SOMO LA NDOTO
Ndoto
ni njia mojawapo ambayo Mungu husema,na kuwaelekeza watoto wake waleo.
YOWELI
2:28-29
Shetani
pia huzungumza,hushambulia na kuwamiliki watu kupitia ndoto.Maombi yenye nguvu
yanaweza kukuwezesha kuyashinda mashsmbulizi kama hayo ya ndoto.Jifunze
kushughulika na ndoto ili kupambana na ndoto za vitisho na za uongo za shetani.
ZEKARIA
10:2
VYANZO VYA NDOTO
1.
Mungu.
AYUBU 33:14-15
2.
Shetani.
AYUBU 4:13-16
KUMBUKUMBU LA TORATI 13:1-4
3.
Shughuli nyingi.
MHUBIRI 5:3
MATHAYO 13:22
LUKA 10:38-42.
Ndoto hii si ya kupuuza, angalia jinsi unavyoutumia
muda.
4.
Hali ya kiroho
ya Mahali ulipolala/Mazingira ya kiroho
MWANZO 28:10-22.
Hii ni kwa sababu tunapolala hatupaombei bali
tunajiombea sisi wenyewe tu.
AINA
ZA NDOTO.
i)Ndoto
za ki-binadamu.
Hizi
hutokana na shughuli nyingi tunazoshinda nazo za kila siku.
MHUBIRI
5:3
ii)Ndoto
za ki-pepo(shetan).
Hizi
ni ndoto za vitisho ,uwongo na mashambulizi juu ya wanadamu zisababishwazo na
nguvu za giza ili kuwamiliki na kuwatawala wanadamu.
YUDA
1:8
iii)Ndoto
za Ki-Mungu.
Hizi
ni ndoto zitokanazo na Mungu ili kutupasha taarifa Fulani katika maisha
yetu.Mungu hutupa maelekezo mbalimbali kwa njia ya ndoto ili tuweze kumshinda
mwovu.
HESABU
12:6
YEREMIA
23:28
KITABU
CHA AYUBU 33:13-17
Ifuatayo
ni mifano ya watu waliopewa maelekezo na Mungu kwa njia ya ndoto kibiblia.
i)
ABIMELEKI
Mungu
alimkemea Abimeleki mfalme wa Gerari kwa ajili ya Ibrahimu.
MWANZO
20:3-7
ii)
YAKOBO
Mungu
alimfunulia Yakobo kuhusu mateso ya Israeli kwa Wamisri na mwisho wake.
MWANZO
46:2-4
iii)
PAULO
Mungu
alimpa maelekezo Mtume Paulo kuhusu huduma yake kupitia ndoto.
MATENDO
YA MITUME 16:9
iv)
YUSUFU
Mungu
aliyatunza na kuyalinda maisha ya motto YESU kupitia ufunuo wa ndoto kwa
Yusufu.
MATHAYO
2:12-13,19-20
TAFSIRI
ZA NDOTO
MATHAYO 1:18-24
Tafsiri ya Ndoto inaweza kuja hapohapo au baadaye.
MATHAYO 2:13-15
BAADHI
YA NDOTO NA MAANA ZAKE.
01.WANYAMA:
Kuota unakimbizwa na wanyama wakali inaasshiria mashambulizi ya kipepo,yaaani
nguvu za giza zimejizatiti dhidi ya maish yako.
02.DAMU:
Kuota/kuona damu kunaonesha kuna hatari mbele.Inaashiria kifo na ajali.Kwa mama
mjamzito huashiria kuharibu mimba.
03.NYUKI:
Kujiona au kumuona mtu amezingirwa na nyuki ni ishara ya shambulizi la kiroho
na kutofanikiwa kimaisha.
04.KUOGA:
Inaonesha/inaashiria utakaso wa rohoni(utakatifu).
05.BIBLIA:
Kuipoteza biblia yako inaashiria kurudi nyuma kiroho na kukosa imani.
06.PAKA:
Kuota paka ndotoni huashiria kuwa wachawi wanafuatilia maisha yako.
07.KUIBIWA
TAJI:Inaonyesha kupoteza umaarufu na kurudi nyuma .pia inaweza kuashiria
kushushwa cheo au wadhifa ofisini au katika nafasi yako kiuchumi au kisiasa.
08.MLANGO
ULIOFUNGWA:Unapo ota mlango wa ofisini kwako umefungwa dhidi yako inaashiria
kupoteza kibali au kufukuzwa kazi.kama ni mlango wa biashara yako inamaanisha
kunahatari ambayo itaua biashara yako.
09.JENEZA:Inaonesha
kuwa roho ya mauti (kifo)inafuatiria maisha yako au umpendaye (rafiki wa
karibu)
10.AGANO:Kufanya
agano/kuingia kwanye agano na mtu yeyote ndotoni ni kifungo cha kiroho.
11.MSALABANI:Inaashilia
mzigo mkubwa na shida /taabu.
12.GIZA:Inaashiria
kuchanganyikiwa na kurudi nyuma.Iinaashiria kuzolota kiroho.
13.DENI:Kukupa
ndotoni au kudaiwa kuashiria kudorora kiuchumi kiasi cha kuonyesha dalili zote
za kufilisika.
14.MBWA:Kucheza
au kumbeba mbwa kunaashiria roho chafu (uovu) hasa wa usherati (uzinzi)
15.NDGU
ALIYEKUFA:Kuota cha ndugu inaashiria uwepo wa mzimu wa familia.Uwe mwangalifu
na ujumbe unaoweza kuonekana kama unapata taarifa muhimu lakini mungu hatumii
njia za kipepo kusema na watoto wake SOMA 2WAKORINTHO 11:14 NA
MHUBIRI 3:21.
16.KUNYWA
POMBE:Kuota unakunywa pombe inaashiria kupenda ya dunia
17.ALAMA
ZA KIPEPO:Unapoumizwa ndotoni au
unapoamka na kukutwa alama mwilini mwako inaashiria magereza ya kiroho na
kutumikishwa na mapepo.
18.PUNDA:Inaashiria
ugumu wa mateso au shida katika maisha.
19.MITIHANI:Unaashiria
majaribu na hali,kipindi kigumu.
20.KUPAA:Inaashiria
kutawaliwa na wachawi,shambulizi la kiroho yaani kwamba huenda
utachanganyikiwa.
21.KUVUA
SAMAKI:Kuvua samaki inaashiria kuhubiri injili ya wokovu(soul winning)kama
ilivyo katika biblia.
22.MOTO:Inaashiria
kupoteza na majanga.
23.MAUA:Kupokea
maua kutoka jinsi nyingine (kwa ambao hawajaoa au kuolewa)inaashiria kuwa
mwenzi wako huenda atakujakuwa huyo huyo kwa maisha yako.
24.KUPIGWA
RISASI(KUJERUHIWA):Inaonyesha udhaifu wa kiroho,shambulizina maadui wamejipanga
kuharibu maisha yako.
25.KUPIGWA
RISASI (ISIKUJERUHI):Inaonyesha ulinzi waakiungu na ushindi juu ya adui zako.
26.KUVUNA:Unapoota
unavuna viazi,mihogo n.k.inaashiria Baraka za Mungu.
27.ASALI:Inaashiria
Afya na mafanikio maishani mwako.
28.NYUMBA
TUPU:Inaashiria hili ngumu na umaskini.
29.KUJIFICHA:Inaashiria
maadui wanapigana/wanafuatilia maisha yako lakini uko chini ya ulinzi wa Mungu.
30.SAFARI:Unapoona
na kujiona /kuona upo kwenye safari isiyokuwa na mwisho(kikomo)ina maanisha
unachofanya au unachotaka kufanya itakuwa ni kupoteza-poteza muda na
nguvu.Hakutakuwa na matunda.
31.KUPOTEZA
FUNGUO:Unapopoteza ufunguo wako ndotoni,inaashiria mlango wa Baraka zako
utafungwa.Inaweza hali hiyo ikakuletea hitimisho la mipango chanya,matarijio na
matumaini yako kuhusu mafanikio.
32.
FUNGUONYINGI:Unapoota na kukuta au kugundua umeshika funguo nyingi,inaashiria
Baraka za fursa nyingi zinakusubiri maishani mwako.
34.KUPOTEZA
PESA AU MALI:Inaashiria mambo mabaya au wezi wanaweza kuiba pesa au vitu
vyako.Inaweza kumaanisha unataka kufanya biashara isiyo sahihi au kuangukia
kwenye mitego ya matapeli na makundi ya mafisadi.
35.MZIGO:Kubeba
mzigo inaashiria hili mbaya katika mateso na umasikini.
36.PESA:
Unapoota mtu anakupa msaada au akukupa pesa bure,inaashiria kibali au neema
maalumu na mpenyo wa kipesa mbele yako.
37.MOCHWARI:Inaonyesha/inaashiria
mauti inakufuatilia/imekuzunguka wewe au mtu uliye muona kwenye hiyo ndoto.
38.UKICHAA:Unapoota
umekuwa kichaa ndotoni,inamanisha shetani anataka kusababisha mvurugano katika
maisha yako.Inamaanisha shetani anataka/yuko tayari kukudhuru.unapoota unacheza
na vichaa au watu wenye ukichaa pia inaashiria shambulizi la kiroho ili
kukusambaratishia amani na utulivu.
39.WAHUNI:Unapoota
umekimbizwa/umefukuzwa na wahuni,inaashiria nguvu za giza na wachawi wanajaribu
kukuharibu(kukuua).
40.RUNGU:Niishara
ya nguvu,pia inaashiria ukakamaavu
kiroho na ulinzi wa kiungu.
41.
NDOA:Unapoona unafunga ndoa na mtu asiyemjua,inaweza kuashiria mume/mke wa
kipepo (kama ni mtu unayemjua lakini ameao/ameolewa,ni ishara ya kufanya kosa
kubwa/hatari katika ndoa.Kama ni mtu unayemjua vizuri na wote mko na vijana na
kama huna tama za mwili kwake (naye)hiyo inaweza kuwa ishara ya mwenzi wa
maisha.
42.MIMBA
KUTOKA/KUHARIBIKA:Kama mwanake mjamzito ,umeota mimba
imetoka/imeharibika,usilichuklie kirahisi,pasipo kuangalia ni nani
aliyesababisha hilo,kwani linaweza kutokea kiuhalisia.
43.UCHI/KUVUA
NGUO:Inaashiria aibu au fedheha .
44.SIMBA:Kama
katika ndoto yako umeshambuliwa na simba na ukafanikiwa kumuua,inamaanisha
umemshinda na kumua mtu aliyekuwa anataka kuharibu maisha yako.
45.BUNDI:Kuona
bundi ndotoni inaashiria ubaya.ni taarifa kwamba kitu kibaya
kitatokea/kinakwenda kutokea.
46.MTU
ANAKUFUKUZA/ANAKUKIMBIZA:Kama katika ndoto yako umeota mtu unayemjua
amekukimbiza akitaka kukua, mtu huyo anaweza kuwa hana mawazo/makusudi mazuri
juu yako.Hata hivyo katika nyakati zingine wachawi hutumia sura ya mtu yeyote
kulaghai,ilimradi tu ayaweke maisha yako hatarini.
47.NGURUWE:Ukijiona
unacheza na nguruwe au hata kuwaona nguruwe ,huo ni uchafu kiroho,uzembe na
kutokuwa makini katika maisha ya kiroho.
48.SHIMO:Inaashiria
shetani ana mipango mibaya dhidi yako ili akuharibu.
49.KUCHEZWA
NANYOKA:Hiki ni kuashiria kwamba umefungwa/unatawaliwa na Yule nyoka shetani.
50.KONOKONO:Inaashiria
kudumaa na kuzuiliwa kwa (maendeleo)au kukua kwa mtu.
51.SHULE:Unapoota
mara kwa mara kurudi shule kusoma au kuwa shuleni,inamanisha unahitaji
(mafunzo)kupata/kupitia mafunzo ili kufanya vizuri katika taaluma yako au
utumishi wako katika maisha.kurudi shule za chuni au madarasa inaashiria
kudumaa,yaani badala au kupiga hutua mbele unaridi nyuma kimaendeleo.
52.NGONO.Kufanya
mapenzi na mtu ambaye siyo mwenzi wako wa maisha ni njia ya kwanza
inayothibisha kutawaliwa na tama ya mwili,pili inaweza kuwa msukumo wa pepo kama unaendelea kufanya
mapenzi na mtu usiyemjua.Roho ya uzinzi imeshakutawala.
53.MAJOKA:Inaashiria
imetawaliwa na roho za majini au umeigia/umeingizwa kwenye agano hilo la
mapepo/majini ya pwani baharini au mtoni.
54.NYOTA:Inaashiria
ukuu.
55.MOSHI:Inaashiria
shutuma na majaribu.
56.RADI:Kamakulikuwa
na mvua kubwa iliyoambatana na mawe ngurumo na radi,inaashiria matatizo na
kuchanganyikiwa siku za usoni.
57.KIJIJI:Unapoota
kijiji chako mara kwa mara wakati wewe unaishi mjini hali hiyo inaashiria kuwa
laana za mizimu zinajitokeza kukurudisha nyuma.
58.KUNGURU:Inaashiria
kifo au mauti mbele yako.
59.PETE
YA NDOA(1):Kama mwanandoa umeota unapoteza pete yako ya ndoa,inaweza
kuonyesha/kuashiria unahitaji kuwamwangalifu sana (ndoa)pia inaashiria matatizo
ya ndoa mbele yako.
60.PETE
YA NDOA(2)Kama umepewa pete ya harusi ukiwa kijana,inaashiria kuolewa hivi
karibuni,pia inaweza kumaanisha mtu (mhusika)ni mwenzi wako wamaisha
61.KUTEMBEA
BILA VIATU:Inaashiria shetani anataka kukuchanganya kukupa aibu na hali ngumu
(shida au taabu) .
KUSHAMBULIWA KATIKA
NDOTO INA MAANA GANI?
Mashambulizi ya kila namna yana maana yake.
Kupigwa katika Ndoto inamaanisha ADHABU ya AGANO LA
URITHI.
MAANA YA MASHAMBULIZI KATIKA NDOTO.
Unajulishwa kuwa umevunja kawaida/Miiko ya Mungu wa
Eneo.
2WAFALME 17:24-29
Unajulishwa kuwa umepata ADHABU litokanalo na Mungu
wako.
HESABU 21:4-6
1WAFALME 13:20-26
HITIMISHO:
Ndoto hutoa taarifa ya
jambo Fulani kwa mhusika. Taarifa hiyo inaweza kuwa:-
a.
Mbaya
b.
Nzuri
CHANGIA SADAKA YA UNUNUZI WA CHOMBO
CHA UINJILISTI VIJIJINI
Mpendwa
nakusalimu katika jina la Yesu! Mimi ni ndugu yako Mchungaji Amos E. Onesmo.
Licha ya kuchunga Kanisa, nimekuwa nikifanya UINJILISTI vijijini Katika mikoa
na maeneo mbali mbali. Nimekuwa nikimwona Mungu kwa viwango vya juu sana.
Kumekuwa
na changamoto kubwa kwa wahubiri wengi kutofika vijijini kutokana na mazingira
ya vijijini kuwa magumu sana. Usafiri ni mgumu, malazi, hata chakula wakati
mwingine si bora sana. Kiukweli, watu wa vijijini wanamhitaji Mungu sana wapo
katika vifungo vikubwa vya giza vinavyosababishwa na:-
·
MIZIMU
·
MAAGANO
·
MAPEPO
·
MAJINI n.k
Katika
huduma hii ninayoifanya ninauhitaji mkubwa wa SPEAKER moja ambayo ikishachajiwa
inaweza kutumika bila ya kuunganishwa moja kwa moja kwenye Umeme. Nina uhitaji
wa SPEAKER hii kwa sababu vijijini kuna shida kubwa ya umeme.
Kwa
heshima kubwa, naomba mchango wako ili kuniwezesha kupata SPEAKER hiyo yenye
thamani ya LAKI 3 (Tsh300,000/=). Unaweza
kunichangia FEDHA au Unaweza kuninunulia SPEAKER hiyo ukaniletea, Baraka za
Mungu zitamiminika kwako maana utakuwa umehudumu pamoja nami.
Unaweza kuchangia kwa namba hii;
NAMBA
|
JINA LA USAJILI
|
0658727799
|
AMOS
ONESMO
|
Pia, unaweza kuchangia kwa account ya BENKI.
NAMBA YA ACCOUNT (NMB BANK)
|
JINA LA ACCOUNT
|
51010032134
|
AMOS
EZEKIA ONESMO
|
Ukichangia
nitumie jina lako na mahitaji yako ili nikuombee kwa namba hizi za mawasiliano;
0759199463 / 0658727799
Whatsapp number:
0759199463
MPENDWA
JISIKIE KUTUMIKA PAMOJA NAMI KWA NJIA YA SADAKA.
…………………………..…….BARIKIWA MNO!..................................................
By
Pastor Amos E. Onesmo
July 2018