MILANGO
SABA (07) AMBAYO SHETANI HUTUMIA KUINGIZA ROHO ZAKE KATIKA MAISHA YETU.
Ili shetani ayatese
maisha ya Wanadamu anaingiza kwanza Roho zake katika maisha yetu. Roho za
kishetani zikishaingia ndani yetu huyawezesha mambo ya kishetani
kufanyika/kutokea katika maisha yetu.
Zipo njia nyingi ambazo Shetani
hutumia kuingizia Roho zake katika maisha yetu. Zifuatazo ni njia, milango saba
ambayo Shetani hutumia kuingiza Roho zake katika maisha yetu;
1. MAAGANO.
Haya ni makubaliano
yaliyofanyika baina ya mtu na nguvu za giza, vizazi na nguvu za giza. Hii ni
mikataba iliyofanyika na inayofanyika ambayo humpa Shetani Uhalali wa kufanya
kila analotaka kufanya. Unaweza kuwa katika Agano hata bila kujua. Maarifa
inahitajika kutoka chini ya maagano ya ki-shetani. HOSEA 4:6
Kuwa ndani ya Agano maana yake,
“Umenunuliwa kihalali”. Pia, unaweza kuwa umeokoka ila mwili wako Shetani akawa
anautumia kihalali. ITIMOTHEO 1:20
2.URITHI
Urithi unampa mtu
kumiliki kihalali kitu Fulani baada ya Yule aliyekuwa anakimiliki kufariki.
Kuna mambo yanatesa maisha ya watu kutokana na kuyarithi kutoka kwa watangulizi
wetu yaani Wazazi, Mababu n.k. WAEBRANIA 9:16
MWANZO 25:11
Shetani ametumia nafasi hiyo kwa
kupandikiza Roho zake ndani yetu baada ya wale waliokuwa na ROHO hizo kufariki
au kuwa hai.
Mfano: Unamkuta mtu ni mlevi, Muhuni
au mwongo sana baadaye katika uzao wake wanakuwepo watakaorithi tabia yake.
Anaweza kurithi mtoto wa kwanza au mtoto mwingine.
3.NDOTO
Hii ni njia nyingine
shetani anayoitumia kuingiza Roho zake kwa watu. Wengine wamejikuta wanaota
ndoto mbaya kama vile kufukuzwa na nyoka, kula nyama n.k wakidhani ni jambo la
kawaida lakini si hivyo maana ni njia inayoingiza nguvu za kishetani na
kuyatesa maisha yetu.
Kuna aina tatu za ndoto;
i) Ndoto za Ki-Mungu 1WAFALME 3:5-12
ii)Ndoto za Ki-shetani AYUBU 4:12-21
iii)Ndoto za ki-binadamu/kawaida.
Ndoto mbaya za kishetani, Shetani
huzitumia kuingizia uharibifu.
4. NDUGU
Mungu anaweza kukuadhibu
kwa kosa lililofanywa na mwingine. Shetani anaweza kuingiza vifungo vyake kwako
hata kama wewe haukuhusika moja kwa moja. KUTOKA 20:5
5.ENEO
Unaweza kuwa kwenye eneo
linalomilikiwa na Shetani kihalali katika Ulimwengu wa giza.
Mfano: Jiulize swali, kwanini kuna
sehemu zingine ukienda nguvu ya kuomba au kusoma Biblia haipo kabisa?
Shetani anapoenda Sehemu analenga
Vitu Vikuu vitatu.
i) Ardhi (Lengo kuweka Ufalme wake).
ii)Miguu (Lengo kukamata nafsi ZABURI
56:6)
iii)Masikio (Lengo kuzuia usikivu)
AMOS 3:11-12
6.VITU UNAVYOTUMIA
Kuwa na mazoea ya kuombea
vitu unavyotumia kwani Shetani anaweza kupitisha mapepo kwenye vitu kama nguo.
Upako wa Uponyaji wa Yesu ulikuwepo mpaka kwenye nguo aliyokuwa amevaa (MATHAYO
9:20-21), Vivyo hivyo na Roho za kishetani zinaweza kuingilia kwenye nguo pia.
7.FIKRA
Shetani anaweza kuingia
kwenye fikra zako ili upinge kusudi la Mungu (MATHAYO 16:23). Unaweza kuwa na
Yesu lakini Shetani bado akaingia kwenye fikra zako.
MAMBO YA WALAWI 19:28
…………………………….……………………………….……………….
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni