LEADERS POSITION AND ABILITY.
NAFASI YA KIONGOZI NA UWEZO.
1.
Kiongozi ni lazima awe msimamizi wa
mambo.
a) Andaa
watendakazi – Organize Workers. Kuandaa Watenda kazi ni kazi ya Kiongozi.
Shirikisha watu wengine huduma za Kanisa.
b) Andaa
Utendaji – Kama vile Mikutano ya Injili, Mikutano ya Vijana, Kina mama, Watoto
na kila kazi ipangwe kwa Utaratibu.
c) Tawala
mambo ya Fedha. I Timotheo 6:10 Ebr 13:5
d) Gawa
Watendaji, wapange watenda kazi ili uwepo daima katika Uwepo wa Roho Mtakatifu.
2.
Uwe na Uwiano mzuri “BE BALANCED MAKE
TIME FOR ALL THESE”.
a) Uwe
na muda wa kusoma.
b) Uwe
na muda wa Maombi.
c) Uwe
na muda wa kuhudumia familia.
d) Uwe
na muda wa kufanya mazoezi.
e) Uwe
na muda wa kupumzika.
f) Uwe
na muda wa matembezi.
g) Uwe
na muda wa kuwa Ofisini.
3.
Uwe mtu mwenye huruma, “BE COMPASSIONATE”
Neh 1:4
a) Kugusa
wengine.
b) Kufundisha
wengine.
c) Kumgusa
Mungu.
d) Gusa
wenye masikio ya kusikia.
e) Gusa
wenye kujisikia.
f) Gusa
mikono ya wengine iwafikie wengine.
Watu wa muhimu ambao
wanatakiwa wawe na huruma ni watumishi wa Kanisa, maana Roho inayokuwa ndani ya
Kristo inakuwa ndani yetu. Zile tabia zote za Kristo zinakuwa ndani yetu. Mith
19:17 Kut 23:21 Kumb 15:7-8 Mith 21:13 28:27
4.
Simamia kuyatenda yale uliyosema, “BE
DELIGENT” Hes 18:26-32. Fanya kile unachofundisha Ezra 7:10. Toa sehemu ya
kumi, Sadaka, Shukrani na michango mingine.
5.
Uwe na Mzigo mkuu – BE ETHUSIASTIC. Kama kiongozi, jitahidi kumshukuru Mtenda
kazi mwenzako hata kama hakutenda vizuri. Tusianze lawama mbele ya wale
tunaofanya kazi nao. Mwishoni waweza
kumwonyesha kile hakufanya vizuri.
6.
Uwe mwaminifu – “BE FAITHFUL”
a) Kwa
Mungu.
b) Kwa
kusanyiko lako.
c) Kwa
Huduma yako.
d) Kwa
muda.
7.
Uwe Mlinzi mzuri – “BE A GUARDIAN”
a) Linda
kundi.
b) Linda
wale wenye migawanyiko. I Kor 3:3 Rum 16:17
Tito 3:10 IKor 1:10.
c) Epuka
masengenyo na Wivu.
8.
Uwe mnyenyekevu “BE HUMBLE”
a) Uwe
mnyenyekevu kutumika kwa mikono yako.
b) Yesu
naye alikuja kutumika siyo kutumikiwa.
9.
Ujihusishe – Husika – BE INVOLVED.
a) Wewe
kama Kiongozi husika katika matukio yote.
b) Jihusishe
na Vijana, Kina mama, Wanaume na watoto.
10.
Uwe mwenye haki na usawa, “BE JUST AND
FAIR”
a) Wakati
wa maamuzi Usiamue kwa upendeleo.
b) Vitu
vyote viwe kwa wote.
c) Pokea
wote sawa sawa.
d) Wanatakiwa
watu aina mbalimbali Kanisani.
KANUNI
MUHIMU KUHUSU VIONGOZI NA WATAWALA WA KANISA.
1.
Kiongozi wa Kiroho ni mtu anayeweza
kufikiwa na watu kwa Urahisi. Neh 1:2
Mfano
mzuri: Tunajifunza kutoka kwa Nehemia 1:2 wakati watu walipokuwa wametoka Yuda
Nehemia alijitokeza kuwasalimu na alichukua muda kuongea nao. Huu ni mfano ulio
mzuri kwetu kufuata.
Wakati
wetu tunao viongozi wengi wenye kiburi na majivuno, huwezi kuwaona kwa Urahisi,
hadi wengine wameweka kiwango cha fedha ili upate kuwaona.
2.
Wewe kama Kiongozi uwe na shauku ya
kutaka kujua jinsi wengine wanavyoendelea Neh 1:2
Nehemia
alihitaji kujua habari za watu wengine jinsi walivyokuwa wanaendelea. Nehemia
alikuwa na maono yaliyopanuka si maono finyu. Na viongozi walio na mafanikio ni
wale wanaopendelea kusikia na kuona wengine wakifaulu.
3.
Kiongozi Sharti ajue jinsi ya
kukabiliana na taarifa mbaya zinazomjia. Neh 1:3
Kwa
kweli hatuwezi kutegemea kupata habari nzuri kila wakati, kwa maana hiyo
Kiongozi anatakiwa kusitahili kuwa na moyo mkuu ulio tayari kusikia na kupokea
habari mbaya na kuweza kuikabili na masaibu yake. Neh 1:3
4.
Kiongozi mzuri wa kiroho ni Yule ambaye
ni Mwombaji. Neh 1:5
Kiongozi
unapoweza kusikia habari za kutatanisha sharti uchukue hatua za kuomba Mungu
juu ya jambo hilo na kumkumbusha juu ya Ahadi zake, Neh 1:6-8. Kwa hiyo Omba
Mungu afanikishe malengo yako Neh 1:11.
Kabla
ya kufanya maamuzi Kiongozi sharti ufanye Maombi, Neh 2:4. Usijitegemee akili
zako Uwe na bidii kuomba Mungu kabla ya kufanya Maamuzi yoyote kwenye Mikutano
au vikao vya kanisani. Kama Viongozi watakuwa makini kuhusu hili mitafaruku na
kutofanikiwa kwa Miradi kungepungua, tuwe kama Yesu alivyokuwa.
5.
Viongozi sharti wajue jinsi ya kuutumia
muda ili kujituma. Neh 2:6
Kila
kiongozi ambaye ana hamu ya kuwa Kiongozi bora sharti ajue jinsi ya kuutumia
muda wake vizuri na kupanga ratiba ya kazi, kama Nehemia 2:6
Jua
jinsi ya kupanga kazi na kutazama mbele unakokwenda, kile kinachosumbua moyo
wako ndicho kitakachosukuma mikono yako kutenda kazi na kuisukuma midomo yako
kuomba.
Nehemia
alimpa ratiba Mfalme juu ya mikakati yake ya ujenzi wa Yerusalemu. Viongozi
wengi huwa hawana ratiba wala misimamo na maneno yao hayawezi kutegemewa.
Malengo
yasiyo na mwelekeo na muda maalumu hayawezi kumshawishi au kumhamasisha mtu
yeyote. Biblia inasema---ndiyo yenu iwe ndiyo na siyo yenu iwe siyo.
6.
Viongozi wazuri wa Kiroho ni wale walio
na uwezo wa kuona mbali. Neh 2:7-8
Nehemia
aliyefaulu kuwa kiongozi bora, anatufundisha jinsi yeye alivyoona mbali
matatizo ambayo yangemkabili katika safari yake. Kwa hiyo alifanya matayarisho
ya kutosha tena mapema. Hakutaka kukutana na vizuizi katika kuvuka majimbo
kadha wa kadha, hivyo alichukua pasi yake ya kusafiria, Viza na ruhusa kutoka
Irani hadi Israel. Hivyo, viongozi wazuri ni vizuri wajue wazi mahitaji yao na
kuweka mikakati kwa makini.
7.
Viongozi wa kiroho waliopevuka
humshirikisha Mungu na Wanadamu. Neh 2:8-9
Nehemia
alimtegemea Mungu, kwanza alimpa utukufu wote kwa mahitaji yake yote, pili
alimwomba Mfalme amsaidie kwa kumpa ruhusa na vibali vifaavyo, nyenzo za ujenzi
na Ulinzi katika safari yake.
Sisi
sote tunahitajika kumtegemea Mungu na Wanadamu wengine wanaoweza kutusaidia.
8.
Viongozi sharti wajue jinsi ya kutumia
mamlaka. Neh 2:9
Barua
alizopewa Nehemia na Mfalme zilikuwa hati muhimu za utambulisho, kwa maana hiyo
hakuzificha alitambua thamani ya hati hizo na akazitumia kikamilifu.
Twahitajika
kujua kama Viongozi kujizoeza kutumia rasilimali zetu tulizopewa na Mungu hivyo
tujue ni wapi tutumie asilimali gani na wakati upi?.
9.
Viongozi wa kiroho sharti wajue jinsi ya
kutunza Siri. Neh 2:11,16
Viongozi
wa kiroho ni mawakili wa Siri za Mbinguni. Wanazo hekima, maarifa na akili za
kawaida hawana upungufu katika fahamu zao hivyo hawapaswi kuwa Waropokaji
hovyo. Nehemia alijua jinsi ya kuficha Siri. Viongozi tunapaswa tuwe kama
Nehemia. Kuna mambo ambayo hayatakiwi kusemwa wazi kabla ya Wakati wake,
haujafika.
Tuwe
watu wa Siri kupitia Mikutano yetu ya Kiofisi, Mikutano ya Bodi, kumbukumbu za
Mikutano hii haistahili kutolewa nje.
Mfalme
Hezekia aliingia Shida hii ya kutoa Siri akawa habari kauzwa. Tukiwa habari
kauzwa katika jamii sisi tulio Viongozi matokeo yake watu hawatatuamini tena.
10.
Viongozi wa kiroho ni vizuri wawe ni
watu wanaoweza kufanya Utafiti. Neh 2:13-15
Nehemia
alitaka kujua hasa uharibifu wa Yerusalemu ulikuwa wapi na ni mahali gani
panapohitajika kukarabatiwa.
Utafiti
utakaoufanya na uchanganuzi utakusaidia wewe kuweka maazimio Fulani. Aidha
utakusaidia wewe kuweka mikakati yako vizuri. Ukifanya hivyo utajua ni kiwango
gani cha fedha unachohitaji na kazi yenyewe itachukua muda gani.
11.
Viongozi wa Kiroho wanatakiwa wawe wa
kwanza kutoa habari mbaya. Neh 2:17
Nehemia
aliwaambia watu wazi wazi kile walichokuwa wanakiona kwa macho yao kila siku.
Hata watu wa Yerusalemu wenyewe walikuwa wamechoshwa na kukiona kifusi katika
mji wao. Kwa hiyo hawakuweza tena kuvumilia dhihaka kutoka kwa maadui zao.
Ikiwa
unataka kuwashirikisha watu jambo Fulani anza pale mnapokubaliana kila mmoja
huweza kusikia maumivu, hivyo panahitaji msaada . Na kwa pamoja mtatafuta
ufumbuzi.
12.
Kama Viongozi wa kiroho na wasimamizi wa
Utendaji kazi ni sharti wawe tayari kutoa sababu kwa nini kazi ifanywe. Neh
2:17-18
Kama
Viongozi tunaitajika kuwasiliana na watu tunaowaongoza kwa njia ambayo ni ya
kueleweka na kuweka wazi lengo la kuwaomba kuifanya kazi, tujaribu kuvuta
tuwezavyo kuvuta mantiki yao, hadhi yao na Umakini wao katika kuelewa mambo pamoja
na hisia zao. Usiwaombe wakutii tu pasipo kuwaelezea faida za Utii wao, kwa
kufanya kazi ile.
13.
Viongozi wa kiroho sharti waweze
kuambukiza wengine. Neh 2:18
Katika
kuwapa watu changamoto na kuwaonyesha suluhisho lililoko juu ya jambo Fulani.
Viongozi sharti wawe na mtazamo mzuri wa kutarajia mafanikio. Tuwe na ile hali
ya kuwaambukiza wengine, ikiwa wewe ni kiongozi asiye na haiba kubwa wala
kipawa cha Usemi, basi ni bora kumtafuta msemaji mzuri kama Musa alivyotafuta
na kumchagua nduguye Haruni.
Viongozi
wazuri huwatoa watu kutoka kwenye mawazo butu ya kitumwa, mawazo ambayo
humfanya mtu kujiona kama mtu asiyefaa asiye na uwezo wowote wa kuyadhibiti
mazingira yake. Ni jukumu lako kuwatia moyo kuwa wana uwezo.
14.
Viongozi wa kirohoni Sharti wawe tayari
kupambana na Upinzani. Neh 2:19.
Mtihani
mgumu kwa Kiongozi wa kiroho ni pale ambapo unakwenda kupambana na kukabiriana
na hali Fulani ya hatari na upinzani. Adui alimdhihaki Nehemia na kusema kwamba
yeye alikuwa akiasi sheria. Nehemia hakubishana na Adui wala kujitetea bali
alisema tu kila alichokuwa anaamini kwamba Mungu alikuwa amewafanikisha kwa
kusisitiza aliongeza kusema kila mtu alihusika kujenga ule ukuta wa Yerusalemu.
Ni
juu yetu kama Viongozi kupambana na Upinzani ambao unaweza kujitokeza kwenye
huduma zetu, Makanisa yetu na nyumba zetu.
15.
Viongozi wa kiroho sharti wamjulishe
Adui yao hatari zinazomkabili.
Nehemia
aliwajulisha Maadui zake kwamba hawana sehemu katika kazi yake, na pia
wasifikirie kuwa kazi itakapokwisha watafurahia matunda yake, ni wazi wao wako
kinyume na mpango wa Mungu. Kule kumwambia Adui waziwazi kwamba hana Urithi
wowote katika kazi ya Mungu, kulijenga Imani ya kiongozi pamoja na wale
anaowaongoza, wale waliokuwa wanajenga walitambua kwamba kazi yao siyo bure.
16.
Viongozi wa kiroho sharti wasiwabague
wanawake. Neh 3:12
Katika
kujenga upya Ukuta wa Yerusalemu, Nehemia aliwahusisha wanawake pia. Wanawake bila shaka yoyote wana sehemu za
Uongozi Neno linasema, “Mimi niliwatoa katika nchi ya Misri, Nilikomboa kutoka
Utumwani niliwapeni Musa, Haruni na Miriam ili kuwaongoza. Huyu Mama Miriamu
naye alikuwa Kiongozi. Wanawake katika Uongozi hutoa mchango mkubwa ambao
hauwezi kupatikana kwa Wanaume, wanawake ni Viungo muhimu katika kufanya maamuzi
katika kazi ya Mungu na hata Biashara.
17.
Viongozi wa kiroho wanatakiwa wawape
watu Uongozi au majukumu kulingana na Uwezo wa mtu alivyo. Neh 3:13-14
Nehemia
kama msimamizi mkuu alijua vema ni nani anafaa kwa kazi ipi na wap. Ni vizuri
kuwajua wasaidizi wako kila mmoja anaweza kufanya nini na ukishawagawia
ujitahidi kama Kiongozi kupata ripoti za mara kwa mara. Hakikisha unajua kila
mtu anafanya kazi gani, chunguza ujue iwapo kazi anayofanya mtu huyo ina
matokeo mazuri au ni kazi ya kupoteza wakati tu.
Jiulize,
je unaoufahamu wa kutosha kuhusu kazi zinazofanywa? Je, unamjua kila mtu na
kazi yake? Je, utafanya nini uwe kama Nehemia?
18.
Viongozi wa kiroho waliokomaa wawe
tayari kukabiliana na shutuma. Neh 4:1-2, 4.
Kukabiliwa
na shutuma ni sehemu moja katika Uongozi, ikiwa wewe kama Kiongozi hushutumiwi
basi huenda wewe siyo kiongozi mzuri au hata labda Uongozi wako hauna athari
zozote nzuri. Pamoja na kwamba kuna shutuma mbaya, pia zipo nzuri. Watu wanaweza
kushutumiwa kwa njia ya upendo na kututoa katika makosa Fulani ya Kiuongozi kwa
njia hii tunaweza kuboresha Uongozi wetu.
Njia
pekee ya kupambana na Upinzani mkali katika kazi siyo kujitapa na kupayapaya
bali ni kulipeleka mbele za Mungu kwa njia ya Maombi. Nehemia alimimina moyo
wake kwa Mungu wake na kwa njia hiyo akaweza kupata nguvu mpya za kumwezesha
kuendelea na kazi ya ujenzi.
19.
Kiongozi wa kiroho ni Sharti awe
anaandika ripoti za Maendeleo ya kazi yake. Neh 4:6
Wewe
kama kiongozi hakikisha unafuatilia kwa makini maendeleo ya kazi na halafu
unawataarifu watu juu ya maendeleo hayo. Watu huwa wanataka kujua jinsi kazi
inavyoendelea.
20.
Viongozi wa kiroho ni lazima wajue jinsi
ya kuyatatua matatizo. Neh 4:9
Nehemia
aliambatanisha Maombi pamoja na Vitendo. Kazi nyeti ya Kanisa na hata kama kazi
nyingine ni kutatua matatizo kama Yesu alipokuja alikuja kuyatatua matatizo
Duniani. Matatizo hayawezi kutuondokea kwa kuyafumbia macho na kuyachukulia
kama hayapo. Wewe Kiongozi usiharakishe kusuruhisha matatizo. Kama wewe
Kiongozi huna Uwezo wa kutatua tatizo Fulani tafuta mtu anayeweza kukusaidia
kutekeleza kazi hiyo.
21.
Kiongozi wa kiroho aliye makini
huwasikiliza watu waliovunjika Moyo. Neh 4:10
Wajenzi
wa Ukuta wa Yerusalemu walikuwa wanazifuata hisia zao na kuathiriwa na Uchovu
uliowazunguka. Walipotazama mlima wa kifusi hali ya kujiamini ilitoweka. Wakati
tunapokosa kujiamini hali ya kuvunjika Moyo hujipenyeza ndani yetu. Viongozi
sharti wawe makini kutambua wakati unaposikia shutuma Fulani jaribu kutafuta
chanzo chake, kwa sababu watu wanaokashifu hudidimiza hamasa na matumaini ya
watenda kazi. Inapofikia hapo ni jukumu la Viongozi kuingilia kati na kujenga
upya Imani ya Watenda kazi. Kufaulu kwako kunategemea hamasa ya watenda kazi
wako, kwa hiyo ni lazima Uwatie Moyo.
22.
Kiongozi mzuri ni Yule anayesikiliza
malalamishi ya watu. Neh 5:5-8
Katika
mji wa Yerusalemu kulikuwa na Unyanyasaji uliokuwa kama Utumwa. Wayahudi
matajiri waliwanyanyasa wale waliokuwa maskini. Basi shida zilipozidi watu
walimkimbilia Kiongozi wao kutoa kilio chao.
Viongozi sharti wawe watu wanaoweza kusikiliza vilio vya watu.
Usiyafumbie macho matatizo ya watu. Ikiwa wewe husikilizi malalamiko ya watu,
basi unaishi katika ulimwengu usiokuwa halisi. Watu hawatakuheshimu ikiwa
utayapuuzia malalamiko yao na kutowasaidia kwa njia yoyote ile.
23.
Viongozi wazuri wa kiroho sharti wawe
watu wanaoweza kutenda kile wanachosema. Neh 5:15.
Ukiwa
wewe ni Kiongozi usiache kuonyesha mwenendo wako waziwazi. Wakati watu wanauona
mwenendo wako kuwa mzuri na jinsi unavyoishi na kuyatekeleza mambo yako ya kila
siku kwa njia ifaayo watakutegemea na kukuiga. 2 Kor 8:21
24.
Viongozi makini sharti wawe tayari
kupuuzia baadhi ya Mialiko isiyo na maana. Neh 6:1-2
Viongozi
sharti wawe na uwezo wa kuweza kutambua mitego iliyotegwa ili kuwanasa. Sisi
sote twastahili kuwa na Uwezo wa kugundua hila Fulani inapopangwa. Ijapokuwa
makongamano ni muhimu na huleta Baraka nyingi, wakati mwingine yanaweza kuwa
njia ya kupoteza wakati. Nehemia alitambua kwamba mwaliko ule ulikuwa mtego tu.
Viongozi lazima tugundue ni mkutano upi tuhudhurie na upi tusihudhurie.
Usiitikie kila Mwaliko unaoupata.
25.
Kama Kiongozi jitahidi kutumia Vipawa
vya watu wengine. Neh 8:2-3, 7-8
Wewe
kama Mchungaji Kiongozi sharti uwaalike watu wengine Kanisani kwako kuja kuhudumia.
Alika watu wenye Vipaji tofauti na wewe ili waweze kulisaidia kanisa lako
kulikuza kiroho. Alika wale walio wanyenyekevu katika huduma zao.
SEHEMU YA MWISHO.
VIONGOZI WA KANISA NA
WATAWALA WANAVYOWEZA KUONGOZA MIKUTANO NA VIKAO.
UTANGULIZI.
Mikutano
na Vikao vimekuwa ni sehemu ya kazi na mila popote ambapo kuna jumuia au
mkusanyiko wa watu hasa kipindi kile cha kutaka kufikia maamuzi ya pamoja. Na
umuhimu wa Vikao utazidi kuongezeka kadri maendeleo ya mitazamo tofauti
inavyoongezeka. Kuna kipindi watu hawana haja ya vikao kwa sababu wanadai Vikao
vingi vinadhoofisa utekelezaji Kwakuwa vikao vingi huwa havina lengo la wazi au
huchukua muda mrefu kuliko inavyostahili. Lakini ukweli usiopingika kwa sasa
watu hupenda vikao sana ingawa nayo pia ina kasoro zake maana watu hupenda
kuzungumza mno kwenye vikao, na hutumia muda mwingi na kudhoofisha utekelezaji.
Kazi
ya kuandaa na kuendesha mikutano na vikao ni miongoni mwa kazi zinazokwepwa
sana na watu wengi sababu kubwa ya kukwepakazi hii ni kuwa hawajui namna ya
kuifanya. Hatuwezi kuwalaumu watu hawa kwa sababu hawajapata bahati ya
kuendelezwa wala kupewa mbinu za utaratibu wake.
Kiongozi
anapokabiliwa na kazi ya kuandaa au kuendesha mikutano kwa mambo mengi ya
kushughulikia.
1.
Kutafakari na kuzielewa shabaha za
Mikutano.
2.
Kuyaelewa mambo vizuri yatakayojadiliwa.
3.
Kuitisha mikutano na Vikao.
4.
Kuendesha Vikao na kuhakikisha kuwa
Shabaha zake zinafikiwa.
5.
Kuweka kumbukumbu za vikao na Mikutano,
kwa njia ya Mihutasari.
Mafanikio
yoyote ya Vikao na Mikutano hutegemea sana maandalizi na Uendeshaji wake. Mbinu
za uandaaji na uendeshaji wa mikutano na vikao hutofautiana, kwa mfano Uandaaji
na Utendaji wa Mkutano wa Kamati ni tofauti na ule wa Mkutano mkuu. Kwa hiyo
Viongozi ni vema kuelewa mahitaji ya kila aina ya Mkutano au Kikao.
Mwongozo
huu utaweza kuwasaidia Viongozi wote wanaohusika na Mikutano na Vikao
mbalimbali kama vile Wenyeviti, Makatibu, Wakurugenzi na Wahudumu waaandaaji
wote watajua jinsi ya kuendesha Vikao na Mikutano kwa kufuta Miongozo mizuri.
I.
MAHITAJI
YA MKUTANO.
Kwa
kawaida Mkutano aina yoyote unahitaji vitu vinne, Mwenyekiti, Katibu, Ajenda na
Wajumbe.
a) Mwenyekiti
– huyu ndiye kiongozi wa mkutano aliye na majukumu yafuatayo.
1. Kutoa
Uamuzi wa kuitisha mkutano.
2. Kuidhinisha
Ajenda za Mkutano.
3. Kufungua
mkutano.
4. Kuendesha
Mkutano.
5. Kuhakikisha
kuwa shabaha za mkutano zinatimizwa.
6. Kuhakikisha
kuwa Wajumbe wanapewa nafasi sawa za kuuliza maswali, kushiriki katika
majadiliano na kutoa mapendekezo.
7. Kupiga
kura ya Uamuzi iwapo kura za wajumbe zitalingana.
8. Kufunga
Mkutano.
b) Katibu
– Huyu ni mwandishi katika Mkutano aliye na majukumu yafuatayo.
1.
Kutoa taarifa au tangazo la mkutano
baada ya kuagizwa na Mwenyekiti.
2.
Kuhakikisha kuwa watu wote wanaohusika
wanapata taarifa ya Mkutano.
3.
Kuhakikisha kuwa watu walioalikwa
kuzungumza kwenye Mkutano wanapewa Taarifa mapema ili waweze kujitayarisha.
4.
Kuandaa mahali pa mkutano.
5.
Kusoma na kufafanua Ajenda za Mkutano.
6.
Kusoma muhitasari wa Mkutano uliopita.
7.
Kuandika muhitasari wa Mkutano.
c) Ajenda
– Ni mambo yatakayozungumzwa kwenye Mkutano.
1. Kufungua
Mkutano.
2. Kuthibitisha
muhitasari wa mkutano uliopita.
3. Yatokanayo
na muhitasari wa mkutano uliopita.
4. Taarifa
zitakazotolewa kwenye mkutano.
5. Mambo
yatakayojadiliwa.
6. Matatizo
yanayohitaji ufumbuzi.
7. Mengineyo.
8. Kufunga
mkutano.
d) Wajumbe
– Hawa ndiyo washiriki wa mkutano. Halimashauri au wanakamati.
Majukumu ya hawa wajumbe ni kama
ifuatavyo:-
1. Kuitikia
Wito wa mkutano kwa tarehe zilizopangwa.
2. Kubuni
Ajenda za mambo yanayostahili kujadiliwa na kuzipeleka kwa Katibu mapema kabla
ya kujadiliwa.
3. Kuthibitisha
muhtasari wa mkutano uliopita.
4. Kutoa
mapendekezo.
5. Kuuliza
maswali.
6. Kushiriki
katika majadiliano.
7. Kupiga
kura.
8. Kushiriki
katika maamuzi.
9. Kushiriki
na kufuatilia maamuzi yanayotekelezwa.
II.
MATAYARISHO.
Mafanikio yoyote ya
Mikutano hutegemea sana maandalizi mazuri. Baada ya kuitisha mkutano inabidi
Ajenda zipangwe na taarifa ya Mkutano iandaliwe na kusambazwa, na mahali pa
kufanyiwa Mkutano paandaliwe.
a)
Taarifa ya mkutano izingatie mambo
muhimu kama vile:-
1. Taja
jina la Mkutano.
2. Taja
siku na tarehe ya mkutano.
3. Taja
saa ya kuanza mkutano.
4. Taja
mahali pa mkutano.
5. Taja
Ajenda za kujadiliwa.
Kwa mfano:-
1. Kufungua
mkutano.
2. Kuthibitisha
muhitasari wa Mkutano uliopita.
3. Yatokanayo
na muhitasari wa Mkutano uliopita.
4. Kupanga
tarehe za Crusade.
5. Kupanga
bajeti za Crusade.
6. Mengineyo
7. Kufunga
kikao.
b)
Baada ya kuandaa hii taarifa inapaswa
isambazwe kwa Wajumbe wote bila ubaguzi.
c)
Mahali panapofanyiwa mkutano paandaliwe
mapema ili kuondoa usumbufu.
d)
Viandaliwe vifaa muhimu vya mkutano huo
na katibu ndiye mhusika – andaa Meza, Viti na vitendea kazi vingine.
e)
Mahali pa Mkutano panga viti kimuduara
au pembe msitatili au pembe mraba kwa kusudi la Wajumbe waweze kuonana wakati
wa kuzungumza.
III.
NAMNA
YA KUENDESHA MKUTANO.
a)
Shughuli za mwanzo.
Kabla
ya Mkutano kuanza wanatakiwa mwenyekiti na katibu wawe wamefika mahali pa
mkutano. Mwenyekiti atawakaribisha Wajumbe wakati watakapofika eneo la mkutano.
Kama
kuna Muhitasari wa Vikao vilivyopita katibu agawe zile Mihutasari Wajumbe
waanze kuzipitia kabla ya mkutano kuanza. Mkutano ufunguliwe Wajumbe wanapokuwa
wametimia koramu. Kiwango kinachotumika mara nyingi katika mikutano mingi ni
mbili ya tatu au nusu ya Wajumbe wote jumla yao ni pamoja na wale waliotoa
taarifa ya kutohudhuria.
b)
Kufungua mkutano.
Iwapo
kiwango kimetimia Mwenyekiti atafungua rasimi mkutano kwa kuwashukuru Wajumbe
waliofika. Ataeleza madhumuni ya mkutano kwa kifupi akitilia mkazo mambo yale
ya muhimu yatakayojadiliwa. Pia, kama kuna wageni awatambulishe kwenye mkutano.
c)
Kukariri
Ajenda.
Mara
baada ya Ufunguzi wa Mkutano ni vizuri katibu awasomee wajumbe Ajenda za
Mkutano. Pengine inaweza kuwa na Msaada zaidi kama zitaandikwa kwenye Ubao kama
upo.
d)
Kuthibitisha Muhitasari wa mkutano
uliopita.
