Jumatano, 26 Oktoba 2016

SOMO LA MAOMBI


SOMO LA MAOMBI 

Mombi ni nini?
Ni mawasiliano/masemezano/mazungumzo kati ya Mungu na mwanadamu.
ISAYA 1:18
Pia
Maombi ni kitendo cha kumwita Mungu ili ahusike katika haja/hitaji lako.
YEREMIA 33:3   ISAYA 41:21
Mwana maombi mkuu tunayejifunza kwake ni YESU KRISTO. Muda wake mwingi alioishi Duniani alikuwa akiomba.
MATHAYO 4:1-2  MATHAYO 26:36-41  LUKA 22:43-44
Je, ni nani awezaye kuwasiliana/kuzngumza na Mungu kwa njia ya maombi?
1 PETRO 3:12  YOHANA  9:31   WAEBRANIA  12:14
JIBU:
Bwana huwasikiliza wenye haki wasio na dhambi.
Je, tunapoomba tunaweza kupata/kufanyiwa lile tuliombalo?
MATHAYO 7:7-8    YEREMIA  29:12-13
JIBU:
Bwana hutufanyia lile tuliombalo maana ni AHADI yake kwetu.
Je, tuombe lini?
LUKA 18:1    1THESALONIKE  5:17
JIBU:
Imetupasa kuomba siku zote, bila kukoma.
KANUNI ZA MAOMBI/SIFA ZA MUOMBAJI.
ü  Mwenye SIRI- Asiwe mtu anayesemasema SIRI za Mungu kwa watu wasiohusika bila ruhusa ya Mungu mwenyewe.
1WAKORITHO 4:1
ü  Mwenye uwezo wa kumshawishi Mungu.
KUTOKA 32:11-14
ü  Mtu anayenyenyekea mbele za Mungu.
WAFILIPI 2:8                 WAEBRANIA 12:2, 5:8
ü  Kumtafuta Mungu kwa Moyo wote.
YEREMIA 29:13          YEREMIA  24:7
ü  Kutokuwa na mashaka.
MATHAYO 21:21-22                MATHAYO   17:20
ü  Kuwa na bidii.
ISAYA 62:1       MITHALI 13:4           YAKOBO  5:17
ü  Utakatifu
MATHAYO 5:8   MWANZO 3:8-11   HESABU  12:1-8        1SAMWELI 1:20
ZABURI 93:5B    ZABURI 16:3         ISAYA 33:13-19         ZABURI  34:18
WARUMI 6;12     ZABURI 15:1-5      YOHANA 14:21         ZABURI 4:4
ü  Shauku
1NYAKATI 29:2-3 ZABURI 26:8 ZABURI 84:1-2, 10-19  YOHANA 20-1-18
ü  Kufuatilia Ahadi za Bwana (NENO)
YEREMIA 1:12    1NYAKATI 17:1-27   DANIEL 9:1-21 YOHANA 15:7 ISAYA 55:11
ü  Imani
WAEBRANIA 11:1,16 WARUMI 4:20-21    ISAYA 54:17     2WAKORINTHO 4:16
ü  Kuomba katika jina la Yesu
YOHANA 14:13-14                 YOHANA  16:23-24
ü  Mahitaji yaeleweke
MARKO 10:46-52
ü  Kuomba katika Roho mtakatifu
MATENDO YA MITUME 1:8        1WAKORINTHO  14:14
ü  Kumtumikia Mungu
YEREMIA 23:23
ü  Maombi yenye hoja
ISAYA 41:21
ü  Kuwa na Subira.
LUKA 11:9    ZABURI  27:14
VIASHIRIA VYA MTU ASIYEOMBA.
a)      Kuomba kidogo.
b)      Anaweka muda mdogo wa maombi.mfano kufunga mara moja mara moja.
c)      Hupoteza muda kwa vitu visivyo na maana.
d)     Hutumia muda mwingi wa vikao, matangazo kuliko maombi.
e)      Hufikiri/hupanga mambo  makubwa na kufanya bila kumshirikisha Mungu.
WARUMI 1:28
UMUHIMU/FAIDA ZA MAOMBI.
a)      Maombi huleta kufunguliwa vifungo vya waliofungwa.
YEREMIA 29:13-14
b)      Maombi hutuweka karibu na Mungu.
YOHANA 1:12
c)      Maombi huleta mafunuo.
WAKOLOSAI  1:26-19
d)     Maombi huleta majibu/Ushindi katika maisha yetu.
WAEFESO 6:11   MATENDO YA MITUME  12:1-9
e)      Maombi hutuepusha kuingia majaribuni.
LUKA 22:45-46
f)       Maombi hutupa ujasiri.
ZABURI 34:4        2WAFALME  6:15-17
ZINGATIO:
·         Maombi hutufanya kuishi maisha ya ushindi, maisha ya Baraka, maisha ya Amani.
·         Maombi hutupa nguvu (kututia nguvu) katika safari tuliyonayo ya kwenda mbinguni.
                                ISAYA 41:10

UBARIKIWE KWA SOMO HILI!.
NI MATUMAINI YANGU SOMO HILI LIMEKUONGEZEA KIWANGO CHA KUMJUA MUNGU.
                               Pastor.AMOS E.ONESMO-0756391498/0658727799

KIONGOZI NA MAHUSIANO


MAFUNZO YA BIBLIA KWA WACHUNGAJI
SOMO: KIONGOZI NA MAHUSIANO
I.Maana ya Mahusiano.
Ni mfumo unaotumiwa na kila kiongozi wa kiroho au wa kimwili anpotaka kufanikiwa katika huduma yake.
Ni hatua za kimakusudi kabisa anazochukua kiongozi kumtegemea na kumhusisha Mungu alimwita amsaidie kufanya kazi kwa ufanisi. Pamoja na hatua hiyo ni lazima aende mbali kutafuta mahusiano na kazi yake na watenda kazi wenzake na mwisho na watu walioko juu na walioko chini yake.
Mungu ni mwanzilishi wa mahusiano, anaposema katika uumbaji kwamba,”Na tumfanye mtu kwa mfano wetu kwa sura yetu….”(Mwanzo 1:26) Mungu anahusisha nafsi zake Tatu(yaani utatu mtakatifu,Mungu Baba, Mungu mwana, Mungu Roho mtakatifu) katika tendo kuu la kumfanya mwanadamu awepo duniani.
Hivyo uhusiano wa kiongozi na watu mbalimbali ni jambo la kutilia manani kama unataka kufanikiwa.
II.Mungu na kiongozi.
Mamlaka yote ya kiongozi hutoka kwa Mungu iwe ni uongozi wa kiroho au wa kimwili(Rumi 13:1). Hivyo, kiongozi wa kanisa anahitaji mahusiano ya karibu sana na Mungu kwa wokovu wa kweli, kwa kumtukuza Mungu na kumsifu daima, akitumia maombi kupeleka haja zake kwa Mungu na kupokea majibu ya Mungu kwa kusoma Neno la Mungu na kumsikiliza Mungu kwa makini. Ndani ya kanisa,kiongozi anajikuta akihusiana na mamlaka za aina mbili, yaani;
A.Mamlaka ya kitaasisi ambayo ina tabia zifuatazo:-
1.      Ni ya kuteuliwa au kuchaguliwa kwa kura.
2.      Hii inategemea mamlaka ya kibinadamu.
3.      Hii ni ofisi na inahusiana na cheo.
4.      Ina mamlaka ya kisheria na inaambatana na vyeo.
5.      Mara nyingi sifa za kielimu ni moja ya vitu vya lazima
B.Mamlaka ya Kiroho ina tabia zifuatazo:-
1.      Kwa asili ni kiroho;chanzo chake ni Mungu(YOSHUA 3:7)
2.      Cheo cha Nabii au Mtume cha huduma hakiamriwi kwa kuteuliwa au kuchaguliwa.
3.      Inaamuliwa na karama na upako wa kiroho.
4.      Ikiwa unatembea katika Nguvu za Roho mtakatifu huna haja ya kutafuta cheo au nafasi(Matendo ya Mitume 4:13;6:10)
5.      Mamlaka ya kiroho haipatikani kwa juhudi za mtu binafsi. Ni Mungu atoaye. Kwa mfano Musa (Matendo ya mitume 7:20-36) ni baada ya kutumwa na Mungu ndipo alipopata mamlaka ya kuiongoza Israeli kutoka Misri.
6.      Asili ya wito wako unaambatana na mamlaka yako ya kiroho ambayo mara nyingi hayana vyeo;
a)Yesu aliwapa mamlaka wanafunzi wake bila ufalme,madaraka bila vyeo(Mathayo 28:19;Luka 10:3-10;20)
b)Mamlaka ya Petro na Yohana na wengine hayakuwa ya kibinadamu.
c)Ni kosa kufikiria kuwa vyeo vitatoa uhakikisho wa mamlaka.
C.Alama zamamlaka(Nguvu)zitokazo kwa Mungu.
1.      Upendo-Mamlaka yatumikayo kutendea wema wengine.
2.      Unyenyekevu-Mamlaka yaliyo na kiasi. Madaraka ya kuhudumia kwa majivuno(kiburi)ni hatari zaidi.
3.      Kujinyima-Mamlaka yanayozuia kutenda vitu Fulani, hata kama ni vizuri, kwa ajili ya kujiheshimu.
NB:
Kwa kadri unavyokuwa juu katika ngazi ya uongozi, ndiyo unavyokuwa na uchaguzi mdogo.
4.      Shangwe-Kuona ufalme wa kristo ukipenya katikati ya giza na mafadhaiko, kimsingi ni kuona shangwe.
5.      Kujisalimisha-Kujisalimisha kwetu kunatusimamisha chini ya uongozi wa kristo na chini ya mamlaka yaw engine na kutupatia msimamo wa kiroho.
D.Mamlaka katika Huduma ya Yesu.
1.      Yesu alitumia mamlaka kupindua Ufalme wa giza na kudhibitisha ujumbe wake kwamba Ufalme wa Mungu umewasili.
2.      Huduma ya Yesu iliashiriwa na mamlaka-nguvu za kiroho na mamlaka ya kiroho haiwezi kutenganishwa.
3.      Mamlaka na Upako hutenda kazi pamoja.
4.      Huduma ya Yesu huwapatia wengine mamlaka.(Yohana 20:21-22)
5.      Tupambane na Shetani kwa mamlaka tuliyopewa na Yesu (Luka 10;20), tuongoze watu kuokoka, tuombee wagonjwa, na kuwatumikia watu katika nguvu za Roho Mtakatifu.
E.Karama za Kiroho za Uongozi.
1.      Dhana ya mwili wa Kristo(1Kor 12:12-31) kiongozi mwenye kufanikiwa lazima ahusiane na Roho Mtakatifu(Rumi 12:8)
2.      Ni muhimu kwa kiongozi kugundua, kukuza na kutumia karama zetu za kiroho.
3.      Jinsi ya kukuza karama yako ya kiroho;
a)Katika matendo(2Tim 4:6)
b)Soma habari kuhusu karama(1Col 12:3,4)
c)Zungumza na wengine wanaotumiwa katika karama hiyo.
d)Mruhusu Roho Mtakatifu akufundishe(Yoh 14:26)
e)Kumbuka-ni karama ya kiroho
                 -ni uwezo maalumu utolewao na Mungu.
                 -uikuze kwa kuitumia.
      4. Kukua kwa karama yako ya uongozi maana yake ni:-
           a)Kukua katika mamlaka ya kiroho.
           b)Kukua kwa ujuzi wa kimatendo katika uongozi.
            c)Kukua kwa hekima ambayo ni sifa ya nguvu ya karama ya uongozi (Mdo 6:10;7:10;    
               Dan 1:17,20)
            d)Kukua kwa ufahamu ambao ni matokeo ya asili.
III.Kiongozi na Viongozi wenzake
A. Kila kiongozi anatakiwa kuwa na mahusiano binafsi na viongozi wenzake walio juu au chini yake. Hali hii itamjengea msingi mzuri wa heshima pamoja na ufanisi katika huduma yake ya uongozi.
1.      Wathamini wengine na kuwapa nafasi ya kukua katika huduma yako.
2.      Waruhusu wengine kuwa na mchango kwenye maisha yako.
3.      Shirikiana na viongozi wenzako katika huduma yako.
4.      Usivunje siri ya kiongozi mwenzako kwa washirika wa kanisa lako.
5.      Epuka kuonyesha tofauti zilizoko kati yenu viongozi mbele za watu mnaowaongoza.
6.      Wape heshima wanayostahili viongozi wenzako(Rumi 13:7)
7.      Watie moyo wenzako katika kazi.
8.      Onyesha shukrani kwa kazi inayofanywa na viongozi wenzako.
9.      Tumia lugha nzuri kwa viongozi wenzako.
10.  Waelekeze kwa upendo na wasaidie wafanye kazi vizuri na kwa viwango.
11.  Thamini huduma ya kiongozi mwenzako kana kwamba ni yako mwenyewe.
12.  Waheshimu viongozi wenzako na wewe utaheshimiwa (Math 7:12)
B.Kiongozi na Kazi yake
Kiongozi anayetarajia kufanikiwa ni lazima awe na mahusiano mazuri na kazi aliyoitiwa na Mungu kufanya.
1.      Ipende kazi yako ya uongozi. Mungu aliyekupa kazi anaipenda kazi yake, hivyo ili uweze kutenda sawa na mapenzi ya Mungu ni lazima uipende kazi yake.
2.      Fanya maandalizi mazuri kabla ya kuanza kazi yenyewe. Fanya mazoezi ili ufanye kazi kwa ustadi mkubwa wa kutosha.
3.      Boresha namna ya utendaji wako kwa kubuni mbinu mpya kila inapohitajika.
4.      Uwe mwepesi wa kujisahihisha au kusahihishwa unapokosea katika utendaji kazi.
5.      Usiridhike na kiwango ulichokifikia, fanya bidii kuinua viwango vya utendaji kazi wako mara kwa mara.
6.      Maisha yako na matendo yako yaeleze sifa za kazi yako, wala yasiwe kwa maneno tu.
7.      Maandalizi muhimu ya kiroho yajumuisha maombi ya mara kwa mara, na pia upate muda wa kumsikiliza Mungu kwa maelekezo zaidi.
8.      Jenga tabia ya kuhudhuria semina/mafunzo ya kukuza na kuboresha huduma yako ya kiuongozi. Jizoeze kusoma vitabu, na hasa vile vinavyohusiana na huduma yako.
9.      Uwe kiongozi mfikiriaji kuhusu kazi yako. Faida za kuwa kiongozi mfikiriaji wa kazi yako.
a)Unapata uwezo mkubwa wa kufumbua matatizo magumu(Mith 4:1)
b)Uwezo wa kufanya maboresho(Mith 4:4)
c)Kusikia Roho wa Mungu akimnong’oneza mwelekeo(Mith 24:32)
d)Kuwa wazi kupokea mawazo bora na yenye kubadili maisha(Mhubiri 9:13,16)
e)Uwezo wa kuwa na malengo na maono mapya(Mhubiri 1:16)
f)Kupokea hekima(Mhubiri 1:13)
    10.  Funguo za Jinsi ya kuwa mfikiriaji mkubwa
           a)Msubiri Mungu.
           b)Soma vitabu ambavyo vinapanua fikra zako na mipaka ya ufahamu.
           c)Fikiria kwa kina kile unacho kiona na kusikia. Ruhusu akili yako kujali mabo wakati
              yajapo. Usichukulie mambo katika hali ya juu juu.
11.Heshimu na tunza kanuni za Huduma yako.
   a)Maana ya kanuni:-
      i)-ni sheria ya msingi ambayo huwa msingi wa tendo
     ii)-ni ukweli wa msingi ambao ni msingi wa kufikiri kwetu.
     iii)-ni sheria ya jumla ambayo ni msingi kwa ajili ya uamuzi.
NB:
Kanuni huondoa upendeleo, umakundi na ulaghai. Ikiwa wavunja kanuni, kanuni zitakuvunja.
12. Athari za kutotumia kanuni katika matendo na maamuzi ya viongozi wa taasisi:
a)Taasisi inayoongozwa kwa ulaghai wa kisiasa kuliko kanuni huangamia.
b)Taasisi ambayo kwa sehemu kubwa huendeshwa kwa kutoa upendeleo kwa ndugu kuliko kanuni huanguka(Yak 3:17)
c)Kiongozi achukuaye maamuzi ili kujipatia faida binafsi ya kifedha huangusha taasisi yake ghafla.
d)Kanisa/taasisi liongozwalo kwa tamaa badala ya kanuni litaishia kwenye umasikini mkubwa.
e)Kanisa/taasisi liongozwalo kwa ubinafsi kuliko sheria na kanuni linaangamia.
f)Taasisi/kanisa iongozwayo kwa upendeleo na ubaguzi linaangamia.
g)Taasisi iongozwayo kwa ukabila inajitengenezea mgawanyiko na vita na kuanguka.
13.Uwe kiongozi mbunifu.
-Ulimwengu unatawaliwa na Mungu mbunifu.Dunia hii hutawaliwa na watu wabunifu. Hivyo kiongozi wa kiroho hana budi kuwa mbunifu kuboresha kazi yake.
-Hatua za kuwa kiongozi mbunifu:-
a)Mwombe Roho mtakatifu kukufundisha cha kufanya pia.
b)Kubali asili (vutiwa na vitu vya kiasili,mfano wanyama)
c)Shinda upinzani wa kawaida wa mabadiliko.
d)Vutiwa na uumbaji wa ajabu wa watu wa kawaida (mfano upasuaji, ndege, kompyuta n.k)
e)Uwe wazi kwa mbinu mpya.
f)Uwe tayari kuanza mradi wa kushangaza.
g)Jaribu kuanzisha utofauti kwenye mifano iliyopo tayari.
14.Uwe kiongozi mwenye uamuzi sahihi.
-Uwezo wa kuamua ni sifa kuu ya kiongozi. Kushindwa kuchukua uamuzi unaweza kuharibu yote unayoyajenga.
-Sababu Nne kwa nini lazima uwe mwenye kuamua.
a)Mungu ni mwenye kuamua(Efeso 5:1)
b)Viongozi wote wakuu ni wenye kuamua(Hebrania 6:12)
e)Kushindwa kuamua ni kushindwa kuongoza. Asilimia 80 ni maamuzi, asilimia 20 utendaji.
d)Kushindwa kuamua ni sawa sawa na kuamua kutofanya chochote.
-Funguo 6 kwa ajili ya uchukuaji maamuzi.
a)Uwe jasiri (1Falme 2:2)
b)Tazama mbele.
c)Zingatia athari ya kushindwa kuchukua uamuzi (Mwa 13:8,9)
d)Tenda kwa haraka wakati taarifa zote sahihi zimekufikia(1Falme 2:6)
e)Tekeleza maamuzi yaliyokwisha chukuliwa.
f)Zungukwa na watu waliookoka kukupatia ushauri mwema.
15. Maamuzi Kumi ya Jehova
a)Mungu alichukua uamuzi wa kuumba Mbingu na nchi(Mwa 1:2).
b)Alichukua uamuzi wa kumuumba mwanamke(Mwa 2:18)
c)Alichukua uamuzi wa kuua wanadamu wote na kuwaacha hai Nuhu na familia yake(Mwa 5:5-7)
d)Wakati Mungu alipoona dhabihu ya Nuhu alichukua uamuzi wa kutoharibu viumbe vyote tena(Mwa 8:21)
e)Ushoga wa Sodoma na Gomora ulimfanya Mungu kuamua kuufuta mji huo milele (Mwa 18:20,21)
f)Alichukua uamuzi wa kuwaokoa Waisraeli kutoka katika nchi ya Farao(kutoka 2:23-25)
g)Alichukua uamuzi wa kuwaweka Waisraeli Jangwani kwa miaka 40 zaidi(Heb 3:9-11)
h)Wakati alipoona kuwa Lusifa alikuwa muasi, alichukua uamuzi wa kumtupa kutoka Mbinguni (Ezek 28:17,18)
i)Wakati alipotambua kuwa Waisraeli hawakutaka kuongozwa na nabii aliamua kuwapa mfalme(1Samweli 8:7)
j)Kwa sababu ya dhambi kupoteza wengi aliamua kumtuma Mwanawe kuja kuokoa(Yoh 3:16,17)
B.Kiongozi na Wafuasi wake. 
-Uhusiano mzuri wa kongozi na watu/wafuasi wake hurahisisha na kuboresha kazi.
1.Saidia wanaokuzunguka kukamilisha mambo makubwa katika maisha yao.
-Malenngo 4 ya kiongozi kwa wafuasi wake.
a)      Wakusudie wafanikiwe kiroho (3Yohana 4)
b)      Kusaidia wafuasi wako wafanikiwe kifedha.
c)      Kusudia wafuasi wako kuwa na Afya njema kimwili,kijamii na kindoa(3Yoh 2, y oh 16:23,24)
d)     Kusudia wafuasi wako kutimiza huduma yao.
   2.Wahudumie watu kwa usawa lakini onyesha tofauti kwa uwazi
       -Njia 5 za kumfanya kila mmoja aliye karibu ajisikie kuwa yeye ni muhimu.
a)      Jichanganye na watu wa aina zote- Yesu alijichanganya na watu wa aina zote.
b)      Usiwaite au kuelezea wafanyakazi wenzako ofisini wa walio chini yako kama watumishi (watumwa) (Yoh 15:15).
c)      Waeleze wafanyakazi wenzako ofisini kama marafiki zako (Yoh 15:14).
d)     Waeleze watu wafanyao kazi kwa ajili yako kama familia yako (Mathayo 12:48-50)
e)      Wambie wachungaji au wale walio chini yako juu yako mwenyewe na juu ya mipango  yako (Yoh 15:15b)
-Njia 6 za kufanya tofauti ziwe Dhahiri.
a)      Wafundishe.
b)      Watume (Yoh 4:8)
c)      Wabariki (Hebr 7;7)
d)     Sema wewe ni nani?
e)      Uogope kuwa tofauti.
f)       Jiruhusu mwenyewe kuheshimiwa.
3.Husiana na wakubwa na wadogo.
            (1 Korintho 1;26)
           -Kwa nini ni Muhimu uhusiane na wakuu.
a)      Yesu alihusiana na watu wakuu (Yoh 3:1,2;Math 27:57)
b)      Watu wakuu wa majukumu ya kushiriki kanisani (Math 27:57,59,60)
c)      Watu wakuu hutumiwa na Mungu kufadhili Injili (2Kor 8:15)
d)     Uchangiaji wa mtu maarufu unaweza kusababisha Wokovu wa Taifa zima (Esta 4:14).
-Sababu 3 kwanini ni muhimu uhusiane na masikini.
a)      Wito mkuu wa kristo ulikuwa kwa masikini (Luka 4:18,19)
b)      Watu wengi duniani ni masikini kwa hiyo huduma zetu ni lazima ziwafikie Masikini.
c)      Alama ya upako mzuri ni kuwa tunahudumu kwa masikini (Mith 11:3-5)
4.Wafanye wafuasi wako wakupende.
-Kiongozi mzuri huzungukwa na watumishi walio tayari kutekeleza matakwa yake (2 Sam 23:15,16)
-Jinsi ya kuwafanya Wafuasi wako kutokuchukia.
a)      Wafanye watu wajisikie kuwa kiuhalisia wanaheshimiwa nawe.
b)      Wabadili watu wakufuatao kuwa wenye heshima, wa kipekee, wa kufurahiwa na wenye mvuto.
c)      Jitoe dhabihu kwa ajili ya wafuasi wako.
5.Uwe Kiongozi mtiifu na mwaminifu.
-Moja ya sifa kuu za kiongozi ni utiifu na uaminfu.
a)      Uwe mtiifu na mwaminifu kwa watu wanaofanya kazi kwa ajili yako.
b)      Uwe mtiifu na mwaminifu kwa wakuu wako,(Mfano wa Daudi kwa Sauli)(1Samweli 26;8-11)
c)      Uwe mtiifu na mwaminifu kwa marafiki zako (2Sam 9:1) mfano wa Daudi na Jonathani.
d)     Uwe mtiifu na mwaminifu kwa mwenzi wako wa ndoa (Tim 3;2)
e)      Uwe mtiifu na mwaminifu kwa maono yako (Mith 24:21).
f)       Uwe mtiifu na mwaminifu kuwa Mungu wako.
MAWASILIANO (COMMUNICATION).
I.MAANA YA MAWASILIANO
A.    Mawasiliano maana yake ni njia ya kubadilishana taarifa/habari na ufahamu kwa kutumia njia sahihi AU
B.     Ni kitendo cha kupeana au kubadilishana habari kati ya watu wawili au zaidi. Inahusisha kuhamisha mawazo, hisia, ufahamu na maarifa.
C.     Ni kitendo cha kupitisha ujumbe toka mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Kitendo hicho hufanywa kwa maneno au kupitia maneno yaliyoandikwa au kwa alama zisizo na maneno (paralinguistic devices).
D.    Mawasiliano ni sehemu muhimu ya uongozi. Kiongozi huwa mara kwa mara mbele za watu wake. Huweza kutoa matangazo, kufundisha masomo, kukaribisha wanenaji.
II.MAWASILIANO MAZURI
Ni aina ya mawasiliano yenye kuleta matokeo
au
Ni yale yanayotimiza makusudi yaliyotakiwa bila kuvunjika kwa mawasiliano.
III.MAMBO YA MSINGI YA MPANGO WA MAWASILIANO.
A.    Mtumaji   -chanzo cha ujumbe (Encoder)
B.     Mpokeaji  -anayepokea ujumbe (Decoder)
C.     Njia(Medium) -Njia itumikayo kuwasiliana. Mfano; kusema, kuandika, taarifa, barua, kompyuta, radio, Televisheni, Simu..
D.    Ujumbe –Kile cha kuwasiliana.
E.     (Feedback)   Mrejesho- Kauli toka kwa mpokeaji kwenda kwa mtumaji kuonesha kwamba ujumbe umepokelewa.
F.      Mazingira –Hali ambayo ndani mwake ujumbe umepitishwa. Mfano; furaha, hasira, fundisho, n.k
IV.NGAZI YA MAWASILIANO.
Kiongozi huweza kuwa na mawasiliano kwa ngazi kuu tatu.
A.    Kiongozi wa kanisa na mshirika- Mfano; kuhusiana na huduma itolewayo kanisani kama muhubiri, mafundisho ya Neno, maombezi n.k.
B.     Viongozi mbalimbali wa kanisa/taasisi kuwa na mawasiliano kati yao. Mfano; Mchungaji na Mwinjilisti, Mchungaji na Askofu n.k
C.     Kiongozi wa kanisa na Jumuiya inayozunguka kanisa lake na uongozi wa Jumuiya hiyo. Mfano; Kufanya uinjilisti katika Jumuiya, kutafuta huduma za jamii.
D.    Mawasiliano hayo yanaweza kutafsiriwa/kuelezwa kwa njia tatu
1.      Mawasiliano toka juu kwenda chini – maana yake kutoka kwa mkubwa kwa mdogo (kutoa amri, maagizo).
2.      Mawasiliano toka chini kwenda juu – maana yake mdogo kwa mkubwa (kutoa mapendekezo, maombi).
3.      Mawasiliano toka kushoto kwenda kulia (lateral communication) maana yake; kutoka kwa watu wenye Ngazi sawa, viwango sawa (kupeana taarifa, kuchangiana mawazo).
V.MASWALI YA MSINGI KATIKA MAWASILIANO.
A.    Kwa nani? (To whom?)- Mawasiliano na nani?, Atapokea?, Ataelewa? Atapokeaji? Ni sehemu yake?
B.     Kwa nini? (Why?) –Kwa nini unasema hayo? Je, ni ya muhimu? Kwa nini apokea habari hiyo?
C.     Kwa vip? (How) –Atasikiliza vipi? Ameelewa lugha? Atajisikiaje? Tumwambieje?
D.    What? (Nini?) –Nini tutangaze? Nini tuache? Kipi cha kutangulia?
E.     Lini(when?) –Lini jambo lifanyike? Lini litangazwe? Kabla au baada ya mahubiri.
F.      Wapi?(where?) –Wapi tuelekeze mawasiliano? Wapi tupeleke taarifa?
VI.VIZUIZI VYA MAWASILIANO BORA.
A.    Lugha- kutumia lugha isiyoeleweka.
B.     Taarifa ndefu sana.
C.     Mazingira –kelele iliyopo mahali hapo.
D.    Umbali –Upokeaji unatatizwa na umbali.
E.     Kukosa Elimu –Elimu ndogo huathiri mawasiliano.
F.      Vizuizi vya asili –kukosa nguvu ya umeme, kuharibika kwa simu.
G.    Ujumbe kutokuwa wazi –Ni vigumu kueleweka.
H.    Mwonekano wa mnenaji –Wapokeaji huangalia mnenaji.
I.       Tofauti ya maadili, Imani –Wapokeaji huzingatia maadili ya mnenaji.
J.       Maadili hafifu –Taarifa lazima iandaliwe kwa makini.
K.    Utayari wa kujibu kabla ya kusikiliza –Wapokeaji wengi wakimbilia kujibu kabla ya kupokea na kutafakari ujumbe.
L.     Kukosea katika kutoa taarifa –Wapokeaji hupokea kosa kiluko habari yenyewe.
VII.KUSHINDA VIZUIZI VYA MAWASILINO BORA.
A.    Tumia Lugha inayoeleweka.
B.     Tumia miundombinu inayofaa.
C.     Tuma ujumbe unaoeleweka.
D.    Mtumaji awe na ufahamu na uzoefu wa somo
E.     Sikiliza vizuri kabla ya kujibu.
F.      Jiulize maswali sita ya msingi kabla ya kutuma ujumbe.
G.    Tuma taarifa kamili –Usikatekate ujumbe.
H.    Fupisha taarifa yako ili iwe rahisi kupokelewa.
I.       Kagua ujumbe wako kabla ya kutuma.
J.       Tambua hisia za wapokeaji.
VIII.FAIDA ZA MAWASILIANO BORA.
A.    Inapelekea usimamizi mzuri –Ushawishi mzuri kwa wadogo.
B.     Mipango salama –Inafanya uamuzi kufahamika kwa mmoja na kwa wote.
C.     Hamasisho na uadilifu –mfano matokeo katika utendaji sifika.
D.    Utaratibu –Kazi ya  (umma) kikundi.
E.     Ushiriki –Kuaminiana na kujiamini.
IX.AINA ZA MAWASILIANO.
A.    Mawasiliano ya ana kwa ana (Uso kwa uso).
B.     Mawasiliano yaliyoandikwa –kumbukumbu, barua, ripoti.
C.     Usaili –Kusanya habari.
D.    Redio,Tv, Kompyuta.
E.     Maandamano –Wimbo,ngoma.
X.MAWASILIANO NA WATOTO.
A.    Wasiliana na watoto kama wanaweza kufanya hivyo.
B.     Tunafahamu kile ambacho anakifahamu.
C.     Ni haki ya watoto kufanya mawasiliano.
D.    Watoto wanawalinda wazazi.
E.     Kuhusisha watoto katika usemaji wao.
XI.USISEME MAMBO YASIYO SAHIHI HADHARANI.
A.    Kiongozi ni lazima awe mwangalifu juu ya mambo ayasemayo. Kwa maneno yako wajitia mtegoni na kwa maneno yako utahukumiwa. (1 Sam 25:10,11).
B.     Tamko hili lilimgharimu Nabali maisha yake (1 Sam 25:21,22)
C.     Kama wewe ni kiongozi chagua maneno yako kwa uangalifu sana.
D.    Kama kiongozi mwungwana sana, sema hasa kile unachofikiri.
E.     Jifunze sana kusema jambo sahihi kwa jamii au kutokusema chochote kabisa