Jumatano, 25 Februari 2026

IMARISHA ASILI YA NGUVU ZAKO

MTUNZI: REV.AMOS

SIMU/WHATSAPP: +255759199463

SOMO:

IMARISHA ASILI YA NGUVU ZAKO.

➖ NGUVU ni uwezo wa utendaji wa jambo.

➖Kuna aina mbali mbali za nguvu kama vile:- 

       i. Nguvu ya kiuchumi

      ii. Nguvu za ki-mwili

      iii. Nguvu za KIROHO n.k


➡️Shetani ili akuharibu anatafuta kwanza ASILI ya nguvu ZAKO.

WAAMUZI 16:4-5

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

[4]Ikawa baada ya hayo akampenda mwanamke mmoja katika bonde la Soreki, jina lake akiitwa Delila. 


[5]Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.


➖ Samson alipelelezwa na Mke wake ili kujua ASILI ya nguvu zake nyingi.

➖ Shetani akifanikiwa kujua ASILI ya nguvu ZAKO amekuweza.


➡️Chanzo cha Nguvu za Samson kilipogundulika Samson aliteswa.


WAAMUZI 16:19-21

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

[19]Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka. 


[20]Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa BWANA amemwacha. 


[21]Wafilisti wakamkamata, wakamng’oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.


ASILI YA NGUVU YA MKRISTO.

1. KUHUDHURIA IBADA 

➖Kila ibada ina faida katika maisha ya MKRISTO.

➖ Katika ibada kuna jambo unapokea la kukutia NGUVU ili uweze kuendelea mbele.

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

WAEBRANIA 10:25

[25]wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.


2. MAOMBI MENGI NA MIFUNGO MINGI.

➖Kwa maombi tunapokea NGUVU za KIROHO.

➖Omba bila KUKATA TAMAA 

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

LUKA 18:1

[1]Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.


3. UJAZO WA ROHO MTAKATIFU.

➖Roho Mtakatifu ni NGUVU.

➖Omba kujawa Roho Mtakatifu maana yeye ni NGUVU.

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

MATENDO YA MITUME 1:8

[8]Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.


4. IMANI.

➖Imani ni NGUVU.

➖Kiwango chako cha imani ndiyo NGUVU yako ya KIROHO.


➡️AINA ZA IMANI.

a) Imani haba/Pungufu 

MATHAYO 8:26

[26]Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu.


b) Imani kias cha punje ya haradali.

MATHAYO 17:20

[20]Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.


c) Imani timilifu 

I WAKORINTHO 13:2

[2]Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.


d) Imani kubwa 

MATHAYO 15:28

[28]Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.



SWALI:

➡️Umebeba Imani ipi?


KUMBUKA:

➡️Imani yako, Nguvu yako


___________ Mwisho ___________

E-mail: pasteronesmo@gmail.com

+255759199463

+255625313609

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni