SOMO LA
ROHO MTAKATIFU
I. UTANGULIZI
Tangu YESU Kristo alipofufuka na kupaa juu mbinguni hadi atakaporudi mara ya pili Roho Mtakatifu ndiye anayefanya kazi ulimwenguni na katika Kanisa. Yaani:-
1. Ni nguvu za Roho Mtakatifu zinazobadilisha maisha ya wenye dhambi kwa kuwawezesha kuokoka. Yoh 16:7-8
2. Ni Roho Mtakatifu anayelilea na kulifunza kanisa hadi YESU atapokuja kulichukua kanisa. Yoh 16:13
3. Uhai wa kanisa au kufa kwake, kukua na kudumaa vinategemea sana nafasi ambayo Roho Mtakatifu amepewa katika kanisa hilo.
II. ROHO MTAKATIFU NI NANI?
Biblia inafundisha mambo mawili kuhusu Roho Mtakatifu
a. Roho Mtakatifu ni Mungu
b. Roho Mtakatifu ni Nafsi
UFAFANUZI
A. ROHO MTAKATIFU NI MUNGU
1. UUNGU WA ROHO MTAKATIFU
Biblia inamfunua Mungu mmoja katika nafsi tatu yaani Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Mt. 28:19. Hivyo Roho Mtakatifu ni Mungu. Sababu.
a. Maandiko yanamueleza kuwa Roho Mtakatifu ni Mungu. Mdo 5:3-4
b. Roho Mtakatifu anaitwa Bwana 2kor 3:17 – 18 kut 3:15
c. Anafanya kazi pekee za Mungu anazozifanya. Mwa 1:2 → Roho ya Mungu. Ayu 33:4
d. Roho Mtakatifu ana tabia za Mungu
· Tabia za kipekee
- Wa milele Ebr. 9:14
- Yuko mahali pote wakati wote Zab. 139:7-10
- Anajua mambo yote anayoyajua Mungu. 1Kor. 2:11
- Ana uwezo wa kufufua. Rum 8:11
a. Ili Roho Mtakatifu afufue hali iliyo katika kufa
i. Apewe nafasi
ii. Kanisa lijazwe na Roho Mtakatifu Ef 5:18
B. ROHO MTAKATIFU NI NAFSI
Tunapoongelea habari za Nafsi ya Roho Mtakatifu tunamaanisha tabia zake za kiutu
TABIA ZA KIUTU ALIZONAZO
- Ana majina ya kiutu yanayomwelezea kupitia viwakilishi vilivyomo katika sura hii inadhihirisha kuwa ni mtu. Yoh 16:7-14
- Ana akili. 1kor 2:11, Rum 8:27
- Anayo nia (will) 1Kor 12:11, 2Petro 1:20-21 ni nia kwa kufanya atakavyo yeye
- Anaweza kuhuzunishwa. Efe 4:30 kwa sababu ana hisia. Hisia ni jambo lililomo ndani ya mtu linaloamshwa na tukio lolote. Kama tukio baya mtu anahuzunika na kama ni zuri anafurahi.
- Anaweza kudharauliwa Ebr 10:29
- Anaweza akapingwa. Mdo 7:51
- Ana uwezo wa kuhusiana, ushirika (Fellowship) 2Kor 13:14
- Anao uwezo wa kuongoza. Mdo 15:28-29
- Anazungumza au anaongea. Mdo 13:2-4
- Anaombea. Rum 8:26
III. HUDUMA YA ROHO MTAKATIFU KATIKA AGANO LA KALE
Agano la kale linaanza kwa kumtaja Roho Mtakatifu kuwa alihusika kikamilifu katika uumbaji
Katika Agano la kale Roho Mtakatifu aliwajaza watu kwa kuwapa uwezo wa kufanya jambo fulani ambalo Mungu alihitaji litendeke au lililokusudiwa na Mungu. Kut 28:3; 31:1-4; Hes 11:25; 24:1-3; Amu 14:6.
Hapo Samsoni alipewa uweza usio wa kawaida wa kumuua simba kwa mikono. Hapo Roho wa Mungu alimjia kwa nguvu.
v Kazi ya Roho Mtakatifu katika Agano la kale haikuwa ya kudumu kwa sababu aliweza kumjia mtu na akiisha kutekeleza makusudi yake alitoweka.
Kwa maneno mengine Roho Mtakatifu alikuja kwa huduma maalum na kwa wakati maalumu na pia aliweza kutoweka baada ya kutimiza kusudi la Mungu. Amu 16:20; ISam 10:10: 16:14.
Kwa maana hiyo ndiyo sababu kulikuwa na vyuo vya manabii 2Fal 2:3. Chuo cha Betheli of 6:1
2Fal 2:5 Chuo cha Yeriko
Kama jinsi ambavyo Roho Mtakatifu alivyokuwa akiwajaza watu katika Agano la kale ndivyo ambavyo hata sasa anatamani atujaze ili kutupa uwezo wa kufanya makusudi ya Mungu.
IV. HUDUMA YA ROHO MTAKATIFU KATIKA AGANO JIPYA
Tangu siku ya pentekoste tunaona kubadilika kwa kazi ya Roho Mtakatifu tofauti na ilivyokuwa katika Agano la kale. Huduma ya Roho Mtakatifu inakuwa kubwa kiutendaji kazi.
1. Roho Mtakatifu huwaleta wasioamini kwa YESU. Yoh. 16:8
2. Roho Mtakatifu hubadilisha mtu baada ya kuokolewa na YESU kristo. Efe 1:13; 4:30
3. Roho Mtakatifu humkamilisha mtu baada ya kuokolewa na YESU kristo. Efe 1:13; 4:30
4. Roho Mtakatifu hukaa, huishi ndani ya aliyemwamini YESU kristo Yoh 14:20
5. Roho Mtakatifu hututumia kutufanyisha au kututendesha mambo makubwa ya kuushangaza ulimwengu. Efe.3:20; Mdo 14:8; 3:1-6
V. UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU
Ikumbukwe kuwa Roho Mtakatifu ndiye anayewashauri wenye dhambi waokoke kupitia Neno la Mungu. Mtu anapomwamini YESU na kutubu dhambi zake hapo hapo Roho Mtakatifu huchukua nafasi na kukaa ndani ya mtu huyo.
Kitendo hicho cha Roho Mtakatifu kuingia na kukaa ndani ya aliyeamini kinaitwa UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU. Rum 8:8-10; Yoh. 7:37-40 Yoh 1:12
v Kitendo hicho hufanyika mara moja tu katika maisha ya mwanadamu
VI. UJAZO WA ROHO MTAKATIFU
Kujazwa na Roho Mtakatifu ni kitendo cha kuendelea katika maisha ya mkristo ili Roho Mtakatifu aendelee kutawala katika maisha ya mkristo. Na kitendo hicho hutokea pale mkristo anapotii. Efe 5:17-18; Mdo 2:1-4; 4:31.
VII. TOFAUTI KATI YA KUBATIZWA NA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU
1. Kila mkristo au kila aliyemwamini YESU kristo amebatizwa na Roho Mtakatifu, lakini si kila mkristo aliyejazwa na Roho Mtakatifu.
2. Ubatizo hutokea mara moja tu katika maisha ya mwamini, lakini ujazo ni kitendo kinachoendelea au kinachotokea mara kwa mara katika maisha ya muumini.
3. Katika ubatizo wa Roho Mtakatifu mkristo hahusiki katika jambo lolote, Roho Mtakatifu ndiye anayeshughulika lakini katika ujazo mkristo lazima ahusike au ajihusishe katika maombi na utii. Mdo 4:31.
4. Mkristo anayejazwa na Roho Mtakatifu mara kwa mara ana maisha yanayofananishwa na shamba linalopaliliwa mara kwa mara. Lakini mkristo asiyejazwa na Roho mtakatifu ana maisha yanayofananishwa na shamba lisilopaliliwa.
VIII. NAMNA YA KUJAZWA NA ROHO MTAKATIFU
Kuna njia tatu zinazomwezesha mkristo ajazwe na Roho Mtakatifu
1. Mkristo awe na hamu ya kujazwa Roho Mtakatifu. Mdo 1:4 Yoh. 4:14-15; 7:37-39
2. Mkristo awe mtu wa maombi. Mdo 1:12-14; Lk 18:1 Mdo. 4:31
3. Mkristo anapaswa aoneshe utii wakati wote. Efe 5:18 Amruhusu Roho Mtakatifu
IX. KWANINI TUJAZWE ROHO MTAKATIFU?
1. Mkristo anapaswa kujazwa ili tunda la Roho lionekane katika maisha yake Gal 5:22-23
Tunda la roho ni kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya maisha ya mkristo ili ampendeze Mungu. Tunda la roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi.
2. Mkristo anapaswa kujazwa na Roho Mtakatifu ili aweze kutumia karama za Roho Mtakatifu ili kujenga mwili wa kristo. Efe 4:11-12, Rum 12:4-13 1Kor 12:4-11
3. Mkristo anapaswa kujazwa na Roho Mtakatifu ili apate uwezo wa kumshuhudia kristo. Mdo 1:8
4. Ili apate uwezo wa kumshinda shetani. Amu 14:5-6, 2Ny 20:14-17,20-24
- Ni nguvu ishindayo vizuizi
- Ni nguvu ishindayo nguvu za giza
Yehoshafati alipovamiwa na kuonewa na nchi tatu alichokifanya aliitisha taifa lote wakafunga na kuomba na walipoomba Roho Mtakatifu alianza kuwaambia kuwa wasiogope maana vita si yao bali ni ya Mungu.
Na akaanza kuwapa maelekezo jinsi ya kushinda vita hiyo ambayo wasingeiweza.
X. MATOKEO YA KUJAZWA NA ROHO MTAKATIFU
Jambo hili linajibu swali; nawezaje kujua kuwa nimejazwa na Roho Mtakatifu?
1. Furaha. Efe 5:19a – kusemezana Fil 4:4; 2Kor 4:16
2. Sifa – kumsifu Mungu Efe 5:19b
Katika kumsifu Mungu kuliko jazwa na Roho Mtakatifu kuna miujiza ya ajabu, uponyaji na baraka ya ajabu kutoka kwa Mungu ISam 16:13-18
3. Kushukuru – Efe 5:20
Mkristo aliyejazwa Roho Mtakatfu amejaa shukrani mbele ya Mungu siku zote kwa mambo yote. Zab 50:23
4. Unyenyekevu – Efe 5:21
Jambo la msingi linalofundishwa hapa ni kuwa ikiwa wakristo watajazwa na Roho Mtakatifu hakika watanyenyekeana wao kwa wao.
Kunyenyekeana kunabeba maana ya kuheshimiana, kuthaminiana, kumwona mtu mwingine kuwa ni bora kuliko wewe.
UNYENYEKEVU UNAFASIRIWA KUWA
· Mungu
· Wengine katika YESU kristo
· Mimi
Hes 12:3 Musa aliwaona watu wengine kuwa bora
NB: Unyenyekevu si udhaifu, si kujidharau, si unyonge
5. Kupakwa mafuta (Anoints)
i. Upako ni uwezo au nguvu ya pekee anayopewa mtu na Roho Mtakatifu kwa ajili ya kusudi maalumu. Luka 4:18 Kwa mfano: utoaji wa wa mali zetu Lk 8:1-3
ii. Katika kifungu hiki YESU anaeleza bayana makusudi ya kupakwa mafuta na Roho Mtakatifu. Makusudi ikiwa ni kutenda kazi ya huduma ambayo alitumwa na Mungu. Mdo 10:38
iii. Kazi ya upako ni kusababisha matendo ya miujiza na uponyaji katika maisha ya mkristo. Yak 5:14
Matendo ya miujiza na uponyaji ni vya kila mkristo ambaye ameamua kujitoa mbele za Mungu na kuwa anajazwa mara kwa mara yaani awe mwenye hamu ya kujazwa awe mtii wa maombi na mwenye kutii kile aambiwacho na Roho Mtakatifu. Marko 16:17-18
XI. FAIDA ZA UJAZO WA ROHO MTAKATIFU Mdo 2:1-4
- Ishara na miujiza huonekana katika Huduma ya mtumishi. Mdo 3:1-7
- Waumini hawataogopa matisho ya maadui badala yake watafanya kazi ya Mungu kwa ujasiri mdo 4:31cf 4:1-10;7:51-60
- Roho mtakatifu atafunua uovu na dhambi kanisani mdo 5:1-11; 2fal 6:8-23
- Roho mtakatifu hutoa maelekezo ni jinsi gani ambayo unaweza ukashinda tatizo/jaribu lililokukabili 2 nya 20
- Pepo huanguka na kuondoka Mk 3:11
- Dhambi hukimbia na kuwa mbali nawe. Zab 103:12
Ukiona dhambi haitakí kukimbia na kuwa mbali nawe, ikimbie wewe
KM: Yusuph. Mwanzo 39:5.12
XII. KARAMA (UHAI WA KANISA)
Mungu huwapa wakristo vipawa ili vitumiwe kwa makusudi ya kufaidiana, kuinuana na kuujenga mwili wa kristo.
v Karama ni kazi ambazo Mungu alizozitoa alizowapa watu ili wazitumie au wazifanye na hatimaye aweze kuwabariki kupitia kazi hizo.
v Karama hizi zinaitwa UHAI WA KANISA na ziko kama tabia ndani ya maisha ya mtu. Na karama zote saba za Mungu kila mkristo anazo zote.
v Kwa kuwa ni za tabia na wapagani wanazo
Vipawa hivi vimegawanyika katika aina kuu tatu (3)
1. KARAMA ZA MUNGU NI ZA KUTENDA KAZI KATIKA KANISA RUM 12:4-8
Hivi vinaitwa vipawa vya tabia.
2. KARAMA ZA HUDUMA NI KARAMA ZA YESU
Vinaitwa vipawa vya kiofisi. Efe 4:10-13
3. KARAMA ZA MAFUNUO NI KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU
Ni karama za vitendea kazi katika huduma
UFAFANUZI
1. KARAMA ZA KUTENDA KAZI KATIKA KANISA RUM 12:6-8, Gol 6:7.10
Karama hizi huzitoa Mungu baba kwa wanakanisa ili kanisa liweze kufaidiana na kumtukuza siku kwa siku katika maisha yake, vipawa au karama hizi ni pamoja na:-
i. KARAMA YA UNABII
Ni uwezo wa kuhubiri au kufundisha Neno la Mungu katika nguvu ya Mungu na siku zote ujumbe unaotolewa ni sharti ukutane na mahitaji ya wasikilizaji. Ufu 19:10
ii. KARAMA YA HUDUMA (KUJITUMA)
Huu ni uwezo anaopewa mtu na Mungu kufanya kazi ya kumtukuza Mungu na kufanya kazi ya kanisa bila ya kupangiwa.
iii. KARAMA YA KUFUNDISHA
Ni uwezo anaopewa mtu na Mungu wa kufafanua, kulinganisha na kufunua maandiko ili yaweze kueleweka kwa urahisi ili wasikilizaji waweze kuelewa kwa urahisi
iv. KARAMA YA KUONYA
Ni uwezo mtu anaopewa na Mungu ili kuwashawishi wakristo wengine kufanya au kutofanya jambo fulani. Yoh 24:15
v. KARAMA YA UKARIMU
Ni uwezo wa kutoa kwa hiari kwa moyo na kwa furaha tena zaidi ya uwezo ili kuujenga mwili wa kristo pia hata kusaidia wengine. Luka 8:1-3; 1Fal 17:8-16
vi. KARAMA YA KUONGOZA (KUSIMAMIA)
Ni uwezo wa kuwa mfano wa kutangulia wa kufanya kazi ya Mungu pamoja na wengine ili kufanikisha jambo fulani.
Uwezo huo siku zote hukubalika na wale wanaoongozwa na kufanyika katika utaratibu unao wabariki wengi.
vii. KARAMA YA REHEMA
Ni jumla ya matendo ya huruma, matendo yaliyo zaidi ya wajibu wa siku zote.
Mfano. Mwizi au mchawi wanachukiwa na watu wengi lakini mwenye rehema huwa karibu naye ili amuondoe katika hali hiyo.
Kipawa cha rehema kimejaa upendo usio na sababu na unafanya hivyo kwa kumtukuza Mungu.
Wakristo wanamtumikia Mungu kupitia hizi karama kwa njia tofauti tofauti na Mungu amewapa wakristo uwezo usio wa kawaida kwa kutumia karama hizo na siku zote yanapofanyika hufanyika kwa faida ya kanisa.
Karama hizi zinaitwa UHAI WA KANISA na ni tabia ya maisha ya wakristo. Na zote 7 mkristo anazo zote. Kwa kuwa ni karama za Mungu na wasiookoka wanazo kwa sababu ni karama kama Tabia.
ROHO MTAKATIFU ANAPOJAZA WATU HUANZA KUSEMA NA WATU KUPITIA VINYWA VYAO: 2Nya 20:1-19
a. Yuda walipovamiwa na mataifa matatu Vs 1-2
i. Mfalme Yehoshafati alianza kuomba na Yuda yote wakiwa wamefunga Vs 3-13.
ii. Walipoomba Roho Mtakatifu alishuka na kuanza kusema kupitia katika kinywa cha Yahazieli Vs 14.
MAMBO ROHO ALIYOWAAMBIA WA YUDA
i. Bwana awaambia hivi msiogope wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili, kwani vita si yenu, bali ni vya Mungu. V 15
ii. Roho aliwapa maelekezo jinsi ya kufanya ili waishinde vita hiyo kubwa inayozidi uwezo wao.
v Nendeni mkakutane nao. V. 16
v Hamtahitaji kupigana vita jipangeni, simameni mkauone wokovu wa BWANA ulio pamoja nanyi wala msiogope na msifadhaike kwa kuwa BWANA yu pamoja nanyi. V 17.
v Wamsifu Mungu kwa wimbo wakisema, mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake ni za milele. Vs 21
MATOKEO BAADA YA KUFANYA KAMA ROHO ALIVYOSEMA
v Mungu aliwachanganya maadui wakaanza kuuana wao kwa wao. Vs 22-24
v Baada ya kushinda walianza kuteka nyara zao na zilikuwa mali nyingi. Vs 25
v Mahali walipopokelea ushindi pakaitwa Bonde la Baraka mpaka leo. Vs 26
v Walijawa na furaha na kumsifu na kumtukuza BWANA Vs 27-28
v Hofu ya Mungu iliwatiisha na kuwatetemesha falme zote za nchi zote zenye nguvu waliposikia kuwa Mungu amepigana juu ya adui za Israeli. Vs 29
v Ufalme wa Yehoshafati ukatulia kwa sababu Mungu wake alimstarehesha pande zote. Vs 30.
2. VIPAWA VYA HUDUMA – NI VIPAWA VYA YESU
Vinaitwa vipawa vya kiofisi. Efe 4:10-13
Hizi ni karama zinazotolewa na YESU kristo kwa watumishi ili kulijenga kanisa.
Watumishi hao sharti wawekewe mikono ya baraka yaani wanabarikiwa na viongozi husika wa ngazi za juu.
Ikumbukwe kuwa watumishi hao waweza kupewa sehemu mahali pa kusimamia kwa ajili ya utumishi huo na watatunzwa na kanisa. 1Kor 9:7-14
Watumishi hao uongozi husika unaweza kuwahamisha kuwatoa sehemu moja kuwapeleka sehemu nyingine.
a. UTUME
Huduma ya utume katika mtazamo wa Agano jipya ina maana ya mtumishi wa YESU kristo mwenye mamlaka ya juu katika kuliongoza kanisa, baadhi ya sifa za utume:-
i. Aliyetembea na YESU, aliyeshuhudia matendo ya YESU. Mdo 1:21-22
ii. Awe mwenye mamlaka katika uongozi wake
iii. Utume unaandamana na ishara na miujiza. Mark 16:17-18
iv. Wanaotumwa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine (wamisionari)
b. UNABII
Huu ni uwezo wa kuhubiri au kufundisha Nenno la Mungu katika nguvu isiyo ya kawaida yaani nguvu ya Roho Mtakatifu
v Msemaji anasema kama Mungu, hana mzaha
c. UINJILISTI
Huu ni uwezo usio wa kawaida anaopewa mtu kulihubiri Neno kwa ufasaha na kuwavuta watu kwa YESU. Na mara zote mwenye karama ya uinjiisti anapohubiri huwavuta watu kuja kwa YESU.
Mwenye karama ya uijilisti anapohubiri mahubiri yake yamejaa utisho na watu wanakuwa na hofu maishani na mara zote watu watatubu, ijapo baadhi hutubu kwa sababu ya hofu.
d. MCHUNGAJI NA MWALIMU
Vipawa hivi ni uwezo wa kufafanua Neno la Mungu ili lieleweke kwa wasikilizaji.
Mchungaji anajali, anatunza, anasaidia na anahakikisha wakristo wanaendelea katika mambo ya kiroho.
v Mchungaji asiyejua kufundisha huyo si mchungaji
v Mwalimu asiye na huruma ya uchungaji huyo hana kipawa cha ualimu
v Mchungaji anayejali lazima aangalie kundi lake.
*MFANO: Mfugaji wa ng’ombe anajali malisho ya mifugo yake na malazi na afya na kuwalinda maadui
v Hivyo mchungaji lazima ajali:-
v Wakristo anaowaongoza
v Aangalie mahitaji yao
v Aangalie matatizo ya washirika na kuyatatua
v Anatafuta jinsi ya kushibisha kundi lake
Atafute watu wenye karama wafundishe ili kuhudumia kwa upana mahitaji ya kanisa.
NB: Utume, Unabii, Uinjilisti na Ualimu, karama hizi ni za watu maalumu, walio na wito kweli wa Mungu, kwani hukutana na matatizo mengi ya kiroho, kiuchumi.
HITIMISHO: Kanisa wasipowatunza baadhi hutoroka kazi ya BWANA na wengine huingiwa na tamaa ya kupata pesa za aibu. 1Tim 6:10-11
3. KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU – 1KOR 12:7-11
ZINAITWA KARAMA ZA MAFUNUO
ZINAITWA KARAMA ZA VITENDEA KAZI
Ziko karama 9 zinazotolewa na Roho Mtakatifu kwa kanisa. Karama hizi ni tofauti na karama zingine
v Zinatolewa kama roho apendavyo yeye mwenyewe 1Kor 12:11
v Zinasaidia utendaji kazi karama za Mungu na YESU na si za kudumu
Si za kudumu kwa kuwa karama hizi mtu hawezi kusema kuwa hii ndiyo karama yangu. Kwa sababu zinatenda kazi kwa muda kulingana na hitaji lililopo, kwa kuwezesha karama za Mungu na YESU.
KARAMA ZENYEWE
A. NENO LA HEKIMA
Huu ni uwezo anaopewa mtu na Roho Mtakatifu wakati mgogoro, tatizo linapotokea katika kanisa ili kutoa mwongozo au utatuzi wa shida hiyo. 1Fal 3:16-28; 4:29-30.
B. NENO LA MAARIFA (UTAMBUZI)
Huu ni ufahamu anaopewa mtu na Roho Mtakatifu kuhusu mambo fulani au hali ambayo imefichika lakini anaifunua 2fal. 5:20-27 (26) of mdo 5:1-11.
C. IMANI
Huu ni uwezo anaopewa mtu na Roho Mtakatifu uzidio ule ulio wa lazima kwa ajili ya wokovu. Uwezo huu ni ule wa kumwona Mungu akitenda mambo makubwa ya ajabu
Km: Petro atembea juu ya maji
v Uponyaji na imani vimeambatana
D. UPONYAJI
Karama za uponyaji ni uwezo anaopewa mtu na Roho Mtakatifu na kuutumia katika kuponya magonjwa mbalimbali katika jina la YESU.
Aliyepewa karama hii anaponya magonjwa yote, anaweza kuombea mgonjwa akapona hapo hapo au akapona kwa baadaye.
Mf. YESU alitema mate akafanya udongo akampaka mtu akamwambia nenda ukaoge silowamu.
v Magonjwa mengi yanayoponywa na karama hii ni yale yaliyoshindikana.
E. MIUJIZA
Ni matendo ya nguvu ya Roho Mtakatifu yanayotokea wakati wa hitaji maalumu. Mdo 3:1-10
F. UNABII
Ni uwezo ulio wa hali ya juu sana ambao unapitia katika aina za lugha na anaweza kufasiri au mtu mwingine akatumiwa katika kufasiri. Mdo. 2:5-13.
G. KUPAMBANUA ROHO
Ni uwezo wa kujua kama maneno au mambo fulani yanayoendelea katika kanisa kama yanatoka kwa Mungu ama kwa Shetani.
v Karama hii ndio kiini cha karama zote
===========================MWISHO============================
Kwa swali lolote na sadaka wasiliana nami kwa namba
0789994583
0786302099
0766274392
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni