MTUNZI: PASTOR AMOS E. ONESMO
MAWASILIANO: 0683676447 WHATSAPP: 0759199463
SOMO
KUFUTA ALAMA ZA KI-PEPO
Alama ni ishara ya jambo Fulani. Katika ulimwengu wa Roho mapepo, wachawi, majini yana alama zao. Mfano, chale ni alama za Ki-pepo zina ashiria mtu huyo kuna jambo la ki-shetani kafanya au kufanyiwa.
Kama watu wanaishi huku wamewekewa alama za ki-pepo za kuzuia mafanikio na kupona kwao. Ziko alama zinazoonekana kwa macho ya kawaida na zisizoonekana kwa macho ya mwili na nyama. kuna watu wanatembea huku wana alama ambazo waliwekewa kabla na baada ya kuzaliwa.
MWANZO 38:27-30
Katika andiko hili tunaona mtoto anazaliwa ana alama mkononi ya uzi mwekundu.
Alama za ki-pepo huashiria agano Fulani la giza. Na sisi wakristo tumeagizwa kutofanya agano lolote la giza.
KUTOKA 23:32
Alama ya ki-pepo humwangamiza mtu ila alama ya Ki-Mungu humwokoa mtu
MWANZO 4:15
Wengine wana alama za kufa maana wametolewa kafara /dhabibu kwa mashetani.
ZABURI 106:35-37
NAMNA YA KUFUTA ALAMA ZA KI-PEPO
1. ANZA NA TOBA
MATENDO YA MITUME 3:19
Omba Mungu akusamehe ili zirejee nyakati za kuburudishwa. Omba toba ya wazazi na watangulizi wako na ukoo mzima kwa ujumla
2. MAOMBI
ISAYA 41:21
Peleka mbele za Mungu hoja nzito za kufuta alama zote za ki-pepo. Fanya maombi ya vita.
HITIMISHO LA SOMO:
Futa alama za ki-pepo nyumbani kwako, Mwilini mwako, kazini kwako na mahali pengine pote ili ufanikiwe kiroho na kimwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni