MTUNZI: PASTOR AMOS E. ONESMO
MAWASILIANO: 0683676447 WHATSAPP: 0759199463
SOMO: UKOMBOZI WA NYAYO
Nyayo ni sehemu ya chini ya mguu wa mwanadamu.
Katika ulimwengu wa Roho nyayo huashiria utawala. Kila tunapokanyaga kwa nyayo tunamiliki. kwa hiyo kuna muunganiko kati ya mafanikio ya mtu na nyayo.
KITABU CHA JOSHUA 1:3
KUMBUKUMBU LA TORATI 11:24
Nyayo za mtu zikichukuliwa kichawi ina maana mtu huyo amepoteza utawala hivyo atatawaliwa na wachawi badala ya kutawala.
Wachawi hufuatilia nyayo za watu na kuwafunga ili wasifanikiwe. Ili ufanikiwe tumia jina la Yesu kukomboa nyayo zako.
NYAYO ZA MWANADAMU ZINAWEZA:
1. Kufuatiliwa
ZABURI 56:6
Wachawi wanafuatilia nyayo za mtu ili wamuzuilie mafanikio
2. Kunaswa
ZABURI 57:6
Miguu ya Mwanadamu ikinaswa nyayo zimenaswa. Kuna watu wanaishi huku nyayo zao zilishanaswa. Tumia jina la Yesu kuzinasua popote zilikonaswa.
3. Kushikamana na kuzimu
MITHALI 5:5
Hatua za mtu ndiyo nyayo za mtu. Wachawi wanaweza kuzishikamanisha nyayo zako na kuzimu kichawi. Nyayo zikishikamana na kuzimu unakuwa umeshawekwa chini ya utawala wa kuzimu. Yaani mafanikio yako huamriwa na kuzimu.
NAMNA YA KUKOMBOA NYAYO ZAKO
1. Ita nyayo popote zilikowekwa ili zirejee.
2. Tumia jina la damu ya Yesu kuziondoa nyayo zako kila sehemu zilikowekwa kichawi.
HITIMISHO LA SOMO
Katika maombi yote, Kumbuka kuwa mkamilifu kwa BWANA Mungu wako
KUMBUKUMBU LA TORATI 18:13