Jumanne, 3 Oktoba 2017

MAOMBI MAALUMU YA WANAFUNZI


MAOMBI MAALUMU YA WANAFUNZI.



BWANA YESU ASIFIWE!.
Kanisa la INJILI AFRIKA – MLIMA WA MAKIMBILIO IKINDWA Tabora tarehe 08/10/2017 litaendesha maombi maalumu kwa Wanafunzi kuanzia Shule za Msingi hadi Vyuo vikuu. Hii ni kwasababu Wanafunzi wengi wanasumbuliwa na Nguvu za GIZA Mashuleni. Maombi hayo yatafanyika katika ibada ya j.pili ya tarehe hiyo yatakayoongozwa na Mch.Amos E. Onesmo. Maombi hayo yataambatana na Sadaka maalumu ya kuweka WAKFU masomo. Kidato cha Nne wataombewa kwa ajili ya Mtihani wao wa TAIFA October 2017. Wanafunzi wa Madhehebu yote wanakaribishwa. Walioko mbali wanaweza kufanya mawasiliano na Mchungaji au Sms kwa  
Mawasiliano: 0756391498/0658727799

Jumatatu, 14 Agosti 2017

NGUVU ILIYO KATIKA JINA LA YESU.


                                 SOMO:
NGUVU ILIYO KATIKA JINA LA YESU.
UTANGULIZI.
Ø  Wengi wameshindwa kutumia jina hili japokuwa wamekaa makanisani na kwenye Wokovu miaka mingi.
Ø  Hii imepelekea mateso mazito katika maisha yao.
Ø  Wengine ni kwa sababu ya:-
                                                                                  i.            Kutolitambua jina hili na nguvu zake
                                                                                ii.            Kutoliamini jina hili.
Ø  Jina la Yesu ni jina lipitalo majina yote.
                             WAFILIPI 2:9
Ø  Jina la Yesu limebeba nguvu ya Ki-Mungu iwezayo kuponya na kufungua vifungo vyote.
                           YOHANA 16:23-24

FAIDA YA KUTUMIA JINA LA YESU.
Ø  Tunausogeza Msaada wa Mungu karibu yetu.
                           MATHAYO 14:22-30
Ø  Tunapata uponyaji wa Miili yetu.
                           MATENDO YA MITUME 3:1-6

=====================================================================                                                                                                                                         By
Pastor AMOS E. ONESMO - 0756391498/0658727799


VITI VYA ENZI AKAAPO SHETANI


SOMO:
VITI VYA ENZI AKAAPO SHETANI.
Ø  Kuna mahali Shetani anafanya makao/anatengeneza enzi yake.
                                   UFUNUO WA YOHANA 2:12-17
DALILI ZA ENEO ILIKO ENZI YA SHETANI.
Ø  Kutesa na kuua watumishi wa Mungu.
            Mfano.
o   Stephano
                                MATENDO YA MITUME 7:54-60
o   Manabii.
                                MATHAYO 23:31-36
o   Paulo
                                MATENDO YA MITUME 14:19
Ø  Tabia ya kuinua na kuendeleza vita/migogoro isiyoisha.
                              WARAKA WA YAKOBO 4:1
VYANZO VYA MIGOGORO.
o   Madaraka
                              2  SAMWELI 3:1
o   Shetani analenga Ufalme wa Mungu usisimame.
                              1  MAMBO YA NYAKATI 2:8
o   Manung’uniko.
                            MAENDO YA MITUME 6:1
                            WAGALATIA 5:15
=====================================================================                                                                                                                                         By
Pastor AMOS E. ONESMO - 0756391498/0658727799

Jumatano, 26 Julai 2017

SIKU YA KIHISTORIA KWANGU 26/07/2017.


Leo ni siku yangu ya furaha kubwa kwa kuandika historia mpya katika safari yangu ya KI-ELIMU. Siku ya leo nimehitimu rasmi Masomo yangu ya chuo kikuu SHAHADA YA KWANZA YA UALIMU (Bachelor of Arts with Education-BAED).
Kipekee namshukuru Mungu aliyenilinda tangu OCTOBER 2014 nilipoanza chuo hadi leo 2017. Pia, shukrani zangu ziwaendee wafuatao;-
1)    Mke wangu mpendwa CHEUPE kwa kufanyika msaada mkubwa kwangu.
2)    Mama yangu mzazi kwa kunilea hasa katika kipindi kigumu cha ujane wake.
3)    Walimu wangu wa shule ya Msingi, Sekondari, A-level na Chuo kikuu.
4)    Kanisa langu na Wachungaji wenzangu.
5)    Shemeji yangu na Dada yangu.
6)    Ndugu zangu wote.
7)    Walimu wote wa Chuo kikuu cha TEOFILO KISANJI KITUO CHA TABORA na wengine wote waliofanyika msaada wakati wote wa masomo yangu.
Walimu hawa wanamchango mkubwa kuninoa katika somo la kiingereza hadi sasa nimekuwa Mwl wa somo la kiingereza;-
1)    Mwl Rocky – Shule ya msingi.
2)    Mwl Sinkala – Sekondari.
3)    Mwl Safari – A-level.
4)    Mwl Kaswaga –Chuo kikuu.
@Pastor Amos E. Onesmo -0756391498 E-mail: pasteronesmo@gmail.com