Ikiwa
mkutano unaofanyika ulitanguliwa na mwingine, ni wajibu wa Wajumbe kuthibitisha
Usahihi wa mkutano uliopita. Mwenyekiti atamwomba Katibu asome ule Muhtasari na
wajumbe wakiwa wanasikiliza na kufuatilia kwa makini zaidi. Mwishoni
atawaulikza wale wajumbe kama yalivyosomwa ndivyo yalivyo. Kama Wajumbe wataridhika
na ule Muhitasari Mwenyekiti na Katibu wataweka sahihi zao.
e)
Yatokanayo na Mhitasari wa mkutano
uliopita.
Baada
ya Muhitasari wa mkutano uliopita kuthibitishwa, taarifa za utekelezaji wa
maagizo na maazimio yake zitatolewa. Muhitasari ule unachunguzwa kwa makini
tangu mwanzo hadi mwisho. Unaweza kusomwa hatua kwa hatua kama Mwenyekiti
ataamua hivyo.
f)
Mijadala ya Ajenda maalumu.
Baada
ya kushughulika na Mhitasari wa mkutano uliopita Ajenda zitakazofuata zitahusu
mambo mapya ambayo ni maalumu kwa mkutano huo. Ajenda hizo hazina budi
kujadiliwa kwa ukamilifu moja baada ya nyingine.
Mwenyekiti
ahakikishe kuwa wajumbe wanapewa nafasi ya kuuliza maswali kutoa mapendekezo,
kupiga kura n.k
Utaratibu
ufuatayo unaweza kusaidia katika kufanikisha majadiliano kwenye mkutano.
1.
Utaratibu wa maswali na majibu. Mjumbe
yeyote anayetaka kutoa maelezo au kuuliza maswali hana budi kunyoosha mkono ili
kumgutua Mwenyekiti apate kumwona na kumruhusu kusema. Kila mjumbe asizungumze
bila ruhusa ya Mwenyekiti.
2.
Utaratibu wa kujadili hoja. Hoja ni kitu
gani?
Ni neno au jambo lililoungwa mkono baada
ya kutolewa na mjumbe mmojawapo katika mkutano. Linapotolewa kwa mara ya kwanza
huwa ni “Pendekezo” linapoungwa mkono sasa huwa ndiyo hoja. Wakati wa
kujadiliwa hoja Mwenyekiti akaribishe maoni mbalimbali ya Wajumbe na hatimaye
kama ni lazima, kura ipigwe ikiwa na shabaha ya kuunga mkono ile hoja au
hapana. Iwapo wajumbe wengi wataiunga mkono hoja hiyo itakuwa ni Azimio ambalo
lazima litekelezwe.
3.
Taratibu za Upigaji kura.
Kura hupigwa na Wajumbe wa Mkutano,
wale waliokaribishwa pamoja na Wataalamu kama walikuwepo hawaruhusiwi kupiga
kura. Hata hivyo kura zikipigwa na kulingana, Mwenyekiti ataamua apigie Upande
gani ili kukata Shauri.
g)
Mengineyo.
Ajenda
hii hutangulia kabla ya kufunga Mkutano, ikiwa ni nafasi kwa Wajumbe kuuliza
maswali au kutoa taarifa, ambazo hazikuweza kutolewa wakati wa Ajenda zingine.
Wakati huu kwa kuwa Wajumbe watakuwa wanaelekea kuchoka hivyo Mwenyekiti ajibu
maswali kwa kifupi na kama kuna jambo ambalo linahitaji maelezo ya kutosha
liahirishwe hadi mkutano mwingine na jambo hilo lifanywe Ajenda. Mwenyekiti
aangalie sana asiruhusu maswali ya Ajenda zilizopita.
h)
Kufunga Mkutano.
Ikiwa
mkutano utakuwa umeendeshwa vizuri mambo yote yaliyoandaliwa yatakuwa
yamezungumzwa na kujadiliwa kikamilifu. Kabla ya kufunga Mkutano, Mwenyekiti
anaweza kama ataona inafaa kutoa Muhitasari wa mambo muhimu. Yaliyozungumzwa na
maazimio yaliyofikiwa, atawakumbusha na kuwahimiza Wajumbe kutekeleza
yaliyoazimiwa. Atawashukuru Wajumbe kwa kuhudhuria na kutoa mchango wao wa
mawazo na atafunga Mkutano kwa Maombi yake au ya Mjumbe yeyote.
4.
KUANDIKA MUHITASARI.
Mojawapo ya majukumu ya
kikatibu ni kuandika Muhitasari wa Mkutano. Mikutano mingi inakosa mafanikio
kwa sababu ya Ukosefu wa Mihitasari ya kufaa. Mihitasari yenye kufaa hutokana
na kuwa na Makatibu walio makini. Ni wajibu wa Katibu kuhakikisha kuwa
anasikiliza Vizuri mijadala, Maagizo na maazimio ya Mkutano na baadaye ataketi
na kuandika kwa Ufasaha Muhitasari wa mkutano mzima. Wakati wa kuandika
Mhitasari inampasa Katibu aeleze kwa kifupi kila Ajenda peke yake kufuatana na
jinsi ilivyopangwa.
Katika Mhitasari ataje
wajumbe waliohudhuria na pia wale ambao hawakuhudhuria na wale waliomba ruhusa.
Mwisho aandike
MHITASARI
UMETHIBITISHWA.
Katibu Mwenyekiti
……………………… ………………………
HITIMISHO
Ninapomalizia sehemu ya
mwisho katika haya mafundisho napenda nimalizie na haya yafuatayo.
I.Kanuni 5 zilizotolewa
kwa Musa kuhusu Uongozi na Utawala 2. Mpango wa kiasili wa Utawala.
I. KANUNI 5 ZILIZOTOLEWA KWA MUSA.
1.
Wafunze Wengine kukusaidia Kut 18:13-22
Urasimu
wa Utawala wa kidini ni Kujaribu kufanya mwenyewe kazi ambayo Mungu amekuita
kuitimiza bila ya Ushauri wa watu wengine, Urasimu wa utawala wa kidini ni
kujiweka juu, kujiona. Math 20:27 23:11.
Musa alimsikiliza Mungu na Yethro ndipo alipopata Ufumbuzi wa tatizo, nalo lilikuwa
ni kuwafundisha wengine, Hes 11:16
18:21-22. Mtu kufundisha mwingine, Ona mafundisho ya Paulo 2Tim 2:2
2.
Kuwafundisha Biblia.
Tunatakiwa
tuwape Viongozi wa Kanisa mafunzo ya Biblia ambayo ndiyo yanayotoa Uhai na
Uzima wa kiroho kwa watu. Math 22:29
3.
Waelekeze kazi ya kufanya Kut 18:20
Wale
ambao tayari umewapata wawe wasaidizi wasiishie tu kujifunza darasani bali
waelekeze kile watakachofanya. Ukimfundisha Mwanafunzi kuongoa Roho. Mara hiyo
mpeleke kuongoa roho. Math 10:1-8 Luk
9:1-6
4.
Gusisha Upako
Kugusisha
Upako ni sawa na kule kuwasha moto. Washa moto kutoka moto mkubwa na ule moto
mkubwa unabaki na nguvu ile ile. Kutoka 11:16-17. Upako ni muhimu katika
kuendeleza Uongozi. Kiongozi ambaye hana nguvu za Roho Mtakatifu juu yake hana
nafasi ya kufanikiwa. Luk 9:1 Mdo 1:8 Viongozi ambao wana Upako ni vema wafunze
wengine.
5.
Gawia wengine mzigo. Hes 11:16-17
Kutawala
kibiblia ni tofauti na Viongozi wa kidunia wanavyotumia mamlaka yao. Uongozi wa
kibiblia ni kufundisha, kubariki, kuponya, kufungua waliofungwa, kutoa pepo, kusamehe
dhambi na kuwaganga waliovunjika moyo. Luk 4:18
Math 20:20-28. Kumbuka kile Gidioni alisema - Waam 8:23. Ni matumaini
yangu umeelewa kile Mungu alichosema kwa Musa ndicho anachosema kwako leo wewe
ni Musa wa leo.
II. MPANGO WA KIASILI WA UTAWALA.
Mungu ambaye ni
muumbaji na mpangaji alipanga utaratibu wa Utawala tangu mwanzoni, Mungu
alitamani aendelee kuwa mtawala wa Viumbe vyake ingawa hata wao walipewa
kutawala Viumbe. Mw 1:26-27
Kanisa ni vema wajue
Mpango wa kiutawala wa tangu asili katika Kut 19:5-6 tunaona mpango wa Mungu
aliokusudia tangu asili yeye ndiye mtawala mkuu wa dunia yote. Chini yake
ameweka mwanadamu asaidiane naye kama mlinzi mwangalizi. Mpango huu ulikataliwa
na mwanadamu, I Samw. 8:5-9. Mtindo wa Utawala huo uliitwa Theocracy neno ambalo linatokana na neno “Theos” na maana ya neno hilo – “MUNGU NDIYE MTAWALA MFALME” alikuwa
akisaidiana na waamuzi wakati ule.
Baada ya mwanadamu
kukataa huo mfumo wa Utawala wa kitheocracy Mungu aliwaruhusu waendeleze mfumo
walioutaka wa Utawala wa Ki-Monarchy, yaani mwanadamu anakuwa yeye ndiye
mfalme. Kwa Taifa la Israel ndipo walipotokea watawala kuanzia Sauli, Daudi,
Sulemani n.k
Baadaye Utawala wa
namna hii ulipungua na kuanzisha Utawala wa aina nyingine unaoitwa wa Democracy, kupitia mfumo huu mtu yeyote
anachaguliwa kuwa Rais (Presidential).
Leo hii Mataifa mengi
hutumia mfumo huu unaoitwa Democrasia, badala ya Ule wa Kimonarchy hata hivyo
bado kuna mataifa machache ambayo bado wanatumia mfumo huo wa kimonarchy.
Mfumo huu wa tatu ambao
ndio Unaotawala sasa utafika mwisho wake na ule mfumo wa kwanza wa Theocrasi
utajirudia na kwa milele yote. Dan 2:44
4:3 I Kor 15:24-25