Jumamosi, 5 Juni 2021

MWANAMAOMBI MZALENDO KWA TAIFA LAKE

 

WANAMAOMBI TANZANIA

 

“Tanzania bila Maombi inaangamia”

KONGAMANO LA KANDA “F” MKOANI SINGIDA

09-11/06/2021

SOMO LA KITAIFA

MWANAMAOMBI MZALENDO KWA TAIFA LAKE

UTANGULIZI

Taifa  -    Ni watu wanaoishi pamoja, wenye lugha moja, Utamaduni mmoja na Utawala mmoja.

-Katika Taifa kuna mfumo wa Utawala unaowaongoza watu ili waweze kufikia malengo      yao kimaisha ili waifurahie Nchi yao.

                MWANZO 11:6

Mwanamaombi

           - Ni mtu anayepeleka mahitaji mbele za MUNGU siku kwa siku.

           - Ni mtu anayemkumbusha BWANA siku kwa siku.

               ISAYA 62:6

Uzalendo

           -Ni tabia/hali ya kuipenda Nchi yako kwa moyo wako na kuwa tayari kuitumikia bila  kutegemea faida yoyote binafsi.

            -Ni tabia ya kujali maslahi ya Umma na kutumia nafasi yako kuleta maendeleo

Mwanamaombi mzalendo

            -Ni mtu anayejitoa kwa Nchi yake kuibeba kimaombi bila kujali maslahi binafsi.

-Mwanamaombi mzalendo kwa Taifa lake hayuko tayari kuona shetani akilitesa na kuliburuza Taifa lake katika nyanja mbalimbali kama vile Uchumi.

DANIEL 3:15-18

           Shadrack, Abednego, Meshack walioonesha Uzalendo wao kwa Taifa lao.

           Mwanamaombi mzalendo hapaswi kunyamaza kwa ajili ya Taifa lake.

 

SIFA ZA MWANAMAOMBI MZALENDO

        i.            Yuko tayari kutubu na Kuiombea Nchi yake.

Mwanamaombi mzalendo haoni ugumu wowote kutubu kwa dhambi ya Nchi yake. Mwanamaombi mzalendo anachokitazama ni kupona kwa Nchi yake.

2MAMBO YA NYAKATI 7:14-15

Mfano wa Wanamaombi wazalendo kwa Nchi zao

a.   Daniel

DANIEL 9:1-6

Daniel alitubu kwa ajili ya Taifa lake baada ya kusoma historia ya Taifa lake. Mwanamaombi mzalendo hawezi kunyamaza anapoiona historia mbaya ya Taifa lake.

b.   Esta

KITABU CHA ESTA 4:15-16

Esta alitambua uponyaji wa Taifa lake ni kupitia Maombi. Mwanamaombi mzalendo huyu aliagiza maombi yafanyike kabla ya mambo yote ili uponyaji wa Taifa lake utokee. Baada ya Maombi alijitoa mhanga. Esta alisema, “……….nitaingia kwa Mfalme kinyume cha Sheria; name nikiangamia, na niangamie”.

Tujitoe Mhanga ki-maombi kwa ajili ya Taifa letu Tanzania.

 

      ii.            Hupenda kuona Taifa lake likiwa salama.

Mwanamaombi mzalendo yuko tayari kufanya maombi kwa ajili ya watu wote wa Taifa lake. Moyo wa uzalendo wa mwanamaombi humfanya asihesabu gharama ya kuliombea Taifa, kiu yake ni kuona Taifa likiwa salama.

                ITIMOTHEO 2:1-6

                KITABU CHA NEHEMIA 12:30

 

    iii.            Hushirikiana na Wanamaombi wengine Wazalendo kwa maslahi ya Taifa.

Mwanamaombi mzalendo hajitengi na Wanamaombi wengine wazalendo. Huungana nao bila kujali DINI wala Kabila kwa maslahi ya Taifa lake.

               MITHALI 18:1

     iv.            Hahesabu gharama ya Maombi.

Mwanamaombi mzalendo kwa Taifa lake yuko tayari kubeba gharama ya maombi kwa ajili ya Taifa lake. Atatoa muda wake, mali zake (PESA), Nguvu ili kufanikisha maombi ya kuliombea Taifa.

 

SIFA ZA MWANAMAOMBI ALIYEKOSA UZALENDO.

Si kila Mwanamaombi ni mzalendo kwa Taifa lake. Wengine ni Wanamaombi wenye mzigo na Agenda zingine kama vile familia, Uchumi, Ndoa n.k

Zifuatazo ni baadhi ya Sifa za Mwanamaombi aliyekosa Uzalendo kwa Taifa.

        i.            Majivuno

Hana utayari wa kushirikiana na wengine ki-maombi yeye huona ni bora kuliko wengine. Huwahesabu wengine si watu sahihi wakushikamana nao.

MITHALI 18:1

      ii.            Kutowajibika ipasavyo

Mwanamaombi asiyemzalendo hujali sana mambo binafsi kuliko maombi ya kuliombea Taifa. Huyapa kipaumbele majukumu binafsi kuliko Maombi.

FAIDA YA MAOMBI YA UZALENDO.

        i.            MUNGU hutufunulia yaliyositirika(yaliyojificha) katika Taifa

MATHAYO 10:26

      ii.            Tunapata Neema ndani ya Taifa.

Mfano. Amani tuliyonayo Tanzania ni Neema

ZABURI 147:8

    iii.            Nchi hubarikiwa

KUMBUKUMBU LA TORATI 28:1-8

    iv.            Shetani hukosa nafasi ya kupitisha mipango yake katika Taifa.

 

HITIMISHO LA SOMO

Ø  Tuombe kwa bidii kuwa na moyo wa uzalendo kwa Taifa letu ki-maombi, ili kuzibomoa madhabahu mbali mbali za Ki-pepo zilizojengwa Tanzania na Watawala wa Nchi.

2WAFALME 21:1-3

Ø  Kwa moyo wa uzalendo tutawakomboa wote waliotolewa KAFARA kwa Mashetani katika Taifa letu Tanzania.

ZABURI 106:35-37

Ø  Tukikosa uzalendo kwa Nchi yetu, MUNGU ataiponya Tanzania kwa namna nyingine ila OLE! itakuwa kwetu sisi Wanamaombi Tanzania.

KITABU CHA ESTA 4:13-14

Ø  Kila Mwanamaombi Mzalendo asimame katika nafasi yake.

HABAKUKI 2:1

!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! MWISHO !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

BARIKIWA SANA

Limeandaliwa na

PASTOR AMOS E. ONESMO

MKURUGENZI TAIFA

HUDUMA YA WANAMAOMBI TANZANIA

0759199463/0683676447

E-mail: pasteronesmo@gmail.com

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni