Ijumaa, 6 Desemba 2019

NAMBA MPYA YA PASTOR AMOS E. ONESMO

MPENDWA UNAYESOMA BLOG YANGU HII NAKUJUZA KUWA NIMEBADILI NAMBA YA MAWASILIANO BADALA YA 0756391498 NAMBA YANGU MPYA NI
0759199463

JINSI YA KUFUTA LAANA ULIYONAYO NA KUHARIBU MIZIMU YA UKOO WENU.



JINSI YA KUFUTA LAANA ULIYONAYO NA KUHARIBU MIZIMU YA UKOO WENU.

Karibu nikupe siri hizi ambazo zitasababisha uzima kwako na kuishi kwa raha. Neno la kutuongoza ni
Yohana 8:36 inayosema
'' Basi Mwana(YESU) akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli ''

Watu Wengi Wanateswa Na Laana Mbalimbali Zikiwemo Laana Kutoka Kwa Wazazi, Ndugu, Walimu, Majirani, Wachawi, Waganga Wa Kienyeji, Majini, Mizimu Nk. Laana Hizi Ni Mbaya Sana Na Wakati Mwingine Walio Kulaani Kama Ni Wanadamu Walishakufa Tayari, Huna Jinsi Ya Kuwaomba Msamaha Ili Laana Ifutwe, Wakati Mwingine Laana Zingine Ni Sahihi Kabisa Maana Ulifanya Jambo Baya Ukalaaniwa, Umeshindwa Kulivua Hilo Vazi La Laana Ulilovalishwa,
SIRI YA MIZIMU NA ROHO ZA UKOO PIA MADHARA YAKE.
Kila Ukoo Una Mizimu Yake Na Maroho Yake Ya Ukoo.
Mizimu Hii Na Maroho Haya Ya Ukoo, Ni Watenda Kazi Wa Shetani, Mizimu Huwa Haifi Maana Ni Kundi La Malaika Waasi Waliofukuzwa Mbinguni Pamoja Na lucifer(shetani).
Mizimu Kwenye Ukoo Wenu Zina Kazi Tatu.
1. Kuhakikisha Kila Jambo Baya La Ukoo Wako Lililowapata Babu Zako Tangu Vizazi Vingi Nyuma linakupata na wewe .
Kama Kuna Magonjwa Yaliwasumbua Babu Zako Lazima Yakupate Na Wewe, Kama Ukoo Wenu Huwa Hawafungi Ndoa Takatifu Na Wewe Itakua Hivyo Hivyo, Na Kila Lolote La Kishetani La Kiukoo Lazima Likupate Na Wewe.

2. Mizimu Ni Walinzi, Sio Walinzi Wa Uzima Wako Bali Wanakulinda Na Kuhakikisha Hufanyi Lolote Ambalo shetani Hajakupangia.
Na Kumbuka Kwamba shetani Hajawahi Kukupangia Jambo Jema Hata Siku Moja. Kuna watu leo akishika tu Biblia na kuanza kusoma usingizi unampata hiyo ni mizimu inakuzuia, kuna watu leo ukiwaambia twende kanisani anakuambia mwili umekua mzito ghafla hivyo labda siku nyingine mizimu hapo inamzuia.

3. Ni Watoaji Taarifa kuzimu Na Wapeleka Taarifa Zako Kuzimu. Ukipanga jambo lolote jema na la kimungu lazima utaona ugumu maana kabla hujaanza kutenda taarifa zako zimeshafika kuzimu na zinatendewa kazi kinyume na mipango yako. Dawa Ya Kuwaondoa Mizimu Na Roho Za Ukoo Ni Kumpa YESU KRISTO Maisha Yako,
Yohana 8:36 Inasema ''Mwana wa MUNGU akikuweka huru , utakuwa huru kweli kweli,'' Na uzuri wa MUNGU ni kwamba ametoa jina la YESU KRISTO ili kila aombaye awekwe huru kama inavyosema Yohana 14:13 '' Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana. ''

Ndugu jitenge leo na roho hizi za ukoo na mizimu ya ukoo kwa maombi ya vita kupitia jina la YESU KRISTO. Usikubali kuongozwa na mizimu na mapepo ya ukoo maana ukiongozwa na mizimu lazima utaishia tu kuzimu. Mizimu ni Giza kimbilia leo kwenye nuru ambayo ni BWANA YESU.
……………………………………………………………………………

Alhamisi, 18 Julai 2019

ONDOKA KIFUNGONI


ONDOKA KIFUNGONI

 







Na
Pastor AMOS E. ONESMO
Mawasiliano: 0756391498/ 0658727799/ 0683676447
@
2019

UTANGULIZI.
Kipekee namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuandaa Kitabu hiki kiitwacho:-
ONDOKA KIFUNGONI”.
Pia, namshukuru Mke wangu ANES  na Mwanangu GIFT Kwa mchango wao muhimu katika kukamilisha kazi hii.
Shukrani zangu za dhati zimwendee Mama yangu mzazi JOYCE kwa kunizaa na kunilea.
Ndugu msomaji wa kitabu hiki nakukaribisha sana tujifunze masomo Matano muhimu, ambayo ni:
1. VIFUNGO VITOKANAVYO NA MILA
2. AGANO LA KITOVU
3. ROHO YA KIBURI.
4. UKOMBOZI WA ARDHI.
5. MADHABAHU ZA UKOO.
Nakuombea Mungu akupe Uelewa mkubwa na akufanikishe zaidi na za zaidi.
Kwa swali lolote, Ushauri na mengineyo wasiliana nami.
Mawasiliano: 0756391498/ 0658727799/ 0683676447
@
2019
SOMO LA KWANZA
VIFUNGO VITOKANAVYO NA MILA
UTANGULIZI
Mila ni kawaida ya mtu au jamii Fulani. Mila ni taratibu zenye miiko za watu/jamii Fulani. Mfano: Mila ya kunyoa vipara kwa ajili ya wafu.
Mila zisizompendeza Mungu ni chanzo cha vifungo vya kiroho na kimwili kwa watu wengi. Kupitia mila watu wamejiunganisha na mizimu ya ukoo/familia iliyobeba mila hizo. Mila zisizofaa hubeba nguvu ya mizimu inayopelekea vifungo. Mila hugeuka chanzo cha vifungo maana baadhi ya mila zina Maagano yake ambayo zimebeba SIRI kubwa.

MIFANO YA MILA ZILETAZO VIFUNGO
1.     Kunyoa Vipara Kwa Ajili Ya Wafu.
KUMBUKUMBU LA TORATI 14:1
Huu ni utaratibu wa jamii nyingi za waliookoka na wasiookoka hususani jamii za kiafrika. Kuna madhara makubwa yatokanayo na mila hii, maana moja kwa moja ni kujiambatanisha na mzimu wa marehemu. Ndiyo maana wengine baada ya msiba hupata matatizo mengi kama vile ndoto mbaya za kumuota marehemu, magonjwa n.k.

2.     Kuabudu Waliokufa.
KUMBUKUMBU LA TORATI 18:10-11
Hii ni mila nyingine isiyompendeza Mungu inayofanywa na watu wengi. Hizi ni ibada ya kutambikia na kutoa kafara kwa ajili ya jambo Fulani ili mizimu ya marehemu iwasaidie.
Jiulize swali hili, “Tunapaswa kwenda kwa waliokufa kwa ajili ya walio hai?
ISAYA 8:19
Mila ni ibada isiyompendeza Mungu. Mila huambatana na sadaka za miungu ile inayosimamia mila hizo.
MUHIMU: Tambua chanzo na dhumuni ya mila hiyo katika familia yenu. Usikimbilie kufanya mila bila kujua chanzo na madhumuni utajiunganisha na Maagano ya mila bila kujua, na madhara yake yatakuwa makubwa.

MADHARA YA KUJIUNGANISHA N AMILA ZISIZOFAA
i.                   Kukutenga mbali na Mungu.
Hautakuwa na ushirikiano na Mungu maana hizo ni Ibada za mizimu

ii.                 Mikosi, laana vitaambatana nawe.
Shetani atakushambulia katika maeneo mbalimbali kama vile uchumi, maana hauna ulinzi wa Yesu.

NJIA ZA KUVUNJA KIFUNGO CHA MILA
1. Omba toba ajili yako na familia yenu.
Takasa kwa maombi ili kufuta madhara yatokanayo na vifungo vya mila.
2. Rejesha kilichoathirika katika maisha yako.
Kilichotetereka kama ni Afya au uchumi rejesha kwa upya kwa njia ya maombi.
YOELI 2:25
3. Futa kwa damu ya Yesu madhara yatokanayo na mila.
4. Mfukuze shetani aliyekaa katika ukoo wenu kwa njia ya MILA.
HITIMISHO: Usile vyakula vitokanavyo na sherehe za kimila, hii ni kwa sababu vyakula vile
                     hutamkiwa maneno ya kishetani (Agano).
MITHALI 23:8

.xxxx  MAARIFA HIYO JUU YA MILA IKUFUNGUE VIFUNGO …….xxxx

SOMO LA PILI
AGANO LA KITOVU
Agano ni patano/mkataba baina ya mtu na mtu/watu na watu/jamii na jamii.
Kitovu ni kiunganishi cha mama na mtoto awapo tumboni. Yaani alacho mama ndicho alacho mtoto aliyetumboni.
Kama Agano la kishetani linalofanywa kupitia kitovu. Agano hili humpa shetani uhalali wa kuyatesha maisha ya mtu.


Tulitazame Agano hili la kitovu kwa namna mbili:-
i)                   Kuunganishwa na Agano la kipepo la wazazi.
Hii ina maana kwamba, mtoto anarithi baadhi ya matatizo yatokanayo na wazazi wake. Kinachowapata wazazi ndicho mtoto anachopata, ugonjwa uliotesa wazazi hutesa na mtoto pia n.k.   EZEKIEL 16:4-6
Kitovu kutokatwa ni ishara ya uwepo wa mambo endelevu yatokanayo na wazazi wako. Kuna vitu vinakuathiri kwa sababu umerithi kutoka kwa wazazi.
Kitovu kukatwa ni ishara ya kujitenga na maagano ya wazazi wako, na ni muhimu sana kujitenga.

ii) Agano juu ya kitovu kiuhalisia
Yaani kitovu cha mtoto kinawekwa katika maagano ya kutamkiwa, kutambikiwa n.k baada ya kukatwa.  Kuna baadhi ya watu wanapata mateso kwa sababu baada ya kuzaliwa, vitovu vyao viliwekewa MAAGANO.
Maagano hayo yamefanyika kwa:-
Ø Kutambikiwa
Ø Kunuwiziwa
Ø Kuhifadhi ndani ya nyumba.
Ø Kutupwa bahari
Ø Kutupwa (kufukiwa) makaburini n.k


DALILI ZA KITOVU KILICHOFUNGIWA AGANO
-         Mashambulizi ya kitovu kwa njia ya ndoto.
Unakuta mtu anaota ndoto zenye kushambulia kitovu kama vile kuchomwa sindano, kisu au mkuki kwenye kitovu kwanjia ya ndoto.
-         Kufuatiliwa na majanga miaka hadi miaka.
HATUA ZA KUCHUKUA ILI KUWA SALAMA
Ø Kuokoka
Ø Wokovu utakuweka huru kabisa
Ø Kuombewa maombi ya kukata kitovu.
……….………..xxxx… Pokea Maarifa Ya Kiroho xxxx……………………….

SOMO LA TATU
ROHO YA KIBURI
Kiburi ni hali ya mtu kujiinua na kutoondoka kwenye msimamo wake hata kama ni msimamo hasi.
Roho ya kiburi ni kifungo kwa waliowengi kwani roho hii imewafunga waliowengi kiroho na kimwili. Kuna watu wameshindwa kufanikiwa kwa sababu ya kiburi watu wamepoteza marafiki, ndugu, huduma kwa sababu ya Roho ya kiburi.
Kataa roho ya kiburi kwani ni kifungo cha mafanikio yako kiroho na kimwili.  KUTOKA 5:2
Mtu mwenye roho ya kiburi huona kila anachokiwaza kimenyooka wala hawezi kusikiliza ushauri wowote kwa mtu yeyote. MITHALI 12:15
Roho ya kiburi ilimponza rusifa  ISAYA 14:12-15
TABIA 10 ZA MTU MWENYE KIBURI
1.     Hupenda kusikilizwa ila yeye hapendi kusikiliza wengine.
KUTOKA 5:2
2.     Hapendi kushauriwa na wengine ila yeye anapenda kushauri wengine.
MITHALI 29:1-2
3.     Hapendi kukosolewa ila yeye anapenda kukosoa kwa kila jambo.
MITHALI 13:10
4.     Hupenda kudharau wengine lakini yeye hapendi kudharauliwa.
WAKOLOSAI 3:13-14  MITHALI 14:21
5.     Hudai heshima kwa nguvu lakini yeye hataki kuheshimu wengine.
MITHALI 3:34-35.
Kiburi cha mtu kitamshusha, Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa.
MITHALI 14:15
6.     Hufurahi kuwaonea wengine na kuwasimanga lakini yeye hataki kuonewa wala kusimangwa.
OBADIA 1:12
7.     Hupenda kumiliki mali isiyo yake.
Ndugu hata fungu la kumi ni la Mungu hivyo kuacha kutoa zaka ni kumwimbia Mungu na hivyo ni roho ya kiburi.
MALAKI 3:8-9
8.     Anapenda kulaumu wengine ila yeye hapendi kulaumiwa.
9.     Anapenda kutiwa moyo lakini yeye hawezi kuwatia moyo wengine.
10.                        Hupenda kujulikana na hapendi wengine wajulikane.
MAANDIKO MACHACHE YAHUSUYO ROHO YA KIBURI
I SAMWELI 2:3 “Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa maarifa, na matendo hupimwa na yeye kwa mizani”.
MITHALI 13: 10 “Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana”.
MITHALI 15:25 “Bwana ataing’oa  nyumba ya mwenye kiburi; Bali atauthibitisha mpaka wa mjane”
MITHALI 29:23 “Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa”
MITHALI 16:5 “Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa Bawna; Hakika, hatakosa adhabu”.
Hitimisho La Somo
Ni muhimu kuikemea roho ya kiburi, maana Mungu huwapinga wenye kiburi. I PETRO 5:5-7. Mungu huwaangalia wenye roho ya kupondeka  ISAYA 66:2. Tumwombe Mungu atupe Roho ya unyenyekevu tunapomtumikia ili tuyaone mema kutoka kwa Mungu. WAFILIPI 2:3-5




SOMO LA NNE
SOMO: UKOMBOZI WA ARDHI
UTANGULIZI
Somo hili linalenga kujifunza mbinu za kuomba ili hali ya kiroho ya Ardhi iliyokwamisha mafanikio yako iondoke ili uweze kufanikiwa. Ardhi inatoa maamuzi juu ya watu wanaokaa juu yake kwa kutegemea imekabidhiwa kwa Mungu yupi.
-         Mungu wa Ardhi huamua mafanikio ya mtu.
Ardhi inaweza kuolewa na kuzaa matunda kutegemea Mungu aliyeioa.
ISAYA 62:4-5 “Hutaitwa tena aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, ukiwa; bali utaitwa Hefsiba; na nchi yako Beula; kwa kuwa Bwana anakufurahia, na nchi yako itaolewa. Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi harusi. Ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe”.
Ardhi haiwezi kuzaa pasipo kuolewa na kuzaa huko kunategemea Mungu/mungu aliyeioa ardhi hiyo.
Ardhi inaweza kuwa haizai kwa sababu ya LAANA. Ukisemesha Ardhi inaweza kuzaa hata kama haizai kwa ajili ya watu wengine.
Ardhi inaweza kutiwa unajisi na kuwatapika wenyeji.
MAMBO YA WALAWI 18:24-25
Nchi ikiwa najisi kwa sababu ya wanadamu, Mungu anaachilia adhabu juu ya nchi na nchi inaanza kuzaa mapooza 2 WAFALME 2:19-22
Ardhi inao uwezo wa kusikia, kutunza kila ilichokisikia na kutekeleza kile ilichosemeshwa.
KUMBUKUMBU LA TORATI 30:19-20
Ardhi inasikia maneno ya kinywa. Ukiitamkia mabaya inasikia na ukiitamkia mazuri inasikia na kutekeleza.
KUMBUKUMBU LA TORATI 32:1  YEREMIA 22:29-30
Unaweza kufanya eneo kwenye Ardhi kuwa sehemu ya kukutana na Mungu wako.
Madhabahu ya Mungu inajengwa na Yakobo katika Ardhi ili pawe ukumbusho wa Agano.
MWANZO 28:16-22
“16 Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua.
17 Naye akaogopa akasema, mahai hapa panatisha kam anini: Bila shaka hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.
18 Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake.
19. Akaita jina la mahali pale Betheli, lakini jina la mji ule hapo kwanza aliiitwa Luzu.
20. Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendayo na kunipa chakula nile, na nguo nivae.
21 Nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu.
22. Na jiwe hili nililosimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakulea wewe sehemu ya kumi”
Alama unayoiweka kwenye Ardhi ni ukumbusho wako na Mungu wako. MWANZO 35:6-7
Ardhi ina uwezo wa kumuondoa mtu na kumlinda mtu aliye juu yake. Haijalishi kama unajua au haujui kawaida ya miungu/Mungu wa mahali unapokaa, kama ukikosea utashambuliwa/ utapigwa na Mungu/miungu.


2 WAFALME 17:24-28
Mapepo yanaweza kumilikishwa Ardhi na yakadai kisheria kuwa na uhaliali wa kuwepo mahali pale walipomilikishwa.
MARIKO 5:1-10
Msitari wa 10 “Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile  Mapepo yalitaka yasipelekwe nje ya utawala wao.

NAMNA YA KUOMBA ILI HALI YA KIROHO YA ARDHI ILIYOKWAMISHA MAENDELEO YAKO IPATE KUONDOKA.
1.     Tambua Mungu wa Ardhi hiyo
Elewa kwa makini masharti  yaliyopo katika Ardhi yatokanayo na mungu wa eneo.
          2 WAFALME 17:24-29
2.     Omba toba juu ya Ardhi ili Mungu aiponye.
2 NYAKATI 7:12-14
Andiko hili halizungumzii uponyaji wa watu bali uponyaji wa Ardhi.
3.     Futa laana juu ya Ardhi
Futa laana zilizosababishwa na dhambi za waliotangulia, n.k
MWANZO 3:17-19
Dhambi ya Adamu ilipelekea Ardhi kulaaniwa. 
Shughulikia laana iliyo katika Ardhi kwa Damu ya Yesu.

4.     Weka wakfu kwa Mungu eneo hilo.
Mkabidhi Mungu hilo eneo. Mungu anataka umakabidhi rasmi ili alitawale eneo hilo.
5.     Jenga madhabahu ya Bwana katika eneo MWANZO 28:16-22
Hitimisho la somo
Unaweza kuwa kwenye eneo linalomilikiwa na shetani kihalali katika ulimwengu wa giza, hivyo usiridhike pambana kiroho.
  ;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;MWISHO WA SOMO;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;;




SOMO LA TANO
SOMO: MADHABAHU ZA UKOO
Madhabahu – Ni eneo linaloweza kutumiwa na Mungu au shetani/miungu ili kupitisha nguvu, utawala na mamlaka kwa watu wanaokusanyika mbele yake.  Ni sehemu maalumu ya kukutana na Mungu.
Katika Ukoo mtu anaweza kuwa ndiye madhabahu ya ukoo.
MATENDO YA MITUME 16:17-24
Aliyetolewa mapepo alikuwa ni MADHABAHU ya eneo.
Kamwe watu hawawezi kufanya jambo Fulani bila kumuuliza kwanza aliye MADHABAHU ya eneo. Kama vile kugombea nafasi za uongozi.
Madhabahu ya miungu na ya Mungu hujengwa na mwanadamu mwenyewe.
Mifano Kibiblia ya waliojenga Madhabahu
Ø Familia/ukoo wa Nuhu watu walikuwa wamebadilika kwa kutenda maovu, Mungu akaamua kuondoa uharibifu huo kwa kupitia Nuhu.  Nuhu akamjengea Mungu Madhabahu. MWANZO 8:15-22
Ø Abrahamu alimjenga Mungu Madhabahu. MWANZO 12:7
Ø Yoshi alimjenga BWANA Madhabahu. WAAMUZI 6:25-26

Familia/koo haiwezi kwenda mahala popote kama mfumo wao wa maisha, umeshikiliwa kwenye MADHABAHU YA KICHAWI/KISHETANI.
Inawezekana familia /ukoo umeshikiliwa  na mfumo wa madhabahu, ndiyo maana matatizo ya ukoo wako yanafanana.
Ø Kwenye ndoa
Ø Katika masomo
Ø Katika mafanikio

WAAMUZI 6:24
Gideoni kabla ya kuibomoa Madhabahu ya Baba yake alijenga Madhabahu ya Baba yake akaiita jina la Jehova Shalon (Maana yake Mungu wa Amani) familia yake imepata Amani.

Ni vizuri kujua kwamba, je madhabahu unayokwenda kuabudu unamjua anayeabudiwa hapo? Kila Madhabahu kuna Mungu anayeabudiwa hapo.

KAZI YA MADHABAHU

Madhabahu ya kimiungu na Mungu zina kazia kama ifuatavyo:-
i.                   Kutoa majibu ya malalamiko ya watu na kutoa ufumbuzi.
Madhabahu za kimiungu hutoa ufumbuzi usiosahihi
Madhabahu za ki-Mungu hutoa ufumbuzi sahihi.

ii.                 Kutatua matatizo ya watu wa eneo
Madhabahu za kimiungu huongeza matatizo badala ya kuyatatua.
Madhabahu za Ki-Mungu huleta majibu ya matatizo ya watu wa eneo.





MUUNDO WA MADHABAHU
KINACHOTEGEMEWA NA MADHABAHU
MADHABAHU YA KI-MUNGU
MADHABAHU YA KI-MIUNGU/SHETANI
i.  Mungu wa madhabahu
Mungu
Shetani/mapepo/mizimu
ii.     Nguvu ya madhabahu
Nguvu za Ki-Mungu
Nguvu za kipepo mizimu/majini
iii.  Sadaka ya madhabahu
Sadaka
Kafara (Kumwaga damu)
iv.  Kuhani wa madhabahu.
Wachungaji/watumishi mbali mbali wa kiroho
Waganga wa kienyeji /Wachawi na mawakala wengine wa Shetani

Hitimisho la somo
Jenga madhabahu ya Ki-Mungu katika ukoo wenu ili kuiangusha ile ya Ki-Miungu inayoleta madhara mengi katika ukoo kama vile vifo vinavyofanana, kufuatana, magonjwa ya kufanana, tabia za kufanana n.k.


MAWASILIANO

0759199463