Jumatatu, 11 Machi 2019

GHALA LA MAARIFA YA KIROHO



SOMO:
KUAMINIWA NA MUNGU
-Kuaminiwa ni kupata  kibali/kuweka imani kamili   juu ya jambo fulani au mtu.
-Mungu alimwamini musa na kumbebesha jukumu maalumu la  kuwatoa wana wa Mungu utumwani.
KUTOKA 3:4-10
Musa alipata kibali machoni pa Mungu kama musa alivyoaminiwa na Mungu, nasi pia  Mungu ametuamini ili  tuitende kazi yake  bila kutoa udhuru kama   aliotaka  kutoa musa.
-Ili  kuaminiwa na Mungu tunatakiwa kujitakasa,Musa baada ya kusogelea kijiti kinachowaka Mungu alimwambia avue viatu ikiwa ni ishara ya kutakaswa.
-Tunapojitakasa ndipo tunapopata kibali cha kuaminiwa na Mungu ili tuitende kazi yake,Musa  aliaminiwa na Mungu kuwatoa watu MISRI.
VIPINGAMIZI/VISABABU VYA MUSA ILI  KUTAKA
KULIPINGA KUSUDI LA MUNGU.
Musa alitaka kulikwepa kusudi la Mungu baada ya kuaminiwa naye. Wapo watu wanaojaribu kulikwepa kusudi la Mungu pale wanapoaminiwa  na yeye.
Tufuatane pamoja kuziona sababu za   musa
1.Alijidharau
Musa alijiona kuwa hasitahiri kusimama mbele  ya farao kumweleza habari ya kuwaruhusu wana wa Israeli alijiona hafai wakati  ameaminiwa na Mungu
Mpendwa ukiaminiwa na Mungu  usijidharau kwa sababu yoyote ,msikilize  Mungu.
KUTOKA 3:11
2.Alitengeneza maswali yasiyo na sababu
Musa alijitengenezea maswali mengi yaliyo lenga kupinga agizo/kusudi la Mungu kuwatoa wana wa Israeli utumwani kama vile :- “nao  wakiniuliza jina lake ni nani? Niwambie nini?”
KUTOKA 3:13
Pia, wapo watu wa aina hii  Mungu anapowaamini na kuwapa jukumu  huanza kutengeneza maswali kama hayo.
i)Nitaanzaje?
ii)Nitaishije?
3. Mashaka ndani yake
Ndani ya musa iliumbika roho ya hofu katika kulibeba kusudi la Mungu baada ya kuaminiwa.
KUTOKA 4:1
Wapo watu wanapoaminiwa na Mungu wanashindwa kulitumikia kusudi la Mungu kwa sababu ya hofu/roho ya mashaka.Jiepushe na  hali hiyo uitende kazi ya Mungu kama ulivyoaminiwa.

 4.Ulimi mzito
Mungu alimwamini musa huku akijua kuwa anaulimi mzito  (kigugumizi)  musa  alitaka kutumia udhaifu  huu kulikwepa kusudi. Mungu  amekuamini hivyo hivyo bila kujalisha udhaifu ulionao wewe simama kwa Mungu  wako uitende kazi yake.
KUTOKA 4:10

5. Kukosa utajari
Wapo watu hawapo tajari kulitumikia kusudi la Mungu kwa sababu tu hawako tajari.wengine huisi maisha yao yataharibika,watakosa muda wa utafutaji n.k.
Musa alikosa utayari,akamtaka Mungu amwagize mtu mwingine na si yeye.
KUTOKA 4;13

6.Alihitaji mtu wa kusimama naye
Kuna watu katika utumishi hawataki kusimama peke yao  hutaka kusimama kwa miguu  ya watu wengine . Mungu anapokuamini mpendwa simama tu,Mungu atakuwa pamoja nawe  hata kuacha usiruhusu HASIRA ya Mungu kuwaka juu yako.
KUTOKA4:14-17

            Hitimisho la somo------------------
Mungu anapokuamini hupaswi kuweka sababu za kutoa ili  usilitekeleze kusudi la Mungu.
LUKA 14:16-24
………………………+………+Barikiwa mno……….+………………+……………

SOMO:
BADILI  LUGHA  YAKO UFANIKIWE
-Lugha ya mtu huamua maisha ya mtu.Atamkavyo mtu ndiyo nafsi  hujengwa na kisha  kuamua maisha yake.kile kitokacho ndani ya kichwa cha mtu, ndicho  huamua maisha  yake kuanzia rohoni hadi mwilini.
MITHALI 28:7a
-Lugha hujenga fikra(mawazo)ya mtu.

*Fikra ni nini?
i)Ni  jinsi aonavyo mtu.
ii) Ni  kiwango cha kufikiri cha mtu.
iii)Ni  maisha ya mtu.

*Shetani akitaka kuharibu maisha yako ya kiroho na ya kimwili kwenye  nafsi kwa maneno ya kinywa.
HATUA  ZA KUKUFIKISHA KWENYE
MAFANIKIO
Mafanikio ni hatua njema ya mtu ambayo hupitia ngazi mbalimbali.
1.Jitathmini  ili  kujitambua  zaidi ,kijitathmini  ni kujikagua na kujijua kwa kina juu ya mikakati mbalimbali  kuelekea kwenye mafanikio.

WAFALME 4:1-7
Mwanamke alijitathmini baada ya kifo cha mmewe  akaona kupungukiwa .
·         Jitathmini  ili kutambua kwa usahihi  msaada unaohitaji
·         Jitathmini ili  kutambua  msaada unaohitaji  unaupata kwa nani?

  2.Weka mkakati kwa kumshirikisha Mungu.
Weka mikakati iliyo ndani  ya uwezo wako na inayofikika. Ni afadhari kuwa na mikakati  michache iliyo ndani ya uwezo wako kuliko kuwa na mikakati  mingi isiyofikika.
MITHALI 3:5

3.      Kuwa mwaminifu
Ili ufanikiwe ni lazima utengeneze mazingira ya kuamini kwa
(a)Watu
(b)Mungu
Hakikisha katika mapato yako  unakuwa mwaminifu kwa kutoa  sehemu ya kumi ya mapato yako(10), Pia   shughuli zako zisikufanye usahau ibada.
ZABURI 51:6
MATENDO YA MITUME  5;1-11
4. Omba sana kuliko kulalamika ,Tumia muda mwingi kuombea shughuli / kazi za mikono yako kuliko kulalamika na
(a)Kujilaumu
(b)Kumlaumu mwingine/ kuwalaumu wengi
LUKA 18:1
YEREMIA 29:11
Hitimisho la somo
Lugha yako itaamua maisha yako.
……………..*…………BARIKIWA……………….*……….

SOMO:
MAAMUZI/DECISION
Maana
Maamuzi  ni uwingi wa neno uamuzi  linalomaanisha kukata shauri  juu  ya  jambo/kitu Fulani.
-Uamuzi wowote  wa mtu  aliyeokoka  unatakiwa kumhusisha  Mungu  maana  yeye  hutupa  akili  kwa kila  jambo.
2 TIMOTHEO  2:7
-Uamuzi  huamua kesho ya mtu
AINA ZA MAAMUZI
Ziko aina kuu mbili  za  maamuzi  ambazo ni
i)Maamuzi  sahihi
ii)Maamuzi  yasiyo sahihi
I.MAAMUZI   SAHIHI
Hii ni aina ya  maamuzi  inayomfanya  mtu  atende  jambo  jema  na  si  baya.
Mfano:kuamua kumsamehe mtu .MATHAYO  6:14
II. MAAMUZI  YASIYO SAHIHI
Hii ni aina ya  maamuzi  anaoufanya mtu  na  hatimaye  huleta  majuto/jambo baya.
Mfano: Uamuzi  wa mtu  kuvunja ndoa n.k

MATOKEO  YA  MAAMUZI
Yako  matokeo makuu mawili  ambayo  ni
i)Matokeo  mazuri/Raha
ii)Matokeo  mabaya/ majuto
MAMBO  YA  MUHIMU WAKATI   WA  KUFANYA
MAAMUZI
1.Jitambue wewe ni nani  unayefanya  maamuzi
Tambua  wewe  ni wa kristo na siyo   wa  shetani.Usifanye  maamuzi  kama vile mtu wa mataifa.Ukijujua wewe ni nani utafanya  maamuzi  sahihi
2 WAKORINTHO  13:5
2. Tumia  akili  nzuri
Akili  ni  ufahamu  juu  ya  jambo  fulani  na  si  ubongo. Kutumia  akili  humaanisha  kuwa  na  ufahamu  mkubwa  juu  ya  matokeo   ya  maamuzi  yako   unayoenda  kufanya
1 PETRO  4:7
3.Fikiri  kwa  uzito  na kutenda  kwa  HEKIMA
Kufikili  kwa  uzito  humaanisha  kuwa  na  tafakari   nzito  juu  ya  jambo/mambo  yanayohitaji   kufanya maamuzi.
Waswahili  husema  “fikiri  kabla  ya  kutenda”kufikiri  kwa  kina  kutakupa  maamuzi  yenye  ujasiri  na  akili ya  Mungu itakuongoza
2 TIMOTHEO 1:7
ISAYA  55: 8-7
4.Mhusishe  Mungu  katika  maamuzi  yako
Kila jambo  tunalolifanya  tunatakiwa  kutozitumia  akili  zetu  badala  yake  tumtumaini Mungu.
MITHALI 3:5
5.Imalisha nia ya kufanya  mema
Kama mkristo   unatakiwa  kukusudia  mema  katika  maamuzi  yetu  na  si  kukusudia  kutenda  mabaya.
WAFILIPI  2:13
WARUMI  7:18
Hitimisho  la  somo
Fanya  maamuzi  yenye  kuleta  utukufu  na  si  kuumiza /kuuwa  nafsi  za watu  au  wewe  mwenyewe .
Maamuzi  mabaya  huleta  roho  ya  usugu  na  mbaya  ndani  ya  mhusika.
…………………………………………BARIKIWA……………………………………..
SOMO:
SAFARI  YA  MAFANIKIO
Mafanikio- Ni  hali  ya  kufikia  hatima  njema  ya  malengo  ya  mtu.
Mafanikio  ni  safari  lazima tuyatafute
Katika  safari  hii  ya  mafanikio  tambua kuwa  nchi  na vyote  viijazavyo  ni  mali  ya  BWANA
ZABURI  24:11
-Mmiliki wa mali zote   ni  Mungu ,ili upate  mafanikio  ni lazima  umwangalie  na  umwombe  yeye  mtoaji.
-Mafanikio   yatokanayo na  njia  isiyo   sahihi
HAYADUMU.
MAMBO  MUHIMU  YA  KUKUMBUKA  KATIKA
SAFARI  YAKO  YA  MAFANIKIO.
1.Mungu  ndiye  mmiliki  wa kila  kitu  na  ndiye  mtoaji
Ujuzi  na  juhudi  zako  ni  muhimu  sana  katika  kufikia  malengo  yako. Lakini  kumbuka  kwamba  mafanikio  hayo  Mungu  ndiye  anayetoa.
2.Ukimwambia  Mungu  unachohitaji  atakujibu.
Amini na tambua  kuwa  Mungu  anajibu  ukimwaomba  Mungu  anaweza  asijibu  utavyotaka wewe,  lakini  kwa  kuwa  analijua   kabla  ya  kuzaliwa  ana  mawazo  mema  juu  yetu  hicho  alichokunyima  ni  faida  yako.
1 WAFALME 2:3
Njia  pekee  ya  kupokea  jibu  lako  ni  kuwa  na  imani  na  uwezo  wa  Mungu.Amini  anaweza  kabla  ya  yote
3. Kuwa  Baraka  kwa  wengine
Ili  ufanikiwe  usiwe  mchoyo. Mungu anakubariki  ili  na wewe  uwe  Baraka  kwa  wengine
2 WAKORINTHO  9:8-11
WARUMI  12 :13
4.Fanya  kazi  kwa  Bidii
Fanya  kazi  hata  kama  ni  ndiyo  kiasi  gani fanya  kwa  moyo  wako  wote
MITHALI  12;11
ZABURI  90:17

Hitimisho  la  somo
Kwa kila  hatua  kumbuka  kumshirikisha  Mungu  na  umpe  yeye  nafasi  ya  kwanza  usiyaabudu  mafanikio  yako, mwabudu  Mungu pekee.
Mwamini  Mungu  kwanza  na  hayo  mengine  utazidishiwa.

SOMO:
KUAMBATANA/KUENDANA
KUSHIKAMANA,GANDAMANA,BILA KUACHANA.
Watu  tuliokoka tunapaswa kushikamana  katika  mambo madogo madogo  ya  kipuuzi  hutufanya  tushindwe  kuambatana.
WIMBO  ULIOBORA 2:15
Ukosefu au kupoa kwa upendo katika watu hufanya tushindwe kuambatana na kugombana  sisi kwa sisi.
WAKORINTHO 13:1
Chuki ni chanzo cha kushindwa kuambatana
VYANZO  VYA CHUKI
·         Ubinafsi
·         Wivu
Chimbuko  la chuki ni SHETANI.
MAMBO MAKUU KATIKA  KUFANIKIWA  KWA
KANISA.
Siri ya  kufanikiwa kwa kanisa siyo vipawa bali ni mambo makuu matatu(03)
·         Uti
·         Uaminifu
·         Kuambatana
TABIA SABA ZA MTU ALIYEACHA KUAMBATANA/ TABIA SABA (07) ZA KUELEKEA UASI
1.Roho  ya kujiamulia mwenyewe.
Yaani mtu  anafanya kile anachojisikia tu na huamua chochote atakacho
2 SAMWEL 3:20-21
2.Kujikwaa  na  kukwazika
Hii ni tabia ambapo mtu kila jambo/mara kwa mara yeye  hukwazika tu na kalalamika
MATHAYO 24:10
3.Kutojihusisha na lolote
Mtu huyu hufanyakazi kwa ulegevu maana hufanya kile ajisikiacho ,Hii ni laana
YEREMIA 48:10
4.Kukosoa
Mtu aliyeacha kuambatana hujiweka kwenye hali ya kukusoa na kutafuta makosa mbalimabali  katika ibada ,kiongozi wake n,k
Mfano:
*Miriam alianza kumkosea musa
HESABU 12:1
·         Absalam alianza kuyaona makosa ya uongozi wa Daud
2 samwel 15:3
5.Hatua ya kisiasa
Wasioambatana na viongozi  wao huwa wanapenda kujiulizisha  maswali.
Mfano:unayaonaje maubiri ya leo?Ibada umeionaje?
6.Kudanganyika.
Aliyeacha kuambaatana huwa mwepesi wa kudangnyika.
YOHANA 8:44
Ni hatua mbaya pale mtu anapo danganyika na kumsema vibaya kiongozi wake au Baba yake wa kiroho.
MITHALI 30:17
7.Uasi wa wazi wazi
Hii hupelekea kupambana ana kwa ana na mamlaka iliyo juu yao
Mfano:
Musa alipigwa waziwazi na KORA,DATHANI,ABIRAM na  wengine viongzi 250
HESABU  16:1-4
Hitimisho la somo
·         Tujifunze  kuwa na Amani na watu wote
WAEFESO 4:31-32
·         Ufalme wa Mungu unatekwa na watu wenye nguvu.
MATHAYO 11:12
--------------*------------------------BARIKIWA--------------*-----------------

SOMO:
ROHO ZITENDAZO KAZI
Roho-Ni nafsi inayofanya kazi katika ulimwengu wa roho:-
Kuna roho kuu tatu:-
i)Roho ya Mungu (Roho mtakatifu)
ii)Roho ya binadamu
iii)Roho ya kishetani
I.ROHO YA MUNGU (ROHO MTAKATIFU)
Hii ni nafsi ya tatu ya Mungu  inayotenda kazi ndani ya watakatifu  wote.Kila aliyeokoka  anapaswa kujazwa nguvu hii ya Roho mtakatifu
MATENDO YA MITUME 1:8
1 WAKORINTHO 12:14
II.ROHO YA KIBINADAMU
Hii ni roho ambayo hujajua mambo ya binadamu tu
I WAKORINTHO 2:11a
Roho  ya kibinadamu inabeba mapenzi na mawazo ya kibinadamu.
Pia wakati mwingine manabii wa Mungu wanaweza  wakatoa unadii , lakini siyo utokao kwa Mungu  bali ni wao wenyewe.
YEREMIA 23:21-23
III.ROHO YA KISHETANI
Hii ni Roho inayowaongoza watu kutenda mambo ya kipepo/maovu tu. Kama vile uchawi/kuua/ubakaji n.k
MATENDO YA MITUME 16:16
IYOHANA  4:1a
ITIMOTHEO 4:1a
Hivyo tunapaswa kuzipima/kuzijaribu Roho .kipimo kikuuu cha kuzipima /kuzijaribu roho ni NENO LA MUNGU maana hili hutusaidia kupambana na roho
WAEBRANIA 5:14
WAEBRANIA  4:12-13
Neno la Mungu ndiyo kiini cha maarifa yote
ZABURI 119:89
ZABURI  119:97-100
ZABURI 119:104-105
Neno la Mungu ndilo linalotufanya tusiyumbishwe na kila aina ya upepo wa Eimu
WAEFESO 4:13-15
Hitimisho la somo
Tamani sana kuongozwa na roho wa Mungu  na zikae kwa nguvu zote .Roho nyingine chafu na zituishe kabisa.





  


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni