MTUNZI: REV.AMOS
SIMU/WHATSAPP: +255759199463
SOMO:
VITA DHIDI YA MAJIBU YAKO.
➖ Mpendwa kupokea majibu ya MUNGU maishani kuna vita katika ulimwengu wa Roho.
➖Mara nyingi Adui anakutegea kwenye wakati wako wa kupokea.
➖Adui anakuwekea vizuizi katika ulimwengu wa Roho ili usipokee, KATAA KWA JINA LA YESU.
➖MUNGU ANATUWAZIA MEMA.
👇👇👇👇👇
YEREMIA 29:11-12
[11]Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
[12]Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.
➖ Katika mapito yote, ukimlilia MUNGU yeye anasikia.
👇👇👇👇
KUTOKA 22:23
[23]Ukiwatesa watu hao katika neno lo lote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao,
➖MAJIBU YA DANIEL YALIKUTANA NA VITA KUBWA.
👇👇👇👇
DANIEL 10:11-13
[11]Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka.
[12]Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.
[13]Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.
➖ Mpendwa, komboa wakati wako wa kupokea.
➖Kuna Adui amekutegea siku ya kujifungua kwako, Siku ya kuanza KAZI katika Ofisi hiyo, Siku ya malipo yako n.k
➖KATAA MAJIBU YAKO KUCHELEWA.
➖VUNJA ROHO ZA VIZUIZI KATIKA MAISHA YAKO.
➖OMBA MUNGU AKUTUMIE MALAIKA WA KUKULETEA MAJIBU.
Barikiwa!!!
___________ Mwisho ___________
E-mail: pasteronesmo@gmail.com
+255759199463
+255625313609
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni