SOMO:
KUAMINIWA
NA MUNGU
-Kuaminiwa ni kupata kibali/kuweka imani kamili juu ya jambo fulani au mtu.
-Mungu alimwamini musa na kumbebesha jukumu maalumu
la kuwatoa wana wa Mungu utumwani.
KUTOKA
3:4-10
Musa alipata kibali machoni pa Mungu kama musa
alivyoaminiwa na Mungu, nasi pia Mungu
ametuamini ili tuitende kazi yake bila kutoa udhuru kama aliotaka
kutoa musa.
-Ili
kuaminiwa na Mungu tunatakiwa kujitakasa,Musa baada ya kusogelea kijiti
kinachowaka Mungu alimwambia avue viatu ikiwa ni ishara ya kutakaswa.
-Tunapojitakasa ndipo tunapopata kibali cha
kuaminiwa na Mungu ili tuitende kazi yake,Musa
aliaminiwa na Mungu kuwatoa watu MISRI.
VIPINGAMIZI/VISABABU
VYA MUSA ILI KUTAKA
KULIPINGA
KUSUDI LA MUNGU.
Musa alitaka kulikwepa kusudi la Mungu baada ya
kuaminiwa naye. Wapo watu wanaojaribu kulikwepa kusudi la Mungu pale
wanapoaminiwa na yeye.
Tufuatane pamoja kuziona sababu za musa
1.Alijidharau
Musa alijiona kuwa hasitahiri kusimama mbele ya farao kumweleza habari ya kuwaruhusu wana
wa Israeli alijiona hafai wakati
ameaminiwa na Mungu
Mpendwa ukiaminiwa na Mungu usijidharau kwa sababu yoyote ,msikilize Mungu.
KUTOKA
3:11
2.Alitengeneza maswali yasiyo na sababu
Musa alijitengenezea maswali mengi yaliyo lenga
kupinga agizo/kusudi la Mungu kuwatoa wana wa Israeli utumwani kama vile :-
“nao wakiniuliza jina lake ni nani? Niwambie
nini?”
KUTOKA
3:13
Pia, wapo watu wa aina hii Mungu anapowaamini na kuwapa jukumu huanza kutengeneza maswali kama hayo.
i)Nitaanzaje?
ii)Nitaishije?
3. Mashaka ndani yake
Ndani ya musa iliumbika roho ya hofu katika kulibeba
kusudi la Mungu baada ya kuaminiwa.
KUTOKA
4:1
Wapo watu wanapoaminiwa na Mungu wanashindwa
kulitumikia kusudi la Mungu kwa sababu ya hofu/roho ya mashaka.Jiepushe na hali hiyo uitende kazi ya Mungu kama
ulivyoaminiwa.
4.Ulimi mzito
Mungu alimwamini musa huku akijua kuwa anaulimi
mzito (kigugumizi) musa
alitaka kutumia udhaifu huu
kulikwepa kusudi. Mungu amekuamini hivyo
hivyo bila kujalisha udhaifu ulionao wewe simama kwa Mungu wako uitende kazi yake.
KUTOKA
4:10
5. Kukosa utajari
Wapo watu hawapo tajari kulitumikia kusudi la Mungu
kwa sababu tu hawako tajari.wengine huisi maisha yao yataharibika,watakosa muda
wa utafutaji n.k.
Musa alikosa utayari,akamtaka Mungu amwagize mtu
mwingine na si yeye.
KUTOKA
4;13
6.Alihitaji mtu wa kusimama naye
Kuna watu katika utumishi hawataki kusimama peke
yao hutaka kusimama kwa miguu ya watu wengine . Mungu anapokuamini mpendwa
simama tu,Mungu atakuwa pamoja nawe hata
kuacha usiruhusu HASIRA ya Mungu kuwaka juu yako.
KUTOKA4:14-17
Hitimisho la somo------------------
Mungu anapokuamini hupaswi kuweka
sababu za kutoa ili usilitekeleze kusudi
la Mungu.
LUKA
14:16-24
………………………+………+Barikiwa
mno……….+………………+……………
SOMO:
BADILI
LUGHA YAKO UFANIKIWE
-Lugha ya mtu huamua maisha ya
mtu.Atamkavyo mtu ndiyo nafsi hujengwa
na kisha kuamua maisha yake.kile
kitokacho ndani ya kichwa cha mtu, ndicho huamua maisha
yake kuanzia rohoni hadi mwilini.
MITHALI
28:7a
-Lugha hujenga fikra(mawazo)ya mtu.
*Fikra ni nini?
i)Ni jinsi aonavyo mtu.
ii) Ni kiwango cha kufikiri cha mtu.
iii)Ni maisha ya mtu.
*Shetani akitaka kuharibu maisha
yako ya kiroho na ya kimwili kwenye
nafsi kwa maneno ya kinywa.
HATUA ZA KUKUFIKISHA KWENYE
MAFANIKIO
Mafanikio ni hatua njema ya mtu
ambayo hupitia ngazi mbalimbali.
1.Jitathmini ili
kujitambua zaidi ,kijitathmini ni kujikagua na kujijua kwa kina juu ya mikakati
mbalimbali kuelekea kwenye mafanikio.
WAFALME
4:1-7
Mwanamke
alijitathmini baada ya kifo cha mmewe
akaona kupungukiwa .
·
Jitathmini ili kutambua kwa usahihi msaada unaohitaji
·
Jitathmini ili kutambua
msaada unaohitaji unaupata kwa
nani?
2.Weka mkakati kwa kumshirikisha Mungu.
Weka mikakati iliyo ndani ya uwezo wako na inayofikika. Ni afadhari
kuwa na mikakati michache iliyo ndani ya
uwezo wako kuliko kuwa na mikakati mingi
isiyofikika.
MITHALI
3:5
3. Kuwa
mwaminifu
Ili ufanikiwe ni lazima utengeneze
mazingira ya kuamini kwa
(a)Watu
(b)Mungu
Hakikisha katika mapato yako unakuwa mwaminifu kwa kutoa sehemu ya kumi ya mapato yako(10), Pia shughuli zako zisikufanye usahau ibada.
ZABURI
51:6
MATENDO
YA MITUME 5;1-11
4. Omba sana kuliko kulalamika
,Tumia muda mwingi kuombea shughuli / kazi za mikono yako kuliko kulalamika na
(a)Kujilaumu
(b)Kumlaumu mwingine/ kuwalaumu
wengi
LUKA
18:1
YEREMIA
29:11
Hitimisho la somo
Lugha yako itaamua maisha yako.
……………..*…………BARIKIWA……………….*……….
SOMO:
MAAMUZI/DECISION
Maana
Maamuzi ni uwingi wa neno uamuzi linalomaanisha kukata shauri juu ya jambo/kitu Fulani.
-Uamuzi wowote wa mtu
aliyeokoka unatakiwa
kumhusisha Mungu maana
yeye hutupa akili
kwa kila jambo.
2
TIMOTHEO 2:7
-Uamuzi huamua kesho ya mtu
AINA
ZA MAAMUZI
Ziko aina kuu mbili za
maamuzi ambazo ni
i)Maamuzi sahihi
ii)Maamuzi yasiyo sahihi
I.MAAMUZI SAHIHI
Hii ni aina ya
maamuzi inayomfanya mtu
atende jambo jema
na si baya.
Mfano:kuamua kumsamehe mtu .MATHAYO 6:14
II. MAAMUZI YASIYO SAHIHI
Hii ni aina ya
maamuzi anaoufanya mtu na
hatimaye huleta majuto/jambo baya.
Mfano: Uamuzi
wa mtu kuvunja ndoa n.k
MATOKEO YA
MAAMUZI
Yako matokeo
makuu mawili ambayo ni
i)Matokeo
mazuri/Raha
ii)Matokeo
mabaya/ majuto
MAMBO YA
MUHIMU WAKATI WA KUFANYA
MAAMUZI
1.Jitambue wewe ni nani unayefanya
maamuzi
Tambua
wewe ni wa kristo na siyo wa
shetani.Usifanye maamuzi kama vile mtu wa mataifa.Ukijujua wewe ni
nani utafanya maamuzi sahihi
2
WAKORINTHO 13:5
2. Tumia
akili nzuri
Akili ni ufahamu
juu ya jambo
fulani na si
ubongo. Kutumia akili humaanisha
kuwa na ufahamu
mkubwa juu ya
matokeo ya maamuzi
yako unayoenda kufanya
1
PETRO 4:7
3.Fikiri
kwa uzito na kutenda
kwa HEKIMA
Kufikili
kwa uzito humaanisha
kuwa na tafakari
nzito juu ya
jambo/mambo yanayohitaji kufanya maamuzi.
Waswahili
husema “fikiri kabla
ya kutenda”kufikiri kwa
kina kutakupa maamuzi
yenye ujasiri na
akili ya Mungu itakuongoza
2
TIMOTHEO 1:7
ISAYA 55: 8-7
4.Mhusishe
Mungu katika maamuzi
yako
Kila jambo
tunalolifanya tunatakiwa kutozitumia
akili zetu badala
yake tumtumaini Mungu.
MITHALI
3:5
5.Imalisha nia ya kufanya mema
Kama mkristo
unatakiwa kukusudia mema
katika maamuzi yetu
na si kukusudia
kutenda mabaya.
WAFILIPI 2:13
WARUMI 7:18
Hitimisho la
somo
Fanya
maamuzi yenye kuleta
utukufu na si
kuumiza /kuuwa nafsi za watu
au wewe mwenyewe .
Maamuzi
mabaya huleta roho
ya usugu na
mbaya ndani ya
mhusika.
…………………………………………BARIKIWA……………………………………..
SOMO:
SAFARI YA
MAFANIKIO
Mafanikio- Ni
hali ya kufikia
hatima njema ya
malengo ya mtu.
Mafanikio
ni safari lazima tuyatafute
Katika
safari hii ya
mafanikio tambua kuwa nchi
na vyote viijazavyo ni
mali ya BWANA
ZABURI 24:11
-Mmiliki wa mali zote ni Mungu
,ili upate mafanikio ni lazima
umwangalie na umwombe
yeye mtoaji.
-Mafanikio
yatokanayo na njia isiyo sahihi
HAYADUMU.
MAMBO MUHIMU
YA KUKUMBUKA KATIKA
SAFARI YAKO
YA MAFANIKIO.
1.Mungu
ndiye mmiliki wa kila
kitu na ndiye
mtoaji
Ujuzi na juhudi
zako ni muhimu
sana katika kufikia
malengo yako. Lakini kumbuka
kwamba mafanikio hayo Mungu ndiye
anayetoa.
2.Ukimwambia
Mungu unachohitaji atakujibu.
Amini na tambua
kuwa Mungu anajibu
ukimwaomba Mungu anaweza
asijibu utavyotaka wewe, lakini
kwa kuwa analijua
kabla ya kuzaliwa
ana mawazo mema
juu yetu hicho
alichokunyima ni faida
yako.
1
WAFALME 2:3
Njia
pekee ya kupokea
jibu lako ni
kuwa na imani
na uwezo wa Mungu.Amini anaweza
kabla ya yote
3. Kuwa
Baraka kwa wengine
Ili
ufanikiwe usiwe mchoyo. Mungu anakubariki ili na
wewe uwe
Baraka kwa wengine
2
WAKORINTHO 9:8-11
WARUMI 12 :13
4.Fanya
kazi kwa Bidii
Fanya
kazi hata kama
ni ndiyo kiasi
gani fanya kwa moyo
wako wote
MITHALI 12;11
ZABURI 90:17
Hitimisho la
somo
Kwa
kila hatua kumbuka
kumshirikisha Mungu na
umpe yeye nafasi
ya kwanza usiyaabudu
mafanikio yako, mwabudu Mungu pekee.
Mwamini Mungu
kwanza na hayo
mengine utazidishiwa.
SOMO:
KUAMBATANA/KUENDANA
KUSHIKAMANA,GANDAMANA,BILA
KUACHANA.
Watu
tuliokoka tunapaswa kushikamana
katika mambo madogo madogo ya
kipuuzi hutufanya tushindwe
kuambatana.
WIMBO
ULIOBORA 2:15
Ukosefu au kupoa kwa upendo katika watu hufanya
tushindwe kuambatana na kugombana sisi
kwa sisi.
WAKORINTHO 13:1
Chuki ni chanzo cha kushindwa kuambatana
VYANZO VYA CHUKI
·
Ubinafsi
·
Wivu
Chimbuko la
chuki ni SHETANI.
MAMBO MAKUU KATIKA KUFANIKIWA
KWA
KANISA.
Siri ya
kufanikiwa kwa kanisa siyo vipawa bali ni mambo makuu matatu(03)
·
Uti
·
Uaminifu
·
Kuambatana
TABIA
SABA ZA MTU ALIYEACHA KUAMBATANA/ TABIA SABA (07) ZA KUELEKEA UASI
1.Roho ya kujiamulia mwenyewe.
Yaani mtu
anafanya kile anachojisikia tu na huamua chochote atakacho
2 SAMWEL 3:20-21
2.Kujikwaa na kukwazika
Hii ni tabia ambapo mtu
kila jambo/mara kwa mara yeye hukwazika
tu na kalalamika
MATHAYO 24:10
3.Kutojihusisha na
lolote
Mtu huyu hufanyakazi
kwa ulegevu maana hufanya kile ajisikiacho ,Hii ni laana
YEREMIA 48:10
4.Kukosoa
Mtu aliyeacha kuambatana
hujiweka kwenye hali ya kukusoa na kutafuta makosa mbalimabali katika ibada ,kiongozi wake n,k
Mfano:
*Miriam alianza kumkosea musa
HESABU 12:1
·
Absalam alianza kuyaona makosa ya
uongozi wa Daud
2 samwel 15:3
5.Hatua ya kisiasa
Wasioambatana na viongozi wao huwa wanapenda kujiulizisha maswali.
Mfano:unayaonaje
maubiri ya leo?Ibada umeionaje?
6.Kudanganyika.
Aliyeacha kuambaatana
huwa mwepesi wa kudangnyika.
YOHANA 8:44
Ni hatua mbaya pale mtu
anapo danganyika na kumsema vibaya kiongozi wake au Baba yake wa kiroho.
MITHALI 30:17
7.Uasi wa wazi wazi
Hii hupelekea kupambana
ana kwa ana na mamlaka iliyo juu yao
Mfano:
Musa alipigwa waziwazi
na KORA,DATHANI,ABIRAM na wengine
viongzi 250
HESABU
16:1-4
Hitimisho la somo
·
Tujifunze kuwa na Amani na watu wote
WAEFESO 4:31-32
·
Ufalme wa Mungu unatekwa na watu wenye
nguvu.
MATHAYO 11:12
--------------*------------------------BARIKIWA--------------*-----------------
SOMO:
ROHO ZITENDAZO KAZI
Roho-Ni nafsi
inayofanya kazi katika ulimwengu wa roho:-
Kuna roho kuu tatu:-
i)Roho ya Mungu (Roho mtakatifu)
ii)Roho ya binadamu
iii)Roho ya kishetani
I.ROHO YA MUNGU (ROHO
MTAKATIFU)
Hii ni nafsi ya tatu ya
Mungu inayotenda kazi ndani ya
watakatifu wote.Kila aliyeokoka anapaswa kujazwa nguvu hii ya Roho mtakatifu
MATENDO YA MITUME 1:8
1 WAKORINTHO 12:14
II.ROHO YA
KIBINADAMU
Hii ni roho ambayo
hujajua mambo ya binadamu tu
I WAKORINTHO 2:11a
Roho ya kibinadamu inabeba mapenzi na mawazo ya
kibinadamu.
Pia wakati mwingine
manabii wa Mungu wanaweza wakatoa unadii
, lakini siyo utokao kwa Mungu bali ni
wao wenyewe.
YEREMIA 23:21-23
III.ROHO YA KISHETANI
Hii ni Roho
inayowaongoza watu kutenda mambo ya kipepo/maovu tu. Kama vile
uchawi/kuua/ubakaji n.k
MATENDO YA MITUME 16:16
IYOHANA 4:1a
ITIMOTHEO 4:1a
Hivyo tunapaswa
kuzipima/kuzijaribu Roho .kipimo kikuuu cha kuzipima /kuzijaribu roho ni NENO
LA MUNGU maana hili hutusaidia kupambana na roho
WAEBRANIA 5:14
WAEBRANIA 4:12-13
Neno la Mungu ndiyo
kiini cha maarifa yote
ZABURI 119:89
ZABURI 119:97-100
ZABURI 119:104-105
Neno la Mungu ndilo
linalotufanya tusiyumbishwe na kila aina ya upepo wa Eimu
WAEFESO 4:13-15
Hitimisho la somo
Tamani sana kuongozwa
na roho wa Mungu na zikae kwa nguvu zote
.Roho nyingine chafu na zituishe kabisa.