Jumatano, 1 Januari 2025

SIRI YA MAFANIKIO 2025

 MWL. REV. AMOS 

SOMO:

 *SIRI YA MAFANIKIO 2025* .

🛑Mafanikio

➖Ni hali ya mtu kufikia hatima njema ya malengo aliyojiwekea. 

➖Ni haja ya kila mtu afanikiwe. Mafanikio ni hitaji la kila mmoja mwenye kutamani mafanikio. 

➖2025 Utafanikiwa kwa jina la Yesu. 


🛑ZINGATIA YAFUATAYO:-

1. *Uwe mtu wa Maombi* . 

Mwaka huu omba kuliko kawaida. Maombi yataleta majibu kwa mahitaji mengi na utafanikiwa. 


 *1 Wathesalonike 5:17* 

"Ombeni bila kukoma"


2. *Umzalie Mungu matunda* . 

➖Jitahidi kuleta watu kwa Yesu ili uupendeze Moyo wa Mungu ili akufanikishe

Kanuni ya Ki-Biblia, ni kuzaa matunda na matunda yapate kukaa kisha Omba na Mungu akutendee


 *YOHANA 15:16* 

"Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni"


3. *Thubutu* 

➖Jifunze kuthubutu maana katika kuthubutu utafanikiwa

➖Jaribu kile unachoweza kufanya utafanikiwa

➖Thubutu ila usitende dhambi

➖Biblia inatukumbusha kujaribu kila jambo na kulishika jambo jema TU. 


 *1 Wathesalonike 5:21* 

"jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema"


4. *Unyenyekevu* 

➖Unyenyekevu siyo ujinga na anyenyekeaye huinuliwa

➖Nyenyekea ofisini kwako, katika huduma, katika ndoa n.k kwani unyenyekevu utakupa kibali 2025.

➖Nakuombea kiburi na mashindano visikuponze 2025


 *MATHAYO 11:29* 

"Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu"


5. *Marafiki wa Faida* . 

➖Rafiki anaweza kukupoteza na anaweza kukuonesha njia

➖2025 Mungu akupe marafiki walio tayari kula gharama kwa ajili Yako

➖Mwenye kupooza alipata marafiki wema walimaababisha kupokea uponyaji


 *Marko 2:1-5* 

[1]Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani

[2]Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake. 

[3]Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne. 

[4]Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. 

[5]Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.



"" "" "" "" "" "MWISHO" "" "" "" "" "" 

REV. AMOS 0625313609

WHATSAPP+255759199463

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni