Jumatano, 29 Septemba 2021

UKOMBOZI WA NYAYO

 

 

MTUNZI: PASTOR AMOS E. ONESMO

MAWASILIANO: 0683676447 WHATSAPP: 0759199463

SOMO: UKOMBOZI WA NYAYO

Nyayo ni sehemu ya chini ya mguu wa mwanadamu.

Katika ulimwengu wa Roho nyayo huashiria utawala. Kila tunapokanyaga kwa nyayo tunamiliki. kwa hiyo kuna muunganiko kati ya mafanikio ya mtu na nyayo.

KITABU CHA JOSHUA 1:3

KUMBUKUMBU LA TORATI 11:24

Nyayo za mtu zikichukuliwa kichawi ina maana mtu huyo amepoteza utawala hivyo atatawaliwa na wachawi badala ya kutawala.

Wachawi hufuatilia nyayo za watu na  kuwafunga ili wasifanikiwe. Ili ufanikiwe tumia jina la Yesu kukomboa nyayo zako.

NYAYO ZA MWANADAMU ZINAWEZA:

1.      Kufuatiliwa

ZABURI 56:6

Wachawi wanafuatilia nyayo za mtu ili wamuzuilie mafanikio

 

2.      Kunaswa

ZABURI 57:6

Miguu ya Mwanadamu ikinaswa nyayo zimenaswa. Kuna watu wanaishi huku nyayo zao zilishanaswa. Tumia jina la Yesu kuzinasua popote zilikonaswa.

 

3.      Kushikamana na kuzimu

MITHALI 5:5

Hatua za mtu ndiyo nyayo za mtu. Wachawi wanaweza kuzishikamanisha nyayo zako na kuzimu kichawi. Nyayo zikishikamana na kuzimu unakuwa umeshawekwa chini ya utawala wa kuzimu. Yaani mafanikio yako huamriwa na kuzimu.

 

NAMNA YA KUKOMBOA NYAYO ZAKO

1.      Ita nyayo popote zilikowekwa ili zirejee.

2.      Tumia jina la damu ya Yesu kuziondoa nyayo zako kila sehemu zilikowekwa kichawi.

 

HITIMISHO LA SOMO

Katika maombi yote, Kumbuka kuwa mkamilifu kwa BWANA Mungu wako

KUMBUKUMBU LA TORATI 18:13

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni