Jumanne, 7 Oktoba 2025
*KUFUNGULIWA MASIKIO YA KIROHO*
MWL: REV.AMOS
CONT: +255625313609
E-MAIL: pasteronesmo@gmail.com
SOMO:
*KUFUNGULIWA MASIKIO YA KIROHO*
✳️ *Masikio*
➖ Ni mlango wa fahamu kwa kiumbe hai unaotumika kusikia.
➖Kama yapo masikio ya Ki-Mwili basi tambua yapo na masikio ya kiroho.
➖Masikio yako yafunguliwe kwa jina la Yesu ili uweze kumsikia Mungu lile alitakalo kwako.
👇👇👇
Adamu na Eva walimsikia Mungu.
*MWANZO 3:8*
"Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone"
➖Masikio ya mtu yakifungwa hawezi kumsikia Mungu na hawezi kupokea maelekezo ya Mungu kwake.
*➖KATAA KUWA KIZIWI WA KIROHO* .
👇👇
*ISAYA 43:8*
"Walete vipofu walio na macho, na viziwi walio na masikio"
*MATHAYO 13:13-15*
"[13]Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.
[14]Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema,
Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa;
Kutazama mtatazama, wala hamtaona.
[15]Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito,
Na kwa masikio yao hawasikii vema,
Na macho yao wameyafumba;
Wasije wakaona kwa macho yao,
Wakasikia kwa masikio yao,
Wakaelewa kwa mioyo yao,
Wakaongoka, nikawaponya"
*EZEKIEL 12:2*
"Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi"
➖Nyakati tulizonazo ni za mwisho ambazo watu wengi hawataki kumsikia Mungu wala kuyasikia mafundisho yake ya kweli.
👇👇
*2 TIMOTHEO 4:3-4*
[3]Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;
[4]nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
*HITIMISHO*
Omba kufunguliwa Masikio yako ya Kiroho ili umsikie Mungu.
-------------END------------
REV.AMOS
+255625313609
+255759199463
pasteronesmo@gmail.com






















































