NATOA
LAKINI SIPOKEI – NIFANYEJE?
Kuna wakati fulani, unajiuliza hivi; “Kwa nini mimi nimekuwa natoa zaka na
sadaka nyingi lakini sipokei? Hata miradi niliyo nayo haifanikiwi nilivyokusudia
– ni kwa nini iwe hivyo?
Hayo
ni maswali ya msingi na ni muhimu tupate ufumbuzi wake. Hata mkulima ambaye
alipanda mbegu katika shamba, na asipate kitu au apate mavuno machache,
atajiuliza maswali kumetokea kitu gani?
Tukumbuke ya kuwa si mapenzi ya Mungu tuwe maskini – tuwe na hali ngumu
kimavazi, chakula na kiafya. Pia, tukumbuke ya kuwa ni tabia ya kiuungu mtu
kutoa na kutegemea kupokea. Ingawa si lazima upate toka kwa mtu huyo huyo
uliyempa, - maana Mungu anaweza kumgusa mtu mwingine akupe – lakini utaratibu
wa Mungu unabaki pale pale, ukitoa tegemea kupokea.
Ni kitu gani kinasababisha mtu asipokee na huku amekuwa akijitahidi kutoa?
Biblia inatuambia ya kuwa tukiwa waaminifu katika utoaji, Mungu atatumwagia
baraka, “hata isiwepo nafasi ya kutosha ya kuziweka” – Je! umewahi kumsikia
mkristo yo yote akisema amepata baraka nyingi mno hata amekosa mahali pa
kuziweka?
Sababu zifuatazo zitatusaidia kujua
ni kwa nini hatufanikiwi katika utoaji wetu – na hata hatupokei kama
tulivyotegemea na kutarajia;
1. KUVUNJA MIIKO AU UTARATIBU WA UTOAJI
Kila jambo lina utaratibu wake – usipoufuata usitegemee mavuno mazuri. Kilimo cha mahindi kina utaratibu wake wa upandaji na palizi tofauti na kilimo cha ngano au cha kabichi. Ndiyo maana wataalamu wa kilimo, walianzisha kampeni za kuwafundisha wakulima juu ya “kilimo cha kisasa” ili kiwasaidie wakulima kupata “mavuno” zaidi toka katika mashamba yao.

Hata katika “kupanda na kuvuna” au “kutoa na kupokea” katika mambo ya Mungu
kuna utaratibu wake. Ukienda kinyume na utaratibu huo, usitegemee mavuno ya
kuridhisha toka katika utoaji wako
Kwa mfano hebu soma na kutafakari
maneno haya yafuatayo:
“Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna
haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama ilivyokusudia
moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu
humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu” (2Wakorintho 9:6,7).
“….wala si kama kitu
kitolewacho kwa unyimivu” (2Wakorintho 9:5).
Utaona katika mistari hiyo Mungu ametueleza kwa kiasi fulani utaratibu ambao
anataka ufuatwe mtu akitaka kuvuna katika utoaji wake. Je! unafuata utaratibu
huu katika utoaji wako?
Utaratibu huoni huu; utoaji wako uwe si haba (au kidogo) bali uwe kwa
ukarimu. Ukitoa kidogoutapata kidogo – bali ukitoa vingi utapata vingi. Ndiyo
maanaimeandikwa;
“Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha
kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu
watakachowapa vifuani mwenu. KWA KUWA KIPIMO KILE KILE MPIMACHO NDICHO
MTAKACHOPIMIWA” (Luka 6:38)
Kama unataka kutoa sadaka tu “ kama ulivyokusudia moyoni mwako”. Kama
ulikusudia kutoa shilingi 100/= toa shilingi 100/=. Fanya hivi siku zote na
utafanikiwa.
Tena, utoajiunatakiwa ufanyike “si kwa huzuni; wala si kwa lazima; maana
Mungu humpenda yeyeatoaye kwa moyo wa ukunjufu “… na walasi kwa unyimivu”.
Michango mingi iliyomo makanisani siku hizi wakati mwingine inafanyika kwa
kulazimishana.Mtu anatakiwa atoe kwa kupenda kwake toka moyoni mwake – SI KWA
LAZIMA.Kumlazimisha mtu kutoa ni kwenda kinyume cha utaratibu wa utoaji.
Wakristo wengiwamekosa baraka au mafanikio katika utoaji kwa sababu
wanatoa huku WANAHUZUNIKAAU WANALALAMIKA! Wengi wanawanung’unikiaviongozi wa
makanisa yao kuwa wanatumiafedha au vitu vibaya. Kama una wasiwasi na matumizi
ya matoleo yako – yaombeekwa Mungu ayalinde yatumike kwa utukufu wake kuliko
kulalamika.
Wengine
wanahuzunika na kulalamika kuwa michango imezidi. Je! umewahi kumsikia mkulima akihuzunika
au kulalamika kwa kuwa ameongezewa shamba la kulima na kupanda? Hakuna. Mkulima
halalamiki bali anafurahi kwa kuwa amepata eneo kubwa zaidi la kupanda
umeongezewa eneo la KUPANDA ili AVUNE ZAIDI. Ni eneo la kukusaidia kutoa zaidi
ili UPOKEE ZAIDI!
2. IBILISI AMEZUIA BARAKA ZAKO;
Kati ya baraka ambazo zinapatikana kutokana na mtu kuwa mwaminifu katika utoaji wa zaka (fungu la kumi) na dhabihu (matoleo mbalimbali) na kuzidiwa wakati wa matatizo, Mungu alisema hivi;
“Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba ….” (Malaki 3:11).
Ni wazi kuwa aliye nyuma ya kuharibika kwa mazao shambani au biashara ni yule ‘alaye’ ambaye ni Ibilisi. (Hii ni kama mkulima au mfanya biashara amefanya anachotakiwa kukifanya kilicho ndani ya uwezo wake).

Kinyume cha jambo hili ni kwamba usipokuwa mwaminifu kutoa fungu la kumi toka
katika mazao ya shamba lako, usitegemee Mungu akupiganie wakati mharibu
anapoingilia mimea yako na kuiharibu. Vile vile usipokuwa mwaminifu kutoa fungu
la kumi toka katika mapato ya biashara yako, usitegemee Mungu akusaidie wakati
mharibu anapoingilia biashara yako na kuiharibu.
Inawezekana unatoa sadaka, na huoni baraka zozote zinazotokana na kutoa kwako –
hebu angalia na jichunguze kama umekuwa mwaminifu katika kutoa ZAKA KAMILI.
Kwa mfano kama fungu la kumi la pato lako ni shilingi 2,000 – toa zaka kamili
yaani shilingi 200/=. Usitoe pungufu ya hiyo maana haitakuwa zaka KAMILI.
Ikiwa umekuwa mwaminifu katika kutoa Zaka kamili na dhabihu halafu
huoni matokeo yake basi, tumia mamlaka ya Jina la Yesu Kristo – mfunge na
kumkemea ibilisi ambaye ndiye mharibu wa mali yako aondoe mikono yake juu ya
mali yako.
Kumbuka Yesu Kristo alisema;
“Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalofunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni” (Mathayo 16:19).

Kuna mtumishi mmoja wa Mungu ambaye anasimulia jinsi ambavyo mkulima mmoja wa
pamba alivyosaidika na uwezo wa jina la Yesu Kristo.
Huyo Mkulima alikuwa mwaminifu katika kumtolea Mungu fungu la kumi la mapato ya
shamba lake kila mwaka, na alikuwa haelewi kwa nini pamba yake ilikuwa
haifunguki ingawa muda wa kufunguka na kuchanua ulikuwa umefika. Wataalamu wa
kilimo cha pamba walikuja kuliangalia shamba hilo lakini hawakuweza kumsaidia
mkulima huyo kutatua tatizo hilo.
Mtumishi wa Mungu huyo alifika hapo, na alisikia habari ya mahangaiko ya
mkulima huyo. Baada ya kufahamu ya kuwa mkulima huyo alikuwa mwaminifu katika
kutoa fungu la kumi – alimwambia waende shambani ili waombe.
Huyo mtumishi wa Mungu wakiwa shambani na mkulima huyo; - akimkumbusha Mungu
juu ya ahadi yake ya Malaki 3:7-11. Na mwishoni akamwamuru ibilisi aondoke
kwenye pamba hiyo. Mara tu baada ya kumaliza sala hiyo – pamba ilianza
kufunguka na kuchanua! Bwana asifiwe sana kwa uwezo huu ulivyo wa ajabu.
Usibaki unalalamika na kuhangaika kama vile mtu asiyejua ahadi za Mungu.
Simamia haki zako ndani ya Kristo kwa kuwa mtendaji wa neno na utafanikiwa.
3. KUTOKUPANDA KATIKA UDONGO MZURI
Utoaji ni sawasawa na upandaji. Mtu akipanda anategemea kuvuna pia. Kwa hiyo mtu akitoa anategemea kupokea.
Utoaji ni sawasawa na upandaji. Mtu akipanda anategemea kuvuna pia. Kwa hiyo mtu akitoa anategemea kupokea.
Mkulima yo yote akitaka mavuno mazuri toka shambani mwake kati ya vitu
anavyoviangalia ni aina ya mbegu na aina ya udongo. Siku zote atapanda kwenye
udongo mzuri wenye rutuba.
Biblia inatuambia katika mfano wa mpanzi ya kuwa mbegu zingine“…. Zikaanguka penye udongo ulio mzuri, zikazaa matunda, zikimea na kukua, na kuzaa, moja thelathini, moja sitini, na moja mia” (Mathayo 4:8).

Je, “udongo mzuri” unaoleta faida nzuri ni
upi? Sehemu za kutoa zenye matokeo au mavuno mazuri ni hizi zifuatazo;
(a)
Katika nyumba ya Mungu – kanisani ili kuendeleza kazi ya Mungu – soma Malaki
3:10-11; na Kumbukumbu ya Torati 8:18.
(b)
Kuwasaidia watumishi wa Mungu na watakatifu wake kwa vitu/mali ulizo nazo.
Soma 1Wafalme 17:10-24 na 2Wakorintho 9:10-13.
(c)
Kuwasaidia maskini kwa vitu/mali ulizo nazo. Soma 2Wakorintho 9:8-9.
Angalia
upandaji wako katika utoaji – je! umepanda kwenye udongo ulio mzuri?
4. KUKATA TAMAA
Wagalatia 6:9 inasema hivi; “Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho”.
Tafsiri iliyo nyepesi inasema, “maana tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa”.
Wakristo wengi wanatoa lakini hawana uvumilivu. Mkulima asipokuwa mvumilivu kusubiri mazao ya shamba lake yanayokuja kwa wakati wake – hawezi kuvuna alichopanda.
Vile vile mtoaji asiyejifunza kumvumilia Mungu ili amletee matokeo ya utoaji huo kwa WAKATI WAKE – hawezi kuvuna alichopanda.
Mungu si mwongo! Wala ahadi zake hazijui kusema uongo. Alichoahidi atatenda. Ukitoa utapokea KWA WAKATI WAKE USIPOKATA TAMAA.
Usianze kutafuta njia za mkato ili ufanikiwe – uwe mvumilivu ulichopanda kwenye udongo mzuri utavuna.
Mkumbuke Ibrahimu alivyovumilia. Biblia inasema hivi;
“Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi” (Warumi 4:20-21).

5.KUTOA KWA MAJIVUNO NA KUTAFUTA KUSIFIWA NA
WATU
“Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili WATUKUZWE NA WATU. Amin, nawaambieni,wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na BABA YAKO AONAYE SIRINI ATAKUJAZI” (Mathayo 6:1- 4)

*************************************************************************************