Jumanne, 8 Aprili 2025

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU



SOMO:

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU

Karama  - Ni zawadi kutoka kwa Mungu kupitia Roho Mtakatifu apewayo mtu kulingana na apendavyo Mungu.

Lengo la Mungu kutoa Karama ni kwa ajili ya kuujenga mwili wa kristo ambao ni Kanisa. Mungu ametoa KARAMA tofauti tofauti ili tuweze kujengana.

Roho Mtakatifu humgawia kila mtu kama apendavyo yeye

IWAKORITHO 12:4-11

 

KARAMA TISA (09) ZA ROHO MTAKATIFU

1.      Karama ya Ufunuo

2.      Karama ya Neno la Hekima

3.      Karama ya Neno la Maarifa

4.      Karama ya Imani

5.      Karama ya Matendo ya Miujiza

6.      Karama ya Uponyaji

7.      Karama ya aina ya lugha

8.      Karama ya kutafsiri lugha

9.      Karama ya Unabii

 

MAKUNDI MAKUU MATATU YA KARAMA

KUNDI LA KWANZA (KARAMA ZA UFUNUO)

1.      Karama ya Ufunuo (Maarifa)

2.      Karama ya Neno la Hekima

3.      Karama ya Neno la Maarifa

 

KUNDI LA PILI (KARAMA ZA NGUVU)

1.      Karama ya Imani

2.      Karama ya Matendo ya Miujiza

3.      Karama ya Uponyaji

KUNDI LA TATU (KARAMA LUGHA)

1.      Karama ya aina ya lugha

2.      Karama ya kutafsiri lugha

3.      Karama ya Unabii

MAKUSUDI YA KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU

1.      Kumdhihirisha Yesu katika Ulimwengu wote.

2.      Kufundisha kanisa. Mungu anaweza kufundisha kanisa kupitia Unabii au kwa lugha mpya baada ya kutafsiriwa. IWAKAORINTHO 14:5

 

JINSI YA KUPOKEA KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU

1.      Kwa kutaka (Kuomba Mungu)

IWAKORINTHO 12:31, 14:1. Omba Mungu akupe

2.      Kwa kuwekewa Mikono na Watumishi wenye Karama.

ITIMOTHEO 4:14,  2TIMOTHEO 1:6

3.      Kwa kuwa na Ushirika na watu wenye Karama.

2WAFALME 2:1-15

MUHIMU

KARAMA HAZIFANYI KAZI KAMA MTU ANAVYOTAKA BALI KAMA MUNGU ANAVYOTAKA