MWL: REV.AMOS
CONT: 0759199463
WHATSAPP: +255625313609
E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com
SOMO: USITENDE DHAMBI TENA.
Yohana 5:14
"Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi"
➖Usitende dhambi yasije kukupata yaliyo mabaya zaidi
➖Umevuka salama, endelea kunyenyekea usitende dhambi tena.
➖Tunza utakatifu ili Mungu akutendee zaidi na zaidi.
➖Umepata kazi, umeoa, umeolewa, umeinuliwa, umeponywa ugonjwa n.k endelea kutunza utakatifu.
➖Dhambi inatoa nafasi mapepo kukurudia na kukutesa.
👇👇👇
Luka 11
24 Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema,
25 Nitairudia nyumba yangu niliyotoka.
26 Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza.
➖Dhambi inakufanya umilikiwe na Ibilisi.
👇👇👇
1 Yohana 3:8
"atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi"
...................MWISHO......................
REV. AMOS 0625313609