UTANGULIZI.
Kipekee namshukuru Mungu kwa kuniwezesha
kuandaa Kitabu hiki kiitwacho:-
“KULA USHIBE”.
Pia, namshukuru Mke wangu ANES na Mwanangu GIFT Kwa mchango wao muhimu
katika kukamilisha kazi hii.
Shukrani zangu za dhati zimwendee Mama
yangu mzazi JOYCE kwa kunizaa na kunilea.
Ndugu msomaji wa kitabu hiki
nakukaribisha sana tujifunze masomo sita muhimu, ambayo ni:
1. KUAMINIWA NA MUNGU
2. BADILI LUGHA YAKO UFANIKIWE
3. MAAMUZI.
4. SAFARI YA MAFANIKIO.
5. KUAMBATANA/KUENDANA.
6. ROHO ZITENDAZO KAZI
Nakuombea Mungu akupe Uelewa mkubwa na
akufanikishe zaidi na za zaidi.
Kwa swali lolote, Ushauri na mengineyo
wasiliana nami.
Mawasiliano: 0756391498/
0658727799/ 0683676447
@
2019
SOMO: KUAMINIWA
NA MUNGU
Kuaminiwa
ni kupata kibali/kuweka imani
kamili juu ya jambo fulani au mtu.
Mungu
alimwamini musa na kumbebesha jukumu maalumu la
kuwatoa wana wa Mungu utumwani.
KUTOKA 3:4-10
Musa
alipata kibali machoni pa Mungu kama musa alivyoaminiwa na Mungu, nasi pia Mungu ametuamini ili tuitende kazi yake bila kutoa udhuru kama aliotaka
kutoa musa.
Ili kuaminiwa na Mungu tunatakiwa kujitakasa,Musa
baada ya kusogelea kijiti kinachowaka Mungu alimwambia avue viatu ikiwa ni
ishara ya kutakaswa.
Tunapojitakasa
ndipo tunapopata kibali cha kuaminiwa na Mungu ili tuitende kazi yake,Musa aliaminiwa na Mungu kuwatoa watu MISRI.
VIPINGAMIZI/VISABABU
VYA MUSA ILI KUTAKA
KULIPINGA
KUSUDI LA MUNGU.
Musa
alitaka kulikwepa kusudi la Mungu baada ya kuaminiwa naye. Wapo watu
wanaojaribu kulikwepa kusudi la Mungu pale wanapoaminiwa na yeye.
Tufuatane
pamoja kuziona sababu za musa
1.Alijidharau
Musa
alijiona kuwa hasitahiri kusimama mbele ya
farao kumweleza habari ya kuwaruhusu wana wa Israeli alijiona hafai wakati ameaminiwa na Mungu
Mpendwa
ukiaminiwa na Mungu usijidharau kwa
sababu yoyote ,msikilize Mungu.
KUTOKA 3:11
2.Alitengeneza
maswali yasiyo na sababu
Musa
alijitengenezea maswali mengi yaliyo lenga kupinga agizo/kusudi la Mungu kuwatoa
wana wa Israeli utumwani kama vile :- “nao
wakiniuliza jina lake ni nani? Niwambie nini?”
KUTOKA 3:13
Pia,
wapo watu wa aina hii Mungu anapowaamini
na kuwapa jukumu huanza kutengeneza
maswali kama hayo.
i)Nitaanzaje?
ii)Nitaishije?
3. Mashaka
ndani yake
Ndani
ya musa iliumbika roho ya hofu katika kulibeba kusudi la Mungu baada ya
kuaminiwa.
KUTOKA 4:1
Wapo
watu wanapoaminiwa na Mungu wanashindwa kulitumikia kusudi la Mungu kwa sababu
ya hofu/roho ya mashaka.Jiepushe na hali
hiyo uitende kazi ya Mungu kama ulivyoaminiwa.
4.Ulimi mzito
Mungu
alimwamini musa huku akijua kuwa anaulimi mzito
(kigugumizi) musa alitaka kutumia udhaifu huu kulikwepa kusudi. Mungu amekuamini hivyo hivyo bila kujalisha udhaifu
ulionao wewe simama kwa Mungu wako
uitende kazi yake.
KUTOKA 4:10
5. Kukosa
utayari
Wapo
watu hawapo tajari kulitumikia kusudi la Mungu kwa sababu tu hawako
tajari.wengine huisi maisha yao yataharibika,watakosa muda wa utafutaji n.k.
Musa
alikosa utayari,akamtaka Mungu amwagize mtu mwingine na si yeye.
KUTOKA 4;13
6..Alihitaji
mtu wa kusimama naye
Kuna
watu katika utumishi hawataki kusimama peke yao
hutaka kusimama kwa miguu ya watu
wengine . Mungu anapokuamini mpendwa simama tu,Mungu atakuwa pamoja nawe hata kuacha usiruhusu HASIRA ya Mungu kuwaka
juu yako.
KUTOKA4:14-17
Hitimisho la somo
Mungu
anapokuamini hupaswi kuweka sababu ili
usilitekeleze kusudi la Mungu.
LUKA 14:16-24
…………+………+Barikiwa
mno……….+………………+……………
SOMO:
BADILI LUGHA YAKO UFANIKIWE
Lugha
ya mtu huamua maisha ya mtu.Atamkavyo mtu ndiyo nafsi hujengwa na kisha kuamua maisha yake.kile kitokacho ndani ya
kichwa cha mtu, ndicho huamua
maisha yake kuanzia rohoni hadi mwilini.
MITHALI 28:7a
Lugha
hujenga fikra(mawazo)ya mtu.
*Fikra
ni nini?
i)Ni jinsi aonavyo mtu.
ii) Ni kiwango cha kufikiri cha mtu.
iii)Ni maisha ya mtu.
*Shetani
akitaka kuharibu maisha yako ya kiroho na ya kimwili kwenye nafsi kwa maneno ya kinywa.
HATUA ZA KUKUFIKISHA KWENYE MAFANIKIO
Mafanikio
ni hatua njema ya mtu ambayo hupitia ngazi mbalimbali.
1.Jitathmini ili
kujitambua zaidi, kujitathmini ni kujikagua na kujijua kwa kina juu ya mikakati
mbalimbali kuelekea kwenye mafanikio.
WAFALME 4:1-7
Mwanamke
alijitathmini baada ya kifo cha mmewe
akaona kupungukiwa .
·
Jitathmini ili kutambua kwa usahihi msaada unaohitaji
·
Jitathmini ili kutambua
msaada unaohitaji unaupata kwa
nani?
2.Weka mkakati kwa kumshirikisha Mungu.
Weka
mikakati iliyo ndani ya uwezo wako na
inayofikika. Ni afadhari kuwa na mikakati
michache iliyo ndani ya uwezo wako kuliko kuwa na mikakati mingi isiyofikika.
MITHALI 3:5
3.
Kuwa mwaminifu
Ili ufanikiwe
ni lazima utengeneze mazingira ya kuamini kwa
(a)Watu
(b)Mungu
Hakikisha
katika mapato yako unakuwa mwaminifu kwa
kutoa sehemu ya kumi ya mapato yako, Pia
shughuli zako zisikufanye usahau ibada.
ZABURI 51:6 MATENDO
YA MITUME 5;1-11
4. Omba
sana kuliko kulalamika ,Tumia muda mwingi kuombea shughuli / kazi za mikono
yako kuliko kulalamika na
(a)Kujilaumu
(b)Kumlaumu
mwingine/ kuwalaumu wengi
LUKA 18:1 YEREMIA 29:11
Hitimisho la somo
Lugha
yako itaamua maisha yako.
……………..*…………BARIKIWA……………….*……….
SOMO:
MAAMUZI/DECISION
Maana
Maamuzi ni uwingi wa neno uamuzi linalomaanisha kukata shauri juu ya jambo/kitu Fulani.
Uamuzi
wowote wa mtu aliyeokoka
unatakiwa kumhusisha Mungu maana
yeye hutupa akili
kwa kila jambo. 2 TIMOTHEO 2:7
Uamuzi huamua kesho ya mtu
AINA ZA MAAMUZI
Ziko
aina kuu mbili za maamuzi
ambazo ni
i)Maamuzi sahihi
ii)Maamuzi yasiyo sahihi
I.MAAMUZI
SAHIHI
Hii ni
aina ya maamuzi inayomfanya
mtu atende jambo
jema na si
baya.
Mfano:kuamua
kumsamehe mtu .MATHAYO 6:14
II. MAAMUZI
YASIYO SAHIHI
Hii ni
aina ya maamuzi anayoyafanya mtu na
hatimaye huleta majuto/jambo baya.
Mfano:
Uamuzi wa mtu kuvunja ndoa n.k
MATOKEO
YA MAAMUZI
Yako matokeo makuu mawili ambayo
ni
i)Matokeo mazuri/Raha
ii)Matokeo mabaya/ majuto
MAMBO YA
MUHIMU WAKATI WA KUFANYA MAAMUZI
1.Jitambue
wewe ni nani unayefanya maamuzi
Tambua wewe
ni wa kristo na siyo wa shetani. Usifanye maamuzi
kama vile mtu wa mataifa. Ukijujua wewe ni nani utafanya maamuzi
sahihi
2 WAKORINTHO
13:5
2. Tumia akili
nzuri
Akili ni
ufahamu juu ya
jambo fulani na
si ubongo. Kutumia akili
humaanisha kuwa na
ufahamu mkubwa juu
ya matokeo ya
maamuzi yako unayoenda
kufanya
1 PETRO 4:7
3.Fikiri kwa
uzito na kutenda kwa
HEKIMA
Kufikiri kwa
uzito humaanisha kuwa
na tafakari nzito
juu ya jambo/mambo
yanayohitaji kufanya maamuzi.
Waswahili husema
“fikiri kabla ya
kutenda” kufikiri kwa kina
kutakupa maamuzi yenye
ujasiri na akili ya
Mungu itakuongoza
2 TIMOTHEO 1:7
ISAYA 55: 8-7
4.Mhusishe Mungu
katika maamuzi yako
Kila jambo tunalolifanya
tunatakiwa kutozitumia akili
zetu badala yake
tumtumaini Mungu.
MITHALI 3:5
5.Imarisha
nia ya kufanya mema
Kama
mkristo unatakiwa kukusudia
mema katika maamuzi
yetu na si
kukusudia kutenda mabaya.
WAFILIPI 2:13
WARUMI 7:18
Hitimisho la
somo
Fanya maamuzi
yenye kuleta utukufu
na si kuumiza /kuuwa nafsi
za watu au wewe
mwenyewe .
Maamuzi mabaya
huleta roho ya
usugu na mbaya
ndani ya mhusika.
…………………………………………BARIKIWA………………………………
SOMO: SAFARI
YA MAFANIKIO
Mafanikio
- Ni hali ya
kufikia hatima njema
ya malengo ya
mtu.
Mafanikio ni
safari lazima tuyatafute
Katika safari
hii ya mafanikio
tambua kuwa nchi na vyote
viijazavyo ni mali
ya BWANA
ZABURI 24:11
Mmiliki
wa mali zote ni Mungu ili upate mafanikio ni lazima
umwangalie na umwombe
yeye mtoaji.
Mafanikio yatokanayo na njia
isiyo sahihi HAYADUMU.
MAMBO MUHIMU
YA KUKUMBUKA KATIKA SAFARI
YAKO YA MAFANIKIO.
1.Mungu ndiye
mmiliki wa kila kitu
na ndiye mtoaji
Ujuzi na
juhudi zako ni
muhimu sana katika
kufikia malengo yako. Lakini
kumbuka kwamba mafanikio
hayo Mungu ndiye
anayetoa.
2.Ukimwambia Mungu unachohitaji
atakujibu.
Amini
na tambua kuwa Mungu
anajibu ukimwaomba Mungu
anaweza asijibu utavyotaka wewe, lakini
kwa kuwa anatujua
kabla ya kuzaliwa
ana mawazo mema
juu yetu hicho
alichokunyima ni faida
yako.
1 WAFALME 2:3
Njia pekee
ya kupokea jibu
lako ni kuwa
na Imani na
uwezo wa Mungu. Amini
anaweza kabla ya
yote
3. Kuwa Baraka
kwa wengine
Ili ufanikiwe
usiwe mchoyo. Mungu
anakubariki ili na wewe
uwe Baraka kwa
wengine
2 WAKORINTHO
9:8-11
WARUMI 12 :13
4.Fanya kazi
kwa Bidii
Fanya kazi
hata kama ni ndogo kiasi
gani fanya kwa moyo
wako wote
MITHALI 12;11
ZABURI 90:17
Hitimisho la
somo
Kwa kila hatua
kumbuka kumshirikisha Mungu
na umpe yeye
nafasi ya kwanza
usiyaabudu mafanikio yako, mwabudu
Mungu pekee.
Mwamini Mungu
kwanza na hayo
mengine utazidishiwa.
SOMO: KUAMBATANA/KUENDANA
KUSHIKAMANA,GANDAMANA,BILA
KUACHANA.
Watu tuliokoka tunapaswa kushikamana. Mambo madogo
madogo ya kipuuzi
hutufanya tushindwe kuambatana.
WIMBO ULIO BORA 2:15
Ukosefu
au kupoa kwa upendo katika watu hufanya tushindwe kuambatana na kugombana sisi kwa sisi.
WAKORINTHO
13:1
Chuki
ni chanzo cha kushindwa kuambatana
VYANZO VYA CHUKI
·
Ubinafsi
·
Wivu
Chimbuko la chuki ni SHETANI.
MAMBO
MAKUU KATIKA KUFANIKIWA KWA KANISA.
Siri
ya kufanikiwa kwa kanisa siyo vipawa
bali ni mambo makuu matatu(03)
·
Utii
·
Uaminifu
·
Kuambatana
TABIA SABA ZA
MTU ALIYEACHA KUAMBATANA/ TABIA SABA (07) ZA KUELEKEA UASI
1.Roho ya kujiamulia mwenyewe.
Yaani
mtu anafanya kile anachojisikia tu na
huamua chochote atakacho
2 SAMWEL
3:20-21
2.Kujikwaa na
kukwazika
Hii
ni tabia ambapo mtu kila jambo/mara kwa mara yeye hukwazika tu na kalalamika
MATHAYO 24:10
3.Kutojihusisha
na lolote
Mtu
huyu hufanyakazi kwa ulegevu maana hufanya kile ajisikiacho ,Hii ni laana
YEREMIA 48:10
4.Kukosoa
Mtu
aliyeacha kuambatana hujiweka kwenye hali ya kukusoa na kutafuta makosa
mbalimabali katika ibada ,kiongozi wake
n,k
Mfano:
*Miriam
alianza kumkosea musa
HESABU
12:1
·
Absalam alianza kuyaona makosa ya
uongozi wa Daud
2
samwel 15:3
5.Hatua
ya kisiasa
Wasioambatana
na viongozi wao huwa wanapenda
kujiulizisha maswali.
Mfano:
Unayaonaje mahubiri ya leo?Ibada umeionaje?
6.Kudanganyika.
Aliyeacha
kuambatana huwa mwepesi wa kudangnyika.
YOHANA 8:44
Ni
hatua mbaya pale mtu anapo danganyika na kumsema vibaya kiongozi wake au Baba
yake wa kiroho.
MITHALI 30:17
7.Uasi
wa wazi wazi
Hii
hupelekea kupambana ana kwa ana na mamlaka iliyo juu yao
Mfano:
Musa
alipigwa waziwazi na KORA, DATHANI, ABIRAM na
wengine viongozi 250
HESABU 16:1-4
Hitimisho la
somo
·
Tujifunze kuwa na Amani na watu wote
WAEFESO
4:31-32
·
Ufalme wa Mungu unatekwa na watu
wenye nguvu.
MATHAYO
11:12
--------------*------------------------BARIKIWA--------------*-------------
SOMO: ROHO ZITENDAZO KAZI
Roho
- Ni nafsi inayofanya kazi katika ulimwengu wa roho.
Kuna
roho kuu tatu:-
i)Roho ya Mungu
(Roho mtakatifu)
ii)Roho ya
binadamu
iii)Roho ya
kishetani
I.ROHO
YA MUNGU (ROHO MTAKATIFU)
Hii
ni nafsi ya tatu ya Mungu inayotenda
kazi ndani ya watakatifu wote. Kila aliyeokoka anapaswa kujazwa nguvu hii ya Roho mtakatifu
MATENDO YA MITUME 1:8
1 WAKORINTHO 12:14
II.ROHO
YA KIBINADAMU
Hii
ni roho ambayo huyajua mambo ya binadamu tu
I WAKORINTHO
2:11a
Roho ya kibinadamu inabeba mapenzi na mawazo ya
kibinadamu.
Pia,
wakati mwingine manabii wa Mungu wanaweza
wakatoa unabii , lakini siyo utokao kwa Mungu bali ni wao wenyewe.
YEREMIA
23:21-23
III.ROHO YA
KISHETANI
Hii
ni Roho inayowaongoza watu kutenda mambo ya kipepo/maovu tu. Kama vile
uchawi/kuua/ubakaji n.k
MATENDO
YA MITUME 16:16,
IYOHANA
4:1a,
ITIMOTHEO 4:1a
Hivyo
tunapaswa kuzipima/kuzijaribu Roho. Kipimo kikuu cha kuzipima/kuzijaribu roho
ni NENO LA MUNGU maana hili hutusaidia kupambana na roho
WAEBRANIA
5:14,
WAEBRANIA 4:12-13
Neno
la Mungu ndiyo kiini cha maarifa yote
ZABURI
119:89
ZABURI 119:97-100
ZABURI
119:104-105
Neno
la Mungu ndilo linalotufanya tusiyumbishwe na kila aina ya upepo wa Elimu
WAEFESO
4:13-15
Hitimisho
la somo
Tamani
sana kuongozwa na roho wa Mungu na zikatae
kwa nguvu zote Roho chafu na zitiishe
kabisa.
…………………………………………BARIKIWA………………………………
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni