Na
Pastor AMOS E. ONESMO
Mawasiliano:
0756391498/ 0658727799/ 0683676447
@
2019
UTANGULIZI.
Kipekee namshukuru Mungu kwa kuniwezesha
kuandaa Kitabu hiki kiitwacho:-
“ONDOKA KIFUNGONI”.
Pia, namshukuru Mke wangu ANES na Mwanangu GIFT Kwa mchango wao muhimu
katika kukamilisha kazi hii.
Shukrani zangu za dhati zimwendee Mama
yangu mzazi JOYCE kwa kunizaa na kunilea.
Ndugu msomaji wa kitabu hiki
nakukaribisha sana tujifunze masomo Matano muhimu, ambayo ni:
1. VIFUNGO VITOKANAVYO NA MILA
2. AGANO LA KITOVU
3. ROHO YA KIBURI.
4. UKOMBOZI WA ARDHI.
5. MADHABAHU ZA UKOO.
Nakuombea Mungu akupe Uelewa mkubwa na
akufanikishe zaidi na za zaidi.
Kwa swali lolote, Ushauri na mengineyo
wasiliana nami.
Mawasiliano:
0756391498/ 0658727799/ 0683676447
@
2019
SOMO LA KWANZA
VIFUNGO
VITOKANAVYO NA MILA
UTANGULIZI
Mila ni kawaida ya mtu au jamii Fulani. Mila ni
taratibu zenye miiko za watu/jamii Fulani. Mfano: Mila ya kunyoa vipara kwa
ajili ya wafu.
Mila zisizompendeza Mungu ni chanzo cha vifungo vya
kiroho na kimwili kwa watu wengi. Kupitia mila watu wamejiunganisha na mizimu
ya ukoo/familia iliyobeba mila hizo. Mila zisizofaa hubeba nguvu ya mizimu
inayopelekea vifungo. Mila hugeuka chanzo cha vifungo maana baadhi ya mila zina
Maagano yake ambayo zimebeba SIRI kubwa.
MIFANO
YA MILA ZILETAZO VIFUNGO
1.
Kunyoa Vipara
Kwa Ajili Ya Wafu.
KUMBUKUMBU LA TORATI 14:1
Huu ni utaratibu wa jamii nyingi za waliookoka na
wasiookoka hususani jamii za kiafrika. Kuna madhara makubwa yatokanayo na mila
hii, maana moja kwa moja ni kujiambatanisha na mzimu wa marehemu. Ndiyo maana
wengine baada ya msiba hupata matatizo mengi kama vile ndoto mbaya za kumuota
marehemu, magonjwa n.k.
2.
Kuabudu
Waliokufa.
KUMBUKUMBU LA TORATI 18:10-11
Hii ni mila nyingine isiyompendeza Mungu inayofanywa
na watu wengi. Hizi ni ibada ya kutambikia na kutoa kafara kwa ajili ya jambo
Fulani ili mizimu ya marehemu iwasaidie.
Jiulize swali hili, “Tunapaswa kwenda kwa waliokufa
kwa ajili ya walio hai?
ISAYA 8:19
Mila ni ibada isiyompendeza Mungu. Mila huambatana
na sadaka za miungu ile inayosimamia mila hizo.
MUHIMU: Tambua chanzo na dhumuni ya mila hiyo katika
familia yenu. Usikimbilie kufanya mila bila kujua chanzo na madhumuni
utajiunganisha na Maagano ya mila bila kujua, na madhara yake yatakuwa makubwa.
MADHARA
YA KUJIUNGANISHA N AMILA ZISIZOFAA
i.
Kukutenga mbali
na Mungu.
Hautakuwa
na ushirikiano na Mungu maana hizo ni Ibada za mizimu
ii.
Mikosi, laana
vitaambatana nawe.
Shetani
atakushambulia katika maeneo mbalimbali kama vile uchumi, maana hauna ulinzi wa
Yesu.
NJIA ZA
KUVUNJA KIFUNGO CHA MILA
1. Omba toba ajili yako na familia yenu.
Takasa kwa maombi ili kufuta madhara yatokanayo
na vifungo vya mila.
2. Rejesha kilichoathirika katika maisha yako.
Kilichotetereka kama ni Afya au uchumi rejesha
kwa upya kwa njia ya maombi.
YOELI 2:25
3. Futa kwa damu ya Yesu madhara yatokanayo na
mila.
4. Mfukuze shetani aliyekaa katika ukoo wenu
kwa njia ya MILA.
HITIMISHO: Usile vyakula vitokanavyo na sherehe za kimila, hii ni
kwa sababu vyakula vile
hutamkiwa
maneno ya kishetani (Agano).
MITHALI 23:8
.xxxx MAARIFA
HIYO JUU YA MILA IKUFUNGUE VIFUNGO …….xxxx
SOMO LA PILI
AGANO LA KITOVU
Agano ni patano/mkataba baina ya mtu na mtu/watu na watu/jamii na
jamii.
Kitovu ni kiunganishi cha mama na mtoto awapo tumboni. Yaani alacho
mama ndicho alacho mtoto aliyetumboni.
Kama Agano la kishetani linalofanywa kupitia kitovu. Agano hili
humpa shetani uhalali wa kuyatesha maisha ya mtu.
Tulitazame Agano hili la kitovu kwa namna mbili:-
i)
Kuunganishwa na
Agano la kipepo la wazazi.
Hii ina maana kwamba, mtoto anarithi baadhi ya matatizo yatokanayo
na wazazi wake. Kinachowapata wazazi ndicho mtoto anachopata, ugonjwa uliotesa
wazazi hutesa na mtoto pia n.k. EZEKIEL
16:4-6
Kitovu kutokatwa ni ishara ya uwepo wa mambo endelevu yatokanayo na
wazazi wako. Kuna vitu vinakuathiri kwa sababu umerithi kutoka kwa wazazi.
Kitovu kukatwa ni ishara ya kujitenga na maagano ya wazazi wako, na
ni muhimu sana kujitenga.
ii) Agano juu ya kitovu kiuhalisia
Yaani kitovu cha mtoto kinawekwa katika maagano ya kutamkiwa,
kutambikiwa n.k baada ya kukatwa. Kuna
baadhi ya watu wanapata mateso kwa sababu baada ya kuzaliwa, vitovu vyao
viliwekewa MAAGANO.
Maagano hayo yamefanyika kwa:-
Ø Kutambikiwa
Ø Kunuwiziwa
Ø Kuhifadhi ndani ya nyumba.
Ø Kutupwa bahari
Ø Kutupwa (kufukiwa) makaburini n.k
DALILI
ZA KITOVU KILICHOFUNGIWA AGANO
-
Mashambulizi ya
kitovu kwa njia ya ndoto.
Unakuta mtu anaota ndoto zenye kushambulia kitovu
kama vile kuchomwa sindano, kisu au mkuki kwenye kitovu kwanjia ya ndoto.
-
Kufuatiliwa na
majanga miaka hadi miaka.
HATUA ZA
KUCHUKUA ILI KUWA SALAMA
Ø Kuokoka
Ø Wokovu utakuweka huru kabisa
Ø Kuombewa maombi ya kukata kitovu.
……….………..xxxx… Pokea Maarifa
Ya Kiroho xxxx……………………….
SOMO LA TATU
ROHO YA KIBURI
Kiburi ni hali ya mtu kujiinua na kutoondoka kwenye msimamo wake
hata kama ni msimamo hasi.
Roho ya kiburi ni kifungo kwa waliowengi kwani roho hii imewafunga
waliowengi kiroho na kimwili. Kuna watu wameshindwa kufanikiwa kwa sababu ya
kiburi watu wamepoteza marafiki, ndugu, huduma kwa sababu ya Roho ya kiburi.
Kataa roho ya kiburi kwani ni kifungo cha mafanikio yako kiroho na
kimwili. KUTOKA 5:2
Mtu mwenye roho ya kiburi huona kila anachokiwaza kimenyooka wala
hawezi kusikiliza ushauri wowote kwa mtu yeyote. MITHALI 12:15
Roho ya kiburi ilimponza rusifa
ISAYA 14:12-15
TABIA 10
ZA MTU MWENYE KIBURI
1.
Hupenda
kusikilizwa ila yeye hapendi kusikiliza wengine.
KUTOKA 5:2
2.
Hapendi
kushauriwa na wengine ila yeye anapenda kushauri wengine.
MITHALI 29:1-2
3.
Hapendi
kukosolewa ila yeye anapenda kukosoa kwa kila jambo.
MITHALI 13:10
4.
Hupenda kudharau
wengine lakini yeye hapendi kudharauliwa.
WAKOLOSAI 3:13-14
MITHALI 14:21
5.
Hudai heshima
kwa nguvu lakini yeye hataki kuheshimu wengine.
MITHALI 3:34-35.
Kiburi cha mtu kitamshusha, Bali mwenye roho ya
unyenyekevu ataheshimiwa.
MITHALI 14:15
6.
Hufurahi
kuwaonea wengine na kuwasimanga lakini yeye hataki kuonewa wala kusimangwa.
OBADIA 1:12
7.
Hupenda kumiliki
mali isiyo yake.
Ndugu hata fungu la kumi ni la Mungu hivyo kuacha
kutoa zaka ni kumwimbia Mungu na hivyo ni roho ya kiburi.
MALAKI 3:8-9
8.
Anapenda kulaumu
wengine ila yeye hapendi kulaumiwa.
9.
Anapenda kutiwa
moyo lakini yeye hawezi kuwatia moyo wengine.
10.
Hupenda
kujulikana na hapendi wengine wajulikane.
MAANDIKO
MACHACHE YAHUSUYO ROHO YA KIBURI
I SAMWELI 2:3 “Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; majivuno
yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, na matendo hupimwa
na yeye kwa mizani”.
MITHALI 13: 10 “Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao
wanaoshauriana”.
MITHALI 15:25 “Bwana ataing’oa
nyumba ya mwenye kiburi; Bali atauthibitisha mpaka wa mjane”
MITHALI 29:23 “Kiburi
cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa”
MITHALI 16:5 “Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa Bawna;
Hakika, hatakosa adhabu”.
Hitimisho
La Somo
Ni muhimu kuikemea roho ya kiburi, maana Mungu huwapinga wenye
kiburi. I PETRO 5:5-7. Mungu
huwaangalia wenye roho ya kupondeka ISAYA 66:2. Tumwombe Mungu atupe Roho
ya unyenyekevu tunapomtumikia ili tuyaone mema kutoka kwa Mungu. WAFILIPI 2:3-5
SOMO LA NNE
SOMO: UKOMBOZI WA ARDHI
UTANGULIZI
Somo hili linalenga kujifunza
mbinu za kuomba ili hali ya kiroho ya Ardhi iliyokwamisha mafanikio yako
iondoke ili uweze kufanikiwa. Ardhi inatoa maamuzi juu ya watu wanaokaa juu
yake kwa kutegemea imekabidhiwa kwa Mungu yupi.
-
Mungu wa Ardhi
huamua mafanikio ya mtu.
Ardhi inaweza kuolewa na kuzaa matunda kutegemea Mungu aliyeioa.
ISAYA 62:4-5 “Hutaitwa tena aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, ukiwa;
bali utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula; kwa kuwa Bwana anakufurahia, na nchi
yako itaolewa.
Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana
wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi harusi.
Ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe”.
Ardhi haiwezi kuzaa pasipo kuolewa na kuzaa huko kunategemea
Mungu/mungu aliyeioa ardhi hiyo.
Ardhi inaweza kuwa haizai kwa sababu ya LAANA. Ukisemesha Ardhi
inaweza kuzaa hata kama haizai kwa ajili ya watu wengine.
Ardhi inaweza kutiwa unajisi na kuwatapika wenyeji.
MAMBO YA WALAWI 18:24-25
Nchi ikiwa najisi kwa sababu ya wanadamu, Mungu anaachilia adhabu
juu ya nchi na nchi inaanza kuzaa mapooza 2
WAFALME 2:19-22
Ardhi inao uwezo wa kusikia, kutunza kila ilichokisikia na
kutekeleza kile ilichosemeshwa.
KUMBUKUMBU LA TORATI 30:19-20
Ardhi inasikia maneno ya kinywa. Ukiitamkia mabaya inasikia na
ukiitamkia mazuri inasikia na kutekeleza.
KUMBUKUMBU LA TORATI
32:1 YEREMIA 22:29-30
Unaweza kufanya eneo kwenye Ardhi kuwa sehemu ya kukutana na Mungu
wako.
Madhabahu ya Mungu inajengwa na Yakobo katika Ardhi ili pawe
ukumbusho wa Agano.
MWANZO 28:16-22
“16 Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, kweli Bwana yupo
mahali hapa, wala mimi sikujua.
17 Naye akaogopa akasema, mahai hapa panatisha kam anini: Bila
shaka hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.
18 Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe
aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina
mafuta juu yake.
19. Akaita jina la mahali pale Betheli, lakini jina la mji ule hapo
kwanza aliiitwa Luzu.
20. Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami,
akinilinda katika njia niiendayo na kunipa chakula nile, na nguo nivae.
21 Nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana
atakuwa Mungu wangu.
22. Na jiwe hili nililosimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya
Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakulea wewe sehemu ya kumi”
Alama unayoiweka kwenye Ardhi ni ukumbusho wako na Mungu wako. MWANZO 35:6-7
Ardhi ina uwezo wa kumuondoa mtu na kumlinda mtu aliye juu yake.
Haijalishi kama unajua au haujui kawaida ya miungu/Mungu wa mahali unapokaa,
kama ukikosea utashambuliwa/ utapigwa na Mungu/miungu.
2 WAFALME 17:24-28
Mapepo
yanaweza kumilikishwa Ardhi na yakadai kisheria kuwa na uhaliali wa kuwepo
mahali pale walipomilikishwa.
MARIKO 5:1-10
Msitari wa 10 “Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile” Mapepo yalitaka yasipelekwe nje ya utawala
wao.
NAMNA YA
KUOMBA ILI HALI YA KIROHO YA ARDHI ILIYOKWAMISHA MAENDELEO YAKO IPATE KUONDOKA.
1.
Tambua Mungu wa
Ardhi hiyo
Elewa kwa makini masharti yaliyopo katika Ardhi yatokanayo na mungu wa
eneo.
2 WAFALME 17:24-29
2.
Omba toba juu ya
Ardhi ili Mungu aiponye.
2 NYAKATI 7:12-14
Andiko hili halizungumzii uponyaji wa watu bali
uponyaji wa Ardhi.
3.
Futa laana juu
ya Ardhi
Futa laana zilizosababishwa na dhambi za
waliotangulia, n.k
MWANZO 3:17-19
Dhambi ya Adamu ilipelekea Ardhi kulaaniwa.
Shughulikia laana iliyo katika Ardhi kwa Damu ya
Yesu.
4.
Weka wakfu kwa
Mungu eneo hilo.
Mkabidhi Mungu hilo eneo. Mungu anataka umakabidhi
rasmi ili alitawale eneo hilo.
5.
Jenga madhabahu
ya Bwana katika eneo MWANZO 28:16-22
Hitimisho la somo
Unaweza kuwa kwenye eneo linalomilikiwa na shetani kihalali katika
ulimwengu wa giza, hivyo usiridhike pambana kiroho.
;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;MWISHO
WA SOMO;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;
SOMO LA TANO
SOMO: MADHABAHU ZA UKOO
Madhabahu – Ni eneo
linaloweza kutumiwa na Mungu au shetani/miungu ili kupitisha nguvu, utawala na
mamlaka kwa watu wanaokusanyika mbele yake.
Ni sehemu maalumu ya kukutana na Mungu.
Katika Ukoo mtu anaweza kuwa
ndiye madhabahu ya ukoo.
MATENDO YA MITUME 16:17-24
Aliyetolewa mapepo alikuwa ni
MADHABAHU ya eneo.
Kamwe watu hawawezi kufanya
jambo Fulani bila kumuuliza kwanza aliye MADHABAHU ya eneo. Kama vile kugombea
nafasi za uongozi.
Madhabahu ya miungu na ya
Mungu hujengwa na mwanadamu mwenyewe.
Mifano Kibiblia ya waliojenga
Madhabahu
Ø Familia/ukoo wa Nuhu watu walikuwa wamebadilika kwa
kutenda maovu, Mungu akaamua kuondoa uharibifu huo kwa kupitia Nuhu. Nuhu akamjengea Mungu Madhabahu. MWANZO 8:15-22
Ø Abrahamu alimjenga Mungu Madhabahu. MWANZO 12:7
Ø Yoshi alimjenga BWANA Madhabahu. WAAMUZI 6:25-26
Familia/koo haiwezi kwenda
mahala popote kama mfumo wao wa maisha, umeshikiliwa kwenye MADHABAHU YA
KICHAWI/KISHETANI.
Inawezekana familia /ukoo umeshikiliwa na mfumo wa madhabahu, ndiyo maana matatizo
ya ukoo wako yanafanana.
Ø Kwenye ndoa
Ø Katika masomo
Ø Katika mafanikio
WAAMUZI 6:24
Gideoni kabla ya kuibomoa
Madhabahu ya Baba yake alijenga Madhabahu ya Baba yake akaiita jina la Jehova
Shalon (Maana yake Mungu wa Amani) familia yake imepata Amani.
Ni vizuri kujua kwamba, je
madhabahu unayokwenda kuabudu unamjua anayeabudiwa hapo? Kila Madhabahu kuna
Mungu anayeabudiwa hapo.
KAZI YA MADHABAHU
Madhabahu ya kimiungu na
Mungu zina kazia kama ifuatavyo:-
i.
Kutoa majibu ya
malalamiko ya watu na kutoa ufumbuzi.
Madhabahu za
kimiungu hutoa ufumbuzi usiosahihi
Madhabahu za
ki-Mungu hutoa ufumbuzi sahihi.
ii.
Kutatua matatizo
ya watu wa eneo
Madhabahu za
kimiungu huongeza matatizo badala ya kuyatatua.
Madhabahu za
Ki-Mungu huleta majibu ya matatizo ya watu wa eneo.
MUUNDO WA MADHABAHU
KINACHOTEGEMEWA NA MADHABAHU
|
MADHABAHU YA KI-MUNGU
|
MADHABAHU YA KI-MIUNGU/SHETANI
|
i. Mungu wa madhabahu
|
Mungu
|
Shetani/mapepo/mizimu
|
ii.
Nguvu ya
madhabahu
|
Nguvu za Ki-Mungu
|
Nguvu za kipepo mizimu/majini
|
iii.
Sadaka ya
madhabahu
|
Sadaka
|
Kafara (Kumwaga damu)
|
iv. Kuhani wa madhabahu.
|
Wachungaji/watumishi mbali mbali wa
kiroho
|
Waganga wa kienyeji /Wachawi na mawakala
wengine wa Shetani
|
Hitimisho la somo
Jenga madhabahu ya Ki-Mungu
katika ukoo wenu ili kuiangusha ile ya Ki-Miungu inayoleta madhara mengi katika
ukoo kama vile vifo vinavyofanana, kufuatana, magonjwa ya kufanana, tabia za
kufanana n.k.
0759199463
nimefarijika sana kwa somo hilo la kufuta laana ya ukoo
JibuFuta