SOMO LA KUHUBIRI
Kuhubiri ni kutoa Ujumbe wa Bwana
Yesu kwa watu/washirika kwa Wakati Mungu alioukusudia. MATHAYO 28:19
Kuna vitu viwili muhimu sana vya
kuzingatia unapoandaa Mahubiri:-
i.
Ujumbe (Content)
ii.
Namna ya kuwasilisha (Presentation)
MAMBO MUHIMU KABLA YA MUDA/SIKU YA KUHUBIRI.
1. Kuvaa nguo nzuri
na nadhifu
2. Jiandae
kimaombi, kemea roho za kishetani za kuwafanya watu wasilielewe Ujumbe na roho
za mazoea. Omba Mungu akupe ujumbe na akupe Ujasiri.
3. Teua kichwa
cha Ujumbe utakalofundisha, kichwa cha Ujumbe kisiwe kirefu sana utawachosha
wasikilizaji na kiwe cha kueleweka.
4. Andaa maana
ya Maneno magumu kutoka kwenye kichwa cha Ujumbe wako.
5. Tafuta
vifungu vya Biblia vinavyoelekeana kwa uhalisia na Ujumbe uliokusudia
kufundisha/kuhubiri. Kama ni mahubiri na si mafundisho inashauriwa kuwa na
vifungu vichache usiwachoshe wasikilizaji.
6. Andaa
mifano ya Kibiblia pale inapobidi na si kujitolea mfano wewe au maisha yako. Ni
afadhali pale inapobidi kutolea mfano mtu mwingine na si wewe. Kujitolea mfano itaonekana
unajiinua/kujisifia mbele za watu.
MAMBO MUHIMU WAKATI WA KUHUBIRI.
1. Matumizi
sahihi Muda, Tambua Mahubiri yako yanatakiwa kutumia muda gani? Kutumia muda
mrefu utawachosha watu. Na ukitumia muda mfupi utawashangaza watu pia maana
ibada itakuwa fupi.
2. Ondoa hofu,
Mpe nafasi Roho mtakatifu akutumie. Usiwaogope unaowahubiri bali
uwastahi/Uwaheshimu.
3. Tazama watu
unaowahubiri usoni. Watazame usoni na si chini ili kuwafanya wawe makini
kukusikiliza na wasipige kelele (Maintain eye contact), wala kusinzia. Wakazie
macho wasikilizaji.
4. Jiunganishe
na unaowahudumia. Kuwa shemu yao,
usionekane wewe uko juu zidi yao maana badala ya kujifunza Neno watatumia muda
huo kukutafakari wewe ni mtu wa namna gani?
5. Mbinu za
uwasilishaji wa Ujumbe, Tumia mbinu mbali mbali kuhakikisha watu hawalali wala
kuchoka na watamani uendelee kuhubiri. Mfano: Jitahidi kuwafanya Wacheke,
Wafurahi, Wavutiwe na Mahubiri n.k . Hakikisha unalichangamsha Kanisa au
kusanyiko unalolihudumia.
6. Kaa kwenye
uwepo wa Mungu wakati wa Mahubiri ili uyanene aliyoyakusudia Mungu kwa watu
wake.
7. Msukumo wa
ndani yako ukiisha, usiendelee na Mahubiri ishia hapo.
8. Lugha ya
staha, usitumie maneno yasiyo na staha unapowahubiri hasa wakati wa kutoa
mifano. Zingatia kuwa unaowahudumia wana utamaduni na mila tofauti, ambapo
baadhi ya maneno ukiyatamka kwa baadhi ya watu ni MATUSI.
9. Usichanganye
lugha, tumia lugha kwa usahihi bila kuchanganyachanganya ili usikwamishe uelewa
kwa wasikilizaji.
10. Usitumie
sauti ya kuiga.
MAMBO MUHIMU BAADA YA KUHUBIRI.
1. Mshukuru
Mungu kwa kukutumia.
2. Mpe Mungu
utukufu kwa kukutumia na si kujisifia wewe mwenyewe, watu wakikusifu wambie
BWANA AMEJITUKUZA. ISAYA 42:8
3. Endelea
kuiombea Huduma iliyo ndani yako ili Mungu aendelee kukutumia zaidi na zaidi.
4. Epuka
kiburi kisikuharibie Huduma.
------------------------------------------------------------MWISHO-------------------------------------------------------
‘BARIKIWA SANA’
Na;
Pastor. Amos E. Onesmo
0756391498
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni