MWL: REV.AMOS FROM TABORA
CONTACTS: +255625313609
WHATSAPP: +255759199463
SOMO: *UMEBAKIZWA 2023 KWA KUSUDI*
Mungu amekupa Neema ya kuingia 2024 kwa makusudi si Bure.
Ofisi unayofanya kazi wengine 2023 walifukuzwa kazi wewe ukabaki, katika ajali ile wengine walikufa wewe ukabaki, katika magumu mengi uliyopitia wewe ulibaki. Kubaki kwako kuna kusudi si Bure.
Andiko la msingi
*AYUBU 1:13-19*
[13]Ilitukia siku moja hao wanawe na binti zake walipokuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa,
[14]mjumbe akamfikilia Ayubu na kumwambia, Hao ng’ombe walikuwa wakilima, na punda walikuwa wakilisha karibu nao;
[15]mara Waseba wakawashambulia, wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua hao watumishi kwa makali ya upanga, mimi peke yangu nimepona, mimi tu, *kukuletea habari* .
[16]Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, *kukuletea habari* .
[17]Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu, wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam, wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi peke yangu nimepona, mimi tu, *kukuletea habari.*
[18]Huyo alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Wanao na binti zako walikuwa wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa;
[19]mara, tazama, upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona, mimi tu, *kukuletea habari.*
➖ Tumepona katika mitego mingi ya shetani ili t *upeleke habari*
➖ Umebakizwa 2023 kwa kusudi la kupelekea taarifa wengine ya uliyoyaona yaani matendo makuu ya Mungu uliyoyaona maishani kwako.
➖Kuna watu wanasubiri 2024 uwapelekee taarifa za matendo makuu ya Yesu kristo ili wayaamini waokolewe na kufunguliwa katika vifungo mbali mbali vya Giza.
➖Mungu amekupaka mafuta mwaka 2024 kwa kazi maalumu.
*ISAYA 61:1-2*
[1]Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
[2]Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;
1. KUHUBIRI
2. KUWAGANGA WALIOVUNJIKA
3. KUTANGAZA UHURU
4. KUWAFUNGUA WALIOFUNGWA
5. KUTANGAZA MWAKA WA BWANA
6. KUWAFARIJI WALIAO
Beba kusudi la Mungu kwa uaminifu 2024.
➖ Ili kulitimiza kusudi la Mungu 2024 chagua watu sahihi wa kuambatana nao.
*MITHALI 13:20*
[20]Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima;
Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.
➖ Watu wa masengenyo hawatakufaa 2024
*ZABURI 50:20-22*
[20]Umekaa na kumsengenya ndugu yako,
Na mwana wa mama yako umemsingizia.
[21]Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza;
Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe.
Walakini nitakukemea;
Nitayapanga hayo mbele ya macho yako.
[22]Yafahamuni hayo,
Ninyi mnaomsahau Mungu,
Nisije nikawararueni,
Asipatikane mwenye kuwaponya.
.... *2024 NAKUOMBEA USITAWI SANA* ....