UONGOZI NA
UTAWALA WA KANISA.
UTANGULIZI
Asili
yote ya Uongozi na Utawala, unatokana na Mungu mwenyewe, Mwanzo 1:26-27.
Alipanga kila mwanadamu awe mtawala, ila kusudi lake liliharibiwa na dhambi,
Mwanzo 3:1-10.
Dhambi
ya Mwanadamu ilichelewesha Mpango wa Mungu, Kutoka 32:1-6 linganisha na Kut
19:5-6. Hivyo Mpango wa Mungu ulitimizwa kupitia kifo cha Kristo alipokuja hapa
duniani 1Pet 2:5-9.
Uongozi
na Utawala ni Vitu viwili tofauti ndani ya Kanisa, Makanisa mengi hayana
Uongozi bali yana Utawala.
1)
Uongozi ni nini?
Uongozi
ni kutangulia mbele, ni kuonesha njia siyo kuswaga, ni kutenda kile ambacho
unataka watu watende. Hivyo, Uongozi ni kuelekeza wengine kwa vitendo. 1Kor
11:1, Zab 23:2-3.
Uongozi
ni Utumishi siyo Ubwana, bali ni kuwa kielelezo kwa kundi 1Pet 5:3 1Tim 1:16
Uongozi
ni ushawishi, ni uwezo wa mtu mmoja kuwashawishi wengine waweze kufuata Uongozi
wake.
Uongozi
wa Kiroho unaweza kutimizwa na watu wa kiroho pekee.
Neno
Uongozi linatokana na neno Kuongoza, ni ile hali ya mtu kuwatangulia wengine na
kisha wengine hufuata nyuma.
2)
Utawala ni nini?
Ni
kule kusimamia, kumiliki, kunyenyekesha, kuamuru na kutiisha. Kwa hiyo kutawala
ni kutumia Uwezo au Nguvu au daraka ulilonalo kuamuru na kutiisha.
Kupitia
mambo hayo mawili Uongozi na Utawala, Matumizi yake ni sehemu mbili.
a)
Ndani ya Kanisa tutumie Uongozi wa kiroho.
b)
Mambo ya Kiofisi ndipo twatumia Utawala.
UKWELI
HALISI.
Si
vibaya mtu kutamani kuwa Kiongozi, lakini ni vibaya kutumia njia isiyo sahihi
kutafuta Uongozi.
Kama
mtu hana hamu ya kuwa kiongozi anakasoro katika maumbile yake. Maaana Mungu
alishaweka ndani ya kila mwanadamu zile Silika 5.
1. Silika
ya kujilinda ambayo inatuonya juu ya hatari na kutuwezesha ili tujifunze
wenyewe.
2. Silika
yenye nia ya kupata ambayo inatuongoza kujipatia mahitaji yatakayotusaidia.
3. Silika
ya kutaka kula, nguvu ambayo hutuongoza katika hali ya kuitosheleza njaa ya
asili.
4. Silika
ya Uzazi ambayo huongoza viumbe au binadamu ili wadumishe Taifa.
5. Silika
ya kutawala au (kuongoza) ambayo humwongoza mtu au binadamu katika kujitwalia
madaraka, kama vile kuitaita wengine au kutoa Amri juu ya wengine na kutaka
kuwatawala.
Zaburi
8:4 Mwanzo 1:26-27
Ndani
ya kila mtu mna hamu ya kuwa Kiongozi au kutawala maana kila Mwanadamu:
a) Anapenda
sifa.
b) Anapenda
cheo au Uongozi.
c) Anapenda
kuheshimika au kuheshimiwa.
d) Anapenda
kupendwa.
Kwasababu
hizo hutakiwi kumkashifu Mwanadamu yoyote.
MAFUNDISHO
YA MSINGI KUTOKA BIBLIA.
Katika
Biblia Viongozi wadhihirishwa kuwa Watumishi. Musa hakuitwa “Musa kiongozi
wangu” bali Mungu alimwita “Musa Mtumishi wangu”.
Hapa
duniani watu wanaangalia utumishi kana kwamba ni jambo la kudharaulika, bali
Yesu aliuinua Utumishi kwa nafasi ya juu kuliko vyote. Marko 10:42-43
MASHARTI
MAKUU YA UONGOZI
Uongozi
unayo Masharti makuu manne ambayo ni lazima kila kiongozi ayatimize kabla ya
kuanza kazi ya Uongozi, Vinginevyo kiongozi huyo hatafaulu kuongoza.
1.
Sharti la kwanza.
Inampasa
kiongozi atayarishwe kwanza.
a)
Kutayarishwa kimwili na watu.
1. Musa
alitayarishwa kielimu Mdo 7:22
2. Musa
alitayarishwa awe Mchungaji Kut 3:1
3. Samwel
alitayarishwa na Eli 1Samw 2:11-18
4. Sauli
alitayarishwa awe Mfalme 1Sam 9:22-27
5. Daudi
alitayarishwa awe Mchungaji 1Samw 16:11
6. Daniel
alitayarishwa kielimu Dan 1:3-4
7. Saul
(Paulo) alitayarishwa Kielimu Mdo 22:3,
Gal 1:14
b)
Kutayarishwa kiroho na Mungu (Kupakwa Mafuta)
1. Musa
alitayarishwa kwa Maono Kut 3:2 4:1-17
2. Sauli
alitayarishwa kwa kupakwa mafuta 1Samw
10:1
3. Daudi
alitayarishwa kwa kupakwa mafuta 1Samw
16:13
4. Elisha
aliyatayarishwa kwa kupakwa mafuta 1Fal
19:15-16
5. Daniel
alitayarishwa na Mungu Dan 1:17-21
6. Isaya
alitayarishwa na Mungu Isaya 6:6-7
7. Yeremia
alitayarishwa na Mungu Yer 1:9
8. Ezekia
alitayarishwa na Mungu Ezek 3:1-4, 8
9. Bwana
Yesu alitayarishwa na Baba Yoh. 10:36
10. Paulo
alitayarishwa na Bwana Mdo 9:17-19
c)
Kujitayarisha wewe mwenyewe.
1. Kuvaa
silaha zote za Mungu Efeso 6:11
2. Kujitakasa
na kujitenga 2Tim 2:21
3. Kuwa
na bidii katika kusoma au kujifunza 1
Tam 4:13 2Tim 3:14-15 IITim 2:2 Math
11:29
2.
Sharti la pili.
Kiongozi
wa kweli hukubaliwa na Mungu pamoja na Wanadamu (watu) Rum 14:18
Mifano.
1. Samweli
alipata kibali kwa Mungu na watu pia ISam 2:26-3:20
2. Mfalme
Sauli alipata kibali kwa Mungu na kwa watu pia ISamw
10:24
3. Bwana
Yesu alipata kibali kwa Mungu na kwa watu pia
Luk 2:52
A.
KUKUBALIWA NA MUNGU.
Kukubaliwa
ina maana ya kuchaguliwa na Mungu.
1. Timotheo
alihimizwa ajioneshe kuwa amekubaliwa na Mungu
ITim 2:15
2. Mfalme
Sauli alichaguliwa na Mungu ISamw
9:17
3. Mfalme
Daudi alichaguliwa na Mungu ISamw 16:12
Mdo 13:22
4. Bwana
Yesu alikubaliwa na Baba Mungu Math 3:16 Mdo 17:31 Isay 42:1 Ebr 3:1-6
B.KUKUBALIWA
NA WATU.
1. Nabii
Samweli alikubaliwa na Israel wote ISamw 3:20
2. Mfalme
Sauli alikubaliwa na watu wote ISamw 10:24
3. Mfalme
Daudi alikubaliwa na Israel wote 2Samw
5:1-3
4. Bwana
Yesu alikubaliwa na watu wote awe Mfalme
Yoh 6:15 Filip 2:9-11 Mark 11:8-9 Yoh
11:47-48 Math 27:54
3.Sharti
la tatu.
Imempasa
kiongozi ampendeze Mungu na Wanadamu pia. Rum 14:18 Luk 2:52
A. Kumpendeza
Mungu, ni kule kufanya mapenzi yake Yoh
6:38-40 4:34 IYoh 2:17
B. Kuwapendeza
Wanadamu :-
1. Ni
kuwa mwanana kwa watu wote 2Tim 2:24
2. Ni
kuwa na huruma kwa watu wote Math 9:36
3. Ni
kuwapendeza watu wote Yoh
13:1 IThes 4:9
4.Sharti
la Nne
Inatakiwa
watu wamwamini Mungu na pia wamwamini kiongozi, Kut 14:31
a) Watu
wamwamini Mungu Mark 11:22 Yoh 14:1
b) Watu
wanatakiwa kumwamini kiongozi Kut.
19:9 IKor 4:1 Yoh 7:31 Luk 12:42
KUSUDI LA
UONGOZI
Efes 3:7-14
Mungu
ameweka Uongozi ndani ya kanisa kwa kusudi moja kuu, “KUWAKAMILISHA
WATAKATIFU”, Baada ya Watakatifu kukamilishwa ndani ya Kanisa kutatokea mambo 6
1. Kazi
ya huduma itatendeka. Rum 12:4-11
2. Mwili
wa Kristo utajengwa. IPet 2:5
3. Kufikia
Umoja wa Imani. Rum 1:17
4. Kufahamu
sana Mwana wa Mungu Filip 3:8-10
5. Kuwa
mtu mkamilifu Filip 3:15
6. Kufika
kwenye cheo cha kimo cha Utimilifu wa Kristo
Ef 1:22
JINSI
YA KUWAKAMILISHA WATAKATIFU YAMPASAYO KIONGOZI.
1. Kiongozi
mwenyewe awe ameongoka Luk 22:31-32
2. Kiongozi
lazima awe mkamilifu Filp 3:15
3. Kiongozi
sharti awe kielelezo ITim 4:11-16
4. Kiongozi
lazima awe amefuatwa na kundi 1Kor
11:1 4:6
Filp 3:17
5. Kiongozi
anapaswa kulilisha kundi Mdo
20:20 ITim 3:2 5:17
6. Kulionya
kundi
a) Kwa
machozi Mdo 20:31
b) Kwa
Uvumilivu wote na mafundisho 2Tim 4:2
c) Kwa
hekima yote Kol 1:28
d) Kwa
roho ya upole Gal 6:1
7. Kuchunga
na kutunza na kusimamia IThes 2:6-8 IPet 5:1-4
8. Kulihurumia
kundi kwa namna mbili.
a)
Huruma kiroho – Math 9:36 Yuda 1:22-23
b)
Huruma Kimwili-Math 14:14-21 Mark
6:30-32
MATOKEO
1.
KAZI YA HUDUMA ITATENDEKA
Kazi
ya huduma ikitendeka italeta mfungamano wa kazi za Utumishi katika Kanisa Efes
4:1-6
a) Kutatokea
maelewano ya Watumishi na Viongozi Gal
2:7-10 2Pet 3:15 Rum 12:16
b) Kutakuwepo
maelewano katika Utendaji wa kazi kimadaraka (kati ya zile huduma tano za
kanisa) Mdo 13:1 Filip 1:1
IIKor 11:28
c) Maelewano
yatakuwepo kati ya Wahudumu na kanisa. IPet
4:8-11 Filip 2:1-4
d) Kutakuwepo
maelewano ya Utendaji wa Karama za Roho Mtakatifu kanisani IKor 14:14-32, 37-39
2.
MWILI WA KRISTO UTAJENGWA
Mwili
wa Kristo ambao ni Kanisa kwa ujumla kutakuwa na mfungamano wa utendaji kazi
ndani ya kanisa kwa pamoja Viongozi na Waamini.
Mwili
wa Kristo hujengwa na:-
a) Jiwe
kuu la Msingi ambalo ni Bwana Yesu IKor 3:10
b) Mawe
ya kuujenga Msingi ni Mitume na Manabii Efeso 2:20-22
c) Mawe
ya kujengea jengo lote ni Waamini IPet 2:5
d) Wajenzi
ni Watumishi na Waamini Efes 4:16
e) Namna
ya kujenga, tunajenga kwa Upendo Efes 4:16
3.
KUFIKIA UMOJA WA IMANI.
Katika
Warumi 1:17 inaelezea aina mbili za Imani zilizo kuu. Pamoja na hizo kuna aina
zingine:-
1. Imani
ya Karama, hii ni kwa ajili ya Uwezo IKor 12:9
2. Imani
ya Tunda la Roho Gal 5:22
3. Imani
ya kuokoka Rum 10:9
Efes 2:6
4. Imani
ya kuponywa Mdo
14:8-10
5. Imani
ya kutenda Amuz
14:5-6 ISamw 17:34
6. Imani
ya kutendewa Dan 6:21-24 Ebr 11:30
Mdo 12:5-11 16:23-34
4.
KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU
Inatupasa
tufike mahali pa kumtambua Yesu Kristo jinsi inavyopasa.
a) Tujue
Uungu wake Isaya 9:6
Math 16:16 IYoh 5:9-12
b) Tujue
Ubinadamu wake Gal 4:4-5
c) Tujue
uwezo wa kufufuka kwake Filip 3:14
d) Tujue
wema wake Tito 3:4
5.
KUWA MTU MKAMILIFU
Hatuwezi
kuwa wakamilifu kwa nguvu zetu, bali tunakuwa wakamilifu kwa utoshelevu au
kutoshelezwa na Kristo mwenyewe 2Kor 3:4-6
Tunapewa
Ushindi wa Kristo IKor 15:57. Bila yeye
Yesu Kristo sisi ni wakamilifu Filip
3:15 lakini bado tunaendelea mbele ili tufikie Ukamilifu halisi. Filip 3:12.
6.
KUFIKA KWENYE CHEO CHA KIMO CHA UTIMILIFU WA KRISTO.
Hatua
hii ndicho kilele cha mwisho kabisa katika kazi ya kuwakamilisha watakatifu
Efes 5:25-27
Katika
kilele hicho ndipo mahali ambapo Kristo anapotaka kuja kulichukua kanisa la
Mungu na Hekima ya Mungu ni Kanisa la Kristo Efeso
1:22-23
Kanisa
hufikia hatua hiyo baada ya kupitia zile hatua kwa kupitia Mateso, Matengenezo,
Kuthibitishwa na Kutiwa Nguvu IPet 5:10.
Tunalindwa ili tusijikwae. Yuda 1:24 IYoh 5:18-21
3:2-3
NGUZO ZA UONGOZI
Uongozi
wa kiroho una nguzo 4 muhimu. Nguzo hizo ni:-
Mamlaka,
Uwezo, Utendaji na Wajibu.
MAELEZO
YA HAYA MAMBO MANNE.
1.
MAMLAKA. Math 28:18 Luka 9:1
(AUTHORITY)
Kuwa
na mamlaka ni kule kuwa na haki ya kutoa Amri au haki ya kutumia Uwezo.
Pasipo
mamlaka hakuna haki ya kutumia Uwezo na pia pasipo Uwezo mamlaka hayana faida.
Mdo 19:13-16
Katika
Ukristo tumepokea mamlaka, mamlaka ni Urithi tunaoupata katika kumwamini Yesu
kristo. Uwezo wetu ni Roho Mtakatifu.
2.
UWEZO (POWER) Mdo 1:8 EBR 1:3
Uwezo
wa kanisa na viongozi wa kanisa ni Roho mtakatifu. Huu ni uwezo wa kuendesha
Utawala wa kanisa. Ikiwa Kiongozi wa kanisa hana huu Uwezo, atatumia udikiteta
IKor 2:1 Filp 4:3
Uwezo
wetu ni kule kusema Neno tu. Luk 7:7 tunayo haki kisheria ya kutenda au Uwezo
wa kutenda au kutoa nguvu.
Mf.
Nguvu ya Serikali huwezeshwa na Jeshi, Mahakama na Magereza.
Mamlaka
bila Uwezo ni Bunduki isiyo na Risasi
Efes
1:19 3:7,20 Ikor 2:1-4
Uwezo
wetu siyo katika maneno.
3.
UTENDAJI = ETFECTUAL WORKING (OPERATIONS)
IKor
2:6
Utendaji
ni nguvu za utekelezaji, Utendaji ni uwezo wa kuamuru ni uwezo wa
utekelezaji, ni kuweka Imani katika Vitendo kwa kusema na kutenda.
Katika
utendaji kiongozi anahitaji mambo manne:-
1. Kupanga
IKor 14:40 IThes 5:14
2. Kuandaa Luk
14:28-32
3. Kuelekeza
Mark 11:1-10
4. Ufuatiliaji Mdo
20:28
Utendaji
ni kule kuwa na Uwezo wa kuamuru na kutekeleza.
Mifano
hai katika maandiko.
a) Mtume
Petro aliamuru kiwete asimame Mdo 3:6
b) Mtume
Petro aliamuru watu wa nyumbani mwa Kornelio wabatizwe Mdo
10:48
c) Towashi
aliamuru gari lisimame 8:38
d) Mtume
Paulo aliamuru kiwete asimame Mdo 14:10
Katika
utekelezaji kuna mambo mawili muhimu.
1. KUAMURU
Kuamuru
ni kutoa Amri ya kutaka utekelezaji ufanyike Dan 9:23
10:12 Luk 10:19
Tumepewa
Amri ya kuamuru, kazi yetu ni kuamuru.
2. UTEKELEZAJI
Utekelezaji
ni kutimiza kile kinachotakiwa kutendwa Filip 2:13
Kazi
yetu ni kuamuru na kazi ya Mungu ni kutekeleza. Mungu anataka sisi tuwe na ile
hali ya kutaka na Mungu atekeleze IKor 3:9
Filip 2:13
Sisi
tutake, tuwe na nia ya kufanya ili Mungu atekeleze, kazi kuu ya kanisa ni
kuamuru na Mungu ni kutekeleza. Mungu anataka sisi tuwe na hali ya kutaka na
kutenda.
Mara
nyingi tunakosa vitu kwasababu hatujui kuviamuru vitujie. Baraka zote ziko
katika ulimwengu wa kiroho, ni juu yetu kuziamuru zije katika ulimwengu wa
kimwili. Efeso 1:3 Mark 11:23
SABABU
ZINAZOFANYA AU KUZUIA UTEKELEZAJI USIFANYIKE.
1. Kama
jambo hilo liko nje ya makusudi ya Mungu halitatekelezwa. IYoh 5:14 Filip 2:13 Mfano ni Balaamu.
2. Ikiwa
ni jambo liko nje ya mapenzi ya Mungu IYoh
5:14 Mdo 21:14
3. Shetani
anaweza pia kuchelewesha utekelezaji.
4.
WAJIBU (RESPONSIBILITY)
Wajibu
unaambatana na utaratibu wa shughuli za muhimu za kila siku, kila wiki, kila
mwezi na kila mwaka.
Daraka
ni kile kitendo utakachofanya kufuatana na daraka lako. Na katika kufanya haya
lazima uwe na ramani ya kazi (Action plan).
Mfano
huu
TAREHE
|
SIKU
|
SAA
|
SHUGHULI
|
16/04/2017
|
Jumapili
|
Saa 4-8:00
|
Ibada ya Pasaka
|
01/05/2017
|
Jumatatu
|
Saa 8 Mchana
|
Kukutana na Vijana
|
Pia
ni vema kuwepo na mchanganuo wa madaraka na utendaji wa kazi (Scheme of Work), maana Mungu wetu ni Mungu wa Utaratibu IKor
14:40 Kol 2:5
NO
|
JINA
|
WADHIFA
|
DARAKA
|
01.
|
YUSUPH PETER
|
MCHUNGAJI
|
UONGOZI NA UTAWALA
|
02.
|
AMAN KASHESHE
|
KATIBU
|
UTEKELEZAJI
|
03.
|
PAUL SILA
|
MZEE KIONGOZI
|
UINJILISTI
|
04.
|
MARY JUMA
|
MCH. MSAIDIZI
|
SHUGHULI ZA WAGENI
|
Mtume
Paulo alifanya kazi kwa utaratibu, Ona Rum 15:24-29 IKor 16:5-12
IKor 14:40. Safari za Injili zina mifumo miwili.
1. Kutumwa
na Roho Mtakatifu.
2. Kuazimia
Rohoni.
Mtu
anayeweza kutimiza wajibu ni Yule aliye na Mzigo mzito moyoni. Mdo 20:22 5:29
15:36 IIKor 11:28
GOD’S
CALL TO LEADERSHIP
WITO
WA MUNGU KATIKA UONGOZI
Mambo
manne ambayo hutokea kuhusu Wito wa Mungu.
WITO,
JIBU, UJUMBE, UTUMWE
Mfano
ni kutoka kwa wito wa Musa, Ni jinsi gani huita? Mungu hatuiti tunapookoka au
baada ya kuokoka bali hutuita kabla ya kuzaliwa. Musa aliitwa, aliitika,
akapewa ujumbe, Nenda Misri kuokoa Wana wa Israel. Musa aliumwa ili aende
Misri.
Wito
wa Mungu kwa watu wake kuwa viongozi siyo jambo la kuchukulia juu juu bali ni
kitu cha nafasi ya kipekee katika maisha.
VIONGOZI
LAZIMA WAANDALIWE.
Paulo
alimwandaa Timotheo
Musa
alimwandaa Yoshua.
Timotheo
aliandaa Wazee kule efeso
Tito
aliwaandaa Wazee kwa kanisa la Crete
Barnaba
alimwandaa John Marko
Eliya
alimwandaa Elisha.
Wewe
kama kiongozi uliopo sehemu mwandae mtu kwa ajili ya huduma, mwinue kiongozi
kabla ya kwenda kwenye huduma.
Kuza
mtu kwa ajili ya Kesho.
MIIKO SABA YA VIONGOZI.
Kuna
mambo ambayo ni mwiko kwa kiongozi yeyote kufanya na kama atafanya ni lazima
asababishe migogoro na matatizo na kuharibu nidhamu kazini.
1.
Kiongozi kamwe asiwe na upendeleo.
a) Asipendelee
matajiri Yak 2:1-4
b) Asipendelee
ndugu zake Mdo 15:36-40
c) Asipendelee
kabila lake Mdo 6:1
2.
Kiongozi kamwe asisikilize Majungu au Matetano
ITim
5:13 TITO 3:10 Mith 29:12
Kila
kiongozi anatakiwa atambue kuna makundi ya aina tatu kwa wale wanaoongozwa
1. Waliombelembele
2. Waliokatikati
3. Walionyuma.
3.
Kiongozi kamwe asiwe na Majivuno Yer
9:23-25 IIKor 10:12-18
a) Kunia
makuu
b) Kushughulishwa
na manyonge
c) Kutojivunia
akili.
4.
Kiongozi asiwe na tabia ya Upelelezi na kufuatilia mambo madogo madogo Gal 2:4
Kol 3:13 Ef 4:32
5.
Kiongozi asiwe Mgomvi 2Tim 2:24 Tito 3:2
6.
Kiongozi asiwe Mnafiki ITim 1:5 Math 23:27
7.
Kiongozi asiwe kigeugeu Yak 1:17 2Kor 1:11
Math 5:37 Mith 24:21
TABIA
TATU KUU ZA KIONGOZI
1.
Kuwa na Sifa ya Tabia ihusuyo mambo ya kijamii (Social Qualification)
a) Kuwapenda
watu wote
Aina
4 za Upendo
1. Upendo
wa Ndugu Ebr 13:1
2Pet 1:7
2. Upendo
wa kumiminwa (AGAPE) Rum 5:5
3. Upendo
wa kuambatanishwa ISamw 18:1 Mith 18:24 Mw 44:30
4. Upendo
wa Tamaa ambao umekatazwa kanisani 2Samw
16:1-22 Phileo
b) Kuwatembelea
watu wote Mdo 20:20
c) Kusikiliza
kwa makini matatizo ya watu.
d) Kuwafurahia
kundi lako.
e) Kuwa
na upole na utulivu mbele ya kundi.
f) Kuwa
na unyenyekevu mbele ya kundi.
2.
KUWA NA SIFA YA AKILI (MENTAL QUALIFICATION)
a) Uwe
na Busara na akili nyingi Math 10:16
b) Uwe
na Hekima na maarifa Yak 3:7
c) Uwe
na ujuzi wa Neno la Mungu KOL 3:16
d) Uwe
na Hekima ya kuamua mambo IKor 4:5
3.
KUWA NA SIFA YA TABIA YA UPEVU (MATURITY QUALIFICATION)
a) Uwe
na uvumilivu kwa kila jambo
b) Uwe
mstahimilivu wa kulaumiwa
c) Uwe
mjasiri kwa kila jambo
d) Uwe
na uwezo mkubwa wa kutunza siri.
KIONGOZI NA MAJARIBU
1.
AINA TATU ZA MAJARIBU KWA KIONGOZI
a) Kujaribiwa
na Mungu (To prove) Yak 1:12
b) Kujaribiwa
na Shetani (To tempt) Math 4:1
c) Kujaribiwa
na Kanisa ITim 3:10
2.
WAPINZANI WA KILA KIONGOZI
a) Ndugu
zake Hes 12:1 Math 10:21,34
b) Watumishi
wenzake 2Kor 11:25 Gal 2:4-9
c) Washiriki Yoh 6:66, 70
3.
MAADUI WA VIONGOZI
A.
MAADUI WA NDANI Yak 4:1
1. Kiburi,
Sifa, Utukufu Yer 45:5 Zab 12:3
Rum 12:3 Mith 13:10 16:15
2. Wivu Mw 4:5
Hes 11:28
3. Kuvunjika
Moyo
B.
MAADUI WA NJE
1. Shetani
Math 13:27-28 IPet 3:8
2. Dunia IYoh 2:15
3. Fedha
ITim 3:3
4. Ugumu
wa Mambo Math 19:25
HATARI
ZA KIPEKEE KWA KIONGOZI
1. Hatari
kuu IKor 9:27 Math 7:21 IKor 13:5
2. Kujaribu
kujiweka kimbele mbele Rum 12:10 Filip 2:3
3. Kutokutaka
kusahihishwa Yak 3:17
4. Kutokuwa
na Siri Ikor 4:1
5. Kupendwa
sana Mdo 14:11-15 28:6
6. Kujiamini
kuwa hauwezi kukosea Mhub 7:15 Mith
16:2
7. Kutoaminika Ikor
4:12
8. Kujiona
au kung’ang’ania Madaraka Filip 2:3
9. Kujisifu 2Kor
10:12 ITim 3:6
10. Kupenda
Sifa Mdo 12:21-23
Luk 18:9-14
SIRI
YA MAFANIKIO YA KIONGOZI.
1.
TAMBUA WALE ULIO NAO KANISANI
Ndani ya Kanisa mna aina tatu za watu
a) Kuna
watu ambao hawajui yale yanayotokea
Those who do
not know what is happening.
b) Kuna
watu ambao ni watazamaji wa yale yanayotukia.
Those who
watch happen
c) Kuna
watu ambao wao husababisha mambo yatokee
Those who make
things happen
2.
KAA PALE MUNGU ALIPOKUITIA
Siri
ya kufanikiwa kwa kila kiongozi ni kukaa pale Mungu alipokuitia, pana fedha au
hapana fedha. Wewe angalia pale Mungu amekuridhia ukae. Mungu atakuinua mahali
popote.
3.
WEKA WAZI MAONO YAKO NDANI YA KUNDI.
Unapoweka
wazi maono yako utafahamu aina ya makundi uliyonayo Kanisani.
a) Ndani
ya Kanisa mna wabeba Maono (Vision carriers).
b) Ndani
ya kanisa mna Wauaji wa Maono (Vision killers) kazi yao kila unapotoka wao
hupanda Magugu, hubaki kwa kutengeneza kata. Huu ni mfano wa wacheza Mpira.
c) Ndani
ya kundi pia kuna Wainuaji wa Maono (Promoters). Ingawa hawa ni wachache sana
katika Makundi, lakini ni muhimu sana.
SIFA
ZA WAINUA MAONO VIONGOZI
1.
Huongoza kwa kanuni Zab 119:4, 168
2.
Huongoza kwa kumaanisha kile wanachosema.
Siyo
kila mara kusema jamani Samahanini, Manisha unachosema na kutunza muda
ulivyosema.
3.
Huongoza kwa kufanyia mazoezi Math 23:1-3
Kinachoua
Maono ni Unafiki.
4.
Maisha yako yawe mfano au picha ya kuangaliwa. IITim 3:10 Filip 3:17
GHARAMA ZA UONGOZI (KIONGOZI)
Uongozi
unazo gharama zake ambazo yeyote anayeingia katika Uongozi lazima azikabili.
Kukubali kuingia katika Uongozi umekubali kuingia katika mateso na matatizo
mengi kwa hiyo tunahitaji uvumilivu na kuchuliana.
Gharama
zenyewe ni hizi:
1.
Kujikana mwenyewe, au kutoa nafsi iwe fidia ya wengine Mark 10:44-45. Ni kuhukumiwa
kifo IKor 4:9
2.
Upweke
Kiongozi
kwa vyovyote ni mtu wa upweke. Kuna vipindi viwili katika maisha ya kiongozi
a) Kipindi
cha kupendwa Yoh 2:23
b) Kipindi
cha kuchukiwa na watu Yoh 6:66
Bwana
Yesu alipendwa, lakini kuna kipindi walimwacha wakati wa kifo chake.
Mtume
Paulo aliachwa na wenzake IITim 1:15
IITim
4:10 Mdo 15:36-40
Wakati
tunapobaki peke yetu ndipo tunapoimarika.
3.
Uchovu
Upo
wakati ambao kiongozi atachoka, hata Bwana Yesu alichoka Yoh 4:6. Tunaposikia
Uchovu ndipo tunakuwa na nguvu za kiroho
2Kor 12:9-10 4:16
Tunapokuwa
Wadhaifu ndipo Uweza wa Mungu wakamilika.
4.
Malaumu
Hakuna
kiongozi aliyesamehewa kulaumiwa na unyenyekevu wake utaonekana wakati wa
kipindi hiki cha kulaumiwa kuliko sehemu nyingine yoyote 2Kor
6:8
Lakini
ifahamike kuwa kuna utofauti ya lawama na kashifa. Mungu kamwe hatavumilia
kuona watu wake wakikashifiwa na shetani au watu.
1. Musa
alipokashifiwa Mungu aliingilia kati Hesabu
12:1
2. Yoshua
alipokashifiwa na Shetani, Mungu aliingilia kati. Zekaria 3:1 Rum 14:4
5.
KUKATALIWA
Kiongozi
anaweza kukataliwa kabisa na kundi na kudharauliwa Isaya 53:3
Ni
bora kukataliwa na watu kuliko kukataliwa na Mungu.
6.
SHIDA NA FADHAA
Watu
wengi hudhani kuwa kutembea na Mungu muda mrefu au miaka mingi huwafanya wapate
Ushindi nyakati za fadhaa na shida.
Lakini
sivyo, Mungu humwangalia kiongozi kama mtu aliyekomaa na hivyo humwachia uamuzi
wa kiroho kama vile Ayubu.
Mungu
wakati kama huu hutuachilia tujisimamie sisi wenyewe. Soma mifano hai, Mtume
Paulo Mdo 20:22 na Yohana Mbatizaji Luk 7:19
7.
GHARAMA KWA WENGINE
Uwe
na Mzigo kwa watu wengine Mdo 19:29
16:19 20:4 Kol 4:10. Tuwe kama Musa Ebr 11:24-25
HATUA TANO ANAZOPITIA KIONGOZI WA
KIROHO 1PET 5:10
Uongozi
wa kiroho unazo hatua zake muhimu unapoajiliwa Serikalini kuna hatua
unazopitia, ambazo ni:-
1. Kufanyiwa
majaribio/mtihani au kazi kwa muda
2. Kuajiliwa
3. Kuchunguzwa
4. Kuthibitishwa
Ndani
ya Kanisa pia Bwana anazo hatua zake
Wito,
Mateso, Matengenezo, Kuthibitishwa na kutiwa nguvu.
I.
WITO WA MUNGU KATIKA UONGOZI
Mungu
hatuiti baada ya kuokoka bali alituita kabla ya kuzaliwa Rum 11:29
Unapoitwa
lazima utoe jibu kisha aliyekuita
atakupa Ujumbe na kisha atakutuma.
Mfano
ni Musa.
a) Aliitwa
– Musa
b) Aliitika
– Niko hapa
c) Nenda
Misri – Alipewa Ujumbe.
d) Alitumwa.
Walioitwa:
1. Wanamfahamu
Mungu wao Ef 4:4-6 Wafil 1:12 Dan 11:32
2. Wanafahamu
mkono wa Mungu uko juu yao Rum 8:28
Ithes 5:23-24
3. Wale
ambao amewaita Mungu hawakati tama Rum
11:29
Mungu
atakutumia kama ulivyo, usiombe akutumie kama mtu mwingine tumika kwa kile
Mungu alichokupa.
4. Hujiangalia
kama Mungu alivyowaita Rum 9:20-21 ISam 16:7
5. Kila
kiongozi aliyeitwa Mungu humwangalia kupitia Yesu Kristo. Kol 3:3 Efes 2:6
6. Wanyo
asili au Mwanzo wao ndani ya Mungu vile alivyokuwa Yesu Kristo. Yoh 4:34
II.
MATESO IIKOR 1:5-7
Kila
kiongozi aliyeingia katika huduma anapitia eneo hili. Huu ni Ubatizo mojawapo
kati ya zile nne.
1. Kubatizwa
katika Mwili wa Kristo IKor 12:13
2. Ubatizo
wa maji mengi Mark 16:16
3. Ubatizo
wa Roho Mtakatifu Mdo 1:5,8
4. Ubatizo
wa Mateso Mark 10:38-39 2Kor 1:5-7
Kila
mwamini au kiongozi sharti apitie Ubatizo huu 2Kor 4:8-10, 17 Kumb 8:2-3 Mdo 14:22
III.KUTENGENEZWA
– MATENGENEZO
Mungu
aliyetuumba anajua siri ya maisha yetu. Mtu anapookoka hawi mkamilifu mara
moja, lakini yeye ni chombo cha Mungu chenye heshima.
Katika
maisha ya waamini kuna tabia zinazomng’ang’ania na kumsumbua baadhi yake ni
kiburi, majivuno, kujiona, uzinzi, dhambi zote za Siri katika maisha ya
kiongozi Mungu anazishughulikia kwa kumpitisha mhusika kwenye matengenezo.
Isaya 4:4 Yoel 3:21
Ukisoma
Zab 51:3-4, 8,12 tunaona Mungu hutakasa damu kwa Mapatilizo Waeb 12:5-6
IISamw 7:14 12:4 IKor 11:30-32
Tunayo
mifano katika maandiko ya watu wa Mungu walioshughulikiwa – Daudi, Yakobo, Paul
na wengine wengi hadi wakati wetu.
IV.KUTHIBITISHWA GAL 4:19
Katika
mapitio hayo ya matengenezo Kristo hufanya hali mpya katika maisha ya mtu huyo.
Hali
hii inamfanya na kumthibitishia mwamini, kiongozi ukaaji mpya na dalili
maishani mwake. Mawazo yake na nia yake anazama kiroho, anautafuta uso wa
Mungu, ujazo wa Roho Mtakatifu.
Hali
hii inampeleka kwenye hatua ya tano.
V.KUTIWA
NGUVU.
Mtumishi
anatiwa nguvu baada ya kuonekana ni mwaminifu Mdo 1:8 Filip 4:13
Kol 1:29 Efes 3:20
Hali
mpya huja Ay 4:12-13 IFal 19:12-13
Nguvu
za Roho Mt. humtawala mhusika masikio, Macho, Fahamu na kila eneo.
UHUSIANO WA KIONGOZI NA KUNDI
Katika
uhusiano na uwiano wa kiongozi na kundi, kiongozi anayo madaraka pamoja na
Wajibu kwa wale anaowaongoza. Ni makosa kwa kiongozi kufikiria kuwa yeye anayo
madaraka tu bila wajibu kwa kundi. Madaraka na Wajibu vinaenda sambamba katika
uongozi, kwasababu hakuna Uongozi bila Wajibu.
1.
MADARAKA YA KIONGOZI.
a) Kuonya
kundi 2Tim 4:2
b) Kukemea
kundi ITim 5:5-20
c) Kukaripia
kundi 2Tim 4:2
d) Kuadhibu
kundi kwa Upendo IKor 5:13
e) Kutawala
na kusimamia ITim 5:17 IPet 5:2
2.
