Jumatano, 25 Oktoba 2023

UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU


 *UONGOZI WA ROHO MTAKATIFU* .

Ni muhimu sana kwa aliyeookoka kujazwa nguvu za Roho mtakatifu na kuongozwa na nguvu hiyo. 

Roho mtakatifu hutusaidia katika udhaifu wetu.

πŸ‘‰πŸΏ Roho mtakatifu hutusaidia kuomba ipasavyo.


*WARUMI 8:26* 

[26]Kadhalika Roho naye hutusaidia *udhaifu* wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe *hutuombea* kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.



πŸ‘‰πŸΏ Yesu aliongozwa na Roho, nasi tuongozwe na Roho.


*LUKA 4:1* 

[1]Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, *akaongozwa na Roho* muda wa siku arobaini nyikani,


πŸ‘‰πŸΏ Ukifanya mambo ya kiroho kwa kuiga bila kuongozwa na Roho unaishia kupata Aibu. Usiige, tafuta uongozi wa Roho mtakatifu.


*MATENDO YA MITUME 19:13-17* 

[13]Baadhi ya Wayahudi wenye kutanga-tanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. 


[14]Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. 


[15]Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani? 


[16]Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa. 


[17]Habari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawaingia wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa.


πŸ‘‰πŸΏ Kwa kuongozwa na Roho mtakatifu hauko chini ya Sheria.


*WARUMI 8:1-3* 

[1]Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. 


[2]Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. 


[3]Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;


πŸ‘‰πŸΏ Roho mtakatifu ndani ya mtu huleta mafunuo. Usifanye mafunuo ya kuiga, msikilize Roho mtakatifu.


*1 WAKORINTHO 2:9-12* 

[9]lakini, kama ilivyoandikwa, 

Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, 

(Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) 

Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. 


[10]Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. 


[11]Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. 


[12]Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.


➖ *KAZI ZA ROHO MTAKATIFU NDANI YA MTU* 

πŸ‘‰πŸΏKutupasha yajayo

πŸ‘‰πŸΏ Kutusaidia kuomba

πŸ‘‰πŸΏ Kutufunulia

πŸ‘‰πŸΏ Kutufundisha

πŸ‘‰πŸΏ Kuongoza utumishi wetu


HITIMISHO.

Biblia inasisitiza tujazwe Roho mtakatifu.


*WAEFESO 5:15-18* 

[15]Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 


[16]mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. 


[17]Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana. 


[18]Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali *mjazwe Roho* ;


..............,..........................

By

Rev. Amos (Tabora)

E-mail: *pasteronesmo@gmail.com* 

Whatsapp *+255759199463*

Jumatano, 11 Oktoba 2023

NYUMA YA KUOLEWA KWAKO

 *TUBU DHAMBI ILIYO NYUMA YA KUOLEWA KWAKO* .


Siku unaolewa kuna vijana wengi uliwaachia maumivu, machozi, vilio na simanzi.

Kwa ajili yako wengine waliapa hawatapenda tena, wengine walipoteza Imani kwa wanawake hawamwamini mwanamke yeyote, wengine hadi sasa hawaajaoa bado hawaamini kama ni kweli umeolewa ni kama wanaota.


 *HAO VIJANA SI WENGINE, NI WALE* :-


1. ULIOWATAPELI KWA KULA HELA YAO NA KUWADANGANYA KWA KUSEMA "Sina mwingine"


2. WALIOTUMIA MUDA MWINGI KULINDA UCHUMBA BILA KUJUA KUWA WEWE NI MSALITI.


3. WALIOWAKATAA WENGINE KWA AJILI YAKO KWA  KUTUNZA MAKUBALIANO YENU, KUMBE WEWE ULIKUWA TAPELI TU 


4. WALIOKUBALI KUSHINDA NJAA ILI WEWE USHIBE, WALIOACHA KUVAA ILI WEWE UVAE.


5. WALIOKUAMINI WAKATI HUKUFAA KUAMINIWA


Machozi yao Mungu anayaona na kuyasikia, *RUDISHA HELA ZAO ULIZOKULA.* 


USIPOFANYA HIVYO ZITAGEUKA KUWA KIFUNGO KWAKO MAANA USALITI NI DHAMBI


REV. AMOS - TABORA

Whatsapp +255759199463

E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com

Ijumaa, 17 Februari 2023

MKARIBIE MUNGU

 MWL: *REV. AMOS ONESMO* 

CONT. *0625313609* 

WHATSAPP: *0759199463* 

E-mail: *pasteronesmo@gmail.com* 


SOMO:

 *MKARIBIE MUNGU* 

UTANGULIZI

Kumkaribia MUNGU ni kumsogelea MUNGU au kuwa karibu na MUNGU


*YAKOBO 4:8* 

"Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili"


*ZABURI 145:18-19* 

[18]BWANA yu karibu na wote wamwitao, 

Wote wamwitao kwa uaminifu. 


[19]Atawafanyia wamchao matakwa yao, 

Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa"


*YEREMIA 23:23* 

[23]Mimi ni Mungu aliye karibu, asema BWANA, mimi si Mungu aliye mbali.


πŸ“Œ *NAMNA YA KUMKARIBIA MUNGU* 


*MIKA 6:6-8* 

[6]Nimkaribie BWANA na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nimkaribie na sadaka za kuteketezwa, na ndama za umri wa mwaka mmoja? 


[7]Je! BWANA atapendezwa na elfu za kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu? 


[8]Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!


Tunamkaribia MUNGU kwa:-

1. *Kutenda haki* 

2. *Kupenda Rehema* 

3. *Unyenyekevu* .


"""""""""""""BARIKIWA""""""""""""

Rev. Amos (Tabora)


Tembelea blog yangu kwa kufungua google kisha andika

 *"Pastor Amos Onesmo* "

Jumapili, 29 Januari 2023

MADHARA YA DHAMBI

 *IBADA YA LEO TABORA* .

29/01/2023


SOUND OF GOSPEL CHURCH MINISTRY TANZANIA (SCMT)

MNENAJI: REV. AMOS E. ONESMO

SIMU: +255625313609/+255759199463


SOMO:

 *MADHARA YA DHAMBI*

UTANGULIZI

Dhambi ni jambo lolote lisilompendeza MUNGU.

Dhambi inamfanya mwanadamu asifanikiwe kwa lolote.

*MITHALI 28:13* 

Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; 

Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.


Dhambi ina MADHARA makubwa kama ifuatavyo:-

1. Kupoteza uhusiano na MUNGU

πŸ‘‰πŸ½Ni hasara kubwa kukosa uhusiano na MUNGU kwani pale unapohitaji msaada wa MUNGU hautaupata.

*ISAYA 59:2* 

"lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia"



*Mithali 15:29* 

"BWANA yu mbali na wasio haki; 

Bali huisikia sala ya mwenye haki"


2. Jina linafutwa katika kitabu cha uzima

πŸ‘‰πŸ½ Mungu anakuondoa kwenye kitabu chake. Mbingu hazikutambui, utatambulika kuzimu.

*KUTOKA 32:33* 

"BWANA akamwambia Musa, Mtu ye yote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu"


3. Mema uliyoyatenda hayatakumbukwa

πŸ‘‰πŸ½ Dhambi inafuta yote uliyoyatenda.

*Ezekieli 18:24* 

"Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa"


4. Kupoteza Amani na furaha ya MUNGU

πŸ‘‰πŸ½Amani na furaha hutoka kwa Mungu. Ukitenda dhambi unakuwa umepoteza vyote

*ISAYA 57:20-21* 

[20]Bali wabaya wanafanana na bahari iliyochafuka; maana haiwezi kutulia, na maji yake hutoa tope na takataka. 


[21]Hapana amani kwa wabaya; asema Mungu wangu.


5. Kupoteza hofu ya MUNGU


*Zaburi 36:1* 

"Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake, 

Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake"


 *HITIMISHO* .

➡️ Tujihadhari na dhambi, tuyatende mapenzi ya MUNGU

➡️ Omba nguvu ya Roho mtakatifu ikusaidie usitende dhambi 


_______Rev. Amos Tabora _____

Jumatatu, 23 Januari 2023

My second born

 

Mungu mwema ameniongezea familia baada ya kukaa kwenye ndoa miaka miwili na miezi kumi bila kupata watoto.
Huyu ni mtoto wa pili Sasa

Ujumbe muhimu

 MTUMIKIE MUNGU NAYE ATAKUHESHIMU