*IBADA YA LEO TABORA* .
29/01/2023
SOUND OF GOSPEL CHURCH MINISTRY TANZANIA (SCMT)
MNENAJI: REV. AMOS E. ONESMO
SIMU: +255625313609/+255759199463
SOMO:
*MADHARA YA DHAMBI*
UTANGULIZI
Dhambi ni jambo lolote lisilompendeza MUNGU.
Dhambi inamfanya mwanadamu asifanikiwe kwa lolote.
*MITHALI 28:13*
Afichaye dhambi zake hatafanikiwa;
Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
Dhambi ina MADHARA makubwa kama ifuatavyo:-
1. Kupoteza uhusiano na MUNGU
ππ½Ni hasara kubwa kukosa uhusiano na MUNGU kwani pale unapohitaji msaada wa MUNGU hautaupata.
*ISAYA 59:2*
"lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia"
*Mithali 15:29*
"BWANA yu mbali na wasio haki;
Bali huisikia sala ya mwenye haki"
2. Jina linafutwa katika kitabu cha uzima
ππ½ Mungu anakuondoa kwenye kitabu chake. Mbingu hazikutambui, utatambulika kuzimu.
*KUTOKA 32:33*
"BWANA akamwambia Musa, Mtu ye yote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu"
3. Mema uliyoyatenda hayatakumbukwa
ππ½ Dhambi inafuta yote uliyoyatenda.
*Ezekieli 18:24*
"Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa"
4. Kupoteza Amani na furaha ya MUNGU
ππ½Amani na furaha hutoka kwa Mungu. Ukitenda dhambi unakuwa umepoteza vyote
*ISAYA 57:20-21*
[20]Bali wabaya wanafanana na bahari iliyochafuka; maana haiwezi kutulia, na maji yake hutoa tope na takataka.
[21]Hapana amani kwa wabaya; asema Mungu wangu.
5. Kupoteza hofu ya MUNGU
*Zaburi 36:1*
"Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake,
Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake"
*HITIMISHO* .
➡️ Tujihadhari na dhambi, tuyatende mapenzi ya MUNGU
➡️ Omba nguvu ya Roho mtakatifu ikusaidie usitende dhambi
_______Rev. Amos Tabora _____