WAJIBU WA KIONGOZI
a) Kulisha
kundi (Kanisa) Mdo 20:28
b) Kuhurumia
kundi Yoh 6:5-13
c) Kutunza
kundi Mdo 20:28
d) Kufundisha
kundi ITim 5:17
e) Kuonya
kundi kwa machozi Mdo 20:31 Filp 3:18
f) Kulichunga
kundi IPet 5:2
3.
WAJIBU WA KUNDI KWA KIONGOZI WAO.
a) Kumheshimu
kiongozi wao ITim 5:17 Wafil 2:29
b) Kumlisha
kiongozi IKor 9:7-14
c) Kumtii
kiongozi wao Ebr 13:17 IKor 16:17
d) Kumsitahi
kiongozi wao ITim 5:12
e) Kumtambua
kiongozi wao ITim 5:12
f) Kumnyenyekea
kiongozi wao Ebr 13:17 Ikor 16:17
g) Kutokukemea
kiongozi wao ITim 5:1
h) Kutomdharau
kiongozi wao IKor 16:11
4.
KIONGOZI NA MAZINGIRA
a) Kiongozi
na wakati Efes 5:15-16 Mh 3:1-7 Mwanadamu hajali wakati lakini Mungu anajali
wakati.
b) Kiongozi
na maombi (Prayers) Dan 6:10
c) Kiongozi
na kusoma (Studying) ITim 4:13
d) Kiongozi
na Siasa - (Politics) ujiepushe.
e) Kiongozi
na Utawala (Government) Rum 13:1
f) Kiongozi
na Elimu (Education) ujifunze IITim
3:14-16 Mdo 18:25-26
g) Kiongozi
na maendeleo naya jamii (Social Development) Uwe na Elimu juu ya jambo hili.
SEHEMU YA PILI YA MAFUNZO
UTAWALA
WA KANISA EFESO 3:9-10 IKOR 12:28
AINA
NNE ZA UTAWALA WA KANISA
1.
UTAWALA WA MAASKOFU – EPISCOPAL ITim 3:1
Huu
ni utawala wa kanisa unaoamuliwa na Maaskofu, Makasisi na Mashemasi.
Filip
1:1 Rum 15:16 ITim 3:1,8
Ufun 1:6. 5:10 Mdo 6:3
Kupitia
Yesu Kristo Waamini wote ni Makuhani IPet 2:5
Kuna
aina mbili za Makuhani (Watumishi)
a) Makuhani
wa watu.
b) Makuhani
wa kumhudumia Mungu Ezek 44:10-16
Viongozi
wa Kanisa wamegawanyika katika sehemu mbili kuu
1. Vipawa
vya Mungu kwa kanisa Ef.4:8-11
Vipawa
vya Mungu ni wale waliochaguliwa na Mungu mwenyewe.
2. Mashemasi
– ni Watumishi wanaochaguliwa na kanisa ili wamtumikie Mungu Mdo 6:3
Katika
utawala huu kuna aina tatu au madaraja matatu
1. Maaskofu ITim 3:1
Filip 1:1
2. Makasisi Rum 15:16 Ufun 1:6
3. Mashemasi
ITim 3:8 Filip 1:1 Mdo 6:3
2.
UTAWALA WA PAPA (PAPAL) BABA
Katika
utawala huu ni kutokea kwa Papa, kanisa linatawaliwa na Makadirinari, Maaskofu
wakuu, Maaskofu, Mapadri. Hawa Maaskofu wakuu ni wale wote kuanzia lile Baraza
la Rumi hadi chini.
Katika
utawala wa kipapa mshiriki wa kanisa au kanisa la mahali hawana haki yoyote ya
utawala.
a) Wanaamini
Papa hawezi kukosea hata jambo moja anapofanya maamuzi ya kikanisa.
b) Papa
ni mwakilishi wa Mungu duniani.
c) Ni
Makamu wa Yesu, ana uwezo wa kumfikisha mtu mbinguni au kutomfikisha Mbinguni.
d) Anaweza
kufanya yale Mungu anayafanya hapa Duniani.
3.
UTAWALA WA KANISA MOJA MOJA (INDEPENDENT)
Huu
ni namna ya Utawala wa kanisa unaokubaliana kuwa mamlaka ya kanisa yamo
mikononi mwa Washirika peke yao.
Makanisa
yenye mfumo huu yana uwezo wa kuamua mambo katika uongozi wao.
4.
UTAWALA WA WAJUMBE (REPRESENTATIVE)
Huu
ni namna ya Utawala wa kanisa unaokubaliana kwamba mamlaka yamo mikononi mwa
Washiriki wa kanisa – wao hufanya baraza la kuchagua Viongozi wa kuongoza na
kulisimamia kanisa. Katika utawala huu Wachungaji huwekwa mikono mara moja.
Wengine huondolewa kwa kupoteza nafasi zao Huu utawala hapa duniani karibu wote
wanao Uongozi una aina mbili kuu.
1. COLLECTIVE
LEADERSHIP – UONGOZI WA PAMOJA
2. UNITARIAN
LEADERSHIP – UONGOZI WA MMOJA MMOJA
Hizi
ni aina 4 za tawala zote zinafanya huduma katika dunia yetu ndani ya kanisa la
Kikristo. Ingawa zingine zimeleta shida katika kuongoza Waamini kufikia lengo
la Mungu lililokusudiwa. Mungu alisaidie kanisa lake kufuata aina nzuri ya
Uongozi ili kufikia kwenye lengo kuu alilolikusudia Mungu.
Pastor Amos E. Onesmo 0756391498/0658727799