Alhamisi, 11 Machi 2021

HUDUMA YA ZANZIBAR JULY 2020

NILIPOKUTANA NA RAFIKI YANGU ZANZIBAR

NIKISHANGAA MAENEO YA MAKUMBUSHO ZANZIBAR
 

PICHA ZA MATUKIO MBALI MBALI

KATIKA MAOMBI

WATOTO WAKIPATA HUDUMA YA ELIMU KANISANI KWANGU IKINDWA TABORA




NIKIWA URAMBO TABORA KATIKA IBADA ZA MAOMBI









NIKIWA NA WATUMISHI WENZANGU KATIKA HUDUMA ZA MAOMBI


NIKIWA ZANZIBAR KIHUDUMA JULY 2020

 

UKOMBOZI WA NAFSI - PASTOR AMOS E. ONESMO

 

SOMO            :           UKOMBOZI WA NAFSI

MTUNZI        :           PASTOR AMOS E. ONESMO

MAWASILIANO:    0759 199463/0683676447

E-MAIL:                    pasteronesmo@gmail.com

 

UTANGULIZI

Mungu alimuumba Mwanadamu katika sehemu kuu tatu ambazo ni:-

·         Mwili

·         Roho

·         Nafsi

Leo tunaenda kuzungumzia ukombozi wa nafsi, tuanze kwa kuangalia maana ya nafsi

Nafsi: - Ni ufahamu wa mwanadamu (UTASHI)

           - Mwanadamu ni nafsi iliyo hai.

MWANZO 2:7

“BWANA MUNGU akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai”.

Mwanadamu ni nafsi hai. Sifa ya kitu kilicho hai ni kama ifuatavyo:-

-          Kufa au kufishwa

-          Kuongezeka

-          Kusemeshwa

-          Kuamua, n.k

Kwa hiyo nafsi ya mwanadamu inaweza kufa, maana ina sifa ya kuwa hai.

1 WAKORINTHO 15:45

Kazi kuu ya Nafsi ni kuunganisha Mwili na Roho

Ndani ya Nafsi ndiko kunakowekezwa aina zote za elimu na ujuzi.

Nafsi ya Mwanadamu imebeba

Ø  Nia

Ø  Utashi

Ø  Hisia

Nafsi ni mtu mwenyewe

Nafsi ya Mwanadamu inaweza kufanyiwa mambo yafuatayo:-

        i.            Nafsi inaweza kufungwa

Inaweza kuweka na adui katika kifungo. ZABURI 142:7 ”Uitoe nafsi yangu kifungoni.....”

Mwandishi wa Zaburi anatamani nafsi yake ifunguliwe baada ya kuona kuna mambo hayaendi kwa sababu nafsi haiko huru.

      ii.            Nafsi yaweza kuingizwa shimoni. Nafsi ya mwanadamu inaweza kuingizwa shimoni na adui na kupelekea mtu asifanikiwe maana ndani ya nafsi ndimo kuna kila hazina ya mwanadamu.

AYBU 33:18,22

18 ”Yeye huizuia nafsi isiende shimoni.....”

22 “Naam, nafsi yake inakaribia shimoni…”

Wapo watu wanaishi huku nafsi zao zikiwa shimoni. Ni vigumu mtu kufanikiwa akiwa shimoni.

AYUBU 33:28

Nafsi ya mwanadamu inaweza kuchimbiwa shimo

ZABURI 35:7

“….bila sababu wameichimbia shimo nafsi”

Unaweza kuwa unaishi huku nafsi yako imeshafichwa shimoni. Wachawi inawezekana walishakuchimbia shimo na wamekuficha. Unatembea huku uko shimoni.

Nafsi ya mwanadamu inaweza kunaswa shimoni, inaweza kuibiwa, kutekwa na kufichwa katika magereza ya giza.

ISAYA 42:22 “Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa, wote wamenaswa katika mashimo wamefichwa katika magereza, wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye, wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha”.

BAADHI YA DALILI YA NAFSI ILIYOFUNGWA

v  Kupata matatizo ya vipindi/misimu

v  Roho za urithi

v  Pesa hazikai na kufanya kufanya kinachoeleweka

v  Maamuzi yaliyofungwa

v  Ndoto za kutisha

v  Unaanza kitu kinaishia njiani

v  Kuahirisha ahirisha mambo

v  Roho za madeni

v  Kuchelewesha mambo

v  Ukiajiriwa na wengine unawatajirisha ila ukijiajiri hufanikiwi

    iii.            Nafsi inaweza kwenda kuzimu

ZABURI 86:13 “…umeiopoa nafsi yangu na kuzimu”. Unaweza kuwa unatembea huku nafsi yako iko kuzimu, mtu aliyeko kuzimu hawezi kuziona Baraka za Mungu kiroho na kimwili.

    iv.            Nafsi inaweza kukombolewa

Kukomboa ni kuweka kitu katika hali ya uhuru. Ukombozi wa nafsi ni hali ya kuitoa nafsi katika hali ya utumwa (kukosa uhuru) kwa jina la Yesu.

AYUBU 33:28 "Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni.......”

Nafsi yako inahitaji kukombolewa, usiruhusu Adui aitumikishe. Usiruhusu wachawi waishikilie nafsi yako, Ukombozi unapatikana kwa JINA LA YESU. Nafsi yako inahitaji kukombolewa.

ZABURI 124:7 "Nafsi yetu imeokoka kama ndege katika mtego wa wawindaji, mtego umevunjika, nasi tumeokoka”

NAMNA YA KUKOMBOA NAFSI

Mungu ametufunulia akili/maarifa hii ili tuitumie kukomboa nafsi za waliofungwa

LUKA 24:45.

        i.            Tamka Jina la mhusika unayemkomboa katika maombi

-          Mwite kwa njia ya maombi. Simama na Neno la RUDISHA.

      ii.            Taja eneo unayoikomboa/unayotaka kuikomboa.

Mfano:

-          Ukombozi wa nafsi katika eneo la uchumi Ndoa n.k

-          Tafuta nafsi ilikozuiliwa. Mfano: Makaburini, Baharini, Mila

    iii.            Vunja nira ya mapepo ya kila aina ndani ya Nafsi.

    iv.            Teketeza/vunja Roho za ukoo zinazong’ang’ania nafsi ya mtu.

      v.            Bomoa yote yaliyowekwa ndani ya Nafsi.

    vi.            Kataa kumilikiwa na Nguvu za Giza.

Maarifa hii ikusaidie kutoka sehemu moja hadi nyingine.

HOSEA 4:6

UBARIKIWE KWA KUFUATILIA SOMO HILI

Limeletwa kwako na mimi

PASTOR AMOS E. ONESMO

0759199463/0683676447

E-mail: pasteronesmo@gmail.com