Jumatano, 30 Novemba 2022

POKEA JAMBO JIPYA

 *MUNGU AKUTENDEE JAMBO JIPYA MWEZI DECEMBER* 

ISAYA 43:18-19

[18]Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. 


[19]Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.

Jumatatu, 28 Novemba 2022

NAFASI YA MWANAMKE KWA MWANAUME KIUCHUMI

 MWL. REV. AMOS FROM TABORA.

MAWASILIANO: +255759199463

+255625313609

E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com


SOMO:

 *NAFASI YA MWANAMKE KIUCHUMI KWA MMEWE*

➡️Mwanamke ana nafasi kubwa na ya muhimu kwa mmewe kiuchumi kama ifuatavyo:-


1. Kumwinua Mme anapoanguka kiuchumi

 *πŸ‘‰πŸ½MHUBIRI 4:9-10* 

[9]Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; 

Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. 


[10]Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!


2. KUMSHAURI Mme kuhusu mambo ya uchumi

 *πŸ‘‰πŸ½*MITHALI 31:26-28** 

[26]Hufumbua kinywa chake kwa hekima, 

Na sheria ya wema i katika ulimi wake. 


[27]Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; 

Wala hali chakula cha uvivu. 


[28]Wanawe huondoka na kumwita heri; 

Mumewe naye humsifu, na kusema,


3. Kumsaidia Mme mambo ya kiuchumi

πŸ‘‰πŸ½*MWANZO 2:18* 

[18]BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.


4. Mlinzi wa mapato ya Mme

πŸ‘‰πŸ½*YEREMIA 31:22* 

[22]Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana BWANA ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.


5. Mjenzi wa kipato cha Mme

 *πŸ‘‰πŸ½*MITHALI 14:1** 

[1]Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; 

Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.


6.. Kumtia moyo Mme katika mambo ya kiuchumi


*MITHALI 15:4* 

[4]Ulimi safi ni mti wa uzima; 

Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo.


*HITIMISHO* .

➡️Mwanamke wewe ni wa muhimu sana katika ujenzi wa uchumi wa mmeo na FAMILIA.


➡️Mwanaume usimdharau mkeo katika mambo ya kiuchumi.


_______Mwisho_____


Rev. Amos

Tabora

pasteronesmo@gmail.com

+255759199463

+255625313609

Jumatatu, 14 Novemba 2022

UMEFUNGWA NA MACHOZI YAKE

 ~~*MACHOZI YAO/YAKE YAMEKUFUNGA WEWE MWANAUME..!!!*~~ 

πŸ“Œ Kumbuka binti yule uliyemdanganya kwamba akilala na wewe utamuoa kisha akamwacha.

πŸ“Œ Kumbuka binti uliyemchumbia naye akajimimina kwako lakini ukamsaliti.

πŸ“Œ Kumbuka binti wa kazi uliyembaka.

πŸ“Œ Kumbuka binti yatima uliyemfanyia ukatili ukamwongezea machungu.

πŸ“Œ Kumbuka alivyokuamini akakutambulisha kwa marafiki zake, ndugu zake na wazazi wake ila ukamtenda.

πŸ“Œ Kumbuka binti yule aliyekupa vitu na zawadi nyingi akijua utamuoa ila baadaye ukamuoa rafiki yake

πŸ“Œ Kumbuka miaka aliyokaa akikusubiri umalize masomo ila baadaye ukamsaliti.

πŸ“Œ Aliwakataa wengi kwa ajili yako ila baadaye ukajifanya haumjui

πŸ“Œ Alivumilia mangapi kwa ajili yako?

πŸ“Œ Kumbuka uliyempa mimba baadaye ukamkataa. Analea mtoto peke yake. Ana maumivu kiasi gani?

Huyu binti akimlilia Mungu akasema usizae, *utazaa* ??


✳️Unadhani binti huyu anapomlilia MUNGU MACHOZI yake yanapita *BURE* ?

✳️ Machozi ya binti huyu, yamekufunga usifanikiwe.

✳️ Binti alilia Machozi mengi.

✳️ Binti huyu wakati analia kuna maneno alitamka ambayo ndiyo yamekukamata.


➡️ACHA MAHUSIANO YA UONGO UONGO IPO SIKU UTAJUTA.

➡️ Tengeneza na MUNGU


*Ufunuo wa Yohana 2:5* 

[5]Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; *ukatubu* , ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.


.......... Barikiwa.........

Rev. Amos

+255759199463

+255625313609

E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com

Jumamosi, 5 Novemba 2022

KIFUNGO KITOKANACHO NA NADHIRI

 MWL. REV. AMOS

MAWASILIANO: +255759199463

+255625313609

E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com


SOMO: *KIFUNGO KITOKANACHO NA NADHIRI* 


UTANGULIZI

Nadhiri ni ahadi inayotolewa kwa MUNGU.

*MHUBIRI 5:4-5* 

[4]Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri. 


[5]Ni afadhali usiweke nadhiri, 

Kuliko kuiweka usiiondoe.


Nadhiri ya mtu inaweza kuwa.

πŸ“Œ Nadhiri mbaya

πŸ“Œ Nadhiri nzuri


Nadhiri hufanyika kwa

πŸ“Œ Maneno

πŸ“Œ Mawazo


Kuna Nadhiri zimefanywa na watu ambazo zimegeuka mtego kwao.

Nadhiri hizo zimewafunga wasifanikiwe.

✳️ *Matendo ya Mitume 21:23* 

[23]Basi fanya neno hili tunalokuambia. Wako kwetu watu wanne waliofungwa na *nadhiri* .


✳️ *MITHALI 6:2* 

[2]Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, 

Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,


MIFANO YA NADHIRI

➡️ Nadhiri ya Yakobo

*MWANZO 28:18-21* 

[18]Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. 


[19]Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu. 


[20]Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; 


[21]nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo BWANA atakuwa Mungu wangu.


πŸ‘‰πŸ½Mungu aliitazama Nadhiri ya Yakobo

*MWANZO 31:13* 

[13]Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.


➡️ Nadhiri ya Hana

*1 Samweli 1:11,27-28* 

[11]Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe. 


[27]Naliomba nipewe mtoto huyu; BWANA akanipa dua yangu niliyomwomba; 


[28]kwa sababu hiyo mimi nami nimempa BWANA mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa BWANA. Naye akamwabudu BWANA huko.


NADHIRI INAMFUNGA MTU ASIPOITIMIZA.

*HESABU 30:1-2* 

[1]Kisha Musa akanena na wale vichwa vya kabila za wana wa Israeli, na kuwaambia, Neno hili ndilo aliloliagiza BWANA. 


[2]Mtu atakapomwekea BWANA nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa kifungo, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.



✳️ Ukiweka Nadhiri usiiondoe ni dhambi na inakufunga. Nadhiri haisamehewi.


*Kumbukumbu la Torati 23:21* 

[21]Utakapoweka nadhiri kwa BWANA, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako.


✳️ Nadhiri inaweza kuwa ni ya

πŸ“Œ Muda

πŸ“Œ Daima (Milele)


HITIMISHO.

Ondoa Nadhiri yako ili ufunguke 

πŸ“ŒKIMAISHA

πŸ“ŒKIUCHUMI

πŸ“ŒKIROHO



...............END............