Jumanne, 26 Julai 2016

SADAKA YA MAVUNO



SOMO: SADAKA YA MAVUNO.
Hii ni sadaka ya shukrani kwa Mungu kwa Baraka alizotupa.
KUMBUKUMBU LA TORATI 28:1-14
Katika mavuno yetu tunapewa angalizo tusile tukamsahau Mungu.
KUMBUKUMBU LA TORATI 8:10-20
Sadaka ya mavuno siyo ya mazao ya shamba tu. Ni pamoja na kile tunachokivuna katika maeneo ya kazi au miradi yetu kama vile;
        i)Fedha         ii)Mifugo        iii)Mazao na mali nyingine tunazomiliki.
Somo hili limegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni;
i)                    Namna ya kufanikiwa kiuchumi.
ii)                  Kwanini Mungu anatupa utajiri wa mali na fedha.
iii)                Baraka za utoaji wa sadaka ya mavuno.
NAMNA YA KUFANIKIWA KIUCHUMI.
Ni mpango wa Mungu tusiishi masikini ili tuweze kumiliki mali na pesa.
              1TIMOTHEO 6:17                    2WAKORINTHO 9:8-11
HATUA ZA KUFANIKIWA
i)                    Tafuta fursa za kufanikiwa - HOSEA 4:6
ii)                  Epuka uvivu fanya kazi kwa bidii-MITHALI 22:13, MITHALI 20:4 ,MITHALI 19:15
                 Bidii hutufanya tufanikiwe - MITHALI 10:4
iii)                Malengo katika kazi
Usipokuwa na malengo ya kazi zako hutajua kutumia vizuri kipato chako.
KITABU CHA AYUBU 8:7
*Mapato hugawanywa katika sehemu kuu nne kwa aliyeokoka na anayetaka kufanikiwa.
Kumtolea Mungu
 
Akiba
 
Tahadhari
 
Matumizi
 
MITHALI 6:6-11
iv)                Tambua maadui wa kazi zako.
ZINGATIO: Mafanikio kwa viwango vya juu sana hutegemea vitu vikuu viwili:-
                     i)Akili-Uwezo wa kupambanua.   ii)Maarifa-Namna ya kutenda jambo.
KWANINI MUNGU ANATUPA UTAJIRI WA MALI NA FEDHA.
Ili Kuimarisha Agano Na Mungu (Ufalme Wake)* Kumb 8:18 (12-18)
Agano la Mungu kwa siku za leo, ni Agano JIPYA. Kuimarisha Agano lake maana yake; ni kuimarisha kazi ya injili ya Yesu Kristo, ili wokovu uwafikie watu wote.
Gal 3:11,23-26,29; Rum 10:13 – 15; Fillip 4:15 –19
 Ili Kuwagawia Wahitaji *2KOR 9:8-13;
Tunapowapa wahitaji fedha, nguo, viatu, chakula au vitu vya aina nyingine ili
kuwasaidia kimaisha, tunapata thawabu kubwa kwa Mungu. Kumsaidia mhitaji kitu, ni kumpa Mungu. Hebu soma vizuri Mathayo 25:31-40; Mathayo 10:40 – 42 na Yohana 13:20.
2Kor 8:14-15, Mdo 20:35
Ili Kuvitumia Kwa Mahitaji Yetu Binafsi *Yoh16:24
 Mungu kama Baba yetu na kama Mchungaji Mwema, anajali sana mahitaji yetu na haja zetu au shauku za mioyo yetu. (vitu vitupavyo furaha na kuridhika). Ndio maana hutupa utajiri, ili tufurahie maisha. Si mapenzi ya Mungu tuwe masikini. Ndio maana Yesu alifanyika maskini (kimwili) ili kwa umasikini wake, (sisi) tupate kuwa matajiri (kimwili)” 2 KOR 8:9
Ni mapenzi ya Mungu tupate vitu vyote vitakavyotufanya tufurahie maisha yetu duniani. Nyumba nzuri, mavazi mazuri, chakula kizuri, kazi nzuri, magari mazuri, biashara nzuri, mifugo mizuri, mashamba mazuri, mshahara mzuri, n.k.
ZABURI 23:1- 2; WAFILIPI 4:6-7,19; ZABURI 37:4; ZABURI 145:17- 19

KANUNI KUMI ZA KIBIBLIA USIMAMIZI MZURI WA FEDHA
Matatizo mengi ya kifedha tuliyo nayo yanachangiwa sana kwa namna moja au nyingine na usimimamizi mbaya wa fedha zetu,wengi wetu tatizo letu kubwa zaidi ni usimamizi wa fedha kuliko kuzalisha na kupata fedha. Usimamizi mzuri wa fedha utalinda uchumi wako na kuukuza uzalishaji wako,kipato chako.Hata kama unazalisha sana fedha lakini kama una usimamzi mbaya wa fedha  uchumi wako utayumba tu.Matatizo mengi ya kifedha tunakimbilia kuombewa na kukemea,lakini hayo yote bila  kujifunza usimamizi mzuri wa fedha utakuwa hujatatua tatizo katika mzizi.hata ukiombewa kupata mpenyo wa kifedha matatizo ya kifedha yatarudi baada ya muda mfupi kwa kushindwa kuzitendea kazi kanuni za fedha.

1.       MUNGU NDIYE MMILIKI WA FEDHA ZETU
Fedha ni Mali ya Bwana,sisi tu wasimamizi tu au mawakili,hivyo tunawajibika na vile tunatumia kila fedha tuliyoaminiwa na Mungu.( Mathayo 25:1-30 ; Zaburi 24:1,)

2.       TAMBUA FEDHA NI SUALA LA KIROHO.
Kwa mtu wa Mungu fedha ni suala la kiroho,fedha ina athiri na inagusa maisha yako ya kiroho pia.vile unavyoshughulika na fedha zako ni kiashirio cha ukomavu wako kiroho.LUKA 16:10-11 .Fedha inaweza kuwa Mungu wako,fedha ina uwezo zaidi kutuvuta taratibu na kwa ujanja kutoka kwa Mungu kuliko kitu kingine chochote.MATH 6:24,Ina nguvu ya kuwa Bwana wetu. Katika mifano 38 ya Yesu,16 inahusu fedha,katika agano jipya fedha imezungumzwa zaidi kuliko habari za mbinguni na kuzimu vikiunganishwa pamoja.mara tano zaidi imezungumzwa kuhusu fedha kuliko maombi,kuna mistari zaidi ya 1500 inayohusu maombi na imani,wakati kuna zaidi ya mistari 2000 inayohusu fedha na mali.Aslimia 15% ya Biblia  ni kuhusu fedha.

3.       TUNZA KUMBUKUMBU ZOTE ZA FEDHA
Kutunza kumbukumbu ni hatua ya kwanza kukusaidia katika kuandaa bajeti yako ambayo utaishi nayo.tafuta daftari dogo na anza kuweka kumbukumbu za wapi fedha zako zinakwenda,ni kazi ngumu lakini itakusaidi kwa mipango ya muda mrefu ya kifedha.kiasi gani unatumia kwa mwezi kwa usafiri?simu?chakula?matibabu? n.k ni lazima ujue wapi fedha yako inatoka na wapi fedha yako ina kwenda. Nini nina miliki,nini ninadai,nini nina daiwa,natuamiaje(MITHALI 27:23-24, 23:23,)

4.       FANYA TATHIMINI  YA MARA KWA MARA YA FEDHA ZAKO:
Ni muhimu kufanya tathimini kwa uaminifu kuhusu uchumi wako,mapato yako,madeni,vitega uchumi vyako n.k. hii itakusadia kufanya marekebisho unayoyahitaji na  kukusaidia kuishi kwa mpango,kama huwezi kutathimini hutaweza kupanga,ukishindwa kupanga,tayari umeshindwa kusimamia fedha yako.(MITHALI 21:5  LUKA 14:28)
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiRXgHms50vh1rVBfhNHCAoYLR2LDOqFzeDDb_UlZl7M6CzaSYQe3YUx-m6XuOEGnwAzZjI_9EKtH0sbd9g17AMlFq9seit05iAM7AIzt1WUOwDG3rab_rZ0GHgpOJ0swtGAVdGfd-TQs4/s400/482591_624350400912715_249882607_n.jpg

5.       JIWEKEE  MFUMO WA KUPANGA BAJETI NA KUUFUATA:
Bajeti kirahisi nikuandika  katika karatasi nini unategemea kupata kama mapato na njisi gani unategemea kutumia.panga matumizi yako.Ni mpango wa jinsi gani utatumia rasilimali  fedha ambazo unatarajia kupata ,bajeti inapaswa ijumuishe vyanzo vya mapato  pia mpango wa matumizi wa mapato mf.mpango wa chakula,kodi,zaka,utoaji,akiba n.k(Mithali 21:5, Mithali 21:20)

6.       JIWEKEE  UTARATIBU WA KUWEKA AKIBA
Weka Akiba, kwaajili ya dharura,akiba kwaajili malengo maalumu, (Mithali 21:20a ;13:11)

7.       JIFUNZE KUTOA KWA UKARIMU
(MITHALI 11:24-25).kanuni ya uchumi wa Ki-Mungu ni tofauti,kadiri unavyotoa ndivyo unavyo jilimbikizia ndiyo uchumi wako unastawi.Kumtolea Mungu,kutoa kwaajili ya kuwabariki wengine,kutoa kwaajili ya wahitaji(Mithali 28:27 Mithali 11:25.Mithali 19:17,Mithali 3:9-10),Kutoa  kunafungua Baraka za Mungu katika Maisha yako.

8.       TUMIA FEDHA YAKO KWA HEKIMA NA RIDHIKA NA ULICHO NACHO:
Zingatia vipaumbele na umuhimu,Epuka matumizi ya anasa,manunuzi ya bila mpangilio,manunuzi ya papo kwa papo,usifanye matumizi yaliyo nje,yanayozidi kipato chako au uwezo wako wa kifedha.Jifunze kuridhika na kuuepuka tamaa.usifuje fedha kwa matumizi ya ovyo.jifunze kuridhika(Mithali 21:20 ;Waebrania 13:5,Mhubiri 6:9) 

9.       TUNZA VITU NA MALI AMBAVYO UMEVIGHARIMIA FEDHA.
Vitu,mali ni fedha,usipovitunza utatoa fedha tena kununua. Tunza visiharibike ovyo,vitumike kwa uangalifu ili kuokoa gharama ya matengenezo au kununua upya.

10.   EPUKA MADENI.
biblia haijakataza moja kwa moja kuhusu kukopa,ila kwa uwiano wa maandiko Haiti moyo madeni,bali inakatisha tamaa kukopa.inazungumza zaidi madhara ya kukopa.Unapokuwa katika deni unakuwa katika kifungo,Madeni yana haribu uhusiano.usitumie fedha zaidi ya ile unayozalisha utaishia kwenye madeni.weka akiba kidogo kidogo badala ya kukopa.
MITHALI 22:26-27,ZABURI 37:21,MITHALI 22:7

BARAKA ZA UTOAJI WA SADAKA YA MAVUNO.
Udhihirisho Wa Kumheshimu Mungu, Kumtambua Mungu Na Kumthamini Kuwa Ndiye Atupaye Utajiri/Vitu.(Kumbukumbu la torati 8:10 –20, Mithali 3:9 – 10)
“Mheshimu Bwana kwa mali yako, na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, na mashinikizo yako yatafurika divai mpya”… Tena “hawatakuwepo masikini kwenu, kwakuwa Bwana atakubarikia kweli, katika nchi akupayo Bwana Mungu wako, uimiliki, iwe urithi wako.” Kumbukumbu la torati 15:4
Kupata Baraka za Shukrani Kwa Mungu. *Zab 116:18,12-13, Zab103:1-5, Zab 136:1-3
Sadaka zetu ni njia tu ya kumshukuru, ni kiwakilishi cha shukurani zetu kwake, kwa maana hatuwezi kumlipa kwa mema anayotutendea *2Nyak 20:21 (1-30)
Kumuabudu Mungu  *Mwa 8:15-22; Ebr 7:1-3; Mwa 4:1-7
Utoaji ni heshima kwa anayepewa. Ndio maana washindi hutunukiwa zawadi/tuzo, kwasababu wanastahili. Vivyo hivyo kwa Mungu wetu; kwa kuwa yeye ni Mkuu, Mtakatifu, na Muweza wa yote, anastahili kuabudiwa. Hivyo sadaka zetu ni ishara ya kumtukuza, kumheshimu na kumuabudu Mungu.
Ushirika Wetu Katika Kazi Ya Mungu.  * Malaki 3:7-12; Rum 10:13-15;* Hagai 1:3-11
Mungu ametupa mali na utajiri, ili tushiriki katika ujenzi wa ufalme wake duniani Mungu anatutaka tutoe sadaka nzuri “Ili kiwemo chakula nyumbani mwa Mungu” (Kanisani / Huduma ya Injili)
Ni Upandaji Wa Mbegu Ili Kupokea (Kuvuna) Baraka Na Utajiri Mwingi Zaidi
* 2Kor 9:6, 2Kor 9:8,Gal 6:7 – 10, Malaki 3:10 – 12, Luk 6:38
,
Mtoaji wa sadaka ni kama mpanzi wa mbegu shambani. Mbegu moja huzaa nyingi zaidi kuliko ile iliyapandwa. Tunapotoa sadaka, tunatakiwa kutoa huku tukitarajia kupokea vingi kulilo tulivyotoa. Atakaye mavuno mengi ni lazima:-
i. Achague(atenge) mbegu bora zaidi (the best)
ii. Afuate masharti ya upandaji (Kilimo)(Isa 1:19)
iii. Apande mbegu nyingi (2kor 9:8)

 Ni Kuweka Akiba Mbinguni *Luk 12:30-34; Math 6:19-20.
Imeandikwa kwamba “Hazina yako ilipo, ndipo moyo wako utakapokuwepo.Mambo yafuatayo, ni baadhi tu ya kazi za hazina yako iliyoko mbinguni.
(i) Kutusaidia wakati wa uhitaji  WAFILIPI 3:12. WAEBRANIA 4:16
(ii) Kutuandalia makao mazuri mbinguni  YOHANA 14:1-2  MATHAYO 20 : 21 – 23
==============================UBARIKIWE!============================
Pastor.AMOS E.ONESMO-0756391498

Maoni 8 :

  1. Mtumishi Asante kwa SoMo zuri. Nina swali moja tu,
    Ni wapi katika Agano jipya ambapo Yesu au mitume aliagiza na kuhimiza juu ya kanisa kutoa sadaka ya mavuno Kama ilivyokuwa katika Agano la Kale?
    Naomba kusaidiwa maana naona kushindwa kuelewa.

    JibuFuta
  2. Asante kwa somo,nami bado swali langu wapi andiko ktk Agano Jipya linaagiza kutoa sadaka ya Mavuno,au sikukuu ya Mavuno.Naomba nisaidiwe tafadhali

    JibuFuta
  3. Nashukuru sana kwa hili somo Mungu Akubariki Mtumwa wa Mungu aliye Hai

    JibuFuta
  4. Asante kwa somo, naomba kuuliza swali , ukisoma biblia wale walio toa sadaka za mazazo hawakubaikiwa(kuna nini katika sadaka za mazao?)

    JibuFuta
  5. Sadaka ya mavuno INA ms
    isitizo gani

    JibuFuta