Jumatano, 1 Januari 2025

USHAURI MUHIMU KWA WATUMISHI

 *USHAURI KABLA YA KUHAMA DHEHEBU* 

1. Chunguza misingi ya Imani ya Dhehebu unalotaka kuhamia. 

➖Fuatilia kwa kina, tafakari uone kama Misingi ya Imani ya Dhehebu hiyo haikinzani na misingi ya ki-biblia. 


2. Mfumo wa Uongozi (Leadership structure)

➖Fuatilia kufahamu mfumo wa kiuongozi umekaaje? 

➖ Yako madhehebu muundo wa kiuongozi hauko kitaasisi. Yaani mfumo wa kiuongozi umekaa kama Mali ya mtu au wa familia Fulani. Hakuna mfumo wa kupokezana uongozi yaani mamlaka yako ndani ya mtu au familia Fulani. Dhehebu la mfumo huu lina madhara mbeleni yaani kuna haki kama mshirika utazikosa. 

➖Mfumo wa uongozi unaweza kukujenga ama kukubomoa kiimani. 

➖Iko mifumo ya kiuongozi ambayo haina namna ya kumwajibisha kiongozi wa ngazi ya juu pale anapokosea bali yeye ndiye anayewajibisha wengine. 


 *NI USHAURI TU* .


2025 UWE MWAKA WA MAFANIKIO KWAKO.


 *REV. AMOS 0625313609*

KUVUNJA VIZUIZI VYA KIROHO

 MWL. REV. AMOS 

SOMO:

KUVUNJA VIZUIZI VYA KIROHO. 

Utangulizi

Vizuizi ni vikwazo vyovyote vinavyomzuia mtu/kitu kufika mahali fulani. 

➖Jifunze kushughulikia kila kizuizi mbele yako ili shetani asikuzuie. 


🛑1 WATHESALONIKE 2:18

"Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na *Shetani akatuzuia* "


➖Shetani anaweza kukuzuia katika safari yako ya mafanikio.

➖Shetani anaweza kuweka mtego au utisho katika safari yako ya mafanikio, ukajikuta badala ya kuendelea mbele unapoteza mwelekeo.


🛑MATHAYO 8:28

"Naye alipofika ng’ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile"


➖Hapa tunaona wenye pepo wawili walizuia katika njia hata mtu asiweze kuipitia njia ile, kwa hiyo wenye pepo wawili wanasimama kama VIZUIZI Katika njia.


➖Shetani anaweza kukuzuilia majibu yako au Baraka zako/yako kutoka kwa Mungu. 

➖Daniel alizuiliwa majibu kwa muda wa siku 21 (Majuma matatu- 03)


🛑DANIEL 10:11-14

[11]Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka. 


[12]Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako. 


[13]Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi. 


[14]Sasa nimekuja kukufahamisha mambo yatakayowapata watu wako katika siku za mwisho; maana maono hayo ni ya siku nyingi bado.


KIPI CHA KUFANYA??? 

➡️Ingia katika Maombi kupambana na kila kizuizi mbele yako ili uweze kufikia mafanikio yako. 

➡️Pambana katika Ulimwengu wa Roho. 

➡️Ushindi upo katika Maombi. 


###########BARIKIWA!########

REV. AMOS 0625313609

Whatsapp+255759199463

SIRI YA MAFANIKIO 2025

 MWL. REV. AMOS 

SOMO:

 *SIRI YA MAFANIKIO 2025* .

🛑Mafanikio

➖Ni hali ya mtu kufikia hatima njema ya malengo aliyojiwekea. 

➖Ni haja ya kila mtu afanikiwe. Mafanikio ni hitaji la kila mmoja mwenye kutamani mafanikio. 

➖2025 Utafanikiwa kwa jina la Yesu. 


🛑ZINGATIA YAFUATAYO:-

1. *Uwe mtu wa Maombi* . 

Mwaka huu omba kuliko kawaida. Maombi yataleta majibu kwa mahitaji mengi na utafanikiwa. 


 *1 Wathesalonike 5:17* 

"Ombeni bila kukoma"


2. *Umzalie Mungu matunda* . 

➖Jitahidi kuleta watu kwa Yesu ili uupendeze Moyo wa Mungu ili akufanikishe

Kanuni ya Ki-Biblia, ni kuzaa matunda na matunda yapate kukaa kisha Omba na Mungu akutendee


 *YOHANA 15:16* 

"Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni"


3. *Thubutu* 

➖Jifunze kuthubutu maana katika kuthubutu utafanikiwa

➖Jaribu kile unachoweza kufanya utafanikiwa

➖Thubutu ila usitende dhambi

➖Biblia inatukumbusha kujaribu kila jambo na kulishika jambo jema TU. 


 *1 Wathesalonike 5:21* 

"jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema"


4. *Unyenyekevu* 

➖Unyenyekevu siyo ujinga na anyenyekeaye huinuliwa

➖Nyenyekea ofisini kwako, katika huduma, katika ndoa n.k kwani unyenyekevu utakupa kibali 2025.

➖Nakuombea kiburi na mashindano visikuponze 2025


 *MATHAYO 11:29* 

"Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu"


5. *Marafiki wa Faida* . 

➖Rafiki anaweza kukupoteza na anaweza kukuonesha njia

➖2025 Mungu akupe marafiki walio tayari kula gharama kwa ajili Yako

➖Mwenye kupooza alipata marafiki wema walimaababisha kupokea uponyaji


 *Marko 2:1-5* 

[1]Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani

[2]Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake. 

[3]Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne. 

[4]Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza. 

[5]Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.



"" "" "" "" "" "MWISHO" "" "" "" "" "" 

REV. AMOS 0625313609

WHATSAPP+255759199463