anataka kuharibu maisha yako.
45.BUNDI:Kuona bundi ndotoni inaashiria ubaya.ni taarifa kwamba kitu kibaya kitatokea/kinakwenda kutokea.
46.MTU ANAKUFUKUZA/ANAKUKIMBIZA:Kama katika ndoto yako umeota mtu unayemjua amekukimbiza akitaka kukua, mtu huyo anaweza kuwa hana mawazo/makusudi mazuri juu yako.Hata hivyo katika nyakati zingine wachawi hutumia sura ya mtu yeyote kulaghai,ilimradi tu ayaweke maisha yako hatarini.
47.NGURUWE:Ukijiona unacheza na nguruwe au hata kuwaona nguruwe ,huo ni uchafu kiroho,uzembe na kutokuwa makini katika maisha ya kiroho.
48.SHIMO:Inaashiria shetani ana mipango mibaya dhidi yako ili akuharibu.
49.KUCHEZWA NANYOKA:Hiki ni kuashiria kwamba umefungwa/unatawaliwa na Yule nyoka shetani.
50.KONOKONO:Inaashiria kudumaa na kuzuiliwa kwa (maendeleo)au kukua kwa mtu.
51.SHULE:Unapoota mara kwa mara kurudi shule kusoma au kuwa shuleni,inamanisha unahitaji (mafunzo)kupata/kupitia mafunzo ili kufanya vizuri katika taaluma yako au utumishi wako katika maisha.kurudi shule za chuni au madarasa inaashiria kudumaa,yaani badala au kupiga hutua mbele unaridi nyuma kimaendeleo.
52.NGONO:Kufanya mapenzi na mtu ambaye siyo mwenzi wako wa maisha ni njia ya kwanza inayothibisha kutawaliwa na tama ya mwili,pili inaweza kuwa  msukumo wa pepo kama unaendelea kufanya mapenzi na mtu usiyemjua.Roho ya uzinzi imeshakutawala.
53.MAJOKA:Inaashiria imetawaliwa na roho za majini au umeigia/umeingizwa kwenye agano hilo la mapepo/majini ya pwani baharini au mtoni.
54.NYOTA:Inaashiria ukuu.
55.MOSHI:Inaashiria shutuma na majaribu.
56.RADI:Kamakulikuwa na mvua kubwa iliyoambatana na mawe ngurumo na radi,inaashiria matatizo na kuchanganyikiwa siku za usoni.
57.KIJIJI:Unapoota kijiji chako mara kwa mara wakati wewe unaishi mjini hali hiyo inaashiria kuwa laana za mizimu zinajitokeza kukurudisha nyuma.
58.KUNGURU:Inaashiria kifo au mauti mbele yako.
59.PETE YA NDOA(1):Kama mwanandoa umeota unapoteza pete yako ya ndoa,inaweza kuonyesha/kuashiria unahitaji kuwamwangalifu sana (ndoa)pia inaashiria matatizo ya ndoa mbele yako.
60.PETE YA NDOA(2):Kama umepewa pete ya harusi ukiwa kijana,inaashiria kuolewa hivi karibuni,pia inaweza kumaanisha mtu (mhusika)ni mwenzi wako wamaisha
61.KUTEMBEA BILA VIATU:Inaashiria shetani anataka kukuchanganya kukupa aibu na hali ngumu (shida au taabu)
62.KUVIKWA TAJI:Inaonyesha utainuriwa katika kazi yeyote uliyoko au taaluma utafanywa kuwa kiongozi katika muda muafaka.
63.MAHAKAMA:Inaashiria kutoelewana baina yako na jirani zako,wadau wa biashara,ndungu au hata mkeo.
64.KUSHINDA KWENYE USHINDANI:Inaashiria habari nzuri na mpenyo kwako siku za usoni katika shughuli zako.
65.KUTOA/KUFUKUZA MAPEPO KWA  USHINDI:Unapoota unakemea mapepo na yakatii na kukimbia kwa jina la YESU inaonyesha ushindi juu ya adui yako,nguvu za mungu au upako na udhihirisho wakarama za Roho mtakatifu.
66.KUSHINDWA KUTOA MAPEPO:Kama unatoa pepo kwa jina la Yesu na hakuna kinachotokea unashiria udhaifu wa kiroho,uvivu wa kuomba na kukosekana kwa upako (nguvu za Roho mtakatifu)
67.WATOTO(1):Unapokuwa umeolewa au hujaolewa na unatafuta mtoto na kugundua kila ndoto zako una mtoto au kuona motto,inaashiria wake/waume wa kipepo,watoto hao ni wakipepo.
68.WATOTO(2):Unapo kuwa umeolewa na kujiona na mtoto mwingine,inaashiria kuwa utapata ujauzito karibuni.
69.KUENDESHA GARI LA GHARAMA:Inaashiria Baraka nzuri.
70.KUSHINDWA:Kama unashindwa vita ndotoni inaonyesha udhaifu wa kiroho na tayari uko kwenye mtego au wavu wa adui yako.
71.NYWELE ZENYE MVI:Inaashiria uzee,inaashiria utaishi maisha marefu.
72.MAANDISHI YA MKONO:Haijarishi kama yameandikwa kwenye ukuta au karatasi,kama maandishi hayo yako kwa muajibu wa biblia (fahamu kwamba Mungu anakupa maelekezo muhimu (taarifa muhimu).
73.UPONYAJI:Kupona ndotoni anaashiria tatizo(ugonjwa)lako limekwisha katika ulimwengu wa roho.uponyaji wa mwilini utathibitika kwa haraka.
74.BARUA/SIMU:Inaonyesha hivi karibuni utapokea ujumbe utakaobadilisha maisha yako,kwa uzuri au ubaya.
75.SIMBA:Kama katika ndoto anashambuliwa na samba na ukafanikiwa kumuua,inamaanisha umemshinda na kumua mtu aliyekuwa anataka kuharibu maisha yako.
76.NZIGE:Hii inaashiria/inaonyesha hasara na njaa.inaashiria mashambulizi ya aduii yako kwenye uchumi (fedha)yako,yaani umelengwa uwe duni/lofa.
77.WOSIA/MIRATHI:Inaashiria mauti/kifo,mazishi na shughuli za misiba kushamiri.
78.MAFUTA MEKUNDU/NGUO NYEKUNDU:Inaashiri hatari kwa mwanamke mjamzito inaashiria kuharibika kwa mimbi,kama umevaa mavazi mekundu (ndotoni)inadhihirisha pia matambiko ya kipepo.

==============================UBARIKIWE!============================
Pastor. AMOS E.ONESMO-0756391498