MTUNZI: REV.AMOS
SIMU/WHATSAPP: +255759199463
SOMO:
YESU NI SULUHISHO.
👇👇👇👇
*MAOMBOLEZO 3:25*
"BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao,
Kwa hiyo nafsi imtafutayo"
➡️Yesu ni MWEMA maishani mwetu.
➖Maisha ya mwanadamu yana changamoto nyingi zinazohitaji ufumbuzi.
➖Yesu huleta ufumbuzi wa changamoto za Maisha yetu.
➖Uwepo wa Yesu katika maisha yako ni ufumbuzi wa changamoto zako.
➖Mpe nafasi Yesu afanyike SULUHISHO.
➖Pale akili yako inapofika mwisho ndipo Neema ya MUNGU inapojidhihirisha kwako.
➖YESU NI SULUHISHO LA SHIDA YAKO, MPE NAFASI NA FUATA MAELEKEZO.
➖Uwepo wa Yesu katika Arusi ya KANA ulileta SULUHISHO LA DIVAI ILIPOISHA.
👇👇👇👇👇
*YOHANA 2:1-10*
[1]Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.
[2]Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.
[3]Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai.
[4]Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia.
[5]Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni.
[6]Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.
[7]Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu.
[8]Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka.
[9]Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,
[10]akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.
➖Fuata maelekezo ya Yesu afanyike SULUHISHO.
➖Mama wa Yesu (Mariam), aliwaeleza watu wafuate maelekezo atakayoyatoa Yesu ili kupata SULUHISHO LA DIVAI, nami nasema FUATA MAELEKEZO
➖YESU YUKO KARIBU YETU
👇👇👇👇
*YEREMIA 23:23*
[23]Mimi ni Mungu aliye karibu, asema BWANA, mimi si Mungu aliye mbali.
___________ Mwisho ___________
E-mail: pasteronesmo@gmail.com
+255759199463
+255625313609